Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, September 5, 2012

Rudi Tena Ukaswali, Kwani Hukuswali




Sehemu Ya Kwanza

Katika usiku wa giza, Abu Lu’lu’ Al-Majuusi alijificha katika vivuli akijiandaa kwa ajili ya Swalaah ya Alfajiri, wakati ambapo ataendesha mipango yake ya kishetani kumuua Amiyr wa waumini – ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allahu ‘anhu).




‘Umar (Radhiya Allahu ‘anhu) alikuwa (na kawaida) ya kuongoza Swalah ya Alfajiri huku akisoma surah ndefu, akiwapa wafuasi wa jamii, muda wa kuhudhuria mkusanyiko (wa Swalaah). Katika siku hii, wakati (‘Umar) akisoma (Qur-aan), Abuu Lu’Lu’ akachukua hatua kutoka kwenye nguzo inayofifia, hali ya kuwa ana kisu cha sumu katika mkono wa vazi lake. Akaruka mbele ya ‘Umar (Radhiya Allahu ‘anhu) na akamkata tumbo wazi kwa (kile) kisu. Baada ya hapo, akajaribu kuukimbia mkusanyiko. Akiwa ana chana chana mbele na nyuma, akiwauwa watu wengi zaidi ambao walikuwepo katika njia yake. Swahaabah mmoja akamtupia nguo juu yake na alipo tahayari kwamba keshakamatwa Abu Lu’lu’ akajiua. 

‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (Radhiya Allahu ‘anhu) akaikamilisha Swalaah ya Alfajiri ambayo aliianza ‘Umar (Radhiya Allahu ‘anhu). ‘Umar (Radhiya Allahu ‘anhu) alikamilisha Swalaah yake hali ya kuwa ni miongoni mwa watu (maamuma) katika Jama’ah na akafariki dunia baadaye katika kitanda chake, (Radhiya Allaahu ‘anhu).

Umuhimu wa Swalaah katika Uislamu hauwezi kudharauliwa. Ni nguzo ya kwanza ya Uislamu iliyotajwa na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya tamko la Imani (shahaadah), ambayo kutokana nayo mtu huwa Muislamu.

Swalaah imefaradhishwa kwa Manabii na watu wote. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alitangaza hadhi yake ya kuwa ni faradhi katika tukio Tukufu. Kwa mfano, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Alipozungumza na Muusa (‘Alayhis Salaam), Amesema:

{{Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayofunuliwa. Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Swalah kwa ajili ya kunikumbuka Mimi}} [Twaaha: 13-14]

Hivyo hivyo, Swalaah imefaradhishwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipopelekwa mbinguni. Zaidi, wakati Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anawasifu waumini kama katika Suratul-Al-Mu-uminuun, moja katika sifa ambazo Anazitaja kuhusiana nao ni kule kushikana kwao na Swalaah:
{{Hakika wamefanikiwa Waumini. Ambao ni wanyenyekevu katika Swalah zao}} [Al-Mu’minuun: 1-2]

Umuhimu wa Swalaah unaendelea kuonyeshwa katika kauli nyingi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa mfano, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:

“Jambo la kwanza ambalo mja atahukumiwa katika Siku ya Hisabu ni Swalaah. Kama ikiwa ni nzuri basi amali zake zilizobakia zitakuwa nzuri. Na ikiwa ni mbaya, basi amali zake zilizobakia zitakuwa mbaya.” [At-Twabaraaniy].

Kwa kweli, ikiwa Swalaah imeswaliwa vizuri ikiambatana na ukumbusho  wa kweli wa kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), na kumgeukia Yeye kutaka msamaha, itakuwa na athari kubwa juu ya mtu kwa kipindi  kirefu. Mtu anapokamilisha Swalaah yake, moyo wake utajaa ukumbusho wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Atakuwa ana hofu na pia vilevile matarajio juu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Baada ya tukio hilo, hatotaka tena kuondoka kutoka katika sehemu hiyo ya fakhari kuelekea kwa ile ambayo ndani yake atamuasi Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) anaitaja hali hii ya Swalaah katika Qur-aan:  

{{Hakika Swalah inazuilia mambo machafu na maovu}} [Al-‘Ankabuut: 45].

Lakini katika wale ambao wanaoswali, utakuta kuna vitendo vya kivivu ambavyo vinahitaji kumulikwa. Kwa mfano:

·         Wengine hawazingatii kile ambacho wanakisema.
·         Wengine wanafanya haraka katika Swalah zao
·         Wengine wanaachilia nadhari yao ya macho izurure wakati wa Swalah
·         Wengine mara kwa mara husahau nambari ya rakaa zilizotimizwa.
·         Dunia inakumbatia mioyo ya baadhi ya watu wakati wa Swalah na inafunika akili zao.
·         Na watu wengine katika Jama’ah wanaanza kusujudu kabla hata ya Imaam kusema “Allaahu Akbar”

Linganisha hii (hali yetu katika Swalaah) na Swalaah za watu ambao walikuja kabla yetu. Watu walikuwa wanafikiria ya kwamba Ar-Rabiy’ bin Khaytham alikuwa ni kipofu kwa sababu ya kuinamisha macho yake mara kwa mara. Alikuwa akiishi nyumbani kwa AbduLlaah bin Mas’uud (Radhiya Allahu ‘anhu) kwa miaka ishirini na mtumwa wake wa kike akimuona alikuwa akisema: “Rafiki yako kipofu anakuja” na AbduLlaah alikuwa akimcheka kwa kauli yake.

Ndani ya AL-Bukhaariy na Muslim, Abuu Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu) anatueleza ya kwamba, kuna mtu aliingia msikitini, ambao Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amekaa. Akaswali rakaa mbili na kisha akaja kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akatoa salamu. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaijibu salamu yake na halafu akasema, “Rudi tena ukaswali kwani hukuswali.” Hivyo, yule mtu akarudi, akaswali (rakaa mbili) kama alivyofanya mara ya kwanza, akaja tena na kurudia kutoa salamu. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaijibu salamu na akasema “Rudi tena ukaswali kwani hukuswali.” Hivyo, yule mtu akarudi, akaswali (rakaa mbili) kama alivyofanya mara ya kwanza akaja tena na kurudia kutoa salamu. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alijibu salamu kwa mara nyingine tena na kwa mara nyingine tena akasema: “Rudi tena ukaswali kwani hukuswali”. Hadi kufikia mara hii ya tatu, mtu huyo alisema: “Naapa kwa Yule ambaye alikutuma wewe na ukweli, Ewe Mtume wa Allaah, sijui vyovyote isipokuwa hivi, Nifundishe.” Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

“Ikiwa unasimama kwa ajili ya Swalaah sema “Allaahu Akbar”. Halafu soma ambacho kitakujia kwa wepesi katika Qur-aan. Kisha rukuu mpaka utakapohisi kwamba umetulia katika rukuu yako. Kisha, simama mpaka uwe umesimama wima kisawa sawa. Kisha, sujudu mpaka uwe umetulia katika sujudu yako. Kisha keti mpaka uwe umetulia katika juluus yako. Kisha sujudu mpaka uwe umetulia katika sujudu yako. Na uwe unafanya hivi ndani ya Swalaah yako yote”.


