Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, November 7, 2013

Mbunge Afungwa Jela


MAHAKAMA ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, imemwamuru kwenda gerezani siku 14 Mbunge wa Ukerewe, Salvatori Machemli (CHADEMA), kwa kosa la kudharau mahakama.
Machemli ambaye anakabiliwa na kesi ya uchochezi, aliamriwa kwenda gerezani jana baada ya kushindwa kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi yake.
Taarifa kutoka mahakamani hapo, zilisema kuwa katika kesi hiyo, Machemli anadaiwa kutumia maneno ya uchochezi katika mikutano mbalimbali ya hadhara wilayani humo mwaka jana, na kwamba amekuwa akienda nje ya wilaya hiyo na hata nje ya nchi bila idhini ya mahakama.
Inadaiwa kwamba, Machemli alipofika mahakamani hapo jana kwa lengo la kuhudhuria kesi yake hiyo, alifutiwa dhamana kisha kuamriwa kuwekwa ndani.
“Ni kweli mahakama imetoa amri ya kuwekwa ndani mheshimiwa Machemli kwa kosa la kudharau mahakama. 
Alikuwa hahudhurii tarehe za kesi yake, kutokana na hali hiyo, leo alipokuja mahakamani kuhudhuria kesi yake aliondolewa dhamana kisha akaswekwa ndani,” kilisema chanzo chetu.

AU yakosoa UN kwa kupuuza Afrika


Kikao cha Muungano wa Afrika kilichofanyika Addis Ababa mapema mwaka huu
Muungano wa Afrika AU umekosoa baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kwa kupuuza sauti za Waafrika katika maamuzi yake.
Mkurugenzi wa Baraza la Amani na Usalama la AU El Ghasim Wane anasema wakati mwingi, baraza la usalama hutoa maamuzi bila kuzingatia maoni ya Muungano huo.

Wane ameonya kuwa huenda mapendekezo ya baraza hili yakapuuzwa, iwapo hali itaendelea kama ilivyo.

Wane alikuwa akizungumza kwenye mkutano uliandaliwa kuangazia suala la ufadhili wa mipango ya usalama na amani barani Afrika, lakini suala tata la uhusiano wa AU na baraza la Usalama la umoja wa mataifa, lilijitokeza.

Mkurugenzi wa baraza la amani na usalama la AU El Ghasim Wane, alisema wakati umefika kwa baraza la usalama la umoja wa Mataifa kusikiza kwa makini sauti ya Afrika.

Tetesi hizo zinajiri huku baadhi ya wanachama wa baraza la Usalama la Umoja wa mataifa wakiripotiwa kupuuza ombi la Umoja wa Afrika la kutaka kesi inayomkabili rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kusimamishwa kwa muda.

Hata hivyo balozi wa Uingereza katika AU Greg Dorey alisema suala muhimu kuhakikisha kuwa uhusiano wa Umoja wa mataifa na AU unaimarishwa.

Huku akitaka muungano huo kuwa katika mstari wa mbele kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili bara hili.

Walikuwa wakizungumza katika mkutano wa kujadili jinsi wafadhili wa kimataifa wanavyoweza kuboresha juhudi za AU kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Katika mkutano huo, AU ilikiri kuwa inaweza kufanya vyema zaidi katika kukabiliana na vita kama vile nchini Mali na katika Jamhuri ya Afrika ya kati.

Tuesday, November 5, 2013

Daraja Ziro Lipo-Mulugo


WIKI moja tangu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome, atangaze mfumo mpya wa upangaji alama za matokeo ya wanafunzi wa sekondari kwa kufuta daraja sifuri na kuanzisha daraja la tano, naibu waziri ameibuka na kupingana naye.

Naibu waziri huyo, Philipo Mulugo, aliibua mkanganyiko huo bungeni jana, akisema si kweli kwamba serikali imefuta daraja la sifuri katika mitihani ya kidato cha nne kama ilivyoeleweka.

Kutokana na kukinzana huko, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliiagiza serikali kuleta bungeni mabadiliko ya madaraja hayo ya ufaulu kwa  wanafunzi wa kidato cha nne na sita yaliyotangazwa hivi karibuni.

“Naibu Waziri nenda mtuletee kauli ya Serikali kuhusiana na utaratibu huo ili kuweza kupata majibu ambayo yanaridhisha,” alisema.

Awali akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM), Mulugo alisema taarifa zilizoenea kwamba daraja la sifuri limefutwa si za kweli.

