Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, September 12, 2012

HARAKATI ZA UAMSHO ZAANZA RASMI



Na Masoud ali…
Waislamu nchini Zanzibar wamehimizwa kuwa na umoja na mshikamano katika kudai maslahi ya nchi yao. kwani umoja wa waislamu ndio utakaoleta ushindi licha ya kwamba wapo baadhi ya waislamu hawapo pamoja na wenziwao.
Hayo yameelezwa na Amir wa jumuiya ya uamsho Zanzibar {JUMIKI} wakati alipokua akiwahutubia waislamu wenye uchungu na kuchoshwa na muungano uliopo baina ya Tanganyika na Zanzibar katika muendelezo wa harakati za mihadhara ya kuamsha wananchi kuhusu matatizo mbali mbali yanayotokana na muungano.
Mhadhara huo ulifanyika katika msikiti wa Afraa kidongo chekundu ambao ulihudhuriwa na maelfu ya waislamu wanaume na wanawake kwa ajili ya kusikiliza kitu gani kipya kimejiri baada ya kuonekana kukaa kimya kwa harakati hizo kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  Shekh Mselem amebainisha kuwa lengo la JUMIKI ni kutaka kurejesha heshima na hadhi ya Zanzibar kwa njia ya AMANI na utulivu bila ya kumwaga damu wala kupoteza roho za waislamu. Hivyo waislamu  wasikubali kupotezewa lengo  lao na baadhi ya watu wachache ambao wanapata maslahi kwa kuwakandamiza wenzawo.
Wakati huo huo naibu amiri wa JUMIKI fadhiilat shekh AZZAN  amewapongeza waislamu kwa umoja wao waliouonesha katika kutii amri za viongozi wao dini hasa hasa kuhusu suala zima la sensa.
Vile vile amesisitiza ya kwamba JUMIKI hawajakaa kimya kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema msimamo wake wa kudai maslahi ya zanzibar  hauzimiki ingawa kuna mbinu nyingi zinaandaliwa juu yao za kutaka kuwapoteza viongozi wa harakati hizo.

Monday, September 10, 2012

Sababu 21 Za Kumfanya Muislam Asisherehekee Maulidi

 
Zifuatazo ni sababu na hoja ambazo Muislam mwenye kupenda kufuata haki na mwenye kutaka apate uongofu ili abakie katika njia iliyonyooka na ajiepushe na mambo ya baatil. Hoja ni za wazi kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Hoja za kupinga jambo hili ziko nyingi sana, lakini tulizozikusanya tunatumai kuwa zitamtosheleza Muislamu aikinaishe nafsi yake kuwa Maulidi ni jambo la uzushi katika dini kwa hiyo ni bora kutenda amali zile tulizopata mafundisho yake kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم, Maswahaba wake na Salafus Swaalih (Watangu wema) .

SABABU YA KWANZA: Kumpenda Mola Mtukufu Aliyetuumba:
Kwanza kabisa ni kwa sababu  ya kumpenda Mola Mtukufu Aliyetuumba Ambaye Anataka kuhakikisha kuwa mapenzi yetu Kwake ni kumfuata Mtume صلى الله عليه وآله وسلم. Naye tokea kuzaliwa kwake hadi kufa kwake hakufanyiwa wala hakusherehekea siku yake ya kuzaliwa. 

Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

 ((قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ)) 


((Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni na Atakufutieni madhambi yenu. Na Allaah ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu)) [Al-'Imraan: 31] 

SABABU YA PILI: Kufuata amri yake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم    ya kushikamana na Sunnah Zake na Sunnah za Makhalifa wake:

 (( أُوصِيكُمْ بِتَقْوى اللَّه، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وإِنْ تَأَمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حبشيٌ ، وَأَنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيرى اخْتِلافاً كثِيرا . فَعَلَيْكُمْ بسُنَّتي وَسُنَّةِ الْخُلُفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ ، عضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ ، وإِيَّاكُمْ ومُحْدثَاتِ الأُمُورِ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضلالَةٌ ))  رواه أبو داود ، والترمذِي وقال حديث حسن صحيح

((Nakuusieni kumcha Allah, usikivu na twaa hata ikiwa kiongozi wenu (Au atakayekuamrishen) ni Mtumwa  wa Habash. Mtakaoishi miongoni mwenu mtaona ikhtilafu nyingi. Kwa hiyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa waliongoka baada yangu.  Ziumeni kwa magego (zikamateni kwa nguvu wala msiziache). Na tahadharini na mambo ya uzushi kwani kila bid'ah ni upotofu)) [Abu Daawuud, At-Trimidhiy kasema Hadiyth Hasan Swahiyh]   

Kwa hiyo inamtosheleza Muislamu hoja hii pekee ya kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala Maswahaba zake hawakusherehekea Maulidi, kumfanya naye asisherehekee.