(Kwahiyo turudi tukarudie Swalah zetu)

Kwanini tunakuja msikitini; nini sababu yetu ya kutekeleza Swalah? Tunafanya hivyo kwa kufuata amri ya Muumba wetu (Subhaanahu wa Ta’ala). Kwanini hasa tupoteze baraka na thawabu kwa sababu ya moyo usiotulia na mkono unaowasha. Khushuu ni kiini cha Swalaah zetu. Khushuu ni matunda ya imani yetu. Lakini, hata baada ya kujua haya, watu hawafanyi juhudi kukamilisha Swalah zao na kwa hiyo huandikiwa sehemu ndogo tu. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema;

“Kwa hakika, mtu ataondoka (katika Swalaah yake) na ataandikiwa (thawabu) kumi za Swalaah yake; tisa, nane, saba, sita, tano, nne, tatu, nusu.” [Abu Daawuud na at-Tirmidhiy]


‘Uthmaan bin Abii Dahshah (Radhiya Allahu ‘anhu) alisema: “Sijawahi kuswali Swalah ambayo baada yake nilikosa kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anisamehe kwa upungufu wangu katika Swalah ile.”

Mtu ambaye anaharakisha Swalah yake ni mwizi.  Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema katika Hadiyth sahihi, “Mwizi muovu kuliko wote ni yule ambaye anaiba katika Swalaah yake”. Swahaaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wakauliza: “Ewe Mjumbe wa Allaah, anaibaje katika Swalah yake?” Naye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Hakamilishi rukuu na sujudu zake”


Kwa sababu ya kasi ya jinsi ya watu wanavyoswali, wanaonekana kama ndege, wanaodonoa juu na chini. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza  mtu kudonoa (katika Swalah) kama kunguru.


‘Umar (Radhiya Allahu  ‘anhu) wakati mmoja alisimama katika Minbari akiuhutubia umati wa watu kwa sauti ya nguvu akisema, “Mtu anaweza akakulia mpaka utu uzima katika Uislamu na asiweze kamwe kukamilisha kwa ajili ya Allaah hata Swalah moja!” (Watu) wakasema, “Vipi hali hii?” (‘Umar) (Radhiya Allahu ‘anhu) akasema: “Hakamilishi khushuu yake, hata unyenyekevu wake, hata nadhari yake juu ya Allaah ‘Azza wa Jalla.”

Wakati mmoja, Ma’aruuf Al-Karkhiy (Rahimahu Allaah) aliposimama miongoni mwa wanafunzi wake, mmoja wao akamwambia mwenziwe, “Tafadhali swalisha Swalaah ya ‘Ishaa”. Mwanafunzi wa kwanza akakubali lakini akasema “Nitaswalisha Swalaah ya ‘Ishaa kwa sharti ya kwamba wewe utaswalisha Swalaah ya Alfajiri sio mie” Ma’aruuf Al-Karkhiy alishtushwa na kauli aliyoisema na akasema, “Naapa kwa Allaah, ikiwa unafikiria ya kwamba utakuwa hai wakati wa Alfajiri, basi naapa kwa Allaah, hujakamilisha Swalah yako”.


Sehemu Ya Pili

Jinsi ya kuwa na Khushuu ndani ya Swalah

Al-Qaasim bin Muhammad (
Rahimahu Allaah) alisema: “Nilikwenda nje siku moja, na kila nilipotoka ni lazima nipite kwa mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allahu ‘anha) na kumsalimia. Siku hiyo nilitoka na nilipomkuta mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allahu ‘anha) akiswali Swalah ya Dhuhaa, akisoma tena na tena Aayah ya Allaah:
 
{{Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa (adhabu ya Allaah). Basi Mwenyezi Mungu Akatufanyia hisani na Akatulinda na adhabu ya Moto.}} [At-Twuur: 26-27]

Alikuwa analia na akimwomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na huku akirudia Aayah hiyo. Nilisimama pale mpaka nikachoka, hali ya kuwa yeye amebaki kama nilivyomkuta. Nilipoona haya nilijiambia, “Hebu niende sokoni, nifanye ninachotakiwa kufanya, halafu nije tena”. Kwa hiyo, baada ya kumaliza kufanya nilichotaka kufanya sokoni, nilirudi kwa mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allahu ‘anha). Alikuwa kama nilivyomuacha, akirudia Ayaah, akimuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na akilia”.
 




Vipi tuwe na khushuu katika Swalaah?

Katika Sunnah ya Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam tunafundishwa yafuatayo:


1.     Njoo mapema kwa ajili ya Swalaah na jitayarishe kuwa na khushuu.
Fuatiliza adhana pamoja na Mu’adhin na baada ya adhana, sema dua iliyoamriwa. Omba dua baina ya Adhaana na Iqaamah. Tia wudhuu vizuri, hali ukisukutuwa mdomo wako, na vaa nguo zako nzuri kabisa.




2.     Nuia kupata dhawabu zote za Swalaah yako.
Abu Bakr bin ‘Iyaash alisema, “Nilimuona Habiyb bin Thaabit katika sujudu. Ukimuona utadhania kwamba kashakufa (kwa urefu wa sujudu zake).”


3.     Zingatia Aayah na adhkaar ambayo inasomwa ndani ya Swalaah.

Fikiria kuhusu maana za Aayah ambazo unazisoma. Je haivunji moyo ya kwamba mtu anaweza kuswali miaka kumi baada ya kumi, siku baada ya siku na pia bado hajui anasema nini? Qur-aan iliteremshwa ili itafakariwe! Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Kateremsha (katika Qur-aan Ayaah inayosema):

{{Na hiki Kitabu, Tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.}} [Swaad: 29].


4.     Swali Jama’ah. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anaamrisha:

{{Na shikeni Swalah, na toeni Zakaah, na rukuuni pamoja na wenye kurukuu.}} [Al-Baqarah: 43].


5.     Usikose kamwe kuswali Swalah zako za nawaafil (Sunnah zilizotiliwa mkazo), hasa zile ambazo Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali siku zote, kama vile Witri na Sunnah ya Alfajiri.


6.     Usiharakishe Swalah yako.

Chukua muda wako na usikubali kuifanya Swalah yako kuwa kitendo kilichokuwa hakina thamani katika siku yako. Ibn Wahb (Rahimahu Allaah) alisema: “Nilimuona Ath-Thawriy (Rahimahu Allaah) kwenye Kaa’bah.  Baada ya Swalah ya Magharibi, alinyanyuka kuswali na kisha akasujudu. Hakunyanyuka katika ile sujudu mpaka adhana ya ‘Ishaa ilipoadhiniwa.”


