Saturday, October 12, 2013
AU: ICC isiwashtaki viongozi walioko madarakani
Dola milioni 500, pato la M23 kwa magendo ya madini
Gazeti la Los Angeles Times
linalochapishwa nchini Marekani limeandika kuwa waasi wa M23 walioko
mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hujipatia takribani dola
milioni 500 kila mwaka kutokana na magendo ya dhahabu nchini humo.
Uchunguzi uliofanywa na taasisi ya kutetea haki za binadamu ya Enough
ya Washington nchini Marekani unaonyesha kuwa, waasi wa M23
waliojizatiti mashariki mwa nchi hiyo hufanya magendo ya madini ya
dhahabu na kujipatia mamilioni ya dola kila mwaka, pesa ambazo hutumiwa
kununulia silaha na kufanya jinai na mauaji ya halaiki katika eneo
hilo. Taasisi hiyo imeeleza kuwa, licha ya kinara wa kundi hilo Bosco
Ntaganda kupelekwa kwenye mahakama ya ICC kwa tuhuma za kutenda jinai za
kivita, lakini wasaidizi wake wamefanikiwa kutorosha kwa njia za
magendo dhahabu za Kongo na kuziuza nchini Imarati, kupitia nchi jirani
za Burundi na Uganda. Uchunguzi huo umeeleza kuwa, kila mwaka tani 12 za
magendo ya madini ya dhahabu yenye thamani ya dola milioni 500
hupelekwa nje ya nchi hiyo kinyume cha sheria.
AU kuongeza askari wa AMISOM nchini Somalia
Hata hivyo uamuzi huo unapaswa kuthibitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Imeelezwa kuwa gharama za kuendesha operesheni za AMISON zinadhaminiwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika na wanajeshi wengi wa kikosi hicho wanatoka nchi za Uganda, Burundi na Kenya. Kundi la al Shabab limeshadidisha operesheni zake dhidi ya majeshi ya kigeni na hasa baada ya kupoteza udhibiti wa ngome zake hasa hasa katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.
Wednesday, October 9, 2013
Ikhwan yaondolewa katika orodha ya NGO Misri
Harakati ya Ikhwanul Muslimin sasa imefutwa kikamilifu nchini
Misri baada ya serikali kuamuru kundi hilo liondolewe katika orodha ya
mashirika yasiyo ya kiserikali NGO nchini humo. Uamuzi huo wa serikali
ya Misri wa kuiondoa Ikhwanul Muslimin katika orodha ya NGO umechukuliwa
siku kadhaa baada ya kundi hilo la kisiasa kupigwa marufuku.
Baada ya kuingia madarakani serikali ya mpito inayoungwa mkono na jeshi nchini Misri zimechukuliwa hatua kali dhidi ya harakati ya Ikhwan hasa baada ya kupinduliwa rais wa zamani wa nchi hiyo aliyechaguliwa na wananchi Muhammad Musri mwezi Julai. Wengi wanaamini kuwa uamuzi huo sasa unaandaa mazingira ya jeshi la Misri kuwatia mbarozi zaidi wafuasi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin.
Baada ya kuingia madarakani serikali ya mpito inayoungwa mkono na jeshi nchini Misri zimechukuliwa hatua kali dhidi ya harakati ya Ikhwan hasa baada ya kupinduliwa rais wa zamani wa nchi hiyo aliyechaguliwa na wananchi Muhammad Musri mwezi Julai. Wengi wanaamini kuwa uamuzi huo sasa unaandaa mazingira ya jeshi la Misri kuwatia mbarozi zaidi wafuasi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin.
Mhadhiri Saudia ahukumiwa kwa kumnajisi binti yake
Mhadhiri mmoja wa kidini nchini
Saudi Arabia amehukumiwa kifungo cha miaka minane jela na kuchapwa
viboko 800 kwa kosa la kumnajisi bintiye mdogo wa miaka mitano na
kumtesa hadi kufariki dunia. Mahakama ya Saudi Arabia Jumatatu hii
ilimuamuru Fayhan al Ghamdi kumlipa mke wake wa zamani yaani mama wa
binti huyo fedha za diya ya damu dola za Kimarekani 270,000. Mke wa pili
wa mahdhiri huyo aliyekutwa na hatia ambaye naye ameshtakiwa kwa
kushiriki kwenye jinai hiyo amehukumiwa kifungo cha miezi kumi jela na
viboko 150. Binti huyo wa Saudia aliyekuwa na umri wa miaka mitano
alilazwa hospitali mwezi Disemba mwaka juzi akiwa na majeraha kadhaa,
michubuko, majeraha ya kuungua moto na kupasuka fuvu la kichwa.
Wanaharakati nchini Saudi Arabia na wa nchi za nje wamelaani vikali
jinai hiyo iliyofanywa na baba huyo kwa bintiye na kuitaja adhabu
iliyotolewa na mahakama ya nchi hiyo kwa mtenda jinai huyo kuwa ya
kiwango cha chini mno. Wanaharakati hao wamesema mtenda jinai huyo
alipaswa kufungwa jela maisha au kunyongwa ili iwe mfano kwa wengine.
Waliokufa kwenye ghasia Sudan ni 70
Maandamano yalianza nchini Sudan baada ya bei ya mafuta ya petroli kupanda karibu mara dufu. Nchi hiyo ilipoteza mabilioni ya dola baada ya Sudan Kusini kujitenda mwaka 2011, na inasemekana kuwa tangu wakati huo serikali ya Khartoum imekuwa ikikabiliwa na mfumoko wa bei, kuanguka thamani ya sarafu na kupungua akiba ya pato la kigeni.
HII NDIO TAARIFA YA
POLISI KUHUSU VIJANA WALIOKAMATWA WAKIFANYA ZOEZI POLINI HUKO MTWARA
Written By umar makoo on Wednesday, October 9, 2013 | 4:42 AM
45
3
1
Hizi ni moja ya CD zilizokamatwa na askari wa jeshi la polisi Mtwara
ikiwemo na kuwakamata vijana 11 ambao wanadaiwa walikua wakifanya
mazoezi ya kijeshi waliyokua wakijifunza kutoka kwenye CD za magaidi
zilizokua na mafunzo kutoka kwa makundi ya Al Shabaab na Al Qaeda.
Taarifa zaidi unaweza kuzisoma hapo chini kwenye hiyo taarifa
iliyotolewa na jeshi la polisi. 2
Original from: http://www.googlehabari.blogspot.com/2013/10/hii-ndio-taarifa-ya-polisi-kuhusu.html
Copyright EXEIdeas - All Ri
Original from: http://www.googlehabari.blogspot.com/2013/10/hii-ndio-taarifa-ya-polisi-kuhusu.html
