Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayefuatilia masuala ya haki za
binadamu nchini Myanmar amesema kuwa fujo na ghasia dhidi ya Waislamu
zinatishia mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini humo. Tomas Ojea
Quintana amesema kuwa, kuendelea kushambuliwa na kutengwa Waislamu wa
kabila la Rohingya katika jimbo la Rakhine kunaisawiri na kutoa picha
mbaya kwa nchi hiyo na kunaitumbukiza katika hatari ya kuzuka vita
vikubwa vya kidini katika miaka ijayo. Quintana amesema inasikitisha
kuona kuwa, hata maafisa wa usalama pia wamejihusisha na vitendo vya
manyanyaso dhidi ya Waislamu na baya zaidi ni kwamba serikali imekaa
kimya bila ya kuchukua hatua zozote dhidi ya maafisa wake. Mjumbe huyo
wa UN amesema hayo mbele ya kamati ya Baraza Kuu la umoja huo
inayoendelea kupokea ripoti za hali ya haki za binadamu duniani.
Sunday, November 3, 2013
US kuipa Iraq zana za kijeshi kukabiliana na magaidi
Wakenya wapinga adhabu ndogo dhidi ya wabakaji
Mamia ya wanawake wa Kenya wameandamana wakipinga adhabu ya
kufyeka majani katika ua wa kituo cha polisi waliyopatiwa wabakaji wa
mwanafunzi. Maandamano hayo yaliyofanyika katika mji mkuu wa Kenya
Nairobi yamewashirikisha mamia ya akina mama ambao wanalalamikia adhabu
ya kukata majani katika uwanja wa uwanja wa kituo cha polisi
waliyopatiwa genge lililombaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.
Maandamano hayo yaliishia katika vituo vya polisi jijini Nairobi kwa
kukabidhi majina zaidi ya watu milioni moja yanayotoa wito wa kufanyika
uchunguzi wa kiadilifu dhidi ya kundi lililombaka msichana wa miaka 16
na kumfanyia vitendo vya kinyama. Taarifa zaidi zinasema kwamba,
msichana huyo wa miaka 16 alipigwa vibaya na kisha kubakwa na wanaume
sita wakati alipokuwa akitoka katika mazishi ya babu yake magharibi mwa
Kenya Juni mwaka huu.
Baada ya kubakwa msichana huyo alitupwa katika mtaro wa maji machafu. Kwa sasa binti huyo anatembelea baiskeli ya magurudumu kutokana na madhara ya mgongo aliyoyapa ambayo inasadikiwa yalitokana na kutupwa mtaroni au kupigwa. Polisi ya Kenya imeahidi kufanya uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo.
…SB/habari-Ijumaa mchana

Maharamia Somalia wamepata $ milioni 413 tokea 2005
Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa pamoja uliofanya na Banki ya Dunia, Umoja wa Mataifa na Interpol. Imebainika kuwa fedha za uharamia hutumika katika vitendo vya uhalifu kama vile usafirishaji haramu wa silaha na wahamiaji pamoja na kufadhili makundi ya waasi . Aidha fedha hizo pia hutumika katika biashara za kawaida kama vile biashara ya miraa n.k. Mtaalamu wa Banki ya Dunia Stuart Yikona amepongeza juhudi za kikosi cha kimataifa cha majeshi ya wanamaji wanaokabiliana na maharamia. Ameongeza kuwa jamii ya kimataifa pia inapaswa kushirikiana ili kuzuia fedha za maharamia. Uchunguzi huo unaonyesha kuwa uharamia ni shughuli inayoratibwa kwa utaalamu mkubwa na kwamba aghalabu ya maharamia wanaendesha oparesheni zao kutoka ndani ya Somalia.
Inafaa kuashiria hapa kuwa meli za kivita za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinalinda doria katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi kwa lengo la kukabiliana na maharamia. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya bahari IMO limepongeza mafanikio ya Jeshi la Wanamaji la Iran katika kupunguza uharamia.
Wapalestina watungua ndege ya kijasusi ya Israel
Wanamapambano wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza wamefanikiwa
kuitungua ndege ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni katika anga ya ukanda
huo na kuiteka.
Televisheni ya al Mayadin imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, vikosi vya wanamapambano wa Palestina katika Uganda wa Ghaza, vimefanikiwa kuitungua ndege ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni katika anga ya kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza na kuiteka.
Viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamethibitisha habari ya kuanguka ndege hiyo na kudai kuwa haikutunguliwa, bali imeanguka kutokana na matatizo ya kiufundi. Itakumbukwa kuwa juzi Ijumaa, jeshi la utawala wa Kizayuni liliwaua shahidi Wapalestina wanne kaskazini mwa Ghaza na kuwajeruhi wengine kadhaa. Wanamapambano wa Palestina hao walijibu mashambulizi hayo na kujeruhi wanajeshi kadhaa vamizi wa utawala wa Kizayuni.
Israel inadai kuwa, shambulizi la kifaru cha utawala huo liliwalenga wapiganaji wa Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la HAMAS hata hivyo watu walioshuhudia walisema kuwa shambulio hilo lililenga nyumba za wakulima wa Kipalestina. Maafisa wa Hamas kwa upande wao walisema helikopta moja ya Israel aidha ilivurumisha maroketi kadhaa kwenye eneo hilo.