7.     Jua ya kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anajibu Swalah yako. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:

“Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Aliyetukuka alisema: “Nimeigawa Swalah kati Yangu na mja Wangu  katika nusu mbili, na mja Wangu atapata alichokiomba” [Kutoka katika Surat ul- Faatiha ] Wakati mja anaposema, “Sifa njema zote ni za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), Mola Mlezi wa viumbe vyote,” Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema, “Mja Wangu Amenihimidi” . Wakati mja anaposema “Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.” Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema, “Mja wangu Amenisifu.” Wakati mja anaposema, “Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo”, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema mja Wangu Amenitukuza”.  Wakati mja anaposema, “Wewe tu tunakuabudu na wewe tu tunakuomba msaada.” Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) anasema, Hii ni kati Yangu Mimi na mja Wangu, na mja Wangu atapata alichokiomba”. Wakati mja anaposema “Tuongoze katika njia iliyonyooka, njia ya  uliowaneemesha, sio ya wale uliowakasirikia, wala ya wale waliopotea,” Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)  Anasema, “Hivi vyote ni kwa ajili ya mja Wangu, na mja Wangu atapata alichokiomba” [Muslim]


8.     Swali pamoja na kizuizi (weka sutrah) mbele yako na swali karibu yake.

Kitu chengine ambacho kitakusaidia kuwa na khushuu’ [utulivu] ni kushughulika (au kuwa makini) katika suala la kuwa na kizuizi (sutrah) na kuswali karibu yake. Kuwa na sutrah kutazuia uoni wako, kutakulinda juu ya Shaytwaan, na kutazuia watu kupita mbele yako, kitu ambacho husababisha wasiwasi na hupunguza thawabu za Swalah. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: 

“Ikiwa mmoja wenu ataswali basi na aswali akielekea kwenye sutrah, na awe karibu nayo” [Abuu Daawuud].


9.     Tafuta ulinzi] kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kutokana na Shaytwaan.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitufundisha vipi tupambane na wasi wasi wa Shaytwaan. Abu’l- ‘Aas (Radhiya Allahu ‘anhu) kasimulia ya kwamba alisema, “Ewe Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Shaytwaan ananisumbua wakati ninaswali, na hupata wasiwasi katika kisomo changu.” Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, “Huyo ni Shaytwaan  ambaye jina lake ni Khanzab. Ikiwa utahisi kwamba yupo, jilinde kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kutokana naye, na tema mate (makavu) katika upande wako wa kushoto mara tatu”. Abu’l –‘Aas (Radhiya Allahu ‘anhu) alisema: “nilifanya hivyo na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Akaniondoshea.” [Muslim].

10.            Swali kama kwamba umeambiwa kuwa baada kumaliza Swalah utarudi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Abu Bakr Al-Muzaniy (Subhaanahu wa Ta’ala), alisema, “Kama unataka Swalah yako ikufae, basi sema: “Nitakufa baada tu ya Swalah hii!”  

Yampasayo Maiti



Kila sifa njema anastahiki Allah na rehma na amani zimfikiye Mtume Muhamad na ahli zake na sahabaze na wenye kufuwata wayo kwa ihsani mpaka siku ya mwisho,

Ama baa’d
Watukufu Waislamu taratibu za kumfanyia mmoja wetu, anapofikwa na umauti ni muhimu sana kwa kila muislamu kuzijuwa, kwani wengi wetu hawalifahamu vyema somo hili kama alivyotufundisha Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam], kwa maana hiyo tumechukuwa muda mwingi kuandaa maudhui haya yaliyo muhimu sana, tunaomba kila Muislamu kusoma kwa makini maudhui haya ili aweze kuufahamu vyema mchakato mzima wa ibada ya maziko, tunaanza darsa hii mwanzo kabisa, tunaomba sote tuwe wenye kuzingatia.

Kumlaqinia afikwaye na umauti
Amesema Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] walaqinieni wafikwao na umauti, kwa neno LAILAHAILALLAH na mwenye kufa hali ametamka neno hili bila shaka ataingiya peponi. Tazama  Swahihi Muslim vol.2, uk. 631, Swahihi Bukhari vol.1, uk.532. Vile inajuzu kwa Muislamu kumtembelea kafiri na kumlaaqinia ili asilimu

Dalili: alikuwa kijana mmoja wa kiyahudi akimuhudumia Mtume[swalallahu alaihi wasalam] akawa amepatwa na maradhi kijana huyo, Mtume akenda kumzuru kijana huyo, akamkuta yuko hoi kitandani na baba yake yuko pembeni , mtume alipoingiya akawa ameketi karibu na kichwa cha kijana huyo akamsalimia, kisha akamwambia silimu, yule kijana akawa anamuangalia baba yake, baba yake akamwambia mtii Abal Qasim[Mtume] ewe mwanangu! Kijana akamtii Mtume [swalallahu alaihi wasalam] na akasilimu, Mtume akatoka huku akisema namshukuru MwenyeziMungu ambaye amemuokowa kijana na moto, alipokufa huyo kijana Mtume [swalallahu alaihi wasalam] akasema kuwaambiya masahaba msalieni rafiki yenu.
Tazama Musnad Ahmad, vol. 3, uk.175, Swahihi Bukhari Vol.1, uk.575.

Yanayowapasa walio karibu na Maiti
Inapokuwa roho imechukuliwa na Malakul-mauti yaani [Malaika wa mauti] na ndiyo jina lake khaswa [siyo izrael] kama watu wengi walivyozowea, jina hili la malakul mauti ndiyo Allah Ta’ala alivyomuita malaika huyo katika Quraan surat Assajdah aya ya 11; Sema ewe [Mtume] uwaambie kuwa atakufikieni Malaika wa mauti aliyewakilishwa kwenu.
Yawapasa Walio karibu na maiti kufanya yafuatayo:
Mosi linalowapasa walio karibu na maiti ni kumfumba macho,
        Dalili: aliingia Mtume nyumbani kwa Abi salman na alikuwa Abi Salman amekodoa macho yake, Mtume akayafumba kisha akasema roho inapochukuliwa macho hufuatisha ile roho inapokwenda. Tazama Musnad Ahmad vol.6 uk.297, Sunan Baihaqi uk.334.
      ii. Jambo la pili ni kumuombeya Duwa Maiti
Dalili: Mtume[Swalallaahu alaihi wasalam] alipofumba macho ya Abi Salman, na huku watu wa Abi  Salman wanaliya kwa kupiga kelele akasema Mtume kuwaambiya; msiombe katika nafsi zenu ila muombeeni kheri kwani hakika Malaika wanaitikia aamin! Juu ya mnayoyasema, kisha Mtume akasema ewe MwenyeziMungu msamehe Abi Salman na inyanyue daraja yake iwe katika watu waliongoka, na utusamehe sisi na yeye ewe Mola wa walimwengu wote na uitanue kaburi yake na utie nuru ndani yake. Taz. Musnad Ahmad vol.6 uk.297
Jambo la tatu; ni kumfunika maiti kwa nguo yenye kusitiri mwili wake wote, 
Dalili: Amesema Bibi Aisha [Radhiyallaahu 'anha] alipokufa Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] alifunikwa kwa nguo iliyositiri mwili wake wote. Rejea Swahih Bukhari Vol.2 uk.651, Sunan Baihaq Vol. 3 uk.385, na jambo muhimu sana kwa wafiwa ni kuwa na subira na kuridhia kwa kile kilichowafika ameema MwenyeziMungu katika Quraan “Na tutakutieni katika msuko suko wa hofu, na njaa na upungufu wa mali, watu na matunda na wapashe habari njema wanaosubiri [al-Baqara aya ya 155] , muhimu ni kutaraji kwa MwenyeziMungu kwa lile lililowafika.