Copyright EXEIdeas - All Ri
Tuesday, October 8, 2013
Rwanda yatakiwa iache kuwasaidia waasi Kongo DRC
Marekani imeitaka serikali ya Rwanda
kutoa ushirikiano utakaosaidia kukomeshwa mapigano huko Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo. Samantha Power, mwakilishi wa Marekani katika
Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Rwanda ikiwa ni nchi jirani na Kongo
inapaswa kuwa na nafasi ya moja kwa moja katika mchakato wa kuleta amani
na utulivu nchini Kongo. Bi. Power amesisitiza kwamba nchi zote za eneo
la Maziwa Makuu ya Afrika zinapaswa kufanya juhudi maradufu za
kuwatokomeza waasi walioko mashariki mwa nchi hiyo. Hapo jana ujumbe wa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliyataka makundi ya waasi
mashariki mwa Kongo kuacha kuendeleza machafuko katika eneo hilo. Inafaa
kuashiria hapa kuwa, mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Kongo na
waasi wa M23 kwa upatanishi wa Uganda bado yanaendelea, lakini hadi sasa
hayajakuwa na natija yoyote ile.
Makanisa ya Kenya yajitosa kwenye mgogoro wa ICC
Wakiongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa la AIPCK, Mugecha Karume, viongozi hao wa makanisa wamesema kuwa, kesi hiyo ina mambo mengi yasiyoeleweka na kwa mantiki hiyo, hakuna haja Rais Kenyatta kwenda Hague kwa ajili ya kesi dhidi yake mbele ya mahakama hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na mtangazaji wa radio Joshua Sang wanakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya Wakenya 1000 waliuawa. Kwa sasa Naibu Rais wa Kenya, William Ruto na Joshua Sang wako mjini Hague ambako kesi zao zinaendelea. Kesi ya Rais Kenyatta inatarajiwa kunza mwezi ujao wa Novemba. Umoja wa Afrika AU pia umetaka kesi hizo zisimamishwe au kuhamishiwa jijini Nairobi ili zisikizwe na mahakama za Kenya.
UN na AU kujadili mgogoro wa Sudan Mbili
Wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika
na wale wa Umoja wa Mataifa watakutana leo Addis Ababa mji mkuu wa
Ethiopia kwenye kikao cha kila mwaka, ambapo mwaka huu ajenda kuu
itakuwa ni kuujadili kwa kina mgogoro wa mpaka kati ya nchi za Sudan na
Sudan Kusini. Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imeeleza kuwa,
licha ya mgogoro wa Sudan mbili, wajumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja
wa Afrika watajadili pia hali ya mambo katika eneo la Maziwa Makuu ya
Afrika, Pembe ya Afrika, Jamhuri ya Afrika ya Kati na eneo la Sahel.
Sudan Kusini ambayo awali ilikuwa sehemu ya Sudan, ilijitangazia uhuru
wake mwezi Juni 2011. Hata hivyo, nchi hizo mbili zimetumbukia kwenye
mgogoro mkubwa baada ya kila upande kudai haki ya umiliki wa maeneo
matano ya mpakani na hali kadhalika tuhuma za kila upande za kuwaunga
mkono waasi wa upande wa pili. Hadi sasa, Sudan imeshaishitaki Sudan
Kusini mara tano kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa
kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Khartoum.
Kenya kutoa zawadi kwa wafichuaji wa Westgate
Polisi ya Kenya imetangaza kuwa iko tayari kutoa kitita cha
shilingi laki tano za nchi hiyo ambazo ni sawa na dola 5, 827 kwa mtu
atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa mwenye gari linalosadikiwa
kutegwa mabomu kwenye shambulio lililofanywa zaidi ya wiki mbili
zilizopita kwenye jumba la biashara la Westgate jijini Nairobi, Kenya.
Mkuu wa kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi nchini Kenya ameeleza
kuwa, gari hilo linashukiwa lilikuwa limesheheni mada za milipuko na
silaha na kuongeza kuwa kikosi hicho bado kinaendelea kumsaka mmiliki wa
gari hilo. Amesema kuwa, awali mmiliki wa gari hilo alikuwa Mkenya
mwenye asili ya Kisomali. Kundi la al Shabab la nchini Somalia
lilitangaza kuhusika na shambulio hilo lililopelekea watu wasiopungua 67
kuuawa ingawa hadi sasa watu wengine 39 waliokuwepo kwenye eneo hilo
hawajulikani walipo. Kundi la al Shabab limeitaka serikali ya Kenya
kuondoa majeshi yake nchini Somalia, kinyume cha hivyo itakabiliwa na
mashambulio mengine kwenye maeneo nyeti ya nchi hiyo. Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya amesikika akisema kuwa, serikali ya Nairobi
haitayaondoa majeshi yake nchini Somalia hadi pale hali ya amani na
utulivu itakaporejea nchini humo.
Watoto 362 wafariki kutokana na lishe duni Niger
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa,
watoto 362 walio chini ya umri wa miaka mitano wamefariki dunia kutokana
na lishe duni nchini Niger. Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa,
watoto hao wamefariki dunia katika eneo la Zinder mashariki mwa Niger
kati ya mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu. Taarifa hiyo imeeleza
kuwa, asilimia 90 ya vifo katika maeneo ya Zinder, Magaria na Mirriah
inatokana na lishe duni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Zinder ni mji wa pili kwa wingi wa watu nchini Niger, na eneo hilo
hukabiliwa mara kwa mara na ukosefu wa chakula unaosababishwa na ukame,
huku watoto na wanawake wakiwa wahanga wakubwa wa balaa hilo.
Monday, October 7, 2013
MAKAMU WA RAIS MH:BILAL AFUNGUA MRADI WA UKARABATI WA NJIA ZA KUSAFIRISHA UMEME

