Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, June 14, 2012

MAMA,,,,, KISHA MAMA,,, KISHA MAMA

Tutakuwa pamoja nanyi tukizungumzia moyo wenye huruma, moyo wenye ulaini, moyo ulio umbiwa huruma. Tutakuwa tukizungumzia moyo ambao umeumbwa siku ulipoumbwa, ukapandikizwa huruma, tutakuwa na moyo wenye kuhurumia hata kama unafanyiwa ukali. Je, mmeufahamu moyo huo? Hakika si mwingine bali moyo huo ni mama.
Tunamzungumzia mama ambaye maadui wa Allaah wamemuwekea siku moja tu na wakaiita "siku ya mama" na hili si katika Uislamu kwa chochote. Uislamu umeamrisha kumfanyia wema mama (kila siku) mwaka mzima.
Huyo ndiye mama enyi waja wa Allaah. Kiumbe ambaye ameendelea kuwa mbele na mshindi daima.
Mama yako enyi waja wa Allaah, ni mara ngapi amehuzunika (ameingia katika jambo la kumhuzunisha) ili wewe ufurahi, na akashinda au kulala njaa ili ushibe, na akalia ili ucheke, na akakesha ili ulale, na akabeba mambo magumu na mazito katika njia ya furaha yako (ili ufurahi). Unapokuwa umefurahi naye ndipo hufurahi, na ukihuzunika, umemhuzunisha, ukipatiwa na mfadhaiko, basi maisha yake yako katika shida kubwa. Matumaini na matarajio yake, yako katika shida kubwa. Matumaini na matarajio yake (yote) ni wewe uishi maisha ya kiungwana (matukufu) ya kuridhisha yenye kuridhiwa.
Mama kiumbe dhaifu ambaye hutoa bila kutaraji malipo yoyote. Anayemimina (kheri zake zote kwako) bila kutumai shukrani zozote kwako. Je umewahi kumsikia kiumbe anayekupenda kuliko mali yake? Hapana, bali zaidi kuliko dunia yake? Hapana bali zaidi kuliko nafsi yake iliyopo kati ya mbavu zake? Ndio, anayekupenda zaidi kuliko nafsi yake, hakika huyo si mwengine bali ni mama yako, mama pekee ndio alama ya huruma. 
Hebu fikiria kwa makini ewe ndugu yangu mpendwa, hali uliyokuwa nayo udogoni mwako (fikiria) kumbuka udhaifu wa uchanga wako, hakika alikubebea mimba tumboni mwake miezi tisa kwa hali ya unyonge (udhaifu) juu ya unyonge. Amekubebea mimba kwa taabu na akakuzaa kwa taabu, kuendelea kukua kwako tumboni mwake kulimzidishia udhaifu na anabeba mzigo (taabu) zilizo nje ya uwezo wake, na mama (kama alivyo mwanamke mwengine) ni mdhaifu wa kiwiliwili, mnyonge wa nguvu, na wakati wa kujifungua huyaona mauti mbele ya macho yake, machozi na masikitiko, vikwazo na machungu, lakini yeye anajilazimisha kusubiri (mpaka anakuzaa) na pale tu anapokuona u-pembeni mwake na akakukumbatia kifuani mwake, na akashumu (akanusa) harufu yako, na akazihisi pumzi zako zikikariri (kuingia na kutoka), basi husahau maumivu yake yote, na husahau machungu yake yote.
Anakuona na kufungamanisha matumaini yake yote kwako. Na huona kwako uzuri wa maisha na mapambo yake, kisha anageukia kukuhudumia mchana wa maisha yako na usiku wake. Akikulisha kwa ajili ya siha yako, na akikukuza kwa kujichakaza (kujizeesha) yeye, na kukuimarisha (kukutia nguvu) kwa kujidhoofisha yeye, chakula chako ni chuchu zake, nyumba yako ni mapaja yake, na gari lako ni mikono yake (au mgongo wake). Amezunguka na kukuchunga (usipatwe na balaa lolote). Yuko radhi yeye abaki na njaa ili wewe ushibe, na akeshe ili ulale, na yeye kwako ni mwenye huruma nyingi. Na ana uchungu mwingi juu yako, akikaa mbali nawe (kidogo tu) unamuita, na akikupa nyongo unamuomba akuelekee. Na likikupata la kukuchukiza unaomba wokozi kwake. Unadhani kheri zote (kila jambo zuri) ziko kwake tu. Na unadhani shari haitokufikia akikukumbatia kifuani mwake, au akiwa anakuangalia kwa jicho la mazingatio.
Na baada ya kutimia kuacha kwako ziwa ndani ya miaka miwili (mara nyingi), na ukaanza kutembea huanza kuuzungusha umuhimu wake wote kwako, na macho yake hukufuatilia (popote uendapo). Hukufuatilia haraka nyuma yako kwa kukuhofia (kuanguka na mengineyo) kisha ukakua, na kuchukua kwako miaka. Ikampata na kumuingia shauku na huruma, sura yako ni nzuri zaidi mbele yake kuliko mwezi unapokamilika (duara lake), sauti yako kwake ni tamu zaidi masikioni mwake kuliko sauti za bulbul na nyimbo za ndege wengine. Harufu yako inanukia vizuri zaidi kwake kuliko manukato yote na maua yote, utukufu wako ni kitu cha ghali sana kuliko dunia, lau itapelekwa kwake pamoja na mapambo yake yote hakuna kitu ghali, bali kila kitu ni rahisi kwake katika kuhakikisha unapata raha. Mpaka hata nafsi yake iliyopo kati ya mbavu zake mbili si lolote si chochote, na huchagua kufa ili wewe uishi salama salimini mwenye afya tele!!

Ni Mama Yako Ewe Mja Wa Allaah
Hebu sikiliza kwa makini ewe mja wa Allaah, na ujue ya kwamba aliyenyimwa kheri, aliyepotea na kuruka patupu (kula hasara) duniani na Akhera, ni yule atakayepoteza haki za wazazi wawili na hasa hasa mama. 
Amepokea Hadiyth Imaam Ahmad na An-Nasaaiy na Ibn Maajah, kutoka kwa Mu'awiyah Ibn Jahimah As-Salamiy (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema. Nilimuendea Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) (siku moja) na nikamwambia; Ewe Mtume wa Allaah, hakika mimi nahitaji kupigana jihadi pamoja nawe, nikitaraji kupata radhi za Allaah na nyumba ya akhera, Mtume akasema: ((Nakuonea huruma (Usifanye Hivyo), hivi yuko hai mama yako?)) Nikasema: Ndiyo. Mtume akasema: ((Rudi ukamfanyie wema usiende kupigana Jihadi)). Kisha nikamuendea kupitia upande mwingine, nikamuambia: Ewe Mtume wa Allaah, hakika mimi nataka kupigana Jihadi pamoja nawe, nikitafuta kwa hilo radhi za Allaah na nyumba ya akhera, Mtume akasema ((Nakuhurumia, usifanye hivyo, je mama yako yu hai?)). Nikasema ndiyo ewe Mtume wa Allaah. Mtume akasema: ((Rudi kwake ukafanye wema)). Kisha nikamuendea kwa mbele yake nikasema: Ewe Mtume wa Allaah, hakika mimi nataka kupigana jihadi pamoja nawe, nikitafuta kwa hilo radhi za Allaah na nyumba ya akhera, Mtume akasema: ((Nakuonea huruma, usifanye hivyo, Mtume akasema: ((Nakuonea huruma, jilazimishe na mguu wake hapo ndipo palipo na pepo)), Hakika mama ni pepo namuapa Mola wa al-Kaabah, Lazimiana (shikamana) na mguu wake hapo ndipo ilipo pepo)).
Imepokewa Hadiyth (nyingine) kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: Mtu mmoja alimjia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akasema: Ewe Mtume wa Allaah, mimi nimekuja nataka kupigana jihadi pamoja nawe nikitaraji radhi za Allaah na nyumba ya akhera, na kwa hakika nimekuja, huku wazazi wangu wawili wanalia; Mtume akasema: ((Rudi kwao ukawachekeshe kama ulivyowaliza)). [Ameisimulia Ibn Maajah na akaisahihisha Al-Albaaniy].
Na kutoka kwa Anas bin Nadhwiri Al-Ashijainiy amesema: Siku moja mama yake Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anha) alitaka maji ya kunywa na ilikuwa usiku – kwa mwanawe Ibn Mas'uud, akaenda kumletea maji, kurudi akamkuta keshalala, Ibn Mas'uud akabaki amesimama na maji mbele ya kichwa chake mpaka asubuhi, na walipofika Abu Muusa Al-Ash'ariy na Abu 'Aamir kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakampa Bay'ah (kiapo cha utii) na wakasilimu. Mtume akawauliza (amefenya nini yule mwanamke, miongoni mwenu aitwaye kadhaa wa kadhaa? Mtume akasema: (Kwa sababu ya kumtendea mama yake akasema, alikuwa ana Mama bibi kizee, mara akawajia muonyaji akisema, hakika adui anakusudia kuwadhuruni, Mama huyu (Mama Ibn Mas'uud) akambeba mama yake mgongoni mwake, akichoka anamtua chini (anapumzika) kasha anakutanisha tumbo lake na tumbo la Mama yake (yaani anambeba kwa kumkumbatia tumboni) ikawa miguu yake iko chini ya miguu ya Mama yake kutokana na kumkinga na joto kali, mpaka akaokoka na adui yule). [Ameitoa 'Abdur-Razaaq katika Muswannaf yake].
Huyo ndiye Mama, ewe mwenye kutaka kuokoka, basi lazima ana miguu yake, hapo ndipo ilipo pepo yake.