Mufti wa Libya aonya kuhusu kugawika nchi hiyo
Mufti huyo wa Libya amesema, kitendo cha serikali ya Tripoli cha kutowajali wananchi, kimetoa msukumo kwa raia hao kutoa ombi hilo la kutaka kuifanya Libya kuwa shirikisho. Ameongeza kuwa viongozi wa serikali wanapasa kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao ili kuzuia kukiukwa umoja wa mamlaka ya nchi. Wakati huohuo umoja wa maulamaa wa Libya pia umesema kuwa, kuifanya Libya kuwa shirikisho ni kitendo haramu na marufuku na kusisitiza kuwa mfumo wa shirikisho una madhara makubwa kwa nchi hiyo.
Friday, November 1, 2013
Kiongozi wa mapinduzi Mali kupandishwa kizimbani
Amadou Sanogo ameitwa mahakamani kufuatia machafuko yaliyofanywa siku chache zilizopita na kundi moja na wanajeshi walioshiriki katika mapinduzi ya mwaka jana. Sanogo anahusishwa na machafuko yanayofanywa na wanajeshi waliokuwa chini ya usimamizi wake katika mapinduzi ya Machi mwaka 2012 na kwamba anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria za kuhusika na machafuko yote yanayofanywa na kundi hilo.
Polisi ya Mali jana ilipokea kibali cha kumfikisha mahakamani Jenerali Amadou Sanogo na kibali hicho kitakabidhiwa kwa Wizara ya Ulinzi kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo. Haijajulikana bado lini Jenerali Sanogo atapandishwa kizimbani.
Machi mwaka jana Jenerali Amadou Sanogo aliongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali ya kiongozi wa wakati huo wa Mali Amadou Toumani Toure na kukomesha kile kilichotambuliwa kuwa demokrasia iliyopiga hatua zaidi baraniA frika.
Al Maliki atoa wito wa kuanzishwa vita dhidi ya ugaidi
Waziri Mkuu wa Iraq Nuori Al Maliki ametoa wito wa kufanyika
mkutano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi. Al Maliki ambaye alikuwa
akizungumza jana katika Taasisi ya Amani ya Marekani mjini Washington
amesema taifa la Iraq linalengwa na magaidi wa kundi la al Qaida ambalo
linataka kufikia malengo yake kupitia njia ya umwagaji damu.
Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza juu ya udharura wa kuwepo ushirikiano wa kuanzisha vita vya kimataifa dhidi ya magaidi wanaoua watu wasio na hatia.
Vilevile ametahadharisha juu ya hatari ya makundi ya kigaidi yanayoendelea kuua watu nchini Syria na kusisitiza kuwa taifa la nchi hiyo lina haki ya kuishi kwa uhuru na amani. Ametahadharisha kuwa moto na fitina za makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za Magharibi kama lile la Jabhatu Nusra huko Syria zinaweza kuyakumba maeneo na nchi nyingine dunia.

Watumiaji wa Yahoo, Google waandamwa na ujasusi wa NSA
Gazeti la Washington Post limesisitiza kuwa Wakala wa Usalama wa
Taifa wa Marekani (NSA) umekuwa ukifanya ujasusi dhidi ya mamilioni ya
watumiaji wa Google na Yahoo wakiwemo raia wa Marekani kwenyewe.
Hayo yanakuja katika kilele cha mgogoro mkubwa wa ujasusi wa Marekani uliofichuliwa na myaraka zilizoanikwa na mfanyakazi wa zamani wa wakala wa NSA aliyekimbilia nchini Russia, Edward Snowden.
Washington Post limeandika kuwa, wakala wa NSA unatumia programu inayoitwa MUSCULAR inayofanya kazi pamoja na programu nyingine ya Waingereza kwa ajili ya kukusanya data na ripoti za watumiaji wa Google na Yahoo.
Nyaraka za siri zinasema kuwa mwezi uliopita Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani ulikusanya taarifa milioni 181 zinazojumuisha sauti, video na maandishi yanayotumwa au kupokewa na watumiaji wa intanet hususan Yahoo na Google.
Ujasusi wa Marekani katika maeneo mbalimbali dunia umezusha mvutano mkubwa kwani haukuwaonea huruma hata waitifaki wa karibu wa serikali ya Washington zikiwemo nchi za Ulaya.