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Miradi ya
ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha
Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo,
Oktoba 7, 2013 katika Kituo cha kupoza umeme cha Makuyuni Wilaya ya
Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro. Kutoka kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felician Mramba, Waziri wa Nishati na
Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto kwa Makamu) ni Balozi wa Japan
nchini, Masaki Okada na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal na baadhi ya viongozi wakitembelea kukagua mitambi ya
kusambaza umeme ya Kiyungi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka Jiwe la
msingi, katika uzinduzi rasmi Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza
Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo, Oktoba 7, 2013 katika Kituo cha
kupoza umeme cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa
wa Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo na nyuma yao ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akiangalia moja ya mtambo wa kisasa wa kusambaza umeme
uliopo katika kituo cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya
Himo Mkoa wa Kilimanjaro, wakati alipofika kituoni hapo kuzindua rasmi
Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya
kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro, leo.

akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa
Tanesco, Felician Mramba, wakati alipotembelea kukagua Kituo cha
kusambaza Umeme cha Kiyungi, mkoani Kilimanjaro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Moshi
Vijijini, mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kusambaza umeme cha
Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro leo
kwa ajili ya kuzindua rasmi miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza
Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas gama, akizungumza kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madidi, Prof. Muhongo, aliyemkaribisha
Makamu wa Rais, kuzingumza.

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo.

Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.

Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco baada ya uzinduzi huo. Picha na OMR
Subscribe to:
Posts (Atom)