Katika swali lake, Magige alitaka kujua kama uamuzi wa serikali wa kushusha madaraja katika mitihani ya kidato cha nne lengo lake ni kuwaokoa wanafunzi wanaofeli.

“Serikali haijafuta divisheni sifuri na wala hakuna daraja la tano, yaliyopo ni la kwanza, pili, tatu, nne na sifuri kama kawaida,” alisema.

Alisema unamuzi wa kushusha madaraja uliofanywa haukuwa na lengo la kuwaokoa wanafunzi wanaofeli bali ni kuondoa mrundikano wa alama katika daraja moja.

Alisema serikali imeweka madaraja mapya kwa kutofautisha alama kumi kumi kutoka daraja moja kwenda jingine na kwamba hata hivyo alama za ufaulu bado ni 40 ambazo ni daraja la C.

Awali akijibu swali la msingi la Magige, Mulugo alisema serikali haina mpango wa kuanzisha programu maalumu hasa za ufundi kwa wanafunzi waliofeli katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.

“Kwa mwaka 2013, jumla ya wanafunzi 60,507 wa kujitegemea, wamejisajili kufanya mtihani huo, watahiniwa 3,578 wakiwamo wasichana 2,020 na wavulana 1,558 waliofeli katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wamejisajili kurudia mtihani huo,” alisema.

Alisema kwa sasa katika vyuo vya Ufundi Stadi kuna programu za fani mbalimbali za muda mfupi na muda mrefu ambazo wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi na sekondari wanaweza kujiunga kwa vile mafunzo yatolewayo katika vyuo hivyo huzingatia stadi moja tu.

“Serikali imekuwa ikiongeza na kuboresha vyuo vya ufundi na kuweka mazingira rahisi kwa wanafunzi ili waweze kupata stadi mbalimbali,” alisema.

Mulugo aliongeza kuwa kati ya mwaka 2010 hadi 2012, serikali kupitia VETA imesajili jumla ya vyuo vya Ufundi Stadi 75 sawa na asilimia 75 na asilimia 10.8 ya vyuo 618 vilivyokuwapo.

Naibu waziri huyo alifafanua kuwa  katika kipindi hicho, jumla ya vyuo vinane sawa na asilimia 3.2 ya vyuo 248 vilivyokuwepo vilisajiliwa na NACTE.

Watekaji Wakamatwa Moshi.


Polisi imemtia mbaroni mtuhumiwa muhimu katika tukio la mwanamke mmoja mjini Moshi aliyetekwa nyara na watu wasiojulikana na kwenda kutelekezwa jijini Dar es Salaam.
 

Mwanamke huyo alichukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa upelelezi kutoka Dar es Salaam na kwamba, walikuwa wametumwa kumkamata kwa tuhuma za kuuza dawa za kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema mtuhumiwa huyo muhimu (jina tunalo) alikamatwa Dar es Salaam na kusafirishwa hadi Moshi mwishoni mwa wiki iliyopita. 

Tukio hilo lilitokea Oktoba 13 mwaka huu eneo la Soweto NHC, watu hao walimchukua mwanamke huyo, Asha Amini hadi Dar es Salaam na kumpora Dola 11,000 za Marekani.
Boaz alisema aliyetoa taarifa hizo polisi, ni Jerome Mushi na alijitambulisha kuwa ni mume wa mwanamke huyo.
“Aliporudi nyumbani (Mushi) hakumkuta mkewe akaambiwa amekamatwa na polisi na amepelekwa Kituo Kikuu akaamua kwenda hadi kituoni wakamwambia hakuna tukio kama hilo,” alisema Boaz.
Kamanda Boaz alisema jalada la uchunguzi lilifunguliwa na siku hiyo hiyo watu walioondoka na mwanamke huyo, walimpigia simu mumewe wakitaka walipwe Sh2 milioni.
Hata hivyo, Boaz alisema watu hao walimwachia huru mwanamke huyo eneo la Bunju Dar es Salaam bila kumdhuru na kumpa Sh50,000 za nauli ya kumfikisha katikati ya jiji.
Kwa upande wake, Jerome Mushi alisema waliomchukua mkewe walikuwa na bastola moja, pingu mbili na redio moja ya upepo na walichukua dola 11,000 za Marekani.

Mtoto Suleiman Aanza matibabu



Hoyce Temu mwendeshaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania na Juma Rashid Mkurugenzi wa Munira Blog wakitafakari mustakbari wa mtoto Suleiman anayesumbuliwa na ugonjwa wa ajabu.