Na hiyo ndio sababu kubwa ya Waislamu kukhitilafiana na kugawanyika makundi makundi. Amesema Imaam Maalik رحمه الله "'Hakuna kitakachotengeneza Ummah huu wa mwisho ila kwa kile kilichotengeneza Ummah wa mwanzo". Na maadam Salafus-Swaalih (watangu wema) hawakufanya bid'ah kama hii, sisi ni lazima tuwe na khofu kubwa ya kuifanya.


SABABU YA TATU:  Ametuamrisha Allaah سبحانه وتعالى tufuate aliyotuletea Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na tujiepushe na aliyotukataza:
   
 ((وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا))

((Na anachokupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho)) [Al-Hashr:7]


SABABU YA NNE: Kufuata amri ya Kumtii Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake صلى الله عليه وآله وسلم :

Anasema Allaah سبحانه وتعالى katika Aayah nyingi kwenye Qur-aan:

((وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ))

((Na mtiini Allaah na mtiini Mtume )) [At-Twaghaabun:12]

Na kumtii Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni kumtii Allaah سبحانه وتعالى

((مَّنْ يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللّهَ))

((Mwenye kumtii Mtume basi ndio amemtii Allaah)) [An-Nisaa:80]


SABABU YA TANO: Kutokufuata amri ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni kumkhalifu na kupata adhabu kali:
  
 ((فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيم))

((Basi nawatahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu)) [An-Nuur:63]



SABABU YA SITA:  Kumpinga Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ni sababu ya kuingizwa motoni:

 ((وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَى وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءتْ مَصِيرًا))

((Na anayempinga Mtume baada ya kumdhihirikia uongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza alikoelekea, na tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu)) [An-Nisaa 115]


SABABU YA SABA: Kukhofu upotofu unaompeleka mtu motoni:
  
Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Alikuwa akitanguliza khutba zake kwa kutoa maonyo hayo:

(( إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمد صلى الله علي وسلم  وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار))  أخرجه مسلم في صحيحه 

 ((Maneno bora  ni kitabu cha Allah (Qur-aan) na Uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Muhammad  صلى الله عليه وآله وسلم  na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika dini) ni bid'ah (uzushi)  na kila bid'ah ni motoni)) [Muslim katika Swahiyh yake]


SABABU YA NANE:  Khofu ya kuwa miongoni mwa kundi litakaloingia motoni:
 

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipoonya katika Hadiyth ifuatayo kuwa makundi yote yanayojiita ni ya Kiislam na hali hayafuati mafunzo kama aliyokuja nayo yeye, yatakuwa motoni isipokuwa kundi moja. Maswahaba walishtuka na wakataka kujua ni kundi gani hilo moja, akawajibu kuwa ni kundi ambalo watu wake watakuwa wanafuata mwendo wake na wa Maswahaba zake.

((افترقت اليهود على إحدى وسبعين فرقة، وافترقت النصارى على اثنتين وسبعين فرقة، وستفترق هذه الأمة على ثلاث وسبعين فرقة كلها في النار إلا واحدة،)) فقال الصحابة: من هي يا رسول الله؟ قال: ((من كان على مثل ما أنا عليه وأصحابي)) الترمذي و الحاكم

((Waligawanyika Mayahudi katika makundi sabini na moja, na waligawanyika Manaswara katika makundi sabini na mbili, na utagawanyika Umma wangu katika makundi sabini na tatu, yote yataingia motoni ila moja!)) Maswahaba wakasema: 'Ni kundi lipi hilo Ee Mtume wa Allaah?  Akajibu: ((Ni lile ambalo litakuwa katika mwenendo wangu hii leo na Maswahaba zangu)) [Imepokewa na Maimaam At-Tirmidhiy na Al-Haakim]


SABABU YA TISA: Kuitikia wasiya wa Allaah سبحانه وتعالى  ili kubakia katika njia iliyonyooka:

Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

 ((وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ))

((Na kwa hakika hii ndiyo Njia Yangu Iliyonyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya Amekuusieni ili mpate kumcha Mungu)) [Al-An'aam: 153]


SABABU YA KUMI: Vitendo visivyokuwa vya Sunnah havipokelewi:

 (( من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد)) البخاري

((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika dini yetu) basi kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy]

Hivyo mtu atapoteza muda wake, labda na gharama ya kutekeleza bid'ah hii na kumbe amali hii haina thamani yoyote mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).


