Saturday, June 1, 2013
Serikali ya Ghana yaondoa ruzuku ya fueli
Sunday, April 21, 2013
Wabahrain wapinga mashindano ya langa-langa
Watu wa Bahrain wanataka mashindano hayo yasimamishwe kwa sababu utawala wa ukoo wa Aal Khalifa unakandamiza maandamano ya amani ya wanaotaka mabadiliko nchini humo. Wabahrain wanasema utawala wa kifalme unataka kutumia mashindano hayo ya langa-langa kuonyesha kila kitu ni shwari katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.
Kwa miaka miwili sasa Bahrain imekumbwa na mgogoro mkubwa uliosababisha mashindano hayo ya magari yasifanyike mwaka 2011. Mwaka 2012 utawala wa Aal Khalifa ulifanya mashindano hayo kwa kustafidi na uungaji mkono wa vikosi vya usalama vya Saudia. Lakini mwaka huu wananchi na wapinzani wa Bahrain wamesisitiza kuendelea na malalamiko yao dhidi ya hatua kama hizo za kimaonyesho, licha ya ukandamizaji wa utawala wa kifalme wa Aali Khalifa.
Nigeria yaanzisha kampeni dhidi ya uvumi
Wakuu wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Bayelsa nchini Nigeria
wameanzisha kampeni maalamu yenye kauli mbiu ya 'sema la kwa waeneza
uvumi'.
Kampeni hiyo imeanzishwa kufuatia kuibuka taharuki baada ya kuenea uvumi kuwa gavana wa jimbo hilo amefutwa kazi. Katika mabango yaliyowekwa barabarani Wanigeria wanahimizwa kutosikiliza uvumi wala kuuhimiza. Wanaoendesha kampeni hiyo wanasema uvumi umeathiri vibaya utendaji kazi katika jimbo hilo.
Msemaji wa gavana wa jimbo hilo Daniel Iworiso-Markson amewaambia waandishi habari kuwa kampeni hiyo haina lengo la kuwanyima watu uhuru wa maoni. Ili kukabiliana na tatizo la uvumi katika jamii, wakuu wa jimbo hilo wamebuni kamati ya wataalamu watakaowaelimisha watu kuhusu uovu wa kueneza uvumi. Aidha serikali ya jimbo hilo imetangaza nambari maalumu za simu ili kila mwenye kutaka habari rasmi azipate kupitia njia hiyo badala ya kutegemea uvumi. Jimbo la Bayelsa ni nyumbani kwa Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria.
Kampeni hiyo imeanzishwa kufuatia kuibuka taharuki baada ya kuenea uvumi kuwa gavana wa jimbo hilo amefutwa kazi. Katika mabango yaliyowekwa barabarani Wanigeria wanahimizwa kutosikiliza uvumi wala kuuhimiza. Wanaoendesha kampeni hiyo wanasema uvumi umeathiri vibaya utendaji kazi katika jimbo hilo.
Msemaji wa gavana wa jimbo hilo Daniel Iworiso-Markson amewaambia waandishi habari kuwa kampeni hiyo haina lengo la kuwanyima watu uhuru wa maoni. Ili kukabiliana na tatizo la uvumi katika jamii, wakuu wa jimbo hilo wamebuni kamati ya wataalamu watakaowaelimisha watu kuhusu uovu wa kueneza uvumi. Aidha serikali ya jimbo hilo imetangaza nambari maalumu za simu ili kila mwenye kutaka habari rasmi azipate kupitia njia hiyo badala ya kutegemea uvumi. Jimbo la Bayelsa ni nyumbani kwa Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria.
Mufti wa Tunisia: Vita dhidi ya serikali ya Syria si Jihad
Akizungumza na waandishi habari siku ya Ijumaa, mwanazuoni huyo wa ngazi za juu Tunisia amesisitiza kuwa, 'Mwislamu hapaswi kupigana dhidi ya Mwislamu mwenzake' kwa kisingizio chochote kile.
Sheikh Battikh ametoa matamshi hayo baada ya kubainika kuwa vijana wengi wa Tunisia wanajiunga na mitandao ya kigaidi inayowatuma Syria kupigana dhidi ya serikali halali ya Rais Bashar al-Assad. Mwanazuoni huyo wa Tunisia aidha amesema kile ambacho sasa kinajulikana kama 'jihad ya ngono' ni zinaa na ukahaba. Amesema wasichana wadogo wa Tunisia wenye umri wa miaka 16 wamehadaiwa na kuenda Syria kushiriki katika kile Mawahabi wanakitaja kuwa ni ngono au ndoa ya jihad.
Monday, April 15, 2013
OIC yataka kutuma kamati yake nchini Myanmar
Na Salum Bendera
Watu 20 wauawa katika machafuko C.A.R.