Ndoto ya kuanza kupata matibabu na hatimaye angalau kuwa kama watoto wengine wenye kwenda watakapo inaanza kumuangazia mtoto Suleima Rajab.

Matumaini hayo yamekuja baada ya kufikishwa katika Hospitali ya CCBRT ilioyopo mikocheni Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupata matibabu.

Munira blog ilimtembelea mtoto huyo mapema leo hii na kumkuta akiwa katika Private Ward (wodi binafsi) chumba namba tatu akiwa amekaa kitandani mwenye matumaini tele.

Bwana Rajab ambaye ni baba mzazi wa Suleiman ameiambia Munira blog kwamba wana siku ya nne tangu wafike na madaktari wamechukuwa vipimo.

"Tunasubiri matokea ya vipimo kutoka kwa wataalamu,ndipo tujuwe kinachoendelea"alisema.

Kwa upande wake Suleiman amesema anachoka kuka pamoja kwa muda mrefu na angependa aone anaanza matibabu.

Mratibu wa matibabu hayo Hoyce temu ambaye ni mwendashaji wa kipindi cha mimi na Tanzania kupitia kituo cha Channel ten amesema "tunasubiri ripoti ya madaktari ndiyo itakayotujuza mtoto Suleiman ana sumbuliwa na nini na anahitaji matibabu ya aina gani".

Naye bwana Abdul Kajumuro ambaye ni Afisa mawasiliano wa CCBRT amesema "ni vyema wananchi wakawa na subra,muda si mrefu tutapata ufumbuzi wa hili,kwani furaha yetu ni kuona mtoto huyu anakuwa kama watoto wengine".

mtoto suleiman anasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu wa kuvimba miguu yake kadri siku zinavyokwenda.

kwa mujibu wa baba yake,mtoto huyo hajawahi kusimama dede tangu azaliwe na hajiwezi kujihudumia yeye mwenyewe hadi asasidiwe.


Mtoto Suleiman akiwa kitandani katika Hospitali ya CCBRT,nyuma yake ni baba mzazi na mbele yake ni Hoyce Temu.
Abdul Kajumuro meneja mawasiliano wa CCBRT akiwa na Mtoto Suleiman.

Monday, November 4, 2013

Michenzani Kuwa Kituo Kikuu Cha Biashara


SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia  kuliendeleza na kulifanya eneo la Michenzani kuwa  kituo kikuu  cha biashara ikiwa ni  pamoja na  kujenga mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Mpinduzi ya Zanzibar.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dk. Khalid Salum Mohammed, alisema hayo jana wakati akiwasilisha muongozo mbele ya wahariri na waandishi wa habari katika hoteli ya Ocean View mjini Zanzibar.

Alisema Michenzani itachukua nafasi ya biashara badala ya kituo kikuu kilichokuwa Darajani kuhamishwa kwa kuepusha msongamano wa magari na watu.

Dk. Khalid alisema kivutio kikubwa kitakachokuwepo katika maeneo hayo ni kujengwa kwa mnara utakaokuwa na urefu wa mita 30 utakaogharimu sh bilioni 1.5.

Ujenzi wa mnara huo ulioanza kujengwa unatarajia kukamilika baada ya miezi miwili ambapo gharama za ujenzi zitagharamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF).

Mnara huo utatoa fursa ya kiuchumi pamoja na ajira kwa vijana kwa  kuwepo migahawa na maduka pamoja na vivutio vingine vya utalii ikiwemo sehemu ya mapumziko ya bustani.

Mkurugenzi wa mipango miji, Ramadhani Bakari, alisema azma ya serikali ya kuboresha eneo hilo ni hatua mpya ya kuonyesha mawazo ya mabadiliko ya mji wa Zanzibar, ili kuendeleza azma ya Rais wa kwanza, marehemu mzee Abeid Amani Karume.

Alibainisha kuwa azma ya serikali kupitia mipango miji ni kufanya mji wa Michenzani kuwa mji bora kwa kisiwa cha Unguja na vile vile kufanya mji wa Chake Chake kuwa ni mji bora kwa Pemba.

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WALIMU WA MADRASSA ZA QUR-AN.




WAZIRI WA KHABARI UTAMADUNI,UTALII NA MICHEZO AL-USTADH SAID ALI MBAROUK AMEWATAKA WAZAZI NA WALEZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU WA MADRASSA ZA QUR-AN ILI KUWAPA NGUVU KATIKA UTOAJI WA ELIMU YA QUR-AN NA SUNNA ZA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KWA VIJANA WAO.