SABABU YA KUMI NA MOJA: Maulidi  yamezushwa karne ya nne (miaka mia nne) baada ya kufa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  na watu wenye kufru:


Walioanzisha Maulidi ni viongozi wa Faatwimiyyun huko Misr (hawa walikuwa ni Rawaafidh (Mashia) katika dhehebu la Ismailiyah [Makoja] walianza kusherehekea  Maulidi ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allahu ‘anhu), na Maulidi ya Hasan na Husayn (Radhiya Allahu ‘anhuma), na Maulidi ya Faatwimah az-Zahraa (Radhiya Allahu ‘anha), na Maulidi ya kiongozi wao aliye hai kwa wakati ule. Sasa kwa nini tuwafuate wao? Na kama alivyotujulisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwamba watu bora kabisa wa kuwafuata ni wa karne tatu pekee aliposema:

    ((خير الناس قرني ثم الذين يلونهم ثم الذين يلونهم))  متفق عليه 

((Watu bora kabisa ni wa karne yangu, kisha wanaowafuatia kisha wanaowafuatia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


SABABU YA KUMI NA MBILI: Makafiri wanafurahi Waislamu wanapofanya Bid'ah kwani ni kuacha mafunzo sahihi ya dini na ni kuzifuta Sunnah za Mtume صلى الله عليه وآله وسلم :

Napoleon Bonaparte alimpa Shaykh Al-Bakriy Riyaal mia  nane za Ufaransa (inasemekana ni mia tatu kwenye sehemu zingine) ili arudishe bid'ah ya Maulidi naye akahudhuria mwenyewe Maulidi. Maana makafiri wanajua kuwa Waislam wanaposhughulishwa na vipumbazo kama hivyo, husahau matakwa yao ya msingi na muhimu.

SABABU YA KUMI NA TATU: Baadhi ya maneno katika Maulidi yana kufru ya kumpandisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم cheo cha usawa na Allaah سبحانه وتعالى wakati yeye ametuonya tusifanye hivyo:

 ((لا تطروني كما أطرت النصارى المسيح ابن مريم، إنما أنا عبد، فقولوا: عبد الله ورسوله))  متفق عليه

((Msinitukuze Kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi na mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Mjumbe Wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


SABABU YA KUMI NA NNE:  wanapoinuka kumswalia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wanaamini kwamba roho yake inahudhuria wakati huo:

Hii ni fikra ovu kabisa, na pia yeye mwenyewe alikuwa hapendi kuinukiwa alipokuwa hai, vipi mtu anayempenda amfanyie jambo analolichukia wakati amekufa?

Siku moja Maswahaba walikuwa wamekaa msikitini pamoja na Abubakar رضي الله عنه  ambaye alikuwa akisoma Qur-aan. 'Abdullah ibn Ubbay ibn Saluul, mnafiki mkubwa alikuja akaweka takia na mto wake akaketi. Alikuwa ni mwenye sura nzuri na mwenye lugha ya ufasaha. Alisema: "Ewe Abu Bakar, muulize Mtume صلى الله عليه وآله وسلم atuonyeshe alama ya utume wake kama walivyotuonyesha Watume wengine. Mfano, Muusa عليه السلام  ametuletea Ubao (wa Tauraat), 'Iysa عليه السلام alituletea Injiyl na meza ya chakula kutoka mbinguni, Daawuud عليه السلام alituletea Zabuur, Swaalih عليه السلام alitulietea ngamia wa kike" Abu Bakar رضي الله عنه aliposikia akaanza kulia. Mara akaingia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na Abu Bakar رضي الله عنه akawaambia Maswahaba wengine wainuke kumpa heshima Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na kumpa malalamiko ya mnafiki. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: ((Sikizeni! Msiniinukie mimi bali….