Waja Wema Na Kuamiliana Kwao Na Mama  
Siku moja Ibn 'Umar alimuuliza mtu mmoja, je, unaogopa kuingia motoni? Na unapenda kuingia peponi? Yule mtu akasema ndiyo. Ibn 'Umar akamwambia: Basi mfanyie wema Mama yako, kwani namuapa Allaah, Kama utamlainishia maneno na ukamlisha chakula, hakika utaingia peponi endapo utajiepusha na madhambi makubwa yenye kuangamiza. 
Hakika kuwafanyia wema wazazi wawili ni tabia ya watu wema, na ni mwendo wa wacha-Mungu. Inasimuliwa kuwa siku moja Ibn Al-Hasan At-Tamiymiy alimpiga Ng'e akaingia shimoni na yeye akaingiza kidole chake nyuma yake ndani ya hilo tundu, ng'e akamgonga kwa mwiba wake wa sumu; akaulizwa kuhusu jambo hilo? Akasema: "Nilihofia asije akatoka na kumgonga mama yangu''
Na amesema Muhammad Ibn Siyriyn: ''Ulifikia mtende mmoja wakati wa Khalifa 'Uthmaan kuuzwa kwa Dirhamu elfu moja. Usaamah bin Zayd akajitahidi akanunua mtende mmoja akautoboa na kutoa utomvu wake akamlisha Mama yake. Watu wakamuliza, ni kipi kilichokupelekea kuuchezea mtende namna hii na wewe unaona mtende umefikia kuuzwa ghali namna hii; dir'hamu alfu moja? Akasema: "Hakika mama ameniomba. Na hawezi Mama yangu kuniomba kitu chochote ninachokiweza isipokuwa nitampa).
'Abdullaah bin 'Awn nae siku moja aliitwa na mama yake, na yeye akanyanyua sauti yake ikawa juu ya sauti ya mama yake. Kwa kosa hilo tu akaamua kuadhibu nafsi yake kwa kuacha huru watumwa wawili!  
Na Zaynul-'Aabidiyn (pambo la wacha Mungu) naye alikuwa ni mtu mwenye kufanya wema sana kwa mama yake. Lakini hakuwa akila naye sahani moja, siku moja akaulizwa mbona wewe ni mwenye kufanya wema kwa mama yako kuliko watu wote lakini hatukuoni ukila nae sahani moja? Akajibu akasema: "Ninaogopea mkono wangu kutangulia kufika pale mahali lilipotangulia kuona jicho lake hivyo nikawa nimemvunjia heshima"    Hakika washatangulia mbele yetu watu hawakuwa akirefusha mmoja wao nyumba yake kupita kimo cha mama yake!!
Hakika ni pepo, ewe mtafuta pepo lazimiana (shikamana) na nyayo zake hapo ndipo ilipo pepo.
Amepokea Hadiyth hii At-Tirmidhiy na akaisahihisha kutoka kwa Abu Dardaa (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Mzazi ni mlango wa katikati ya milango ya pepo, ukitaka upoteze mlango huo au uhifadhi)).
Na katika At-Tirmidhiy, kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Radhi za Mola zinatokana na radhi za mzazi, na chuki zake zinatokana na chuki za mzazi))   
Amesema Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhu): "Hakuna Muislamu yeyote mwenye wazazi wawili Waislamu akaamka akitaka thawabu kwa Allaah kupitia kwao, isipokuwa Allaah Hufungua milango miwili – yaani katika pepo na ikiwa ni mmoja basi utafunguliwa mmoja, na akimkasirisha mmojawapo, Allaah Hatomridhia mpaka mzazi amridhie). Akaulizwa hata kama wamedhulumu? Akasema: Hata kama wamedhulumu.
Anasema mshairi mmoja:
Mama yako ana haki kubwa sana kwako lau ungejua,
kingi chako wewe huyu mbele yake ni kichache.
Ni masiku mangapi amekesha akishitakia shida zako,
kwake akakesha akiungulia moyo wake na kupiga makelele.
Na wakati wa kujifungua hujui mazito yanayompata,
hivyo kwa yanayomkwaza nyoyo zinakaribia kuruka.
Na ni mara ngapi amekuoshea uchafu kwa mkono wake wa kulia,
na halikuwa paja lake kwako ni kitanda.
Na ni mara ngapi amepata njaa na akakupa chakula chake,
kwa sababu ya huruma na uchungu kwako ukiwa mdogo.
Ukamtupa pale ulipomfanyia ubaya katika hali ya ujinga,
na likarefuka kwako jambo na hali ya kuwa yeye ni mfupi.
Majuto ni kwa yule aliyeelewa (ubora wa mama) lakini akafuata matamanio,
na majuto ni kwa kipofu wa moyo hali ya kuwa macho yanaona.
Basi jipendekeze katika kukithirisha kumuombea dua,
kwani wewe unaloliomba una haja nalo zaidi.
Siku moja Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) alimuona mtu mmoja M-yemen akitufu Al-Ka'abah huku amembeba mama yake mgongoni mwake huku akisema: Hakika mimi ni ngamia wake aliyedhalilishwa, ikiwa abiria wake watamkorofisha, basi mimi siogopi, Allaah ndiye mola wangu mwenye utukufu mkuu, nimembeba mara nyingi zaidi kuliko alivyonibeba, Je, ewe Ibn 'Umar unahisi nitakiwa nimeshamlipa? Ibn 'Umar akasema: ''Hapana, hujamlipa hata pumzi moja''
Nasaha kwa wale wanaowafadhilisha (wanaowatanguliza) wake zao kuliko mama zao;
Na kwa wale wanaowapa wake zao na kuwanyima mama zao.
Usimtii mke ukamkata mama juu yako, ewe kijana wa ndugu yangu umepoteza umri wako.                        
Ni vipi unamkana mama wakati mimba yako kaibeba yeye, tena umegaragara mapajani mwake kwa uzito.
Na akauguza maumivu ya nafsi kwa ajili yako na ni kwa kiasi gani, alifurahi alipozaa mtoto wake akawa ni mwanamme.
Na hakuonyesha mpaka miaka miwili iliyokamilika, na huku akitaka kunyeshelezwa katika kifua chake na matiti yake ya lulu.
Na kile ulichokinyonya kutoka kwake unakitoa na kumchafua, bila yeye kulalamikia uvundo wa uchafu.
Na ameamiliana nawe kwa wema na malezi mema mpaka, umelingana sawa na mpaka umekuwa namna unavyojiona.
Hivyo usimfadhalishe mke kuliko yeye milele, na wala usiache moyo wake ukivunjika kwa kumtenza nguvu.
Mzazi ndio mlezi wa kwanza hilo halipingiki, mlinde hasa hasa akifikia utu uzima.
Huwezi kumtekelezea haki zake zilizo juu yako hapo, juu ya macho yako amehiji nyumba tukufu na akafanya 'Umrah.
Enyi waumini, ni masaa mangapi Muislamu ametumia kuwatimizia haja wazazi wawili, kwa hilo Allaah Amekuondolea mawazo ya kufadhaisha shida, ni wangapi katika mtoto wa kiume mwema kwa wazazi wake au msichana mwema kwa wazazi wake, wamesimama mbele ya wazazi wao baada ya salamu au maneno mazuri au zawadi kwa unyenyekevu, huku imefunguliwa milango ya mbingu kwa ajili ya maombi yao yenye kujibiwa kutoka kwa wazazi wao wawili walio dhaifu waliozeeka.          
Hivyo mcheni Allaah kwa wazazi wawili, hasa hasa wanapofikia umri mkubwa na uzee kiasi walipofikia, na kudhoofika kwao mifupa, na kichwa kuwaka mvi, watakapokuwa wamefikia hali waliyoifikia na wakawa wanakuangalia muangalio ambao unangojea tonge kwa furaha au kipawa cha malipo. 
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) anasema katika Qur-aan Suratul Al-Israai aya ya 23 kwamba:
{{Amehukumu mola wako kuwa asiabudiwe (yeyote) isipokuwa Yeye (tu) na wazazi watendewe wema, kama mmoja wao amefikia uzee (naye yuko) pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata aah! Wala usiwakemee, na useme nao kwa msemo wa heshima}}  