WAZIRI MBAROUK AMETOA WITO HUO JANA KWA NIABA YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR AL-HAJJ MAALIM SEIF SHARIF HAMAD WAKATI AKIZUNGUMZA KATIKA SHEREHE ZA MADRASATUL-RAHMA YA NUNGWI WILAYA YA KASKAZINI A UNGUJA.

AMEWASISITIZA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI  NA WAGENI WANAOINGIA NA MAADILI YA KIMAGHARIBI  KATIKA MAENEO YAO ILI KUWAEPUSHA WATOTO WAO KUATHIRIKA NA UTAMADUNI HUO NAKUACHA MILA NA SILKA ZAKIISLAM.

AIDHA KIONGOZI HUYO AMEELEZEA HAJA KWA WAISLAM WNGINE KUFUATA MFANO WA NUNGWI KATIKA KULINDA MILA NA SILKA ZAKIISLAM KWA WATOTO WAO KWA KUANDAA SHEREHE ZA MADRASSA ZAKIISLAM ZINAZOSISITIZA MAADILI MEMA.

KATIKA SHEREHE HIZO WAZIRI MBAROUK AMEKABIDHI VIFAA NA ZAWADI MBALIMBALI IKIWEMO MIFUKO YA SARUJI KWA MADRASSA ZA NUNGWI ZILIZOTOLEWA NA MWAKILISHI WA JIMBO HILO NAKUAHIDI KUCHANGIA SHILINGI LAKI TANO KATIKA MADRASSA HIYO.

NAO WALIMU WA MADRASATUL-RAHMA YA NUNGWI WILAYA YA KASKAZINI A UNGUJA WAMEWAOMBA WAFADHILI NA WATU WENYE UWEZO KUSAIDIA HARAKATI ZA UJENZI WA MADRASSA HIYO ILI KUENDELEZA HARAKATI ZA UISLAM.

WALIMU HAO WAMETOA OMBI HILO KUPITIA RISALA YAO WALIYOISOMA MBELE YA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA MADRSSA HIYO ZINAZOFANYIKA WAKATI WANAFUNZI WANAPOINGIA KATIKA MADARASSA MENGINE.

WAMEFAFANUA KUWA MADRASSA HIYO KWA SASA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VITENDEA KAZI NA UFINYU WA MADARASA YAKUFUNDSHIA.

MADRASSA HIYO ILIYOJENGWA KWA MSAADA WA SHIRIKA LA AFRIKA MUSLIM AGENCY YENYE WANAFUNZI 385 IMEANZISHWA MWAKA 1983.

Washukiwa wa Ugaidi Kenya WafikishwaMahkamani


Wanaume wanne wamefikishwa mahakamani nchini Kenya baada ya kuhusishwa na shambulizi la kigaidi lililofanyika dhidi ya jengo la Westgate nchini Kenya mwezi Septemba.

Wanne hao wote walikanusha mashitaka hayo ikiwemo kosa la kuingia nchini bila vibali halali pamoja na kumiliki stakabadhi bandia za kujitambulisha. Mahakama imeamuru wawekwe rumande.
Kundi la kigaidi la Somalia, Al Shabaab lilikiri kufanya shambulizi hilo la kigaidi ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.

Wanne hao walishitakiwa kwa kosa la kuhusika na shambulizi hilo la kigaidi ingawa hakuna hata mmoja alikuwemo ndani ya Jengo la Westgate wakati wa shambulizi hilo.

Wanne hao raia wa Somalia ni Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah, Adan Adan na Hussein Hassan.
Washukiwa hao ambao hawakuwa na mawakili walizuiliwa rumande kwa wiki moja baada ya kiongozi wa mashitaka kuomba muda zaidi kufanya uchunguzi.

TATHMINI KILIMO CHA BANGI, ARUSHA YAONGOZA...!

IMEBAINIKA kuwa Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kilimo haramu cha bangi ambayo imekuwa ikiharibu vijana wengi.
Akizungumzia ishu hiyo wakati wa uteketezaji wa mashamba ya bangi wilayani Arumeru jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikemea vikali juu ya ustawishaji wa mmea huo huku akisisitiza kula sahani moja na wahusika.

Kamanda huyo aliwataka raia wema kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mara moja wanapogundua uhalifu wa aina hiyo na mwingine wowote.

