Saturday, July 20, 2013
Friday, July 19, 2013
Uvamizi wa Wazayuni al-Aqswa walaaniwa
OIC: Wakazi wa Gaza, Palestina wasaidiwe
UN yataka utulivu urejeshwe Guinea Conakry
Ramadhani yapandisha bei za vyakula Tanzania
Bei za vyakula katika mwezi huu wa Ramadhani zinaripotiwa kupanda
nchini Tanzania hususan katika jiji la Dar es Salaam. Baadhi ya vyakula
ambavyo hutumiwa na Waislamu kama futari zinaonekana kupanda mno katika
masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi zinasema, maeneo
ya Dar es Salaam kama Tabata Kimanga, Bima na hata Segerea yanashuhudia
bidhaa za vyakula zikiwa juu ukilinganisha na maeneo ya Kariakoo,
Vingunguti na hata Magomeni. Bidhaa kama magimbi, viazi zinadaiwa
kupanda kutokana na ugumu wa upatikanaji wake katika masoko. Baadhi ya
wafanyabiashara wanasema, kwa kipindi hiki mahitaji ni makubwa kuliko
upatikanaji wa bidhaa, na kwamba, hali hii imesababishwa na mvua
kutokunyesha kwa wakati na kusababisha uhaba wa mavuno. Aidha katika
mikoa mingine ya Tanzania pia kumeripotiwa kupanda bei za vyakula vya
mwezi wa Ramadhani kama mihogo, magimbi, viazi na maboga. Baadhi ya
wafanyabiashara pia wamekuwa wakilangua kwa makusudi vyakula wakifahamu
kwamba, katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani bidhaa hizo
zinahitajika sana.
Wednesday, July 17, 2013
HUYU NDIYO IMAMU ALIYEMALIZA QUR-AN YOTE RAMADHANI YA PILI KATIKA SWALA YA TARAWEHE.
Imamu wa Msikiti Mkubwa uliyopo kusini nchini Saudi arabia, Sheikh Ahmad Hawashi, alifanikiwa kuhitimisha Qur-an yote juzu 30 ramadhani ya pili kwa tarawehe Tatu, kawaida swala ya tarawehe huanza usiku unaonekana mwezi.
Kwa mujibu wa Gazeti la Ambaa la nchini Kuwait, Sheikh Hawashi ni maarufu kwa kurefusha swala ya tarewehe, na kawaida uhitimisha Qur-an mara 10 kila Ramadhan.
Imamu huyo alirefusha swala hiyo ya tarawehe mpaka karibu na swala ya alfajiri.
Sheikh Hawashi kitaluma alihitimu masomo ya sayansi katika shule ya sekondari na aliwai kuajiliwa na Taasisi ya kuamrisha mema na kukataza maovu, kutoka na utenaji wake mzuri wa kazi, Sheikh Hawashi aliteuliwa kuwa Msaidizi wa rais wa taasisi hiyo.
SHEIKH WA WILAYA YA ARUMERU AMWAGIWA TINDIKALI
Shekhe
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa
kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi
usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha.
Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.
Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei.
Shekhe Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya swala hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao walikuwa wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala.
Alisema hata hivyo, kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu akiwa amesimama jirani na mlango.
Alieleza kuwa wakati akitaka kumwangalia zaidi alishtukia mtu

huyo akiinua mkono na kumwagia maji yaliyompatia maumivu makali usoni na kifuani.
‘’Wakati natoka msalani nikipitia uwani kwangu niliona kama mtu ameinama pembeni yangu wakati najaribu kumsogelea ili nijue ni nani nilihamaki mtu huyo akinimwagia maji yaliyonisababisha maumivu makali sana yenye asili ya moto na ngozi kuanza kubabuka,’’ alisema shekhe huyo.
Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo alianza kupiga kelele kuomba msaada ambapo majirani walijitokeza na kumpa msaada wa kumpeleka hospitali, kwa vile wakati huo macho yake yalikuwa hayaoni na wakati wote alikuwa akilia.
Pamoja na kujeruhiwa vibaya sehemu za usoni, kifuani na mgongoni, pia ana majeraha kwenye mikono na machoni na hali yake bado ni mbaya japo madaktari wanaendelea kumpatia matibabu.
Kaimu Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud akizungumzia tukio hilo alieleza kushitushwa nalo akisema limefanana na lile la Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdulaziz Jonjo ambaye mwaka jana alilipuliwa kwa bomu nyumbani kwake akiwa amelala.
Alisema kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia huku wahusika wakishindwa kutiwa mbaroni na kudai kuwa matukio hayo yanahusiana na masuala ya kigaidi. Aliongeza kuwa pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, lakini wamekuwa hawapati matunda ya kukamatwa kwa watuhumiwa ingawa alisema wanajulikana.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zitatolewa pindi washukiwa watakapotiwa mbaroni kwani uchunguzi bado unaendelea na kwamba hakuna mtu anayeshikiliwa hadi sasa.

