Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, September 17, 2012

OIC kukabiliana na dharau dhidi ya Mtume (saw)



Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) watajadili njia za kukabiliana na vitendo vya dharau na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
OIC kukabiliana na dharau dhidi ya Mtume (saw)Balozi na mwakilishi wa Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Hamid Reza Dahqani amesema kuwa mawaziri hao watajadili njia za kukabiliana na dharau na vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu katika mkutano wao wa 39 utakaofanyika nchini Djibouti na ule utakaofanyika katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Ameashiria mikono ya nyuma ya pazia iliyohusika katika kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kusema kuwa, Wamagharibi daima wamekuwa wakidai kuwa masuala hayo yanatokana na uhuru wa kusema na kujieleza katika katiba za nchi zao. Dahqani ameongeza kuwa taasisi za kimataifa zinasisitiza juu ya udharura wa kuheshimiwa dini za mbinguni, thamani na itikadi za mataifa mbalimbali lakini inasikitisha kuwa hadi sasa juhudi za jumuiya za kutetea haki za binadamu na jumuiya za kimataifa ikiwemo OIC hazijafanikiwa kuwakinaisha Wamagharibi kuhusun ukweli kwamba uhuru hauna maana ya kuvunjia heshima matukufu ya itikadi za watu wengine.

Watu 45 wauawa katika mapigano nchini Somalia


Watu wasiopungua 45 wameuawa na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea kusini mwa kijiji cha Bibi kati ya majeshi ya Kenya na Somalia kwa upande mmoja dhidi ya wapiganaji wa kundi la al Shabaab.
Watu 45 wauawa katika mapigano nchini Somalia
Mapigano hayo yametajwa kuwa ndiyo makali zaidi kutokea huko kusini mwa Somalia tangu majeshi ya Kenya yaingie nchini humo mwezi Oktoba mwaka jana.
Mapigano baina ya pande hizo mbili yalishadidi zaidi baada ya jaribio la majeshi ya Kenya na Somalia la kutaka kuingia katika ngome za kundi la al Shabaab karibu na kijiji cha Bibi.
Hadi sasa hakujatolewa habari kamili kuhusu idadi kamili ya watu waliouwa katika mapigano hayo kutoka pande zote mbili lakini vyombo vya kuaminika vinasema makumi ya watu wameuawa.
Duru za kundi la al Shabaab zinasema kuwa ndege za kijeshi za Kenya zinashiriki katika mapigani hayo makali.

Sunday, September 16, 2012

SHEH AZZAN AMEWATAKA WAZANZIBAR KUSHIKAMANA NA MAFUNZO YA UISLAMU KATIKA UKOMBOZI WA ZANZIBAR..

Na Masoud ali…
Jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar imeendelea na harakati zake za kuitakia mema nchi ya zanzibar ili iweze kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo wanayotaka.
Hayo yameeelezwa katika mhadhara uliofanyika magogoni katika msikiti wa  msumbiji.  kwa upande wake naibu amiri wa  jumuiya hiyo sh Azzan  bin khalid amesema ni wajibu wa kila muislamu kutekeleza wajibu wa kuletwa duniani ili kuweza kufanikiwa siku ya malipo.
Amewataka wazanzibar kuwa na mshikamano na kuwacha sera za vyama vyao ili kuweza kuondoa dhulma inayofanywa na serikali ya muungano wa tanzania.
Aidha naibu amiri wa jumuiya hiyo amebainisha kuwa muda wa kuikomboa zanzibar kupitia mafunzo ya kiislamu umefika hivyo wazanzibar wanatakiwa wasiogope mbinu na vitisho ambavyo vanatolewa na serikali.
Katika mhadhara huo sh Azzan amelaani vakali vitendo ambavyo vimefanywa na maadui wa uislamu duniani vya  kumdhalilisha Mtume Muhammad  S.A.W vinavyoongozwa na Marekani  na Israel.
Akizungumzia juhudi za Jumuiya katika suala zima la kuitetea Zanzibar amesema ni kumuandikia barua ya wazi yenye kurasa 14 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete inayoelezea mustakbali wa Zanzibar.
Nae sh Mselem amesema kwa walipofikia wazanzibar kwasasa ni vigumu kurudi nyuma katika kudai hadhi ya nchi yao  hivyo amesisitiza kwamba juhudi za kuitafutia heshima zanzibar zitaendelea..
Wakati huo huo kumejitokeza kikundi cha watu wasiojuilikana na kuchoma moto maskani ya ccm iliopo kariakoo inayojuilikana kwa jina la Kachorora. wanamaskani hiyo wamehusisha tukio hilo na harakati za jumuiya ya uamsho kwa kuwa tukio hilo limetokea wakati wa kurudi katika mhadhara wao lakin sh mselem kwa niaba ya jumuiya amekanusha dai hilo licha ya kwamba kuna baadhi ya vyombo vya habar haraka vimeihusisha uamsho katika tukio hilo.hivyo ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili Kuweza kuwachukulia  hatua za kisheria wale wote waliohusika na tukio hilo.