Sunday, November 3, 2013

KAGASHEKI WITNESSE THE HAUL OF IVORY IMPOUNDED BY THE POLICE, THREE CHINESE NATIONALS ARE IN CUSTODY IN CONNECTION WITH MORE THAN1,800 KG OF TROPHIES



Natural Resources and Tourism minister, Ambassador Khamis Kagasheki, in disbelief as he looks at a pile of elephant trophies impounded at a Mikocheni house in Dar es Salaam, Saturday Nov 2, 2013.
Three Chinese nationals Huang Qin, Chen Jinzhan and Xu Fujie are in custody in connection with more than 1,800 kg of trophies
Minister Kagasheki, visits inside the residential house used as a were house to hide natural resources at Mikocheni in Dar es Salaam, Saturday Nov 2, 2013

Armed plain police officer, stand guard outside Mikocheni house in Dar es Salaam late on Saturday, where more than 1,800 kgs of ivory were impounded by the police


At a time when poaching has tremendously scaled up in the country, about 706 pieces of ivory, representing more than 200 tuskers killed, were found yesterday in Dar es Salam Mkocheni area at a residence of Chinese nationals.
The incredulous catch was hidden in a manner that needed informed intelligence to uncover as shells of snails mixed with garlic to fool any suspicious minds sniffing about the ivory. Even the minister for Natural Resources and Tourism, Khamis Kagasheki, and police officers at the scene were so stunned with the ingenuity of the residents, evidently agents of Far East ivory traders.
A detailed report made available to the Guardian on Sunday in past months says China is deeply implicated in the wave of killing of elephants owing to its million dollar trade in ivory products.  The report authored by the Tanzania Elephant Protection Society (TEPS) said rising economic relations between China and Tanzania fuel elephant killings in the country, calling for proper government intervention.
The document underlined that though the Chinese investments were important in the country’s economy and development, this shouldn’t compromise the country’s natural wildlife conservation efforts. 

The report affirmed that at the current rate of 30 elephants killed every day and 850 elephants shot every month, there is an unprecedented risk of the country’s elephant population perishing in the next seven years.

“China is the number one investor in Tanzania … but the majority of tusks exported illegally from Tanzania end up in China due to the huge demand for ivory in China,”   it said, noting that Tanzania’s partnership with China risks being at the expense of Tanzania’s vital natural resources and the tourist industry,
This requires political will and strong leadership to resolve, it said, recommending that the Tanzania government “should make investment from China and other countries strictly conditional on China tackling its demand for ivory at home, and stronger law enforcement collaboration to halt the flow of ivory from Tanzania to China.”
Three Chinese, Che Jinzhan, Xu Fujie and Huang Qin, are said to use a special Noah microbus with registration number T713 BXG to transport the ivory pieces to the house.
Until this paper left the house more than 1800 kilogram of ivory pieces were found, although the police were not yet finished with counting.
Inside the house police found a weighing unit that the Chinese used in their illegal business, a number of fresh garlic onions and sacks of shells which were mixed with the ivory during transportation.
Interviewed, the Chinese said that the ivory business is owned by their friends and what they were doing was only the garlic business.
Huang Qin explaining that his friends are the one who used to bring the ivory in their home. He admitted that it is illegal business and if it was in their country they would be executed.
The bus that used to bring the product in the house uses different numbers whereby during a day the used plate number is T713 BXG but at night the number is twisted with plate number T 317 BXG.
According to the information released from the ivory storehouse, the minibus is used to conduct the operation at midnight, specifically from 1:00 am.
Briefing the media at the event, minister Kagasheki said they managed to find the ivory as a follow up to Operation Tokomeza against gangs hunting elephants with automatic rifles, all over the country.
Ambassador Kagasheki said the fight against poachers will not be achieved by suspending public officials but by joining efforts with all stakeholders, including MPs to fight the scourge.
The ivory pieces found yesterday represent a big amount as elephants are steadily diminished, he said, underlining that stopping Operation Tokomeza as MPs are proposing would see elephants cleared out from game parks in a few years.