Hali Ya Mama Na Watoto Wake Katika Maafa Ya Moto  
Anahadithia mmoja wa askari wanaofanya kazi katika kitengo cha ulinzi wa mji (zimamoto) akasema: "Hakika wao walifika katika nyumba moja inayowaka moto na ndani yake alikuwepo mama mmoja na watoto wake watatu. Moto ulianzia katika moja ya vyumba (vya nyumba ile) akajaribu yule mama kutoka kupitia milangoni lakini akakuta milango (yote) imefungwa. Akapanda haraka pamoja na watoto wake watatu mpaka sehemu ya juu ya nyumba ili atokee kupitia mlango huo, akaukuta umefungwa vile vile. Akajaribu kila njia bila mafanikio, akarudia rudia mpaka akachoka. Moshi nao ukapaa na kuenea nyumba nzima, wakawa wanahema kwa taabu. Mama akaamua kuwakumbatia watoto wake akawakumbatia kifuani mwake, na hali ya kuwa chini ili usije ukawafikia moshi mzito. Na mama wa huruma anauvuta moshi huo yeye (lakini si wanae). Baada ya kufika vikundi vya uokozi juu ya nyumba wakamkuta amedondoka (amelalia) tumbo lake, wakamyanyua mara wakawaona watoto wake watatu chini yake wakiwa maiti!!. Kama vile ndege anayewafunika mbawa vifaranga vyake akiwaepusha na hatari. Akiwakinga na adui mvunjaji. Wakakuta ncha za vidole vya mkono wake vimevunjika, kwani alikuwa mara akijaribu kufungua mlango, kisha anarudi kwa watoto wake ili kuwakinga na muwako wa moto na mpalio wa moshi kwa mara nyingine, mpaka akafa na watoto wake wakafa!
Katika picha inayopamba uzuri wa kujitoa muhanga, katika ubao uliohifadhiwa kwa rangi za huruma na kunakishiwa na unyoya wa upole na huruma. Pamoja na kujitolea na juhudi zote hizi na aina mbalimbali za kuhifadhi na ulinzi ambao mama anautoa kwa mwanae na kwa kipande cha ini lake, mpaka akasema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kubainisha ukubwa wa haki ya mama pamoja na baba: ((Mtoto hawezi kumlipa mzazi wake kwa wema aliomtendea isipokuwa, amkute akiwa mtumwa na kumnunua kisha amwache huru)). [Ameisimulia Imaam Muslim].
Pamoja na mapenzi yote haya yenye kububujika na upole mwingi na huruma yenye kuchupa tunasikia na tunaona aina mbalimbali za ugomvi na ukanaji wa wema, na ususuwavu wa moyo wa kushangaza, na ukali wa kutisha, na ubaya wa matendo, na ubaya wa kuamiliana (na wazazi) kiasi cha kutokuingia akilini (akili yoyote) wala kubebwa na moyo wowote (kuvumiliwa).