Watu wasiojulikana Wameitia Moto Maskani ya Kachorora.






 Askari wa Kikosi za Zimamoto Zanzibar wakiwa katika zoezi la kuuzima moto uliokuwa wakiwaka katika maskani ya Kachorora Rahaleo unaosadikiwa kutiwa na watu wasiojulikana usiku wa jana katika maskani hiyo na kusababisha hasara ya mali ya moja ya duka la kutengeneza makochi katika maskani hiyo.

Wananchi wakishughudia moto uliokuwa ukiunguza mali katika maskani ya Kachorora juzi usiku.
Mabaki ya Duka la kutengeneza makochi katika maskani hiyo kama inavyoonekana pichani.


Moja ya Uharibifu uliotokea katika maskani hiyo
 Wananchi wakjiangali jengo la maskani ya Kachorora Rahaleo leo asubuhi baada ya sehemu yake kuunguwa kwa moto jana usiku na leo kuipamba maskani hiyo kwa bendera baada ya tukio  la kutiwa moto na watu wasiojulikana na kusababisha hasara

Saturday, September 15, 2012

Hizbullah: Yaitisha maandamano makubwa Lebanon

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imeitisha maandamano makubwa zaidi nchini humo kulaani hatua ya kuvunjiwa matukufu ya dini ya Kiislamu.
Hizbullah: Yaitisha maandamano makubwa LebanonMaandamano hayo yenye lengo la kutetea matukufu ya Kiislamu yanatarajiwa kufanyika Jumatatu ijayo mjini Bairut, Lebanon. Hivi karibuni pia Waislamu mjini Bairut walifanya maandamano makubwa wakilaani filamu iliyomtusi mtukufu Mtume Muhammad (sww) na kuutaka ulimwengu wa Kiislamu uchukue hatua kali za kukabiliana na njama za Marekani. Aidha hapo jana raia mmoja wa Lebanon aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya waandamanaji waliokuwa wamejawa na hasira kali kutaka kuvamia hoteli moja ya Kimarekani nchini humo. Mbali na Lebanon nchi nyingine za Kiislamu kamavile Misri, Libya, Bahrain, Tunisia, Yemen, Iran, Indonesia na Palestina zilishuhudia maandamano makubwa huku idadi ya watu wakiuawa na kujeruhiwa vibaya.

Wanajeshi wa Marekani wawasili San'aa, Yemen



Wanajeshi wa Marekani wawasili San'aa, YemenDuru moja ya kuaminika imeripoti kuwa, wanajeshi wa Marekani wamewasili huko San'aa mji mkuu wa Yemen. Duru hiyo imeripoti kuwa, wanajeshi 150 wa kikosi cha majini wa Marekani wamewasili katika uwanja wa ndege wa San'aa wa nchi hiyo na ndege moja ya kijeshi ya Marekani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi hao wa Marekani wamewasili huko San'aa Yemen ili kuulinda  ubalozi wa nchi yao na kulinda maslahi ya Washington nchini humo. Mitaa minne inayoelekea katika ubalozi wa Marekani mjini San'aa jana ilishuhudia maandamano makubwa ya Wayemeni dhidi ya Marekani, na baadae maandamano hayo yaligeuka na kuwa ghasia baada ya vikosi vya usalama vya Yemen kuingilia kati na kusababisha raia wanne kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa.
Maandamano hayo yalifanyika kufuatia kutengenezwa filamu huko Marekani inayomvinjia heshima Mtume Muhammad s.a.w. Watu walioshuhudia wameleza kuwa, wanajeshi wa Marekani waliwafyatulia risasi raia wa Yemen  kutokea ndani ya ubalozi na kuwauwa.  Mji wa Taiz pia huko Yemen leo umeshuhudia maandamano makubwa ya wananchi dhidi ya filamu hiyo ya udhalilishaji ya Marekani iliyotengenezwa na Sam Bacile.