وَقُومُواْ لِلّهِ قَانِتِينَ

((na simameni kwa ajili ya Allaah))  [Al-Baqarah: 238] (dalili kutoka Tafsiyr Ibnu Kathiyr] 


SABABU YA KUMI NA TANO: Kuchanganyika kwa wanawake na wanaume:


Jambo ambalo limekatazwa katika dini na katika sherehe hii kumedhihirika sana hasa pande za nchi zetu za Afrika Mashariki. Na uovu huu unafikia hadi kuimba kwa pamoja na kuchezesha vichwa kama kwamba ni dansi fulani. Imefika hadi maulidi kuitwa ‘disco maulidi’

SABABU YA KUMI NA SITA:  Kuwaigiza Manaswara:  
Manaswara wanasherehekea siku ya kuzaliwa 'Iysa عليه السلام kama wanavyodai. Na Waislamu haitupasi kusherehekea siku ya kuzaliwa  Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  kwani tumefundishwa kuwa tufanye kinyume na wao katika mambo yetu.
Vilevile Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  kasema:

 ((خالفوا المشركين، أحفوا الشوارب، وأوفوا اللحى)) البخاري و مسلم

((Kuweni kinyume na Washirikina, punguzeni masharubu na fugeni ndevu)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na kufanya hivyo (kusherehekea Maulidi) tutakuwa tunajifananiza nao, na jambo hilo la kuwaiga na kujifananisha na mambo yao limekatazwa kama alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم :

 ((من تشبه بقوم فهو منهم )) أحمد و أبو داود

Anayejishabihisha na watu basi naye ni miongoni mwao)) [Ahmad, Abu Daawuud]


SABABU YA KUMI NA SABA:  Dini imekamilika hakuna tena haja ya kuleta mambo ya dini mapya:

Kuzusha mambo mapya ya dini ni kama kumtuhumu Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kuwa ametukhini mafunzo ya dini na hakuyakamilisha, bali kuna aliyoyaficha na hakutupa yote!! Na hali aliikamilisha dini kama ilivyompasa. Aayah hii chini iliteremshwa kudhihirisha ukamilifu wa dini ya Mola Mtukufu

  ((الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينً))

((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini)) [Al-Maaidah:3]

Sasa vipi watu walete mafundisho ya dini mapya yasiyotokana na mafunzo kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake صلى الله عليه وآله وسلم ? Anauliza Allaah سبحانه وتعالى :

((أَمْ لَهُمْ شُرَكَاء شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّهُ))

((Au hao wana miungu ya kishirikina waliowatungia dini asiyoitolea idhini Allaah?)) [Ash-Shuura 21]

SABABU YA KUMI NA NANE: Kudhihirisha iymaan kwa kupenda yale aliyokuja nayo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم pekee:

عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بِنْ عَمْرُو بِنْ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا  قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم: ((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ )) حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ، رَوَيْنَاهُ فِي كِتَابِ "الْحُجَّةِ  بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ.   

Kutoka kwa Abu Muhammad Abdullah Ibn 'Amr Bin Al-'Aasw رضي الله عنه ambaye alisema:  Mtume صلى الله عليه وسلم  kasema: ((Hatokuwa kaamini (kikwelikweli) mmoja wenu mpaka mapenzi yake yatakapomili (yatakapotii au kuwafikiana) kwenye yale niliyoyaleta)) (mafundisho) [Hadiyth Hasan iliyotoka katika kitabu “Al-Hujjah” ikiwa na mtiriko mzuri wa mapokezi]


SABABU YA KUMI NA TISA: Kuacha mambo yenye shaka na kubakia katika yaliyo wazi: 

 عَنْ أَبي مُحمَّدٍ الحسَنِ بْنِ عليّ بْنِ أبي طَالِب، سِبْطِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَرَيْحَانَتِهِ رضيَ اللهُ عنهُما، قالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ ما يَرِيبُكَ إلى مَا لاَ يَرِيُبكَ )) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ   وَالنَّسَائِيُّ    وَقَالَ التِّرْمِذِيُّ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 

Kutoka kwa Abu Muhammad Al-Hasan Ibn ‘Aliy Ibn Abi Twaalib mjukuu wa Mtume صلى الله عليه وسلم na kipenzi chake رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا  alisema: "Nilihifadhi kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم maneno haya: ((Acha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka)). [Imesimuliwa na At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy akisema kuwa ni hadiyth Hasan na Swahiyh]


SABABU YA ISHIRINI: Mwezi huu wa Rabiy'ul Awwal ni mwezi alioaga dunia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم , sasa vipi Muislamu asherehekee?

Wanachuoni wote wameafikiana kuwa siku hii ya tarehe 12 Rabiy‘ul Awwal ni siku aliyofariki Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Vipi sasa watu watakuwa wanafurahi kwa siku kama hiyo? Anas bin Maalik رضي الله عنه anatuhadithia kuwa: "Hakuna siku ambayo watu wa Madiynah walikuwa na furaha ya hali ya juu kama siku aliyohamia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  katika mji huo. Na hakuna siku ya huzuni kabisa kwa watu wa Madiynah kama siku aliyoaga dunia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ."