Amesema Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] hakuna Muislamu yoyote mwenye kupatwa na msiba kisha akasema yale aliyoamrishwa na MwenyeziMungu, aseme hivi:- Inalillah Wainailaihi Rajiun, Ewe MwenyeziMungu nipe malipo kutokana na msiba wangu na unibadilishie kheri zaidi  kuliko hii, isipokuwa Mwenyezi Mungu humbadilishia zaidi ya hilo. Taz. Swahihi Muslim Vol.3 uk.37, Sunan Bayhaq vol.4 uk.65, Musnad Ahmad Vol. 6 uk 309
Jambo lingine lenye kujuzu ni kwa walio karibu na maiti ni kuingia ndani na kumfunua uso maiti na kumbusu na kulia kwa kutoa machozi tu,na sio kujipiga piga. Dalili: aliingiya Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] kwa sahib wake Uthman Bin Madhoun alipofariki, akamfunuwa uso wake akambusu, na akawa analia mpaka machozi yakawa yanatiririka mashavuni kwake. Taz. Majmau Zawaid ya Haithami Vol. 3 uk 2, Sunan Tirmidhiy Vol.2 uk.130, pia wakati alipokufa Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam], aliingiya Abubakar [Radhiyallaahu 'anhu] kwa Aisha, Mtume alikuwa  ameshafunikwa nguo, Abubakar [Radhiyallaahu 'anhu] akamfunua usoni, kisha akambusu kati ya macho yake na akalia. Taz. Swahihi Bukhar Vol. 3 uk.89, Sunan Nnasai Vol. 1 uk 26, Ibn Hiban hadith namba 2100, Sunan Bayhaq Vol. 3 uk. 406.
Kumbuka mtukufu Muislamu yule tu aliyekufa akihirimia katika ibada ya Hija, haitakiwi kumfunika uso wake wala kichwa chake
Tunakumbusha ndugu waislamu kuwa haifai kabisa kulia kwa sauti ya makelele, wala kwa kujipiga piga usoni, kutimuatimua nywele, kujichania nguo, kujikwarua kwarua, kujipaka unga na kujimwagia mchanga, haya si katika maomboleo ya kiislamu yapaswa tujihadhari nayo sana.
Dalili: amesema Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] si katika sisi Waislamu mwenye kulia kwa kujipigapiga, kujichania nguo na kuomboleza kwa maombolezo ya kijahiliya, Taz. Swahihi Bukhar Vol.3 uk.127, Swahihi Muslim Vol.1 uk.70
Na amesema tena Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam], jambo hili la kulia kwa kelele si katika mwenendo wangu, bali moyo unahuzunika na macho yanatoa machozi na wala asikasirikiwe Mwenyezi Mungu. Taz. Mustadrak ya Hakim Vol. 1 uk. 382, Ibn Hiban uk 743
Dalili: amesema sahaba wa Mtume[Swalallaahu alaihi wasalam]Anas Bin Malik ya kuwa amesema Mtume, subira inatakikana mwanzo wa pigo[matatizo], Taz, Swahihi Bukhari hadith namba 1252, Swahih Muslim hadith namba 15, Abu Dawd hadith namba 3124

 KUHARAKISHA KUMTAYARISHA MAITI
Amesema sahaba Jaabir Bin Abdillah [Radhiyallaahu 'anhu] kwamba alikufa mtu mmoja, haraka tukamuosha na kumvika sanda na tukamtia manukato na tukaweka linapowekwa jeneza ili Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] amswalie. Taz. Mustadrak ya Hakim Vol.2 uk.58, Sunan Bayhaq vol.6 uk.74, Majmau Zawaid ya Haitham vol.3 uk.39, Musnad Ahmad vol.3 uk 330.

 UTARATIBU WA KUOSHA MAITI
Amesema Imam Abu Hanifa na Imam Malik yakuwa:-anapooshwa maiti avuliwe nguo zake na isitiriwe sehemu zake za siri, wala asikatwe kucha, ndevu, nywele, wala kwapa wala sehemu za siri. Taz. Bidayatul Mujtahid uk.192, Al Mizanil kubra uk.93
Amesema Imam Ibn Qudamah: Ataandaa muoshaji vipande viwili vya kitambaa, kisha atapitisha mkono wake wa kulia tumboni kwa maiti, akimkamua tumbo taratibu na kwa upole, kisha atachukuwa kitambaa kimoja na kuanza kumsafisha maiti sehemu za siri kwa kitambaa, kisha amtawadhishe maiti udhu wa sala na wala asiingize maji mdomoni kwake wala puwani, na ikiwa pana uchafu mdomoni au puwani undolewe kwa kitambaa, kisha aanze kumuosha maiti upande wa kulia na kisha kushoto. Taz. Al Mughni ya Ibn Qudama, vol.2 uk.256.
Na amesema Imam Ahmad Bin Hambal yakuwa:-anapomaliza kutawadhishwa maiti aoshwe kuanzia kichwa chake ndevu zake na upande wa kulia.

Na amesema sheikh Abdullah Ibn Baaz:- Utaratibu wa kuosha maiti ni kumsitiri sehemu zake za siri, kukamua tumbo lake kwa taratibu na kwa upole na kumsafisha kwa kitambaa sehemu za siri kisha kumtawadhisha udhu wa sala na kisha kumuosha kichwa chake, ndevu zake, kisha upande wa kulia alafu kushoto mara tatu au tano, jinsi utakavyoona, Taz. Majmou Fatawa ya Ibn Baaz-durusul muhimah uk.12

KUANZA KULIYANI NA SEHEMU ZA UDHU
Dalili: Amesema Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] alipokuwa akiwaambia wanawake walokuwa wakimuosha binti yake, Zainab alipofariki , aliwaambia hivi:- anzeni kuliani kwake na sehemu za udhu. Taz.Swahihi Bukhar hadith namba 1256, Swahihi Muslim hadith namba 43, Sunan Abu Dawd hadith namba 3145.

Na amesema Imam Shafii ya kuwa: Ni bora kumuosha maiti Kwa maji ya kawaida ila ikiwa kuna baridi kali ndiyo akoshwe kwa maji ya moto [vuguvugu], Taz. Al Mizanul Kubra uk.93

KUMUOSHA MAITI KWA MAJI YA MKUNAZI AU SABUNI
Dalili: amesema Ummu Atwiyyah [Radhiyallaahu 'anha]kuwa aliingiya Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam]kwetu alipofariki  binti yake akasema muosheni mara tatu au tano kwa maji ya mkunazi.
Taz. Swahihi Muslim Vol.3 uk 47, Abu Dawd vol.2 uk 6, Sunan Nnasaiy Vol.1 uk 266.
La muhimu piya kwa maiti mwanamke mwenye nywele ndefu zilizosukwa, zitafumuliwa na  kisha kuzichana na kuzisuka upya kwa mistari mitatu na kuitupa nyuma yake.
Dalili: Amesema Ummu Atwiyya [Radhiyallaahu 'anha] tulipomuosha binti ya Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] tulizifumua nywele zake, kisha tukaziosha na kuzichana, na kuzisuka kwa mistari mitatu tukazitupa nyuma yake. Taz.Swahihi Bukhari vol.3 uk.104, Swahihi Muslim vol.3 uk.48, Musnad Ahmad vol.5 uk.408

MAJOSHO KAMILI YAWE MARA MOJAMOJA
Dalili: Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam], aliwaambia wanawake walokuwa wakimuosha binti yake; Muosheni josho kamili mara moja moja na liwe josho hilo mara tatu au tano au zaidi jinsi mtakavyoona , Taz. Swahihi Bukhari hadith namba 1263, Swahihi Muslim hadith namba 41.