UN yatahadharisha kuhusu umaskini barani Afrika



UN yatahadharisha kuhusu umaskini barani AfrikaUmoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu umasikini katika nchi za kusini mwa jangwa kubwa la Afrika. David Gressly Mratibu wa Masuala ya Haki za Binadamu wa nchi za kandokando mwa jangwa la Sahara wa umoja wa Mataifa ameripoti kuwa, maisha ya watu milioni 50 yako hatarini kutokana na uwezekano wa kupungua mazao ya kilimo mwakani.
Gressly ameongeza kuwa kunyesha mvua katika nchi za kandokando mwa jangwa la Sahara ni ishara ya kuwepo mazao mazuri mwaka ujao hata hivyo kupungua kwa mazao na pia kupanda kwa bei za vyakula kutayaweka hatarini maisha ya watu milioni kumi wa eneo hilo.
Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu katika nchi za kandokando mwa jangwa la Sahara wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, tayari wameandaa mpango wa kupunguza lishe duni kwa watoto wa Kiafrika  milioni moja. Hii ni katika hali ambayo, mwaka uliopita watoto laki tano wa Kiafrika walikuwa wakisumbuliwa na tatizo la lishe duni.

Friday, September 14, 2012

Hasira ya ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya filamu inayomdhalilisha Mtume (saw)



Wimbi la malalamiko na hasira za Waislamu dhidi ya filamu inayomdhalilisha Mtume Muhammad (saw) linazidi kuenea katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Hasira ya ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya filamu inayomdhalilisha Mtume (saw)Baada ya mauaji ya balozi wa Marekani na wanadiplomasia wengine watatu wa nchi hiyo katika mji wa Benghazi huko Libya maelfu ya Wamisri waliokuwa na hasira wameendelea kuuzingira ubalozi wa Marekani mjini Cairo kwa siku kadhaa. Wamisri 250 walijeruhiwa baada ya polisi kuingilia kati.
Mjini Sanaa Yemen vijana waliokuwa na hasira jana Alkhamisi walivamia ubalozi wa Marekani na kupanda juu ya ukuta wa uzio wake ambako walitundika juu bendera yenye jina tukufu la Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw). Askari usalama wa Yemen walishambulia maandamano hayo makubwa na kuua watu wanne kati ya waandamanaji hao.
Wananchi wa Saudi Arabia pia wamefanya maandamano katika maeneo tofauti ya nchi hiyo wakilaani filamu ya Kimarekani inayomtusi na kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu. Wasaudia wametoa wito wa kufukuzwa balozi wa Marekani nchini kwao.
Maandamano makubwa kama hayo yamefanyika pia katika nchi za Lebanon, Palestina, Tunisia, Morocco, Pakistan, Afghanistan, Indonesia, Sudan na kwengineko ambako Waislamu wamelaani vikali filamu ya matusi inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) iliyotengenezwa na raia wa Marekani na Israel na kufadhiliwa na Mayahudi 100.
Hapa nchini Iran maelfu ya watu walifanya maandamano jana mbele ya ubalozi wa Uswisi unaolinda maslahi ya Marekani mjini Tehran wakitangaza hasira yao dhidi ya filamu hiyo na kutoa wito wa kufikishwa mahakamani na kuadhibiwa wale wote waliohusika kwa njia moja au nyingine katika kutayarisha na kusambaza filamu ya "Innocence of Muslims" Mamilioni ya wananchi wa Iran pia wanatazamiwa kuandamana kote nchini hii leo kabla na baada ya swala ya Ijumaa kulaani filamu hiyo ya Kimarekani.
Wakati huo huo magazeti ya serikali ya China yamelitaja tukio la kuuawa balozi wa Marekani nchini Libya kutokana na hasira za Waislamu dhidi ya filamu hiyo inayovunjia heshima matukufu yao kuwa ni tukio kubwa zaidi baina ya ulimwengu wa Kiarabu na serikali ya Washington tangu ilipoanza harakati ya mwamko wa Kiislamu Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Gazeti la Watu la chama tawala huko China limezungumzia tabia ya Wamarekani ya kuvunjia heshima mara kwa mara ustaarabu na itikadi za Kiislamu na kuandika kuwa, katika miaka ya hivi karibuni Wamarekani wamekuwa wakikariri vitendo vya kuvunjia heshima itikadi na matukufu ya Waislamu ikiwa ni pamoja na kuchoma moto nakala za Qur'ani, suala ambalo lilizusha malalamiko makubwa kote duniani.
Wimbi la sasa la hasira na malalamiko ya Waislamu dhidi ya Marekani lilianza baada ya video yenye dakika 14 ambayo ni sehemu ya filamu iliyopewa jina la "Innocence of Muslims" kusambazwa katika mtandao wa kijamii wa Youtube.
Mtayarishaji wa filamu hiyo ya kudhalilisha ni Sam Bacile ambaye ni raia wa Marekani na Israel. Mzayuni huyo amesema ametayarisah filamu hiyo kwa dola milioni tano zilizotolewa na Mayahidi 100.
Mashambulizi yanayoendelea kufanywa na watu wa dini mbalimbali dhidi ya balozi za Marekani katika Mashariki ya Kati baada ya kuvunjiwa heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu yanatoa ujumbe wa wazi kwa viongozi wa White House kwamba, tokea sasa dharau na utovu wa adabu utakaofanywa na Mmarekani mmoja dhidi ya Uislamu hautatambuliwa kuwa ni tendo la mtu binafsi bali litahusishwa na mfumo unaopanga hujuma dhidi ya Uislamu huko Marekani na katika nchi za Magharibi kwa ujumla.

