Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, November 19, 2013

'Hujuma ya kigaidi ya Beirut ni njama za Wazayuni'


'Hujuma ya kigaidi ya Beirut ni njama za Wazayuni'Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mkabala na ubalozi wa Iran huko Beirut mji mkuu wa Lebanon ni njama za Wazyuni na vibaraka wao. Bi Marzieh Afkham amelaani mashambulizi hayo ya kigaidi yaliyotokea leo asubuhi huko Beirut mkabala na ubalozi wa Iran mjini humo na kusisitiza kuwa, jinai hiyo ni kitendo cha chuki na uadui kilichofanywa na Wazayuni na vibaraka wao.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kusikitishwa na kuuliwa shahidi na kujeruhiwa raia kadhaa wa Lebanon na wa nchi za nje katika mashambulizi hayo ya kigaidi na kutoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa mashambulizi hayo. Bi Afkham ameongeza kuwa kwa kuzingatia kwamba mripuko huo umetokea karibu na ubalozi wa Iran huko Beirut, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran inafuatilia suala hilo kwa makini na kwa juhudi maalumu na kwamba itatoa taarifa kamili katika uwanja huo. Watu wasiopungua 26 wameuliwa na wengine 150 kujeruhiwa katika mripuko huo.
Wakati huo huo mkuu wa idara ya utamaduni katika ubalozi wa Iran mjini Beirut Sheikh Ibrahim Ansari ameuawa shahidi katika mripuko huo. Habari hiyo imethibitishwa na kaimu waziri wa afya nchini Lebanon.

Monday, November 18, 2013

Naibu Mkuu wa shirika la ujasusi Libya atekwa nyara


Naibu Mkuu wa shirika la ujasusi Libya atekwa nyaraNaibu wa Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Libya ametekwa nyara akiwa pamoja na mmoja wa viongozi waliooongoza mapinduzi dhidi ya Kanali Muammar Gadafi nchini humo. Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa, maafisa hao waandamizi wa Libya wametekwa nyara leo mjini Tripoli. Huku hayo yakiripotiwa, habari kutoka Tripoli, mji mkuu wa Libya zinasema kuwa, hali ya wasiwasi imerejea mjini humo baada ya kutulia kwa muda mfupi. Kwa siku mbili mfululizo mji huo umeshuhudia mapigano kati ya pande hasimu yaliyopelekea zaidi ya watu 40 kuuawa na karibu laki tano wengine kujeruhiwa. Leo wananchi wa Libya wameendelea kuwazika watu waliouawa, maziko ambayo yameambatana na maandamano ambapo wakazi wa mji huo wameitaka serikali dhaifu ya nchi hiyo ikabiliane vilivyo na wanamgambo wenye silaha. Wananchi hao wametishia kufanya uasi wa nchi nzima kama serikali na makundi yenye silaha yatashindwa kufikia makubaliano ya kurejesha amani katika nchi hiyo tajiri kwa mafuta ya kaskazini mwa Afrika. 