Na amesema Imam Ibn Qudama yakuwa anapomaliza kuoshwa maiti, akaushwe kwa nguo ili zisilowe sanda zake, Taz. Al Mughni ya Ibn Qudama vol.2 uk.464.

KUMUWEKA MAITI MANUKATO
Wapendwa waislamu yatakikana tuwapambe maiti wetu kwa manukato mazuri mazuri, Dalili:- Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] aliwaambia wanawake walokuwa wakimuosha binti yake; Na muwekeeni mwisho wa kumuosha chochote katika manukato. Swahihi Bukhari vol.3 uk.99, Swahihi Muslim vol.3 uk.47, Sunan Tirmidhi vol.2 uk 130, Sunan Nnasai vol.1 uk.266

INAJUZU KWA MUME KUMUOSHA MKE
Dalili: Amesema Bibi Aisha [Radhiyallaahu 'anha] mkewe Mtume yakuwa; aliporejea kwangu Mtume akitoka mazikoni, na mimi nikiwa na maumivu kichwani, na huku nikisema Ee! Maumivu ya kichwa changu [kichwa chaniuma] Mtume [Swalallashu alaihi wasalam] nae akasema, Bali hata mimi Ewe Aisha najisikia maumivu ya kichwa changu, maumivu hayo hayatakudhuru, na lau ukifa kabla yangu basi, nitakusimamia, kukuosha na kukuvika sanda, kukusalia na kukuzika.
Musnad Ahmad vol.6 uk.228, Addaarimiy vol.1 uk 7, Siyrat Ibn Hisham vol.2 uk 366

INAJUZU KWA MKE KUMUOSHA MUME
Dalili: Amesema Bibi Aisha [Radhiyallaahu 'anha]; Lau ningekuwa nimelielekeza jambo la kumuosha Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] alipofariki kuwa jambo hilo katika amri yangu mimi, nisingelipa mgongo jambo hilo na wasingemuosha Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] isipokuwa wakeze
Ibn Majah vol.1 uk.446, Ibn Hiban hadith namba 2156, Mustadrak ya Hakim vol.3 uk.59

SHARTI NA FADHILA KWA MWENYE KUOSHA MAITI
Wapendwa Waislamu ibada hii ya kuosha maiti ina sharti na fadhila zake amesema Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam]ya kuwa; Mwenye kuosha maiti muislamu kisha akasitiri aibu aliyoiona kwa yule maiti, husamehewa madhambi yake mara arobaini.
Mustadrak ya Hakim vol.1 uk.354, Majmau Zawaaid ya Haithami vol.3 uk.21, AL Mundhir vol.4 uk 17. Na amesema Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] yakuwa; Hakika Mwenyezi Mungu hakubali amali yoyote ile, mpaka ifanywe kwa ajili ya kutakwa radhi zake yeye MwenyeziMungu. Sunan Nnasai vol. 4 uk.171.

UTARATIBU WA KUMVIKA SANDA MAITI
Amesema Bibi Aisha [Radhiyallaahu 'anha] ya kuwa; alikafiniwa Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] katika nguo tatu nyeupe, hakuna kanzu wala kilemba katika sanda hizo tatu alizokafiniwa Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam]
Sunan Baihaqi vol.3 uk.399, Musnad Ahmad vol.6 uk.40, Abu Dawud hadith namba 3052

Ndugu waislamu ni wajibu kumvika sanda nzuri maiti, na sanda [au] thamani yake itokane na mali ya maiti , ndugu zake, jamaa zake, na isiwe sanda ya thamani  kubwa, na avikwe maiti sanda hiyo kwa utaratibu alofundisha Mtume [Swalallashu alaihi wasalam] bila kuzidisha chochote. Amesema MwenyeziMungu; Hakika mnao mfano mwema wa kuiga kwa Mtume wa MwenyeziMungu [Ahzab aya ya 21]
Kwa muktadha huo sanda iwe nzuri, amesema Mtume [Swalallsahu alaihi wasalam] Mmoja wenu anapomvika sanda ndugu yake, basi amvike sanda iliyo nzuri akiweza,
Swahih Muslim vol.3uk50 Abu Dawd vol.2 uk.62, Musnad Ahmad vol.3. uk.295, Sunan Tirmidh vol.2 uk.133.

Na amesema Imam Ibnu Mubarak: Na muradi wa sanda nzuri ni ile sanda iwe safi na yenye kutosha kumsitiri maiti mwili wake wote, na siyo kufanya isirafu katika sanda kwa kununua sanda ya thamani kubwa.

AINA YA SANDA
Dalili; amesema Mtume [Swalallashu alaihi wasalam]:- Vaeni katika nguo zenu nyeupe, hakika nguo nyeupe ni bora katika nguo zenu na wavikeni sanda maiti wenu kwa nguo nyeupe.
Sunan Abu Dawd vol.2 uk.176, Sunan Tirmidh vol.2 uk.12, Ibn Majah vol.1 uk.449, Sunan Bayhaqi vol.uk.245 kwa maana hii tunakumbusha tena ndugu Waislamu haifai kupoteza mapesa mengi kwa ajili kununulia sanda za thamani kubwa, amesema Mtume [Swalallsahu alaihi wasalam]:- Hakika Mwenyezi Mungu anachukia kwenu ninyi kutokana na mambo matatu:- [a] Porojoporojo [b] Kupoteza mali [c] Kuulizauliza hovyohovyo. Taz. Swahihi Bukhari vol. 3uk 266, Swahihi Muslim vol.5 uk.131, Musnad Ahmad Vol.4 uk.246.

KUHARAKISHA KUMLIPIA MAITI DENI KABLA YA KUSALIWA
Wapendwa Waislamu, yeyote katika sisi akiwa na haki za watu, basi awarejeshee, na ikiwa hana kabisa basi aache wosia kabla ya kufa.
Dalili; Amesema sahaba wa Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] Jabir Bin Abdillah [Radhiyallaahu 'anhu]; Hakika alikuwa Mtume hamsalii mtu mwenye deni, basi inapoletwa maiti kwanza huuliza je ana deni? Masahaba hujibu ndiyo ana deni, kisha anasema Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] msalieni rafiki yenu, akasema sahaba Abu Qatada, deni hilo litakuwa juu yangu,nitamlipia, ndipoMtume akamsalia yule maiti. Swahihi Bukhari hadith namba 2289, Abu Dawud hadith namba 43, Muslim hadith namba 14.