Barua Ya Mama Kwa Mwanawe
Hebu soma hii barua iliyoandikwa kwa wino wa machozi kutoka kwa mmoja wa akina mama. 
Barua yenyewe hii hapa aliyoiandika Mama mmoja kwa wino wa machozi yake. Barua ameituma "Mama Makluumah" kwa kijana wake ambaye ni kama manukato ya moyo wake, maskini yule mama anasema: 
"Ewe kijana wangu, tangu miaka ishirini na tano (iliyopita) ilikuwa ni siku yenye mwanga katika maisha yangu pale aliponifahamisha Daktari wa kike kwamba mimi ni mja mzito. Na akina mama ewe mwanangu, wanajua vizuri maana ya hili neno (uja uzito) nalo linaleta maana ya kuchanganyika na furaha na ni mwanzo wa matatizo na mabadiliko ya kinafsi na ya kimwili kwa mama na baada ya ishara hii ya kuwa mja mzito ewe mwanangu-nikakubeba miezi tisa tumboni mwangu kwa furaha, (nilitaka kusimama) nasimama kwa taabu na ninalala kwa shida, na ninakula udongo, na ninapumua kwa uchungu, lakini yote hayo hayakunipunguzia mapenzi yangu kwako na furaha yangu kwako, bali yakamea mapenzi ya kukupenda kadri siku zinavyosonga mbele.
Na ikakuwa shauku kwako. Nimekubeba ewe mwanangu juu ya uchungu, isipokuwa mimi pamoja na yote hayo nilikuwa nikifurahi na kufurahi kila ninapohisi kutingishika kwako ndani ya tumbo langu, na ninafurahi kwa kuongezeka uzito wako pamoja na kwamba ni mzigo mzito sana kwangu, hakika yalikuwa ni mateso ya muda mrefu, mara ikafika baada ya hayo yote Alfajiri ya usiku ule ambao sikulala ndani yake, na wala sikufumba jicho, na ukanikuta uchungu na shida na hofu na woga ambao kalamu haiwezi kuandika (kusifia) wala ulimi kuelezea, na nikaona kwa mboni ya jicho langu- namuapa Allaah ewe mwanangu nikayaona mauti yakinijia mara nyingi, mpaka ukawa umetokea duniani! Yakachanganyika machozi ya kilio chako na machozi ya furaha yangu. Na yakaondoka machungu yangu yote na majeraha yake. Ewe mwanangu, ikipita miaka katika umri wangu nikiwa nakubeba, moyoni mwangu na ninakuosha kwa mkono wangu, nikajaalia mapaja yangu kuwa kitanda chako. Na kifua changu kuwa ni chakula chako, nimekesha usiku wangu ili ulale, nimetaabika mchana wangu ili uwe muungwana, utukuke, matamanio yangu ni kuona tabasamu lako, na furaha yangu kila wakati ni kukuona unanitaka nikufanyie kitu chochote. Huo ndio mwisho wa utukufu wangu. Siku zikapita na mausiku yakapita nami nikawa katika hali hiyo, nikawa mtumishi bila kupunguza utumishi wangu. Na nikawa mnyonyeshaji asiyesimamisha huduma yake. Na nikawa mfanyakazi asiyechoka, mpaka ikakomaa miguu yako  na kulingana sasa ujana wako, na zikaanza kuonekana kwako alama za kiume, mara nikaanza kwenda mbio kulia na kushoto ili kukutafutia mke umtakae, ukafika muda wa ndoa yako, moyo wangu ukakatika na yakatirizika machozi yangu kwa furaha kwa ajili ya maisha yako mapya yenye utukufu, na nikawa mwenye huzuni kwa kutengana na wewe. Yakapita masaa mazito, mara wewe sio yule mwanangu niliyemjua. Hakika umenikana na umejisahaulisha haki zangu, yanapita masiku sikuoni na wala sisikii sauti yako, umeshindwa kumuelewa mtu aliyesimama kidete kwa ajili yako, umemsahau Mama yako.
Ewe mwanangu sihitaji kwako ila kitu kidogo tu. Nifanye mimi ni katika marafiki zako na machoni kwako, na wengine wasogeze hatua moja mbele yako. 
Nifanye Mimi ewe mwanangu, ni moja ya vituo vya maisha yako ya mwezi ili nikuone humo japo kwa dakika chache. Ewe mwanangu, mgongo wangu umepinda, na viungo vyangu vimedhoofika, na maradhi yamenikondesha, na yamenitembelea maradhi, sisimami ila kwa taabu, na sikai ila kwa mashaka, na haukuacha moyo wangu ukizingazinga kwa mapenzi yako, kama angekukirimu mtu yeyote siku moja ungemsifu kwa kitendo chake kizuri alichokufanyia. Na ewe mwanangu Akulinde Mola wangu, mama amekufanyia wema (ihsani) ambayo huioni, na wema ambao hutaki kuulipia; hakika amekutumikia na kulisimamia jambo lako miaka na miaka, basi yako wapi malipo yake?! Umefikia upeo huu na kuwa na moyo mgumu kiasi hiki, na masiku yakakuzuia kiasi hiki kuja kuniona?!
Ewe mwanangu, kila nikifahamu kwamba wewe ni Muungwana katika maisha yako, furaha yangu huzidi, lakini naona ajabu na hali yakuwa wewe ni bidhaa iliyotengenezwa na mkono wangu, na kujiuliza ni kosa gani nimelifanya mpaka nimekuwa adui yako huwezi kuniona na kuwa mzito kwangu?!
Siwezi kupelekea mashtaka yako kwa Allaah, wala huzuni zangu kwa sababu nikiyapeleka juu ya mawingu na kuyakokota mpaka katika mlango wa mbingu, utapatwa na shari ya kugombana na wazazi, na adhabu itakuteremkia, na utashuka nyumbani kuwa kipande cha ini langu na manukato ya maisha yangu na furaha ya dunia yangu.
Zinduka ewe mwanangu, mvi zimeanza kuenea kichwani mwako, na itapita miaka kisha utakuwa baba mzee, na malipo yanategemea matendo, utakuja andika barua nyingi kwa mtoto wako, kwa wino wa machozi kama nilivyokuandikia mimi barua hii. Na kwa Allaah watakusanyika wagomvi wote ewe mwanangu, mche Allaah kwa Mama yako, mfutie machozi yake, na mpungizie huzuni yake, ukitaka baada ya hapo chana barua yake, na elewa ya kwamba yeyote mwenye kutenda wema, ni kwa ajili ya manufaa ya nafsi yake na mwenye kufanya ubaya ni kwa madhara yake mwenyewe.
(Imetokana na khutbah ya Maazin At-Tuwayjiriy amesema; "nilimuuliza Al-Hasan Al Baswriy: "Ni ipi dua (maombi) ya mzazi kwa mwanae? Akasema Al-Hasan "Ni kuokoka" akasema, nikamuliza tena na kwake (kwa mzazi)? Akasema: "Kuangamia kwake (Yaani mzazi humuombea mwanae kuokoka na kila balaa, lakini mtoto humuombea mzazi wake afe haraka ili apumzike na kero zake)!

Haki Za Mama Yako Anazodai Kwako
Hakika haki za mama kwa  mtoto ni kubwa mno, usimuite kwa jina lake, bali muite kwa jina analolipenda au kun-yah (yaani 'mama fulani') usikae kabla yake, na wala usitembee mbele yake, kutana nae kwa uso mchangamfu, busu kichwa chake na shum mkono wake, na ukimnasihi basi ni kwa mema bila ubaya (usimuudhi) itika wito wake pindi akuitapo bila kumkemea au kumkirihisha. Zungumza naye kwa maneno laini, mlishe akiwa na njaa, au akitamani kitu japo utafika mbali katika kutafuta mletee, mpe zawadi kabla hajakuomba chochote, hisi anachokipenda umpe, kuwa mtumishi mtiifu kwake, mtii katika mambo ambayo si maasi, usimtanulie katika kula au kunywa, umfurahishe kwa kumuombea usiku na mchana rehema na msamaha, funga jicho lako kuhusu makosa yake na kuteleza kwake, usisikitike au kumhadithia makosa yake na kwa mtindo wa kumshtaki au kumshinda.
Muheshimu Mama yako na umkirimu, usimfanyie kibri wewe si chochote si lolote mbele yake kwani uliishi kati ya mapaja yake na mikono yake. Muingizie furaha, kaa naye kwa wema, taka dua kwake kwani milango ya mbingu hufunguliwa kwa ajili yake.

Mama Yako Baada Ya Kifo Chake
Ndugu yangu mpendwa, jua Akurehemu Allaah ya kwamba, hakika kuwatendea wama wazazi wawili hakuishi kwa kifo chao, kwani imepokelewa Hadiyth kutoka kwa Abu Usaydi As-Sa'adiy amesema: "Wakati sisi tuko mbele ya Mtume, mara ghafla akamjia mtu mmoja kutoka kwa Banu Salimah akasema: "Ewe Mtume wa Allaah, je, kumebakia chochote katika wema kwa wazazi wangu wa kuwafanyia baada ya kifo chao? Mtume akasema: ((Ndiyo! Ni kuwaombea rahma kwa Allaah na kuwaombea msamaha na kutekeleza ahadi zao baada yao, na kuunga undugu ambao hauungwi kwa wao, na kuwaheshimu marafiki zao))
Wema kwa wazazi wawili unaendelea katika kizazi cha mwanadamu na kinachofuata baada yake, imepokelewa kutoka kwa Ibn 'Umar, amesema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((wafanyieni wema wazazi wenu, nanyi watoto wenu nao watajiheshimu))
Vile vile wema kwa wazazi wawili unazidisha umri (Akipenda mwenyewe Allaah) kwani imepokewa kutoka kwa Sahal bin Mu'aadh, ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote atakayewatendea wema wazazi wake wawili, kheri nyingi sana ni zake yeye, Allaah Atamzidishia umri wake))
Tunamuomba Allaah Atusaidie kuwafanyia wema wazazi na kuwatii na kuwafanyia Ihsani wakiwa hai na wakiwa wamekufa, na asitufishe isipokuwa pale atakapokuwa Yu radhi na sisi, na tunamuomba Allaah Azishushe Rahma na Baraka na Amani Zake kwa Muhammad na kwa ahli zake na Maswahaba.