A bag of cash owned by Chinese nationals. the cash was in possession by the arrested Chinese nationals

More than 30 million shillings owned by the arrested Chinese nationals was intended to bribe the corps, according to police sources at the scene

Kagasheki (L), in disbelief, as he led the operation to arrest three Chinese national found with ivory tusk at Mikocheni

Ambassador Kagasheki (L), talks to his Permanent Secretary, Maimuna Tarishi at the scene


Che Jinzhan (R), and Xu Fujie

Ring leader of the arrested Chinese nationals, Huang Qin,

Minister Kagasheki, tour the crime scene

Ambassador Khamis Swed Kagasheki, in a shocking mood
The three Chinese nationals, arrested with more that 1,800 kgs of ivory tusk, wait their fate

This is a makeshift house used to cover the real house used by the Chinese to hide national' resources at Mikocheni in Dar es Salaam

Armed police officer, guard a pole of ivory tusk packed in the sucks at Mikocheni residential house in Dar es Salaam, Saturday Nov 2, 2013

Marekani Yamuua Kiongozi wa Taliban


 
Kiongozi wa kundi la wapiganaji la Taliban nchini Pakistan, Hakimullah Mehsud, ameuawa kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani, hii ni kwa mujibu wa afisaa mmoja mkuu wa kundi hilo.

Shambulizi hilo lililenga gari alimokuwa anasafiria Mehsud, Kaskazini Magharibi mwa Waziristan.
Watu wanne waliokuwa wanasafiri na Mehsoud wakiwemo walinzi wake wawili waliuawa katika shambulizi hilo.

Marekani pamoja na Pakistan zimewahi kudai siku za nyuma kumuua Mehsoud ingawa madai yao hayakuwa na ukweli.

Serikali ya Pakistan imetoa taarifa kulaani vikali mashambulizi ambayo Marekani inafanya kwa kutumia ndege zisizo na rubani, ikisema kuwa mashambulizi kama hayo yanakiuka uhuru wa taifa hilo.

Shambulizi hilo lililofanywa siku ya Ijumaa, lililenga gari la Mehsud.

Afisaa mmoja mkuu wa ujasusi nchini Marekani, aliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Marekani ilipokea taarifa muhimu kuthibitisha kifo cha Mehsoud.

Hata hivyo msemaji wa baraza la usalama wa kitaifa la Marekani, alisema kuwa hawawezi kuthibitisha taarifa hizo lakini ikiwa ni kweli basi ni pigo kubwa sana kwa Taliban.

Hakimullah Mehsud alijulikana sana mwaka 2007 kama kamanda wa mwasisi wa kundi hilo Baitullah Mehsud, alipowakamata wanajeshi 300 wa Pakistani .

This is Delphi, A free prem TANZANIA NI NCHI YA KUCHUMA MALI ?: PEMBE ZA TEMBO 706 ZAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM NI BAADA YA TEMBO 353 KUPIGWA RISASI NA KUUAWAWA KATIKA ARDHI YA TANZANIA.



 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki (wa pili kushoto), akiwa ameshika pembe za ndovu zilizokatwa jana jijini Dar es Salaam toka kwa raia watatu wa China katika operesheni aliyoiongoza.

DAR ES SALAAM.
SIKU moja baada ya wabunge kuwataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, pembe 706 za ndovu zimekamatwa jijini Dar es Salaam.



Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.

Waliokamatwa na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China ambao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung .

Raia hao wa China wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mingi wakifanya biashara ya kuingiza nchini vitunguu swaumu kutoka China na kusafirisha nje ya nchi makombe yanayopatikana baharini.

Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Kagasheki ambaye aliambatana na askari polisi na baadhi ya maofisa usalama alishuhudia shehena kubwa ya pembe za ndovu ikiwa imehifadhiwa kwenye viroba vyenye uzito wa kilo 50.

Mbali ya kushuhudia shehena ya pembe hizo, alionyeshwa gari maalumu aina ya Toyota Noah ambalo watuhumiwa hao hulitumia kutoa pembe porini na kuyaingiza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika eneo la tukio mara baada ya kuwakamata alisema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na matokeo ya Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo imesitishwa na Serikali juzi baada ya wabunge kuilalamikia.

Waziri Kagasheki alisema kwamba katika harakati za kutaka kuwakamata watuhumiwa hao walitoa Sh30 milioni kwa ajili ya kujaribu kuwahonga askari.

“Walitaka kuwahonga askari ili wasikamatwe,” alisema huku akionyesha noti za fedha hizo.

Alisema wabunge wanaomtaka ajiuzulu kwa madai kwamba Operesheni Tokomeza Ujangili imesababisha mauaji ya watu na mifugo wanapoteza muda kwa kuwa mwenye mamlaka ya kumtoa ni Rais Jakaya Kikwete pekee.

“Sasa mimi nasema kunitoa haitakuwa rahisi anayeweza kunitoa ni yule aliyeniweka,” alisema.

Alisema ipo mikakati inayofanywa na baadhi ya wabunge kutaka kuwang’oa baadhi ya mawaziri kwa masilahi binafsi ya kisiasa. MWANANCHI