Tukumbuke Waislamu ya kuwa,  ni muhimu sana kuharakisha kumlipia maiti deni lake kutoka katika mali yake na hata kama itatolewa mali yake yote kulipia madeni, ikiwa hana basi ni juu ya dola ya kiislamu kumlipia madeni yake, ikiwa hakuna dola ya kiislamu, inafaa kwa yoyote kujitolea kwa hiyari yake kumlipia madeni maiti.
Dalili; amesema sahaba Abu Hurayra [Radhiyallaahu 'anhu]:- hakika alikuwa Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] inapoletwa maiti ya Muislamu ili amswalie kwanza huuliza je ana deni na ameacha wa kumlipia? Masahaba wakijibu ndiyo kaacha wa kumlipia, ndipo anamsalia maiti huyo. na pakijibiwa hapana hajaacha wa kumlipia basi anasema msalieni rafiki yenu, basi na MwenyeziMungu, alipomkunjulia Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam] Mtume alisema hivi:- mimi nina haki zaidi kwa Waislamu kuliko nafsi zao, na mwenye kufa akaacha deni mimi ndiye nitakayelipa na mwenye kuacha mali basi mali hiyo ni ya warithi wake.
Swahihi Muslim hadith namba 15, Tirmidhi hadith namba 1069, Ibn Majah hadith namba 2407.

DENI NI LA AINA MBILI
Dalili; Amesema Mtume [Swalallaahu alaihi wasalam]:- deni ni la aina mbili, mwenye kufa na hali ya kuwa anayo niya ya kulipa deni , basi mimi ni msimamizi wake, na mwenye kufa na hali ya kuwa hana niya ya kulipa, basi mtu huyo yatachukuliwa mema yake siku ya Qiyama, na haitakuwa siku hiyo kulipa pesa ya aina yoyote ile [Twabaran fil kabir], tunasisitiza wapendwa Waislamu tulipe madeni. siku hiyo yatachukuliwa mema yako na  kupewa mdeni wako, na ikiwa huna mema, basi yatachukuliwa madhambi ya mdeni wako ubebeshwe wewe kisha utupwe motoni.

Itaendelea toleo lijalo InshaAllah

Monday, September 3, 2012

Mwanamke Wa Kiislam: Hadhi Yake Katika Ummah



Siri ya umuhimu wa mwanamke wa Kiislam inatanda katika mzigo mkubwa na jukumu ambao alilowekewa mbele yake, na mashaka ambayo yako katika mabega yake. Jukumu na mashaka ambayo hata mengine mwanamme anaweza kubeba.

Hadhi ya mwanamke katika Uislam ina cheo kikubwa na iliyo na taadhimu, na taathira yake ni kubwa mno katika maisha ya kila Muislamu. Kwa kweli mwanamke wa Kiislamu ni mwalimu wa kwanza katika kujenga jamii njema, ikiwa kama atafuata mwongozo kutoka katika Kitabu cha Allaah na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: “Nakuachieni vitu viwili, hamtapotea kamwe kama mkivishikilia kwa nguvu vyote viwili hivi, Kitabu cha Allaah na Sunnah zangu.”[ii]

Kama ilivyokuwa katika ukawaida wa Qur-aan na Sunnah humwekwa kila Muislamu mwanaume au mwanamke mbali na upotofu kwa njia yeyote. Upotofu ambao mataifa mbali mbali yanaugua, na upotofu wao hauji ila kwa sababu ya kuwa mbali kabisa na njia ya Allaah, ambaye ni Mkamilifu kushinda wote, Aliye juu kabisa, na pia kuwa mbali na yale ambayo Mitume na Manabii wake (Rehma na Amani ziwafike juu wao wote) wamekuja nayo. Umuhimu mkubwa wa mwanamke wa Kiislam ikiwa mke, dada, au binti, haki ambazo zinatakiwa kutimizwa kwake na haki ambazo anatakiwa kutimiza zimefafanuliwa katika Qur-aan Tukufu, na maelezo zaidi ya haya yamefafanuliwa katika Sunnah iliyotakasika.

Siri ya umuhimu wake umetanda katika kazi yake nzito na mamlaka ambayo yamewekwa juu yake, na shida ambazo anabeba mabegani kwake - mamlaka na dhiki ambazo hata mwanaume hawezi kuzibeba.  Ndio maana imelazimishwa kwa mtu kuonyesha hisani kwa mama yake, kuonyesha upole na uhusiano wa ukaribu ulio mzuri kwake. na katika jambo hili, apewe ubora  kuliko baba mtu. Mwenyezi Mungu Mtukufu kasema:
 "Na Tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni Kwangu Mimi ndiyo marudio." [Surah Luqmaan 31:14].

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kasema,
"Na Tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini".  [Surah Ah'qaaf 41:15].

Mtu alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu alayhi wa salam) na akasema,
"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nani miongoni wa watu wote anastahiki uhusiano wangu wa karibu?" Mtume akajibu.  "Mama yako"
Yule mtu akauliza tena, "kisha nani?" Mtume akamjibu 
"Mama yako"
Yule mtu akauliza tena, "kisha nani?" Mtume akamjibu 
"Mama yako"
Yule mtu akauliza tena, "kisha nani?" Mtume akamjibu.
"Baba yako"[iii]

Kwahiyo haya yanasisitiza kwamba mama mtu anapewa heshima mara tatu kuliko baba mtu.

Na kuhusu mke, hadhi yake na taathira yake katika kutuliza moyo na kuliwaza imeonyeshwa wazi wazi katika Aayah Tukufu (kauli ya Allaah), katika msemo wake Mtukufu,
"Na katika Ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri. [Suuratur-Ruum 30:21].

Al-Haafidh Ibn Kathiyr (Aliyefariki 774H) - RahimahuLLaah - alisema katika kufafanua neno Mawaddah na Rahmah ambayo inapatikana katika Ayaah iliyopita, anasema:

"Al-Mawaddah inamaanisha mapenzi na  mahaba na Ar-Rahmah inamaniisha rehma (upole) na huruma - kama ilivyokuwa mtu anamchukuwa mwanamke ama kwa sababu ya mapenzi kwake, au kwa sababu ya mapenzi juu yake au kwa sababu ya upole na huruma juu yake, kwa kumpa mtoto kutokana na yeye..."[iv]
(Ziada: soma chini kuhusu maonyo ya kuchagua mke aliyoyatoa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam).

Na jinsi mke wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Bi Khadiyjah (Radhiya Allaahu 'anha) alivyosimama kwa namna ya pekee kusaidia sana kumliwaza na kumtuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)   wakati Jibriyl ('alayhis-salaam) alipojitokeza kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa mara ya kwanza katika pango la Hiraa.  Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alirudi kwa Bi Khadiyjah (Radhiya Allaahu 'anha) akiwa na wahyi wa kwanza na huku moyo wake unapiga na kutetemeka kwa nguvu, na akamwambia Bi Khadiyjah:
"Nifunika! Nifunike!"
Kwa hiyo, (Bi Khadijah) akamfunika mpaka hofu yake ilipotokomea, baadaye Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamuelezea Bi Khadiyjah (Radhiya Allaahu 'anha) kila kitu kilichotokea na akasema
"Naogopa juu ya kutokewa na kitu kibaya"
(Bi Khadiyjah) akamwambia,
"Abadan! WaLlaahi! Allaah hatokuangusha. Unaweka mahusiano mema baina yako na jamaa zako, unawasaidia masikini na fukara, unawahudumia wageni wako kwa ukarimu na unawasaidia wale ambao wamekumbwa na maafa."[v]

Na usisahau kuhusu mama wa waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) pamoja na taathira yake. Hata Maswahaba watukufu walikuwa wanajipatia elimu ya Hadiyth kutoka kwake., na wengi katika Maswahabiyaat (wafuasi wa kike wa Rasuulu-Allaah) walijifunza vitu mbali mbali kuhusu Sharia zilizowahusu wanawake kutoka kwake.