Tuesday, June 12, 2012

UMOJA

Sheria za Uislamu na adabu zake zinasimama juu ya msingi wa kumzingatia mtu mmoja mmoja kuwa ni sehemu isiyo tengeka na muundo wa jengo la umma. Na ni mwana familia anaye ungana na kiwiliwili cha umma, asiye pambanuka nao. Kwa hivyo basi yeye, atake asitake huchukua fungu/sehemu yake katika yale mafungu yanayo gawiwa kwenye kiwiliwili chote, kuanzia chakula, ukuaji na hisia. Na limeshakuja semezo la kimungu kulikiri weko hili, semezo ambalo halikumuelekea mtu mmoja peke yake kwa amri na makatazo. Na hakika si vinginevyo, semezo hilo limewagusa watu wote kama kundi na jamaa moja, kwa uadabishi na uongozi. Kisha katika darasa linalo tolewa kwa watu wote, mtu mmoja pia husikiliza na kunasihika. Kama hivyo ndivyo ulivyo fuatana ushereizi (uwekaji sheria) katika kitabu (Qur-ani) na Sunna (Hadithi).
“ENYI MLIO AMINI! RUKUUNI NA MSUJUDU, NA MUABUDUNI MOLA WENU MLEZI, NA TENDENI MEMA, ILI MFANIKIWE. NA FANYENI JUHUDI KWA AJILI YA ALLAH KAMA INAVYO STAHIKI JIHADI YAKE...”. [22:77-78]
Kwa hivyo basi, muislamu anapo simama mbele ya Allah ili amnong’oneze na kunyenyekea kwake, ibada hiyo haitapita ulimini kwake kama mja aliye pambanuka na ndugu zake. Bali ibada hiyo hupita ulimini mwake kama sehemu moja ya mkusanyiko ulio shikamana na kufungamana, husema: “WEWE TU TUNAKUABUDU, NA WEWE TU TUNAKUOMBA MSAADA”. [01:05] Na wala hasemi: Wewe tu ninakuabudu, na Wewe tu ninakuomba msaada.
Baada ya kuwajumuisha pamoja ndugu zake katika ibada yake binafsi, kisha ndipo humuomba Allah katika kheri zake na uwongofu wake, basi hajikhusu yeye tu kwa dua, bali hujitakia yeye rehema za Allah na watu wengine, ndipo husema: “TUONGOZE NJIA ILIYO NYOOKA, NJIA YA ULIO WANEEMESHA...”. [01:06-07]
Hakika Allah Atukukiaye hakuwaumba watu ili wapate kugawanyika na kutofautiana. Kwa yakini Yeye amewateremshia sharia ya dini moja na akawatuma mitume wake kwa kufuatana, ili wapate kuwaongoza watu wote kwenye njia moja. Na tangu azali amesha waharimishia kuifarakanisha dini na kutapanyika kuizunguka wakiwa makundi makundi yaliyo tengana. Pamoja na yote hayo ni kwamba matamanio maovu ya wanaadamu yamewasahaulisha wasiya huu mtukufu kutoka kwa Mola wao Mtukufu. Na yakawafanya waugeuze urithi huo wa kimungu, kwa ajili hiyo basi watu wakagawanyika makundi kwa makundi na kila kundi likawa linalipangia njama kundi jingine na kulingojea lifikwe na majanga.
Allah Ataadhamiaye amesema: “ENYI MITUME! KULENI VYAKULA VIZURI NA TENDENI MEMA. HAKIKA MIMI NI MJUZI WA MNAYO YATENDA. NA KWA YAKINI HUU UMMA WENU NI UMMA MMOJA, NA MIMI NI MOLA WENU MLEZI, BASI NICHENI MIMI. LAKINI WALIKATIANA JAMBO LAO MAPANDE MBALI MBALI. KILA KUNDI LIKIFURAHIA KWA WALIYO NAYO. BASI WAACHE KATIKA GHAFLA YAO KWA MUDA”. [23:51-54]
Allah Atukukiaye amebainisha ya kwamba kufuata matamanio, dhuluma, hasadi na uadui, ndio siri ya mfarakano mkubwa uliopo baina ya watu. Na lililo la haki kusemwa, ni kwamba pale elimu inapo kosa akhlaaq (tabia) na ikatengwa na ikhlaasi, elimu hiyo huwa ni balaa na janga kwa mdau wake (aliyo nayo) na kwa watu wengine pia. Watu kabla ya kujiwa na dini, walikuwa wakipotezwa na ujaahili kwenye vijia vyake finyu vihemezavyo. Na pale ilipo kuja dini na viongozi wake wakaifanyia ukiritimba na kuihodhi kama mali yao, na kisha wakazifanyia biashara elimu zake kwa ajili ya manufaa na tamaa zao, hapo ndipo makundi ya watu awaami yalipo potea na kwenda hovyo kwenye njia za dhuluma. Na Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alikuwa akimuomba Allah amuhifadhi na elimu isiyo na manufaa, na akasema: “Hakika yule nimcheleaye mno juu yenu baada ya mnafiki, ni mtu mjuzi mno wa ulimi”. Al-Bazzaar-Allah amrehemu.
Naam, ni kweli, hakika moyo gofu huifanya elimu kuwa ndio silaha ya kufanyia ufisadi/uharibifu. Na ulimwengu wa zamani na huu wa sasa umepatwa na matatizo mengi kutokana na elimu damirishi (hilikishi) hii. Na Allah Ataadhamiaye ametuambia ya kwamba wale walio wanachuoni (maulamaa) kwa ndimi zao na si kwa nyoyo zao, hao ndio walio yaharibu na kuyavuruga mambo ya jamii ya wanaadamu. Allah Atukukiaye amesema: “AMEKUAMRISHENI DINI ILE ILE ALIYO MUUSIA NUHU NA TULIYO KUFUNULIA WEWE, NA TULIYO WAUSIA IBRAHIM NA MUSA NA ISA, KWAMBA SHIKENI DINI WALA MSIFARIKIANE KWAYO. NI MAGUMU KWA WASHIRIKINA HAYO UNAYO WAITIA . ALLAH HUMTEUA KWAKE AMTAKAYE, NA HUMWONGOA KWAKE AELEKEAYE”. Halafu akasema: “NA HAWAKUFARIKIANA ILA BAADA YA KUWAJIA ILIMU KWA SABABU YA HUSUDA ILIYO KUWA BAINA YAO...” [42:13-14]
Na akasema: “...NA WALA HAWAKUKHITALIFIANA ILA WALE WALIO PEWA KITABU HICHO BAADA YA KUWAFIKIA HOJA ZILIZO WAZI, KWA SABABU YA UHASIDI BAINA YAO...”. [02:213]
Ndugu msomaji wetu mwema-Allah akurehemu-hebu liangalie vurugu la elimu pale inapo kosa ikhlaasi kwa Allah na huruma kwa waja wa Allah, namna inavyo chochea mfarakano na kuyakata yale aliyo amrisha Allah kuungwa. Hakika ikhtilafu ya ufahamu na mgongano wa rai/mawazo/fikra, si jambo geni katika mlolongo wa maisha ya wanaadamu. Lakini ikhtilafu hiyo na mgongano huo usiwe ndio sababu halalishi ya watu kukatana pande na kuzozana. Lakini sababu ya mzozano inarejea kwenye kujiunga na vitenda kazi vingine vinavyo itumia fursa ya kugongana kwa mitazamo na fikra, ili kufikia malengo yaliyo jificha .
Na kutokea hapo ndipo utafutaji wa hakika (kweli halisia) ukageuka na kuwa ni aina ya inda (ukhalifu na ukataa haki), isiyo na mafungamano yoyote na elimu kabisa. Lau nia zingeli takasika katika kutafuta hakika na wataka hakika nao wakaja wakiwa mbali na kutafuta kuwashinda wengine, kupata umaarufu, uongozi na mali. Basi isingeli kuwepo mizozo na makindano yaliyo ijaza tarekh (historia) vunju na masaibu. Na tumemsha pata kuona mambo madogo madogo ya kipuuzi, yameleta khilafu kubwa na ikaenea, kwa sababu khilafu hiyo imekutana na manufaa ya kisiasa. Wakati ambapo khilafu imenywea katika mas-ala muhimu na zikaachwa nyajihi za uoni mambo zigote zipatakapo, kwa sababu natija ya khilafu hiyo ni ya maono matupu. Na khilafu itiayo mashaka hii ilipo kuwa ni chombo cha kuifisidi dini ya Allah na Dunia ya watu, Uislamu ukaizingatia ni sawa na mtu kujitoa Uislamuni na ni kufuru. Allah Ataadhamaiye amesema: “HAKIKA WALIO IGAWA DINI YAO NA WAKAWA MAKUNDI MAKUNDI, HUNA UKHUSIANO NAO WOWOTE. BILA YA SHAKA SHAURI YAO IKO KWA ALLAH; KISHA ATAWAAMBIA YALE WALIYO KUWA WAKIYATENDA”. [06:159]
Na Allah akawatahadharisha Waislamu dhidi ya kukhitalifiana katika dini na kurafikiana katika ufahamu wake, wakawa makundi yenye kuchinjana, na kulaaniana kwa walivyo fanya wale wa mwanzo: “WALA MSIWE KAMA WALE WALIO FARIKIANA NA KUKHITALIFIANA BAADA YA KUWAFIKIA HOJA ZILIZO WAZI. NA HAO NDIO WATAKAO KUWA NA ADHABU KUBWA. SIKU AMBAYO NYUSO ZITANAWIRI NA NYUSO ZITASAWIJIKA. AMA HAO AMBAO NYUSO ZAO ZITASAWIJIKA WATAAMBIWA: JE! MLIKUFURU BAADA YA KUAMINI KWENU? BASI ONJENI ADHABU KWA VILE MLIVYO KUWA MNAKUFURU. AMA WALE AMBAO NYUSO ZAO ZITANAWIRI WATAKUWA KATIKA REHEMA YA ALLAH. WAO HUMO WATADUMU”. [03:105-107]
Hakika kuzoeana kwa nyoyo na hisia, na kuwa moja malengo na njia, ni katika jumla ya mafundisho ya Uislamu na ni katika mambo lazima mno ya Waislamu wenye ikhlasi. Na wala hapana shaka kwamba kuungana kwa safu za Waumini na kuwa safu moja na kuwa na sauti moja, mawili hayo ndio nguzo imara/madhubuti ya kuubakisha umma wa Kiislamu na kudumu kwa dola yake na kufanikiwa kwa risala yake. Ijapo kuwa kalima ya tauhidi (LAA ILAAHA ILLAL-LAAH) ndio mlango wa Uislamu, hakika kuwa na sauti moja ndio siri ya kubakia kwake (hiyo tauhidi). Na ndio dhamana ya kwanza ili kukutana na Allah kwa uso umemetukao na kwa kitabu safi (cha amali za mja).