Tuesday, July 16, 2013
MTOTO AZALIWA NA TASBIHI SHINGIONI MWAKE
Inaelezwa
kwamba mama wa mtoto huyo ambaye ana miaka ya kati, Adijat, alikimbizwa
hospitali karibu na nyumbani kwa Pa Mohammed Bello Masaba, mda wa saa 8
mchana na baada ya pilika za uzazi alifanikiwa kujifungua mtoto huyo.
Kwa
mujibu wa mmiliki wa hospitali hiyo ya uzazi, Alhaji Abubakar Baiwa
Shasha ambaye ndiye aliyesimamia zoezi hilo la kujifungua alisema, “Nilishtuka nilipoona mtoto anatoka akiwa na Tasbihi shingoni mwake, na wakati wa uzazi mtoto alizaliwa akiwa na Rozari nyeusi.” Alisema Shasha.
“Ila nilishangaa baada ya muda rozari hiyo ilibadilika na kuwa nyeupe huku kukiwa na watu wengine wamezunguka.”
“Mara
baada ya habari hiyo kusambaa mjini, maelfu ya watu walifika kwenye
hospitali hiyo ya uzazi huku wakisema “Allahu Akibar; Allahu Akibar
(Mungu ni Mkubwa) huku wakifika na kumgusa mtoto huyo.”
Juhudi
za kumpata Baba wa mtoto huyo aitwaye Isah, ambaye anatokea eneo la
Loma ndani ya Jimbo la Kwara State zilishindikana baada ya kukataa
kuongea na mtoa habari.
Mwanachuo mmoja wa Kiislamu, Malam Idiris Ndajiwo alisema, kuzaliwa kwa mtoto huyo akiwa na rozari
“inaonyesha
ukuu wa Allah. Kuzaliwa kwa mtoto huyu leo, kwenye mji huu na eneo hili
(Kutaworo) ni kitu kikubwa kwa Waislamu. Hii hakika inakuja kuonyesha
kwamba Allah ndiye mwenye kupanga kwa lolote kutokea kwa yeyote kwenye
ulimwengu huu.”
RAIS MUGABE AWATAKA MSHOGA NA WASAGAJI NCHINI MWAKE WAZALIANE LASIVYO ATAWAFUNGA JELA
RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametoa kali ya mwaka kwa kuwachimba mkwara Mashoga na Wasagaji kwamba wasipotiana mimba ni lazima atawafunga jela.
Mugabe ametoa kali hiyo Ijumaa wakati akizindua kampeni za chama chake cha kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika mwezi huu.
Isome taarifa nzima ya rais huyo mwenye umri mkubwa aliye
madarakani duniani na ambaye wazungu wanamgwaya kwa misimamo yake
isiyoyumba.
President Robert Mugabe on Friday threatened to jail gay and
lesbian couples who fail to conceive any offspring as he launched his
party’s campaign for this month’s general election.
The Zanu PF leader also attacked bitter rival and coalition
partner Morgan Tsvangirai for his bed-hopping habits saying it was
inconceivable that such a character could want to lead the
country.Mugabe, a rabid critic of homosexuality returned to the theme as
he addressed thousands of supporters in Harare’s Highfield township.He said he was shocked to learn that US President Barack Obama had called on African countries to embrace the practice.
Friday, July 5, 2013
Israel yatishia kujenga hekalu ndani ya al Aqswa
Huku akitoa matamshi ya kufurutu ada na ya kibaguzi waziri huyo wa Israel sambamba na kubainisha kuwa, kuna matakwa ya kuundwa serikali mbili za Palestina na Israel amesema kwamba, njia pekee na ya uhakika eti ni kuwepo serikali moja tu ya Israel katika eneo hilo.
Inafaa kukumbusha hapa kuwa, viongozi wa utawala ghasibu wa Israel wanafanya kila njama ili waweze kuharibu athari na utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu katika mji wa Quds kwa lengo la kuuyahudisha mji huo
Wafuasi wa Mursi kuandamana leo Misri
Maandamano ya mirengo ya Kiislamu yaliyoitishwa na harakati ya
Ikhawanul Muslimin ya Misri yanatarajiwa kufanyika leo nchini humo baada
ya mshuko wa swala ya Ijumaa, ili kupinga hatua ya jeshi ya kumuuzulu
rais Muhammad Mursi. Ikhawanul Muslimin ya Misri jana iliwataka
wananchi wa nchi hiyo kuandamana kwa amani baada ya swala ya Ijumaa
katika maandamano yaliyopewa jina la 'Ijumaa ya Kukataa'. Maandamano
hayo yataonesha ni kwa kiwango gani rais huyo aliyeuzuliwa bado anaungwa
mkono na wananchi, na pia hatua zitakazochukuliwa na jeshi kukabiliana
nayo.
Muhammad Musri kiongozi aliyeondolewa madarakani wa Misri anatoka katika harakati ya Ikhwanul Muslimin na alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokraia na Wamisri baada ya mapinduzi ya wananchi yaliyomng'oa madarakani dikteta Hosni Mubarak.

Serikali ya Kongo DRC yaazimia kukabiliana na M23
Serikali ya Jamhuri ya Kidomekrasia ya Kongo imetangaza kuwa
itakabiliana vilivyo na vitisho vya waasi wa M23 nchini humo. Lambart
Mende msemaji wa serikali ya Kongo DRC jana alitangaza kuwa, serikali ya
Kinshasa inavizingatia vitsho vya waasi wa M 23 hasa baada ya waasi hao
kuuteka tena mji wa Goma, ambao ni makao makuu ya mkoa wa Kivu
Kaskazini.
Msemaji huyo wa serikali ya Kongo ameongeza kwamba, suluhisho pekee kwa waasi hao ni kuendelea na mazungumzo ya kusaka amani huko Kampala Uganda na kuwatahadharisha kuwa, vikosi vya Umoja wa Mataifa viko katika eneo la Mashariki ya Kongo ambako vinashirikiana na wanajeshi wa Kongo, hivyo ni bora M23 waache machafuko.

Subscribe to:
Posts (Atom)