Na Salum Bendera
Rais wa Somalia alaani mauaji ya Mogadishu
Sudan kuheshimu makubaliano na Sudan Kusini
Makamu wa Rais wa Sudan ameyataja mashambulizi ya hivi karibuni katika mji wa Kadukali makao makuu ya mkoa wa Korofani Kusini kuwa ni njama za baadhi ya pande za kutaka kuvunja makubaliano hayo na kwamba mapatano hayo yataendelea kudumu licha ya njama hizo. Nafi Ali Nafi pia ameyataka makundi yote ya kisiasa ya Sudan kuungana na kujiweka mbali na maadui na kuongeza kuwa Sudan itaendelea kuijenga upya nchi hiyo ili kutimiza matarajio ya wananchi.
waliokamatwa na Silaha ni wahusika wakuu wa matukio ya kijambaza Z'bar
Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao
wanasadikiwa kuwa ni mjambazi,waliokamatwa wakiwa na silaha ya SMG
yenye risasi 29 ndani yake.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake makao makuu ya
Jeshi la Polisi Zanzibar ziwani,Kamishna Mussa Ali Musaa aliwataja watu
hao ambao ni Faustine Geogre miaka 36 Msukuma wa geita Ushirombo na
Mohamed Ali Salum wa Bambuu Bububu.
Alisema kuwa awali Jeshi
lake lilifanikiwa kumkamata Faustine wakati akiwa kwenye sehemu za
starehe(baaar ya chuo cha mafunzo)ambae walimfanyia mahojiano na badae
kumpekuwa na kumkuta akiwa na fedha za kigeni Dola za kimarekani
100,Naira za Nigeria 3540 na T,shs,370,000/= pamoja na simu 3 aina
mbali mbali.
Kutokana na hatuwa hio ndipo Jeshi hilo badae
likaamua kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kumkuta na vitu
vyengine kadhaa vikiwemo’’jeki 1 bisbisi 2 koleo la kukatia nyaya na
baadhi ya vitu vyengine kadhaa”alisema kamishna Mussa.
Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao wanasadikiwa kuwa ni mjambazi,waliokamatwa wakiwa na silaha ya SMG yenye risasi 29 ndani yake.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake makao makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar ziwani,Kamishna Mussa Ali Musaa aliwataja watu hao ambao ni Faustine Geogre miaka 36 Msukuma wa geita Ushirombo na Mohamed Ali Salum wa Bambuu Bububu.
Alisema kuwa awali Jeshi lake lilifanikiwa kumkamata Faustine wakati akiwa kwenye sehemu za starehe(baaar ya chuo cha mafunzo)ambae walimfanyia mahojiano na badae kumpekuwa na kumkuta akiwa na fedha za kigeni Dola za kimarekani 100,Naira za Nigeria 3540 na T,shs,370,000/= pamoja na simu 3 aina mbali mbali.
Kutokana na hatuwa hio ndipo Jeshi hilo badae likaamua kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kumkuta na vitu vyengine kadhaa vikiwemo’’jeki 1 bisbisi 2 koleo la kukatia nyaya na baadhi ya vitu vyengine kadhaa”alisema kamishna Mussa.
Friday, April 12, 2013
Njama za Wazayuni dhidi ya al-Aqswa zaendelea
Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kidini wa serikali halali
iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina ametahadharisha kuhusiana na
njama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Masjidul Aqswa. Ismail
Ridhwan amesisitiza kwamba, msikiti mtakatifu wa al-Aqswa uko katika
hatua hatari mno kutokana na hujuma na mipango ya kujitanua ya Israel
sambamba na hatua zake za kuuyahudisha mji wa Baytul Muqaddas. Waziri wa
Waqfu na Masuala ya Dini wa serikali ya Palestina inayoongozwa na
Waziri Mkuu Ismail Hania amewataka Waislamu kote ulimwengu kukabiliana
na njama hizo za utawala ghasibu wa Israe. Ismail Ridhwan amezitaka nchi
za Kiislamu na Kiarabu, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Jumuiya ya
Ushirikiano wa Kiislamu OIC,
MSF: Wakimbizi wa Mali 74,000 wanahitajia msaada
Mpalestina afa shahidi katika gereza la Israel
Mfungwa mwingine wa
Kipalestina amekufa shahidi katika hali ya kutatanisha akiwa ndani ya
gereza la kuogofya la Nafha huko Israel, Palestina inayokaliwa kwa
mabavu.
Kufuatia kifo hicho,
Wapalestina wanaoshikiliwa mateka katika magereza ya Utawala wa Kizayuni
wa Israel waliitisha mgomo kwa lengo la kuwajuilisha walimwengu kuhusu
hali yao mbaya inayowakabili. Mapema mwezi huu, Maisara Abu Hamdia,
Subscribe to:
Posts (Atom)