Monday, June 11, 2012

Ruqa (incantation), Talismans and Amulets


Narrated Abu Bashir Al-Ansari (May Allah be pleased with him):
He was in the company of Allah's Messenger (May the peace and blessing of Allah be upon
him) on one of his journeys, Allah's Messenger (May the peace and blessing of Allah be upon
him) sent a messenger ordering: "There shall not remain any necklace of bowstring or any other
kind of necklace round the necks of camels except it is cut off' (Al-Bukhari and Muslim)
Ibn Mas'ud (May Allah be pleased with him) narrated that he heard Allah's Messenger (May
the peace and blessing of Allah be upon him) saying:
"Ar-Ruqa, At-Tama'im and At-Tiwalah are all acts of Shirk (polytheism)," (Musnad Ahmad;
Abu Dawud)
At-Tama'im is the act of putting an amulet around the necks of children to save them from the
effects of evil eye! If the amulet contains the verses of the Qur'an or Allah's Names or Attributes
then it is allowed by some ancestors and disallowed by some. Ibn Mas'ud (May Allah be pleased
with him) was among those who disapproved it,
Ar-Ruqa or Al-Aza'im is the act of reciting incantations, charm etc. Those are allowed in
which there is no trace of Shirk (polytheism), Prophet Muhammad (May the peace and blessing of
Allah be upon him) has permitted it in case of being bitten by poisonous insects or disturbed
under the effect of an evil eye, At-Tiwalah (bewitchment) is something done by those who claim
they can cause a woman to be more beloved by her husband or vice-versa.
Abdullah bin Ukaim narrated the following Marfu’ Hadith:
"Whoever uses, attaches or wears a talisman to himself, will have that talisman put in charge
of him" (Ahmad & Trimidhi)
Ahmad reported the tradition of Ruwaifi' (May Allah be pleased with him) who said that
Allah's Messenger (May the peace and blessing of Allah be upon him) said to him:
"O Ruwaifi', it may be that you will live a longer time after me, so inform people that
whoever ties a knot in his beard, places any string or cord around the neck (as a charm), or cleans
himself (after toilet) with animal dung or bone, then Muhammad (May the peace and blessing of
Allah be upon him) has disowned him (has nothing to do with him)."
Sa'id bin Jubair said:
"Whoever cut an amulet or talisman from anyone, it would be equal to liberating a slave."
It was Waki', who recorded it and he reported from Ibrahim Nakh'i that they used to dislike
every type of amulets and talismans whether that contained the verses of Qur'an or anything else,
[They were the companions of Abdullah bin Mas'ud (May Allah be pleased with him)
Important issues of the Chapter
1) Explanation of incantations (Ar-Ruqa) and amulets (At- Tama'im).
2) Explanation of bewitchment (At-Tiwalah).
3) That all the three above-mentioned are acts of Shirk without exception.
4) Reciting an incantation (Ruqyah), using words of truth, for seeking protection from evil eye or
scorpion bite is not like Shirk.
5) Ulama have different opinions about using the amulets containing the verses of Qur'an.
6) Putting on necklaces on animals against evil eye amounts to committing Shirk.
7) Anyone tying the bowstring (or committing such practices) has been warned of severe
punishment.
8) The reward of a person who cuts off an amulet of someone.
9) The statement of Ibrahim Nakh'i that early Muslims used to avoid amulets whether it contained
Qur'anic verses or anything else is not contradictory as the reference here is to the
companions of Abdullah bin Mas'ud (May Allah be pleased with him