Thursday, September 13, 2012

Rais mpya wa Somalia aponea chupuchupu kuuawa


Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia umethibitisha kuwa Rais Hassan Sheikh Mahmoud ameokoka kifo katika milipuko miwili iliyotokea jana mbele ya hoteli moja mjini Mogadishu ambako alikuwa akizungumza na waandishi habari akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya.
Msemaji wa jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia Jenerali Ali Hamiid amesema kuwa milipuko hiyo miwili ilitokea jana mbele ya Hoteli ya Mogadishu, alikokuwa Rais mpya wa Somalia. Watu alioshuhudia wamesema maiti mbili zilionekana mbele ya hoteli hiyo, moja ikidhaniwa kuwa ni ya mtu aliyejitoa mhanga.
Kundi la al Shabaab limetangaza kuwa ndilo lililopanga shambulizi hilo. Hata hivyo Rais mpya wa Somalia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya hawakupatwa na madhara yoyote katika shambulizi hilo.
Kundi la Shabaab limemtuhumu Rais mpya wa Somalia kuwa ni msaliti na kusisitiza kuwa litaendeleza mapambano yake dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
Rais Hassan Sheikh Mahmoud alichaguliwa Jumatatu iliyopita na Bunge la Somalia katika uchaguzi uliotajwa kuwa ni wa kihistoria.

Israel yahofia kusambaratika Serikali ya Palestina



Israel yahofia kusambaratika Serikali ya Palestina
Utawala wa Kizayuni umeziomba Umoja wa Ulaya na Marekani kuisaidia kifedha Mamlaka ya Ndani ya Palestina ili kuzuia kusambaratika mamlaka hiyo kutokana na malalamiko ya wananchi katika maeneo ya Palestina. Gazeti la Kizayuni Maariv imeandika kuwa, Israel ina wasiwasi huu kwamba, kusambaratika uchumi katika maeneo yanayodhibitiwa na Serikali ya Ndani ya Palestina kutaibua Intifadha ya tatu ya Wapalestina. Utawala wa Kizayuni unaamini kuwa, hali mbaya ya kiuchumi katika maeneo yanayodhibitiwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina itadhoofisha mamlaka hiyo na idara za usalama za Serikali ya Ndani ya Palestina. Kwa msingi huo utawala wa Kizayuni umetuma barua za haraka kwa Umoja wa Ulaya na Marekani ukizitaka pande hizo kuisaidia kifedha Serikali ya Ndani ya Palestina ili kuzuia