Wamisri wachoma moto picha za Erdogan na Qatar



Wamisri wachoma moto picha za Erdogan na Qatar
Waandamanaji wanaomuunga mkono Abdulfatah al Sisi, Waziri wa Ulinzi wa Misri wamezichoma moto picha za Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan na bendera ya nchi ya Qatar mjini Cairo, Misri. Waandamanaji hao waliokuwa wamekusanyika mbele ya ubalozi wa Uturuki mjini Cairo, wametaka pia kufukuzwa balozi wa Uturuki nchini kwao. Kabla ya hapo na katika kulalamikia matamshi ya viongozi wa Ankara, Cairo ilimuita balozi wa Uturuki nchini humo Hussein Own Butsali sambamba na kumuondoa balozi wake mjini Ankara. Mbali na hapo serikali ya Cairo ilitangaza kuwa, itachunguza uhusiano wake na Uturuki lakini ikatangaza kuwa, katika hali ya sasa haitamrejesha balozi wake nchini Uturuki. Nivyema kuashiria hapa kuwa, baada ya kuuzuliwa madarakani rais Muhammad Mursi wa Misri, Uturuki ambayo ilikuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa hatua hiyo, ilitangazi wazi wazi kwamba, inamtambua Mursi kuwa ndiye rais pekee wa kisheria wa nchi hiyo. Aidha mbali na hapo Ankara iliendelea kulaani hatua ya kuwekwa kizuizini mteja wao huyo sanjari na kusisitiza kutaka kurejeshwa kwake madarakani nchini Misri, suala ambalo lilizidi kupigilia msumari wa moto kwenye siasa za nchi mbili. Inasemekana pia kwamba, Qatar ambayo ni muungaji mkubwa wa Harakati ya Ikhwanul Muslimiin nchini Misri, ilikata misaada yake ya kifedha kwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika baada ya kung’olewa madarakani rais Muhammad Mursi.

Wahamiaji haramu 61 wakamatwa Italia


Wahamiaji haramu 61 wakamatwa Italia
Maafisa wa Italia wamewatia nguvuni wahamiaji haramu 61 katika kisiwa cha kusini mwa nchi hiyo. Kikosi cha ulinzi cha pwani ya Italia leo Jumatatu kimewatia mbaroni wahamiaji haramu 61 waliokuwa na lengo la kuingia katika kisiwa cha Lampedusa kusini mwa nchi hiyo. Kisiwa cha Lampedusa kinachopatikana kati ya kisiwa cha Sicily na Tunisia hutumiwa na makumi ya wahamiaji haramu  kutoka kaskazini mwa Afrika na eneo la Mashariki ya Kati kama njia ya kufika nchini Italia na katika nchi nyingine za Ulaya.
Wahamiaji haramu zaidi ya elfu 36 mwaka huu wameingia Italia wakitafuta hifadhi.

Makumi wafariki dunia katika ajali ya treni Misri


 Makumi wafariki dunia katika ajali ya treni Misri
Ajali iliyohusisha treni na magari mawili katika kivuko cha reli huko Misri imeua watu 24 na kujeruhi wengine wengi. Ajali hiyo imetokea leo asubuhi karibu na wilaya ya Giza huko Cairo mji mkuu wa Misri, wakati treni moja ilipogongana na lori na basi dogo lililokuwa limepakia watu wakitokea kwenye sherehe ya harusi.
Hussein Zakariya Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Misri amesema kuwa basi dogo na lori viliparamia kwa kasi kivuko cha reli  kilichokuwa kimefungwa kwa minyororo na huku kikiwa na taa za tahadhari na  hivyo kusababisha ajali hiyo. Mwezi Januari mwaka huu treni moja ya mizigo iliacha njia na kusababisha vifo vya watu 17. Barabara na njia za reli nchini Misri zimekuwa na rekodi mbaya ya usalama huku wananchi wakilalamika kutokuweko na sheria msingi za usalama  ili kuzuia kutokea ajali mbaya za mara kwa mara.

Waasi wa zamani wa Seleka wamuua jaji huko CAR


Waasi wa zamani wa Seleka wamuua jaji huko CAR
Waasi wa zamani wa Muungano wa Seleka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamewaua kwa kuwapiga risasi jaji mmoja wa nchi hiyo na mshauri wake na hivyo kuibua machafuko huko Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mbali na kuwaua jaji huyo na mshauri wake hapo jana, raia  wengine kadhaa walijeruhiwa pia katika ufyatuaji risasi uliofanywa na waasi hao wa zamani wa Seleka  hapo jana dhidi ya wakazi wa mji mkuu Bangui waliokuwa  wakiandamana kupinga kuuliwa Jaji Modeste Martineau Bria na mshauri wake. Afisa mmoja wa polisi ya Bangui amesema kuwa Jaji Bria na mshauri wake waliuliwa kikatili na waasi wa zamani wa Muungano wa Seleka ambao waliwafyatulia risasi wahanga hao huku wakiwa wamepanda kwenye pikipiki huko katikati mwa Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Baada ya kujiri mauaji hayo, wakazi wa Bangui walimiminika mitaani na kuanza kuweka vizuizi barabarani, kuchoma moto matairi katika kupinga mauaji hayo yaliyofanywa na waasi wa zamani wa Muungano wa Seleka. Hadi sasa haijafahamika sababu halisi iliyopelekea kuuawa jaji huyo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na mshauri wake.