Friday, June 8, 2012

Muungano wa Speed and Standard

Sasa kumepambazuka,mapabazuko mapya yanatarajiwa kutokeza katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sio jambo jengine ni lile linalozungumzwa kila siku la wananchi kutaka kuwepo kwa Muungano wenye kumaliza malalamiko ya miaka mingi. Watu hawataki kusema kweli, sijui wanaogopa kitu gani,lakini hakuna anayeweza kusimama mbele ya umma akisema kwamba wanaodai kuwepo kwa mabadiliko katika muundo wa Muungano ni watu wachache,ikiwa anaamini hivyo, anatakuwa anajidanganya nafsi yake.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Wilson Churchill aliweza kubashiri mabadiliko katika mataifa ya Afrika ambayo yalikuwa yakitawaliwa na wakoloni, waingereza wenzake hawakuamini kama ambavyo aliyekuwa Gavana kule Rhodesia ya Kusini (sasa Zimbabwe) Ian Smith.
Wakati ndio unaofanya watu kuwasukuma kwenye maamuzi, sio jambo jengine kwani mwaka 1970 au miaka ya mwishoni mwa 1980s mijadala ya Muungano haikuwa na nguvu kama hivi leo.
Vyama vingi vilirejeshwa tena katika mataifa mengi baada ya Uhuru mwaka 1992, wapo watu wakati ule waliapa katu hatutaweza kubadili mfumo wetu tuliouzoea tangu mwaka 1961 na 1964.
Miongoni mwa wazee wanaostahiki kupongeza ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyekubaliana na wanamageuzi kuhusu vyama vingi, asilimia 80 walikataa kubadili mfumo,lakini Chama cha CCM chini ya Uongozi wa Rais Ali Hassan Mwinyi ikapima na ikaamua kukubaliana na asilimia 20 ya Watanzania waliotaka mfumo ubadilike na kuwa wa vyama vingi.
Baadhi ya waliopinga vyama vingi mwaka 1992 ndio leo wapo viongozi katika vyama hivyo na wengine Wabunge na wenye nyadhifa kubwa kubwa ndani ya vyama vyao,lakini walikula viapo vya kinafiki kupinga na kuwabeza wanaotaka mabadiliko wanamageuzi ya kweli.
Siku zote wanamageuzi ya kweli hawayumbi, wanakuwa wanaamini na wako tayari kutetea msimamo wao, sio kama popo ambaye anaweza kwenda kwenye vikao vya ndege na pia vikao vya wanyama anaweza kushiriki, wanasiasa wa aina hii hawanaweza kupata mafanikio katika medani za siasa kama alizopata Mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini.
Kuwepo kwa vuguvugu la kutaka mabadiliko hasa Zanzibar ni matokeo ya muda mrefu ya kuchelewa kushughulikia kero za Muungano ambazo zimeundiwa kamati hizi na zile,lakini kasi yake haikuwa kama ile ya Mzee wa Speed and Standard katika Bunge lililopita chini ya Samuel Sitta.
Muungano unahitajika na kila mtu na ukisikiliza hoja za wanaotaka mabadiliko hawakupeleki katika hatua ya kuvunja, wanachotaka ni kuwepo kwa Muungano wenye kukidhi mahitaji ya leo,kesho na miaka hamsini baadaye ambao kizazi cha wakati huo baada yetu nacho kinaweza ama kuufanyia marekebisho au wakaamua kuendelea na mfumo uliopo baada ya kujiridhisha na mahitaji yao ya wakati huo.
Ule usemi wa Mji wa Roma haukujengwa siki moja, unaweza kufaa sana kwa mazingira ya Muungano wetu, ambao hatutaujenga kwa siku moja chini ya katiba mpya, unaweza kufanyiwa marekebisho kila panapohitajika maana Muungano huu haukuumbwa na Mwenyezi Mungu,umebuniwa na binadamu na bila shaka kutakuwa na upungufu wa hapa na pale.
Kwa mfano, kwanini wafanyakazi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliopo Zanzibar makato yao yatokanayo na kodi yasibaki Zanzibar na badala yake yanaingia katika mfuko mkuu wa hazina ya Tanzania!
Kwanini gesi asilia ni jambo la Muungano mbona Zanzibar hainufaiki na mapato yanatokanayo na rasilimali hiyo? Ndio maana SMZ ikaamua kuyaondoa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano kupitia uamuzi wa wananchi katika Baraza la Wawakilishi.
Ukiacha kero hiyo, kuna nile ya watumishi wa Zanzíbar katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukianzia Mabalozi, Mafias Kibalozi na sehemu nyengine katika utumishi wa SMT bado ni tatizo, hakuna usawa katika zile Wiraza za Muungano.
Zanzíbar kwa maumbile yake kijiografia kama nchi ya kisiwa inamahitaji maalum ya kuzingatiwa kama ilivyo kwa nchi zinazofafana nazo ambazo sio kwamba zinalindwa Kimataifa,lakini inatizamwa kwa jicho la huruma na hasa suala zima la mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko la watu.
Dunia ya leo ni ya majadiliano, sio ya ubabe kwani matokeo ya ubabe au kudharau mambo ndio yaliyowakuta katika mataifa mengine ambayo badala ya kuziba ufa yamejenga ukuta, Tanzania ni nchi ya kideokrasia na bila shaka itakuwa tulivu kusikiliza raia wake wanataka nini na kwa namna ipi.
Kisa kimoja kilitokea kule Malaysia kwa watu wawili ambao ni majirani kwa miaka mingi wakiishi mtaa mmoja na nyumba zao kukaribiana sana kama zile za mitaa ya kwetu.
Mzozo wa tofauti yao ulidumu kwa muda wa miaka mitatu waliamua kukubaliana kumaliza tofauti zao kwa kutia sahihi makubaliano ya ushirikiano wa ujirani mwema maana wahenga wanasema hálahala jirani.
Kutokuelewana kwa majirani hao kumeripotiwa na Shirila la habari la uingereza, Reuters ambalo limesema kwamba majirani hao wanaoishi katika jimbo la kusini la Johor Malaysia umedumu kwa miaka mitatu, na hata polisi walishindwa kuusuluhisha.
Gazeti moja la Star limeelezea sakata la ugomvi huo ni mbwa waliokuwa wakipiga kelele, na jirani mwingine kujibu mashambulizi kwa kufungua muziki kwa sauti ya juu katika radio yake.
Hata hivyo baada ya miaka mitatu ya mzozo uliokuwa ni pamoja na kurushiana taka na hata kugonga mageti kwa kutumia magari yao, majirani hao waliamua kutia saini makubaliano ya maelewano kumaliza kero zilizokuwa zikiwakorofisha.
Kwa hivyo katika dunia hii lazima kutakuwa na tofauti ama ya fikra, hulka na mahitaji, ndio maana wengi wanazungumzia sasa kuwepo kwa mfumo wa muundo wa Muungano unaofafana na ule wa Muungano wa nchi za Ulaya.
Ukizungumza na vijana, watu wa rika la kati na hata wazee wanaelezea msingi dhaifu uliojengwa wakati ukiasisiwa mwaka 1964, na kwa hali ya mambo inavyokwenda muundo wa Muungano unahitaji kutamwa na watazamaji wanapendekeza bila kuzunguka kwamba Muungano uwe imara ni kubadili muundo wake.
Wengine wanaweza kusema hata ukibadili kero zinakuwepo,mimi sitaki kuamini hivyo kwani sijapata kusikia Muungano wa Ulaya una kero hata kama zikiwepo basi ni zile ndogo ndogo sio kama hizi za hapa kwetu ambazo karibú Marais wote walioongoza Tanzania wamemaliza vipindi vyao vya uongozi na kuziacha hazijatatuka.
Ni lazima tukabili na tuende na wakati maana wakati ni ukuta, ukitupita hautakuja tena, tukijenga muundo madhubuti tutakuwa tumeijenga vema nyumba yetu hatutavujiwa na mvua za masika wala vuli.
Wapo wenye kufikiri na kubaki na msimamo kwamba Muungano utabaki wenye mfumo wa Serikali mbili kuelekea moja hatuwalaumu,lakini mbona wameachwa nyuma sana maana kasi ya sasa ni sawa ile iliyokuwa imeasisiwa na aliyekuwa Spika, Samuel Sitta, katika Bunge la “Speed and Standard” Muungano nao ni wa kasi na viwango,viwango vya Serikali moja havipo.
Waswahili wa pwani wanamsemo wao lipitalo ,hupishwa,pengine ningewashauri wale wenye ndoto ya kuwa na Serikali moja wakapisha majadala uendelee wa kuwa na mfumo wa Muungano wenye kutakiwa na wananchi.
Kwa kuwa mamlaka ya uendeshaji nchi ni ya wananchi wenyewe hatutegemei kutokea mtu akaanza kubeza mtazamo wa wananchi wenzake maana cheo ni dhana tu na tunatakiwa kutokitumia vibaya cheo kwa maana hiyo viongozi wakiwa na mawazo na misimamo yao inawapasa kupima kwa kipimo sahihi jamii inatakaje.
Sisi wengine tunaweka bayana mawazo yetu,wengine ndio wale wenye kusubiri fwataa kuingia jahazi la Nabii Nuhu wahenga wanatwambia heri karipio la rafiki, kuliko busu la mnafiki.
Katika mchakato wa katiba watazuka watu wenye kuyumba kimsimamo na kimantiki, ingawa hawatapata uungwaji mkono,lakini wataweza wenyewe kujionea hali itakavyokuwa wakati Tume ya Katiba itakapoanza kukusanya maoni kutoka kwa wananchi.

muungano huu unahitaji dawa mseto

Mandhari nzuri ya mji wa Zanzibar yenye kupendeza na kuwavutia watalii wengi kutoka nchi mbali mbali huharibika kwa muda mchache kutokana na vurugu zinazotokea iwapo vurugu hizo zitashindwa kuthibitiwa