Mafuriko na kipindupindu vyaua watu 160 Nigeria



Duru za habari kutoka Nigeria zinaarifu kuwa, mafuriko yaliyosababishwa na kunyesha mvua kubwa tangu mwezi Juni hadi mwezi huu nchini humo, yamepelekea kuuawa watu 160. Ripoti iliyotolewa na ofisi inayoshughulikia masuala ya kibinaadmu ya Umoja wa Mataifa yenye makao yake makuu mjini Niamey, Niger imetangaza kuwa, takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa zaidi ya watu laki tano na 27 elfu wameathiriwa na mafuriko hayo huku watu 81 wakipoteza maisha yao. Awali viongozi Nigeria walikuwa wametoa  ripoti iliyoonyesha kuuawa watu 68 na wengine laki nne na 85 elfu wakiathiriwa vibaya na mafuriko hayo. Aidha ripoti iliyotolewa na ofisi inayoshughulikia masuala ya kibinaadmu ya Umoja wa Mataifa imeashiria kuwa watu wengine 81 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu uliyoyakumba maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo na kufanya idadi ya watu waliopoteza maisha yao kufikia 160.

Maandamano dhidi ya Marekani huko Misri



Misri kwa mara nyingine tena imeshuhudia maandamano ya wananchi dhidi ya Marekani. Maelfu ya Wamisri wameandamana mbele ya ubalozi wa Marekani huko Cairo mji mkuu wa Misri na kuichoma moto bendera ya Marekani. Wafanya maandamano wametaka pia kufungwa ubalozi wa Marekani  huko Misri na kuondoka balozi wa Marekani nchini humo. Wananchi wa Misri wamefanya maandamano hayo wakilalamikia kutengenezwa filamu ya Kimarekani inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (s.a.w). Sambamba na Misri, huko Libya pia baadhi ya waaandamanaji wameuvamia ubalozi mdogo wa Marekani huko katika mji wa Benghazi ambapo imeelezwa kuwa, mfanyakazi mmoja wa ubalozi huo raia wa Marekani ameuawa na mwingine kujeruhiwa. Japokuwa  hii si mara ya kwanza kwa Wamarekani kuzivunjia heshima itikadi za Waislamu, lakini kwa kuzingatia hali maalumu ya sasa katika eneo la Mashariki ya Kati, baadhi ya duru za kisiasa zinaamini kuwa, kuchaguliwa kipindi hiki kwa ajili ya kutengeneza filamu hiyo inayomvunjia heshima Mtume wa Uislamu ni jambo lililoratibiwa na halikutokea sadfa. Kwa ibara nyingine ni kuwa watengenezaji wa filamu hiyo inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (s.a.w) wamefanya hivyo ili kuzusha hitilafu na mivutano kati ya nchi za Kiarabu zilizoshuhudia mapinduzi ya wananchi hivi karibuni. Wataalamu wengi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa  kwa kuzingatia kwamba idadi kadhaa ya watu wa kabila la Kibti la Misri wenye misimamo mikali wameshirikiana na Tery Jones Kasisi wa Kimarekani mwenye chuki dhidi ya dini ya Kiislamu kutengeneza filamu inayomvunjia heshima Mtume wa Uislamu, lengo la hatua hiyo ni kuzusha vita baina ya Waislamu na kabila la Kibti la Misri.  Hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya Wakibti wa Misri hawajafurahishwa na kile kinachojiri sasa katika uga wa kisiasa wa nchi hiyo yaani kuingia madarakani wanaharakati wa Kiislamu nchini humo. Itakumbukwa kuwa Kasisi Tery Jones huko nyuma alikabiliwa na wimbi kubwa la malalamiko ya Waislamu kutokana na kitendo chake cha kishenzi cha kuchoma moto nakala kadhaa za kitabu Kitukufu cha Qur'ani. Hakuna shaka kuwa, hivi sasa pia baadhi ya pande zinafanya kila linalowezekana ili kuitumbukiza Misri katika hali ya mchafukoge na hivyo kunufaika na hali hiyo ya kutokuweko uthabiti nchini humo. Marekani na utawala wa Kizayuni zinafahamu vyema kwamba Misri mpya inatofautiana sana na ile ya zama za dikteta Husni Mubarak, zama ambazo Misri ilikuwa ikifuata kibubusa siasa za Tel Aviv na Washington. Hii ni kwa sababu tofauti hizo zimeathiri pakubwa maslahi ya Marekani na utawala wa Kizayuni huko Misri.