Inaonekana kama sisi tunakwenda kinyume na maadili ya wale watu bora waliokuwa wakimpenda Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hata kuliko nafsi zao wenyewe.


SABABU YA ISHIRINI NA MOJA:  Sababu za Waislamu wanaoshikilia Bid'ah:  

1-Kufuata bila ya kupata elimu sahihi.
Ukitaka kujua hoja za Waislamu wanaofuata bid'ah, hutopata kutoka kwao hoja nyingi kutoka katika Qur-aan na Sunnah, bali ni hoja za kutokana na rai zao tu, au watakwambia, 'kwani kuna ubaya gani?'. Na hata wakitoa hoja kutoka katika Qur-aan na Sunnah basi utakuta kwamba wanazifasiri dalili hizo isivyokusudiwa bali wanazishabihisha na matamanio yao kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى :

((هُوَ الَّذِيَ أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ في قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاء الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاء تَأْوِيلِه))

((Yeye Ndiye Aliyekuteremshia Kitabu (hiki Qur-aan). Ndani yake zimo aayah Muhkam (nyepesi kufahamika) ambazo ndizo msingi (asili) wa Kitabu (hiki). Na ziko nyingine Mutashaabihaat (zinababaisha kama habari ya Akhera, za Peponi na Motoni na mengineyo ambao yamekhusika na Roho). Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu na kutaka kujua hakika yake vipi)) [Al-'Imraan:7]

Na ukizingatia utaona kuwa Waislamu wanaofuata Bid'ah sio wenye elimu kubwa ya juu, kwani ukilinganisha na wanaofuata Sunnah utaona kuwa kuna tofauti kubwa sana. Na hivyo ndivyo Allaah سبحانه وتعالى Anavyomjaalia kumpa elimu ya upeo wa juu yule mwenye kufuata haki. Na tujiulize Maulamaa wangapi wacha Mungu wenye elimu madhubuti wanafuata Bid'ah? Si rahisi kuwapata, bali ukiuliza wanaofuata Sunnah na wenye elimu kubwa ambayo athari yake tunaiona leo hii na itaendelea kizazi hadi kizazi InshaAllah, utakuta  ni wengi sana, miongoni mwao ni Maimamu wanne; Imaam Shaafi'iy, Ahmad bin Hanbali, Abu Haniyfah, Maalik, Sufyaan Ath-Thawry. Wasimulizi wa Hadiyth kina Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na kadhalika. Maulamaa maarufu; Ibn Taymiyah, ibnul Qayyim, ibnul Jawzy, ibnul Mubaarak, ibnu Hajar, ibnu Kathiyr, Imaam An-Nawawy, na waliopita katika miaka ya karibuni kama kina: ibn 'Uthaymiyn, ibn Baaz, Shaykh Al-Albaaniy na kadhalika. Hata katika jamii yetu kuna waliokuwa wamejaaliwa kupewa kipaji cha elimu kama kina Shaykh 'Abdullah Swaalih Al-Faarisy na kina Al Amiyn na Muhammad Qaasim Mazrui, Haarith Swaalih na wengineo wengi, bila kuwataja walio hai ambao hawana idadi kwa wingi wao.

2- Kufuata matamanio ya nafsi
Hufuata matamanio ya nafsi inavyopenda na sio kufuata haki. Wengine kutokana na unasaba wao huwa ni kwao kama utukufu kuwa nao wamo katika unasaba wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

((وَلاَ تَتَّبِعِ الْهَوَى فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ))

((Wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Allaah)) [Swaad:26]

3- Ugumu wa kuacha mila uliotokana na mababa na mababu
Mitume waliopita walikuwa wakiwaita watu wao wawafuate waliyokuja nayo ya haki walipendelea kubakia katika ujinga na mila za mababa zao. Na Waislamu wenye kufuata mambo ya bid'ah nao ni vile vile ukiwauliza kwa nini hamuachi mambo yasiyo katika mafundisho ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wanajibu hivyo hivyo kuwa 'vipi tuache Maulidi na hali tumekulia nayo?, au tutaachaje kitu ambacho mababa zetu walikuwa wakifanya?? Ina maana wao walikuwa hawajui?"

Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

((وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْاْ إِلَى مَا أَنزَلَ اللّهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُواْ حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءنَا أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لاَ يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلاَ يَهْتَدُون))

((Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah, na kwa Mtume, husema: Yanatutosha tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?)) [Al-Maaidah: 104]

Au walikuwa wakisema:

((بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءنَا عَلَى أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَى آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ))
((Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, basi na sisi tunafuata nyayo zao)) [Az-Zukhruf: 22]

4- Kukhofu kutokuungana na wengi wanaofuata bid'ah

Wengine ukiwauliza kwa nini unafuata bid'ah ya Maulidi. Jibu ni kuwa anakhofu kuwa yeye peke yake ataonekana kuwa hasomi Maulidi katika kundi lake, na hii ni hatari ya kukhofu watu badala ya kumkhofu Mola Mtukufu na pia ni kwenda na mkumbo kwa kudhani kuwa wengi ndiyo wenye haki! Haya Anatueleza Allaah kuwa:

((وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللّهِ إِن يَتَّبِعُونَ إِلاَّ الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلاَّ يَخْرُصُونَ))


((Na ukiwatii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Allaah. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu)) [Al-An'aam: 116]

5- Wengine wanasema kuwa ni kudhihirisha mapenzi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم

Je, mapenzi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  yadhihirike siku moja tu? Au katika mwezi huu tu? Na si siku zote? Hayo bila shaka ni mapenzi ya uongo. Mapenzi ya kweli ni yale ya kumkumbuka siku zote na kumtii umpendaye. Haya ya Maulidi hayana moja kati ya mawili hayo.

6- Hoja ya kusema ni Bid'atun-hasanah (uzushi mzuri)
Mojawapo yao ni kuwa Maulidi ni Bid'atun-hasanah. Katika dini ya Kiislamu hakuna bid'ah nzuri kwani Mtume صلى الله عليه وآله وسلم   alipotuonya alisema 'Kullu Bid'atin Dhwaalaah' (kila bid'ah ni upotofu). Na ikiwa kauli hii wanaipinga kuwa sio  KILA bid'ah, basi wanasemaje kuhusu kauli ya Allaah سبحانه وتعالى Anaposema:

 ((كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ))

((Kila nafsi itaonja mauti)) [Al-'Imraan:185]

Je, tupinge pia kauli hii kuwa sio KILA nafsi? Na je, ina maana kuwa kuna watu wengine watabakia hawatokufa na hali tunatambua kuwa hakuna atakayebakia ila Mwenyewe Mola Mtukufu?

Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atuhidi kwa kutuonyesha yaliyo haki ili tuyafuate na Atuonyeshe yaliyo baatil tujiepushe nayo. Aamiyn.

WAZANZIBARI VIJANA, WASOMI TUWASAIDIE UAMSHO.


WAISLAMU WENGINE WAKO WAPI ?
VIJANA TUNA MATATIZO NINI KIFANYIKE
MIKAKATI IANZE TUIGE WENZETU

BY Zdaima
“Hongera Uamsho Hongereni sana Allah atambuwe jitihada zenu na uwezo wenu kwa upande wenu mmeshajitahidi kazi ni kwa vijana wasomi wanaojiita Wazanzibari” ningeanza makala yangu hii kwa salamu hizo.
Naam naandika maelezo yangu haya nikiamini wazalendo mtayasoma kwa umakini mkubwa na mazingatio sana.Si lengo langu kulaumu au kumkwaza mtu .
Tokea kuanza vuguvugu la mabadiliko ya katiba tumeshuhudia mengi mazuri na mabaya kwa hapa kwetu zanzibar. na wengi tumejinasibu kuwa ni wazalendo wa kutaka kuitetea zanzibar kuondokana na kile almaarufu tunachokiita ukoloni wa mtanganyika dhidi ya zanzibar kupitia muungano.Bila shaka hamasa ya kudai mamlaka ya zanzibar yameimarika zaidi baada ya wenzetu ,mashehe wetu kwa umoja wao wa taasisi za kidini hapa zanzibar wakiongozwa na ( JUMIKI) kulivalia njuga bila kutafuna maneno wala kuegemea milengo ya kisiasa ilimuradi lina maslahi na zanzibar. Tunajua harakati za kudai mamlaka ya zanzibar zimeanzia mbali sana na kumetokea mambo mengi zanzibar kwa ufupi wa mambo historia ni ndefu (rejea Mihadhara ya Sheikh Ilunga Hassan) kwenye CDs mbali mbali za Mfumo kristo na muungano.