Sina shaka ya kwamba mama yangu- Allaah Amrehemu - alikuwa na taathira makubwa juu yangu, alikuwa ananihimiza nisome, na alikuwa ananisaidia kwa hilo. Allaah Amuongezee thawabu na Amlipe kwa malipo mema kwa yote aliyonifanyia.

Na pia bila shaka, nyumba ambayo ina huruma, upole, upendo na kujali, pamoja na mafundisho mema ya Kiislam itamuathiri mtu. Kwa hiyo atakuwa - ikiwa Allaah atapenda - mwenye kufanikiwa katika mambo yake na katika kitu chochote - ikiwa kutafuta ilmu, biashara, kupata maisha mazuri, au vingine baada ya hivi. Kwahiyo ni Allaah peke Yake ninayemuomba Anipe mafanikio na Atuongoze sote kwenye yale ambayo Anayapenda na Anaridhia. Na Salam na Amani za Allaah zimfikie Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)    na familia yake, Maswahaba zake na wafuasi wake. 






[i] Ni mtu ambaye anayestahili kufuatwa: Abu ‘Abdillaah, ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz. Alizaliwa katika mji wa Riyaadh (Saudi Arabia) katika tarehe ya kumi na mbili (12) ya Dhul-Hijjah katika mwaka wa 1330H. Alianza kutafuta elimu kwa kuhifadhi Qur-aan kwanza kabla ya hata kubaleghe. Baada ya hapa, alianza kusoma elimu au maarifa ya Kiislam kama vile Aqiydah (Imani au Itikadi), Fiqh (Shari’ah ya Kiislam), Hadiyth, Usuulul-Fiqh (Sayansi ya Sheria), Faraaidh (Mirathi), Nahw (Nahau au Sarufi) na Swarf (elimu ya umbo na ujenzi wa wanyama, mimea na lugha) - Shaykh huyu aliweza kufanya yote haya japokuwa alipata upofu wa macho wa kudumu  wakati akiwa na umri wa miaka kumi na nane. Alisoma maarifa ya Kiislam chini ya wanavyuoni maarafu wa Riyaadh na Makkah, wakiwemo Shaykh Muhammad bin ‘Abdil-Latwif bin ‘Abdir Rahmaan bin Hasan na pamoja na Mufti wa zamani ambaye ni mwanachuoni bora, Shaykh Muhammad bin Ibraahiym - ambaye alisoma kwake kwa miaka kumi. Aliishi miaka thamanini na tisa, alikuwa mpole, mkarimu, mstahamilivu, lakini thabiti katika maumbile yake, alikuwa na busara wakati alipokuwa anazungumza mazungumzo ya haki (ukweli). Alikuwa Zaahid (mtu ambaye anajiepusha) juu ya mambo ya kilimwengu na alikuwa mmoja wa wanavyuoni wakuu wa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah (Wenye kufuata mwendo wa Mtume na Maswahaba) katika umri wake. Shaykh Abu ‘Abdillaah ‘Abdul ‘Aziyz ambaye alikuwa ni mtu bora, kwa rehma ya Allaah aliweka bidii katika maisha yake yote juu ya Uislam na watu wake. Na ni mwandishi wa vitabu vingi vikiwemo vitabu vidogo vidogo, akiwafundisha na kuwatumikia watu chungu nzima, na pia alikuwa na bidii (hodari) katika upande wa Da'waah. Allaah amsamehe Shaykh wetu ambaye ni pia kama baba yetu.
Makala hii ni majibu kuhusu suala maalum ambalo lilihusu cheo na hadhi ya mwanamke wa Kiislamu na imepatikana kutoka Majmu’ul Fataawaa wa Maqaalaatil Mutanawwi`ah (3/348-350) ambayo ni ya Shaykh Abu ‘Abdillaah, ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz.

[ii] Hasan: Imesimuliwa na Maalik katika al-Muwattwaa (2/899) na al-Haakim (1/93), kutokwa kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu). Ilithibitishwa na Shaykh al-Albaaniy katika as-Swahiyhah (Namba 1871).
[iii] Imesimuliwa na al-Bukhaariy (Namba 5971) na Muslim (7/2), kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu).
[iv] Tafsri ya Qur-aan Tukufu (3/439) ya al-Haafidh Ibn Kathiyr.

[v] Imesimuliwa na al-Bukhaariy (1/22) na Muslim (1/139), kutoka kwa masimulizi marefu yaliyopokewa kutoka kwa mama wa waumini  'Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhu).

VIJANA WAKITOA UBANI {SWADAKA}

vijana wakutana na familia ya marehemu fiqhi ,,,,,,  vijana hao walikutana na upandeawa familia ya marehemu na kubadilishana mawazo huku likiwalengo  kuulakikao hicho ni  kutoa ubani juu ya kipenzi chao,  rafiki yao fiqhi


aidha vijana haio walijadili jinsi ya kusaidiana  kwa urifiki wao na siourafiki huokuishia kwenye mitanda ya kijamii kami vile facebook twitet n.k

vile vile alichaguliwa bi zahra muhammed kua nimshika fedha akisaidiana na mustafa pamoja na hussein ambae ni kaka wa marehemu.
 




Alhamdulillah katika kikao cha ambacho kimefanyika Alaasiri ya leo Jamhuri Garden kwa ajili ya kujadili njia ya kuweza kutoa mchango wetu kwa ajili msiba wa mwenzetu FIQHI MOHAMMED HUSSEIN tumeweza kukusanya Shilingi 115,000/- michango bado inaendelea na kuna account za EASY PESA, MPESA, TIGO PESA NA AIRTEL MONEY ambazo zitafunguliwa kuanzia ksho inshallah ili wale ambao hawakuweza kufika gani leo na wana nia ya kuchangia waweze kufikisha michango yao kwa njia hizo ama kwa wenzetu amabao wako nje ya Zanzibar na wangelipenda kutoa michango yao, utaratibu unaandaliwa na watajuulishwa haraka iwezekanavyo