Wabunge wanawake Uturuki waanza kuvaa hijabu
Wabunge wote wanne waliongia bungeni na vazi la Kiislamu la Hijabu ni wanachama wa chama Justice and Development Party (AKP) cha Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Hatua hiyo ambayo imepingwa na vyama vyenye mielekeo ya kisekulari, imechukuliwa mwezi mmoja baada ya serikali ya sasa ya Uturuki kufuta marufuku ya vazi la hijabu katika taasisi za serikali.
Mwaka 1999 mbunge wa kike Merve Kavakci wa chama cha Fadhila aliingia bungeni nchini Uturuki akiwa na vazi la hijabu na kuzomewa na wabunge na baadaye kuvuliwa ubunge.
Chama cha Kiislamu cha AKP kiliahidi kufuta kabisa marufuku ya vazi la hijabu nchini Uturuki wakati kiliposhika madaraka ya nchi mwaka 2002.
Tanzania yajiondoa vikao vya mawaziri wa EAC
Kwa mujibu wa mwandishi wa Radio Tehran mjini Dar-es-Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe amezuiwa kwenda Kenya kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje unaoendela nchini humo huku Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki akizuiwa na serikali asihudhurie mkutano utakaoanza Alkhamisi Oktoba 31 nchini Burundi.
Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta ameliambia Bunge kwamba baadhi ya nchi zinaonekana kuwa na shirikisho lao la Afrika Mashariki hivyo hakuna sababu ya mawaziri wake kuhudhuria vikao hivyo kwa sasa.
Waziri Sitta ametoa ufafanuzi huo Jumatano hii bungeni kufuatia mkutano uliofanyika hivi karibuni nchini Rwanda na kuwashirikisha marais wa Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan ya Kusini.
Wabunge wa Tanzania walipomtaka Waziri Sitta aseme kwa nini Tanzania isijitoe katika jumuiya hiyo amewataka wawe na subira kwa muda wa wiki mbili wakati wanasubiri majibu ya msingi kutoka kwa sekretarieti ya jumuiya hiyo.
Jumuiya ya Afrika Mashariki inapita katika kipindi kigumu kutokana na kile kinachoonekana ni baadhi ya nchi wanachama kuitenga Tanzania katika baadhi ya mambo. Suala hilo limepelekea baadhi ya wananchi na wanasiasa Tanzania kutaka nchi yao ijiondoe katika jumuiya hiyo.
Kenya yashambulia kambi ya al Shabab Somalia
Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia ngome za kundi la al
Shabab ndani ya ardhi ya Somalia. Shambulizi hilo limetajwa kuwa
linahusiana na hujuma ya kigaidi iliyofanywa na al Shabab mjini Nairobi
zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kuua watu karibu 70.
Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) limetangaza kuwa ndege zake za kijeshi zimeshambulia kambi ya mafunzo iliyokuwa ikitumiwa na wanachama wa al Shabab ndani ya Somalia. Shambulizi hilo linafuatia lile la Jumatatu iliyopita ambapo viongozi wawili wa kundi hilo waliuawa.
Msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Cyrus Oguna amesema kuwa shambulizi la jana ni sehemu ya operesheni kubwa zaidi ya kikosi cha jeshi la Umoja wa Afrika AMISOM ambayo inalenga kambi za mafunzo za kundi la al Shabab. Oguna amesema watu waliofanya mashambulizi dhidi ya jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi tarehe 21 Septemba walipata mafunzo katika kambi hiyo.
Kambi hiyo ilikuwa na wapiganaji 300 wa al Shabab na jeshi la Kenya linasema kuwa wengi wao wameuawa au kujeruhiwa.
Kanali Cyrus Oguna amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa al Shabab yataendelea.
Air01/11/13 Araqchi: Urutubishaji

Subscribe to:
Posts (Atom)