Ninachotaka kusema ukitoa vijana wa wakati wa zamani walioegemea milengo ya kisiasa jee vijana wa leo wasomi wanaisaidiaje Zanzibar kudai mamlaka yake.? tunajukumu hapa
Vijana tumekuwa ni wadandiaji tu wa hoja na si waanzilishi wa hoja hii imekuwa ndio khulka yetu na tumekuwa mabingwa wa kuwakosowa wengine. Kwa mfano baadhi ya watu wakiwemo vijana wanawakosowa uamsho kila wakifanya initiatives za kudai maslahi ya wazanzibari na katika utamaduni wa zanzibar uheshimiwe huwakosowa kwa kuangalia maslahi ya kisiasa zaidi bila kujali maslahi ya kijamii zaidi ( utamaduni wa jumla wa Zanzibar ( uislamu). Hata iwe wanakosea basi kwa upande wao uwezo wao umefika hapo na jitihada zao zimefika hapo kutetea maslahi ya kitamaduni na kijamii wewe kijana umefanya lipi kusaidia ? Mimi sikatai watu kuwashauri uamsho katika kuboresha hapana lakini nakataa ile khulka ya kupinga bila kutowa suluhisho na kuwaona wao tu ndio wenye jukumu la kuitetea zanzibar na sisi wengine kurukukia rukia tu kwa nini vijana tumeshindwa kuanzisha chombo cha kutuunganisha tukawa kitu kimoja na tukawa mstari wa mbele kuibuwa hoja na kufanya harakati?

MATATIZO YA VIJANA WENGI.
Tumekosa elimu sahihi ya dini. ( Religious Knowledge)
Sitaki kusemea dini nyengine labda nieleze ile inayonihusu ( islamic knowledge) ambapo mazingira nayajua hapa zanzibar. Vijana wengi hatuijui dini yetu na tunashindwa kujuwa wajibu wetu katika kuitetea dini na tamaduni zetu. tunachanganya mambo bila kujuwa mwelekeo wake. tumeathiriwa na urithi wa dini kitu ambacho hakitakiwi katika uislamu. Jee vijana hatuoni yanayofanyika mitaani na majumbani mwetu ikiwa ni waislamu 99% hatukutegemea mambo machafu kwa asilimia 99% mchango wa vijana uko wapi . hata ukisikia panapigwa kelele ni uamsho pekee si wawakilishi wala wabunge na hata hao uamsho hatuoni uwakilishi wa vijana katika safu yao tuko wapi vijana? Inasikitisha vile vile kuwa na wanazuoni wengi katika idara za serikali na wasomi kadhaa wa kiislamu katika nchi hii lakini kiasi cha kushindwa kuitumia elimu yao ya dini angalau kumpanga nesi wa kuchoma sindano mwanamme kuwa mwanamme na mwanamke kuwa mwanamke mweziwe hata hili basi. elimu yetu ya dini haitusaidii kutatuwa matatizo madogo madogo yanayoendana na tamaduni zetu. hivyo hivyo kwa sheria kandamizi .mahkamani na hata usafiri .baadhi ya vitu hata hizo nchi za magharibi wanafanya kwa tamaduni zai ( ukiristo) wala si tatizo. tumekosa elimu sahihi na kujiamini vijana tuna mchango gani?

Uislamu wetu hauna mwelekeo.
Vijana ndio tunaongoza kwa uharibifu wa tamaduni zetu wenyewe. tumekuwa wazuri wa kuiga mabaya na si mema. hatujuwani kuwa na wapenzi wa kike na kiume kinyume cha utaratibu wa dini.VfUTA FIKRA WEWE NI RAFIKI ZAKO WANGAPI WANA GIRL FRIENDS AU BOY FRIENDS, DADA ZAKO NYUMBANI KWENU, NA HATA MWENYEWE VIPI.wavuta bangi, wezi, hawaswali nk. tumesahau wajibu huu na kuuona ni wa uamsho basi hata huu wa kuitetea nchi nao hatuuoni? tumeiga tamaduni za kimagharibi na kujitwishwa halafu tunasema tuna uchungu na nchi hili la kulinda tamaduni za nchi sisi wenyewe kwanza halimo katika uzalendo au si wajibu wetu kama vijana?
Kuegemea siasa na umajimbo.
Tunapenda kujitukuza kwa asili zetu na maeneo yetu kitu ambacho hakitusaidii.tunavunja mshikamano wetu. labda ni sababu za kihistoria lakini kwa nini vijana tunaendeleza historia ambayo inatunyima utengamano wetu. kwa hapa zanzibar kila mmoja na chama chake na kwao.unaonaje tungekuwa na ajenda za kiinchi katika mtazamo wa vijana kisha vijana bila kujali vyama vyao wakaibeba kwa umoja wao na kufanya harakati hasa zile zinazohusu mustakbali wa kiinchi na vijana wajao? jee tuna mawazo angalau ya kuanzisha chombo cha vijanakwa zanzibar. Hivyo vilivyopo viko kimaslahi ama ya kisiasa, au kimapato sio kimamlaka ya nchi na uzalendo.
Mengine.
- Kutojuwa lengo letu kwa wakati fulani
- Kuburuzwa (baadhi)
- Kutojiamini
- Kukosa ujasiri n.k.