Thursday, November 7, 2013

Mtoto Suleiman Hawezi Kutibiwa Nchini-Madaktari.





Hatimaye imebainika kwamba mtoto Suleiman Rajab anayesumbuliwa na ugonjwa wa ajabu,hawezi kutibiwa hapa nchini.


Kwa mujibu wa mratibu wa matibabu yake Hoyce Temu akiongea kwa njia ya simu na Munira Blog mapema leo hii amesema,madaktari bingwa wa CCBRT wamesema ni lazima mtoto huyo akatibiwe nchini India.

Amesema madaktari hao hawajawahi kufanya upasuaji wa aina hiyo kwa mtoto,kitu ambacho kimewasukuma kuchukuwa maamuzi hayo.

"Tokea jana jioni mtoto suleiman kesha toka hospitali (yupo kwao kivule) na sasa tunaanza harakati za kumpeleka india,ambapo tunaanzia kumtafutia paspoti",mwisho wa kumnukuu.

Munira blog ilimtafuta bwana Abdul Kajumuro ambaye ni meneja mawasiliano  katika Hospitali ya CCBRT ili kuthibitisha hilo,ambapo alikiri kulifahamu hilo.

Aidha aliongeza kwamba "Madaktari bingwa wamekubaliana kumpeleka India kwa kuwa wenzetu wana utaalamu mkubwa na vifaa vya kutosha na tayari wameshaanza mawasiliano na madaktari wa India ili kuangalia namna ya kumsaidia mtoto huyu",alisema.

Munira blog inawaomba watu mbali mbali  kumsaidia Mtoto huyu ili kufanikisha safari yake,sambamba na
kumuomba Mwenyezi Mungu ili mtoto Suleiman apate  matibabu kwa wepesi na amani.

BODA BODA MARUFUKU




Madereva wa pikipiki wamelaumiwa kwa kusababisha ajli nyingi za barabarani

Mamia ya wakaazi wa mji mkuu wa Liberia Monrovia, wamelazimika kwenda kazini kwa miguu baada ya sheria inayoharamisha bodaboda kuingia mjini humo kuanza kutumika.

Polisi waliweka vizuizi barabarani hasa katika maeneo muhimu ya kuingia mjini kuhakikisha huwa madereva wa pikipiki wanatii sheria hiyo.
Hatua ya serikali inatokana na tuhuma dhidi ya madereva wa pikipiki hizo ambazo hutumiwa kwa uduma za Taxi, kwa kuziendesha ovyo na kusababisha ajali nyingi barabarani.

Pikipiki hizi ambazo humilikiwa na watu binafsi, hutumiwa sana na wasafiri wengi mjini Monrovia na pia katika miji mingi barani Afrika.

Baadhi ya madereva wa pikipiki hizo huwabeba hadi watu watano wakati wanaruhusiwa tu kuwabeba watu wawili.

Kwa mujibu wa taarifa ya poliisi, madereva wowote wa pikipiki hizo watakaopatikana mjini watatozwa faini ya dola miambili.

Mmoja wa madereva hao Daniel Howard alisema kuwa wameghadhabishwa mno na hatua ya serikali.

Mapema mwaka huu madereva wa Pikipiki hizo walizuiwa kuziendesha katika baadhi ya barabara za mji baada ya saa nne usiku.

Hata hivyo sheria hii ya sasa inasemekana kutatiza usafiri pakubwa mjini humo.