Sunday, September 2, 2012

Fadhila Za Kumtaja Allaah





 Amesema Allaah سبحانه وتعالى
:{ فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُواْ لِي وَلاَ تَكْفُرُونِ }
“Nitajeni nami nitawataja, na nishukuruni na wala msinikufuru (Suratul Baqaraha 152)
Na akasema:
 { يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْراً كَثِيراً}
“Enyi mlioamini mtajeni Mwenyezi Mungu sana” (Suratul Ahzaab 41 )
Akasema tena:
 { وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيراً وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْراً عَظِيماً}
“Nawasifu wanaume wanaomtaja Mwenyezi Mungu sana na nawasifu wanawake wanaomtaja, Mwenyezi Mungu   kawaandalia wote hao msamaha na malipo makubwa” (Suratul Ahzaab 35 )
Akasema tena :
{ وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعاً وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ وَلاَ تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ }
“Mtaje Mola wako  moyoni mwako kwa  unyenyekevu  na kwa uwoga, pasina kudhihirisha sauti, mtaje asubuhi  na jioni, nawala usiwe nikatika wenye kughafilika” (Suratul A’raaf 205)
Mtume صلى الله عليه وسلم amesema :
 }  وقال صلى الله عليه وسلم :" مثل الذي يذكر ربه والذي لا يذكر ربه مثل الحي والميت {
{Mfano wa anaemtaja Mola wake na asiyemtaja ni mfano wa alie hai na maiti }
Na akasema Mtume صلى الله عليه وسلم
وقال صلى الله عليه وسلم :" ألا أنبئكم بخير أعمالكم , وأزكاها عند مليككم، وأرفعها في درجاتكم ، وخير لكم من إنفاق الذهب والورق ، وخير لكم من أن تلقوا عدوكم فتضربوا أعناقهم ويضربوا أعناقكم ؟" قالوا بلى .قال : "ذكر الله تعالى
{Hivi niwaambieni khabari  yamatendo yenu bora, na ambayo ni masafi mno, mbele ya Mola wenu, na ambayo ni yajuu mno katika daraja zenu, na ambayo ni bora kwenu kuliko kutoa  dhahabu na fedha, na ambayo ni bora kuliko  kukutana  na adui zenu, mkawapiga shingo zao, nao wakakupigeni shingo zenu?))  Wakasema masahaba; Ndio . Akasema  Mtume صلى الله عليه وسلم  ((Ni kumtaja Mwenyezi Mungu))
وقال صلى الله عليه وسلم :" يقول الله تعالى : أنا عند ظن عبدي بي ، وأنا معه إذا ذكرني ، فإن ذكرني في نفسه ذكرتهُ في نفسي ، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم ،وإن تقرب إلى شبراً تقربت إليه ذراعاً ،وإن تقرب إلي ذراعاً تقربت إليه باعاً ، وإن أتاني يمشي أتيتهُ هرولة "
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Mwenyezi Mungu  anasema “Mimi niko mbele ya dhana ya mja wangu kwangu, akinitaja moyoni nami ninamtaja moyoni  na akinitaja katika  kundi, nami namtaja  katika kundi bora zaidi ya hilo lake, na akijikurubisha kwangu paa moja, basi mimi najikurubisha kwake kiasi cha dhiraa, na akijikurubisha  kwangu kiasi cha dhiraa, basi mimi nitajikurubisha  kwake kiasi chakuyoosha mkono hadi kati ya kifuwa, na akinijia kwa mwendo mdogo basi nami nitamjia kwa mwendo wa kasi. 
وعن عبد الله بن بسرٍ رضي الله عنهُ أن رجلاً قال : يا رسول الله إن شرائع الإسلام قد كثرت علي فأخبرني بشيءٍ أتشبث به. قال :" لا يزال لسانك رطباً من ذكر الله  
Imepokelewa kutoka kwa Abdalla Bin Busr رضى الله عنه   kwamba mtu mmoja alisema :
“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ibada za dini zimekuwa nyingi kwangu, basi nieleze kitu  ambacho nitaweza  kudumu nacho.   Mtume صلى الله عليه وسلم  akamwambia : Ulimi wako utaendelea kuwa rutuba  (yaani sio ukavu ) kwakumtaja Mwenyezi Mungu  .
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قرأ حرفاً من كتاب الله به حسنة ،والحسنة بعشر أمثالها ، لا أقول : {الم } حرف؛ ولكن : ألف حرف ،ولام حرف ،وميم حرف
Na amesema tena Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaesoma harufu moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu  basi anapata thawabu za jema moja na jema ni kwa mema kumi, sisemi kuwa ‘Alif Laam Miim’ ni harufu moja lakini ni kwamba ‘Alif’ peke yake ni harufu moja, na ‘Laam’ ni harufu , na ‘Miim’ ni harufu”
وعن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ونحن في الصفة فقال :" أيكم يحب أن يغدو كل يوم إلى بطحان أو إلى العقيق فيأتي منه بناقتين كوماوين في غير إثم ولا قطيعة رحم ؟" فقلنا : يا رسول الله نحب ذلك . قال :" أفلا يغدو أحدكم إلى المسجد فيعلم ، أو يقرأ آيتين من كتاب الله عز وجل خير له من ناقتين ، وثلاث خير لهُ من ثلاث ٍ، وأربع خير لهُ من أربع ، ومن أعدادهن من الإبل
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir رضى الله عنه   amesema :  ‘Ametoka Mtume wa Mwenyezi Mungu   na sisi tuko sehemu iitwayo Assufah, akasema “Nani kati yenu anapenda aende kila siku sehemu iitwayo But-haan au Aqiq aje na ngamia  wawili walio  nenepa pasi na dhambi wala kukata udugu?”  Wakasema  maswahaba “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tunapenda hivyo’ akasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Hivi haendi (asubuhi ) mmoja wenu msikitini  akajuwa  au akasoma Aya mbili, za kitabu cha Mwenyezi Mungu?    Hizo aya mbili  ni bora kwake kuliko  kupata ngamia wawili, na endapo atasoma aya tatu zitakuwa  ni bora   kwake  kuliko ngamia watatu, na aya nne ni bora kwake kuliko ngamia wanne, na vilevile zaidi ya hapo.  Aya zozote atakazo zisoma  basi ni bora kwake kuliko hisabu  yake kwa ngamia”
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قعد مقعداً لك يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة ومن اضطجع مضجعاً لم يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة
Na Anasema Mtume صلى الله عليه وسلم  “Anaekaa kikao chochote  kile asimtaje Mwenyezi Mungu  katika kikao hicho basi ana dhambi kutoka kwa Mwenyezi Mungu,  na anaelala sehemu yeyote ile kisha asimtaje Mwenyezi Mungu   wakati wakuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Mwenyezi Mungu” 
وقال صلى الله عليه وسلم : " ما جلس قوم مجلساً لم يذكروا الله فيه ، ولم يصلوا على نبيهم إلا كان عليهم ترة ، فإن شاء عذبهم وإن شاء غفر لهم
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote  wale, wanaokaa kikao kisha wasimtaje Mwenyezi Mungu humo, wala wasimswalie Mtume wao  ila  watakuwa wana dhambi. Akipenda Atawaadhibu na Akipenda Atawaghufuria.  
وقال صلى الله عليه وسلم :" ما من قوم يقومون من مجلس لا يذكرون الله فيه إلا قاموا عن مثل جيفة حمار وكان لهم حسرة
Amesema Mtume صلى الله عليه وسلم Hapana watu wowote wale  wanaosimama katika kikao walichokaa, kisha wasimtaje  Mwenyezi Mungu  ila watakuwa wanasimama kama  mzoga wa punda, na watakuja juta kwa kutomtaja Mwenyezi Mungu”