TUWAIGE WENZETU.
Mfano mdogo kule bara wenzetu uislamo wao umefika juzi juzi tu lakini kwa wale wanaofuatilia watakubaliana nami kwamba waislamu wa bara wanajitambua zaidi ingawa sio wote hasa vijana na wamekuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii. Hizi harakati zote zinazoendelea chimbuko lake ni kundi la vijana wa miaka ya 80 ambapo harakati zao zilianzia pale UDSM chini ya Professer ( simtaji) kutoka nje aliyewashtuwawaislamu kutoka usingizini . Vijana hawa walileta mwamko wa kielimu kwa waislamu na wakashajiishana kuchukuwa fani mbali mbali ili kuusaidia uislamu hatma yake wakaanzisha maskuli na kupasisha kweli kweli na ndio hizi sisi wazanzibari tunawapeleka watoto wetu. inasikitisha sisi kushindwa kujielewa pamoja na uislamu wetu wa asili kushidwa kuwa na mipango kama vijana. Wenzetu wametumia mtandao wa vijana wasomi kuuelimisha umma wa kiislamu na walianzisha mataasisi mbali mbali na kwa sasa products yake imepatikana vugu vugu la mfumo kristolimeanzia na mkakati wa kuwaelimisha dhima ya vijana wa kiislamu wasomi katika jamii, historia ya ukweli ya tanganyika, nafasi ya waislamu katika serikali yao nk. leo kuna kundi kubwa la vijana wameshaanza kupenya serikalini na huku nje kuna harakati zinaendelea hio ni kazi ya vijana sisi zanzibar kazi na siasa na kujitukuza. Tutumie siasa zetu kama nyenzo kutufikisha kwenye mustakbali vijana tusijisahau.
Kwa mfano hapa zanzibar tuna tatizo la matokeo mabovu kila mwaka na yanaathiri mustakbali wa nchi huko mbele badala ya vijana tukaanzisha forum ya kutatua tatizo hilo labda kwa kuunda mtandao wa vijana zanzibar katika elimu na utaalamu tunasubiri wanasiasa waseme, uamsho waandamane ndio na sisi tuzuke.Huko nyuma tulisikia kuna kundi linaitwa Zanzibar Elite club lilikuwa bale UDSM sasa siwasikii kila mtu na mambo yake ni mifano ya mambo kama haya. tumejisahau inawezekana mfumo wetu wa elimu una matatizo vijana tungesimama kusaidia taifa na jamii tusiwasubiri uamsho au vyama vya siasa ndipo nasi tuunge mkono bila kuwa na mwavuli unaotutambulisha. hata katika uchumi, dini, migogoro nk kwani hakuna wataalamu vijana ? sio ndio wengi ikiwa ni walimu, madaktari, maofisa mbali mbali , wanauchumi, wanasheria n.k. kule bara kuna chombo kinaitwa TAMPRo ( Tanzania Muslim Proffesional ) kina jaribu kuratibu na kushughulikia matatizo ya waislamu. ni chombo kilichowaunganisha wataalamu waislamu kusaidia jamii ya kiislamu na inaongozwa na vijana sisi tumelala.jamaa wanatowa miongozo mbali mbali ya kisheria, kiujasiriamali,taaluma,kibiashara na wanapiga hatua tuwaige kwa yale mazuri wenzetu Zanzibar tumeiacha dini yetu na mifumo yetu na ntumeshindwa kufanya kile kitu kinaitwa ( islamization of Enviroment) na ndio ukakuta wasomi wengi lakini hawana athari katika jamii.
MWISHO.
Vijana wasomi tuujuwe wajibu wetu kuisaidia jamii iwe ni kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi,nk. tuanze sasa nafikiri nitowe changamoto ya kuanzishwa chombo cha kuwaunganisha wazaznibari vijana cha wataalamu kitakachokuwa na mwavuli wa dini ili kuepusha mitafaruku ya kiitikadi na kisiasa. tunaweza tukafika ingawa kuna changamoto ya kiutawala na uwezo wa kifedha . tufikirie hili.
Nawasilisha