Upepo mbaya ulivuma sio ule wa kimbunga, hapana huu ulikuwa ni upepo uliotaka kuyumbisha chombo chetu ili kienda mrama,lakini tumevuka salama katika mtihani tulioupata wa vurugu zilizotokea. Madai ya Wazanzibari ni madai ya miaka mingi tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano huu umeelzwa katika tafiti nyingi za wasomi na wasiokuwa wasomi kwamba muundo wake ndio wenye matatizo.
Kuwepo kwa fursa ya kutoa maoni katika Tume ya katiba ni jambo muhimu hasa kwa Wazanzibari ambao walikuwa na dukuduku la siku nyingi wakilalamika bila kusikilizwa maana wasilikizaji ndio wale wale wanaolalamiwa.
Wananchi walio wengi wamejizatiti kwenda kwa wingi wakati Tume itakapoanza kukusanya maoni, lakini kuna jambo ambalo linazungumzwa sana katika maeneo ya Unguja na Pemba kuhusu Zanzibar kupiga kura ya maoni kwanza kabla ya kuingia katika utoaji wa maoni ya katiba mpya.
Nilibahatika kuwasilikiza viongozi wa Uamsho katika mkutano wao waliofanya msikiti wa Mbuyuni Ijumaa iliyopita, walieza mambo kadhaa wa kadha,kubwa walilonishtua ni kuwa ikiwa maoni ya wananchi wa pande mbili hizi za Muungano yakitofautiana uamuzi utakuwaje?
Hili ni swali la msingi kabisa, Uamsho walisema ikiwa Wazanzibari kwa mfano wanataka Serikali moja, watu wa Tanzania Bara wao wanataka mbili au ikawa kinyume chake, maamuzi yatakuwavipi au Tume inapendekeza inavyoona inafaa?
Kwa kuondoa shaka hiyo, Sisi ndio maana tunashikilia kuwepo kwa kura ya maoni hapa Zanzibar kwanza kuwauliza Wazanzibari kuhusu Muungano” ndivyo alivyokuwa akieleza Kiongozi wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmed.
Je viongozi Zanzibar wanaogopa kitu gani kura ya maoni mbona imeshawahi kufanyika na sio jambo geni machoni mwao, wanahofu ya nini maana atafutwi mshindi katika hili.
Wanaotaka kura ya maoni wanataka kukijenga chombo chao kiwe madhubuti kwa uhakika wa safari wanayotaka kwenda katika maoni ya katiba mpya maana chombo kikitolewa chelezoni na kutiwa majini kitaweza kuhimili misukosuko ya bahari.
Au ndio kuna shinikizo la watu wanaotetea mfumo dhaifu wa Serikali mbili, wengine tuliwasikia zilipotokezea vurugu walitumia fursa hiyo kueleza mambo ya ovyo, wapo walijikweza kisiasa, wapo waliotafuta umaarufu,lakini pia wapo walioendeleza misimamo yao.
Sote tumesikia alivyoambiwa Waziri wa Katiba na Sheria,Abubakar Khamis Bakar ajiuzulu kwa kisa cha watu wanaodhaniwa kuwa Uamsho kufanya vurugu, hivi kuna uhusiano gani na Waziri huyo?
Waliofanya vurugu hawakutumwa na Serikali, wala kiongozi mwengine yoyote yule hivyi,sioni mantiki ya kumtaka Waziri huyu kujiuzulu au labda wanaomtaka ajiuzulu wanatatizo binafsi sawa,lakini katika vurugu zilizotokea hakuna wala sioni sababu ya yeye kuwajibika.
Pengine Rais wa Zanzíbar Dk. Ali Mohammed Shein akatofautiana na wanaotaka Waziri Abubakar ajiuzulu,akisema akaulizwe aliyesema hayo,lakini yeye hana la kueleza kwa maana nyengine Dk Shein haoni sababu ya kutakiwa Waziri wake kuachia ngazi.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, katika hili Waziri Abubakar kaonewa sana kwani hausiki na jambo lolote mbona wale vijana wenu waliposema wanazopesa za kununua nondo za kuwashambulia Uamsho hakuna kiongozi aliyetakiwa kujiuzulu kwa matamshi ya vijana wao kuchochea na kutaka kuvunja amani?
Ni lazima kuelewa kuwa matatizo ya kijamii hayawezi kutatuliwa na hisia za mtu mmoja tena aliyepitwa na wakati anayetumia Nokia ya tochi asiyeweza kuunganishwa na mitandao ya kijamii ya facebook, twitter ambaye anategemea mawasiliano ya mbiu ya mgambo au baragumu katika zama hizi za utandawazi.
Mara nyingi panapotokeza tatizo katika jamii basi sheria ambazo lengo kuu ni kupambana na wahusika, badala yake matatizo ya kijamii yatatatuliwa na sayansi au mfumo ulio sahihi utakao hakikisha haki ndiyo inayotawala katika jamii.
Kelele za kero za Muungano zimeshawachosha Wazanzibari kuzisikia maana kukosekana kwa mfumo sahihi wa muundo wa Muungano ndiko kunakosababisha leo tuanze kujadili upya suala la aina gani ya mfumo wa Muungano ulio muafaka na kwa ajili hiyo, Wazanzibari wengi wanataka Muungano wa mkataba.
Tunaelewa katika kipindi chote cha utawala wa CCM suala la Muungano limeonekana kama ni mwiko kulijadili, halizungumziki, woga umetawala, kumbe wamesahau kuwa wakati unabadilika, kizazi cha leo sio kile cha akina hewala bwana.
Ndio maana yamezuka makundi ya kijamii yanayopigania haki ya kujieleza na ile ya kuamua mambo watakavyo maana katiba ya Zanzibar inasema mamlaka ya uendeshaji wan chi yatakuwa kwa wananchi wenyewe vipi leo waonekane kituko wanapotaka mfumo wa muundo wa Muungano ubadilike?
Vijana hawana kazi, hawana bazi, wapo wapo tu hawana uhakika na wapi watapata chakula cha kutwa hivyo kunapojitokeza fursa kama hizi za madai ya haki hakuna atakayebaki nyuma na ndio maana jaribio la kuwaziba mdomo kuujadili Muungano ni gumu sana pengie ni rahisi Ngamia kupita kwenye tundu la sindano,kuliko Wazanzibari kukatazwa kujadili Muungano.
Leo Wazanzibari wengi wanaponea kuvaa mitumba kuanzia nguo za nje hadi nguo za ndani, chupi, sidiria, soksi na hafu, viatu, vyombo vya nyumbani hivi watu hao wakielezwa kuwa tukiwa na mfumo bora usiokuwa wa kubanana tutapumuwa kwa raha wasikubali?
Makero yamezidi kuota mapembe, hayatibiki kama zilizvyoshindwa zile dawa za kutibu malaria hadi yalipofanyika mabadiliko ya kukubali dawa mseto ya kutibu ugonjwa huo.
Muungano wetu unahitaji dawa mseto itakayokuwa tiba sahihi kwa kuwa na Muungano wa mkataba utakaowaacha Wazanzibari wapumuwe maana miaka 48 wamekuwa katika kitimkim cha kero zisizopatiwa ufumbuzi katika Muungano huu.
Ndio maana kila siku mfumo wa muundo wa Serikali mbili unavyopoteza umaarufu miongoni mwa Wazanzibari kwani watu wengine wanaweza kuanguao kilio, lakini kinachowasukuma kufanya yote hayo siyo ile hali ya roho zao kupenda mabadiliko, bali ni kule kuelemewa na matatizo ya kiuchumi ambayo kimsingi yamesababishwa na mfumo mbaya wa muundo wa Muungano uliodumu kwa miaka 48 sasa.
Kama Muungano ungekuwa wenye mfumo bora,hawa wanaolalamika wekiwemo Uamsho,wanasiasa na wanaharakati wasingekuwa na sababu ya kufanya hivyo, mbona hawalalamiki katika mambo mengine ambayo yamewekewa misingi imara?
Tanzania ilipinga kuharakishwa kwa Shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki kwa madai bado kuna mambo katika Jumuiya yenyewe ya EAC yanayohitajika kuwekwa sawa kama suala la ardhi, ajira na mambo mengine.
Maelezo ya Tanzania ni kwamba ardhi lisiwe katika orodha ya mambo ya Shirikisho la Afrika Mashariki kwa maana nyengine wasiwasi wa Watanzania ni mfumo wa Shirikisho hilo, sasa kwanini Wazanzibari wanapokuwa na wasiwasi na muundo wa Muungano wachukuliwe kuwa ni wakorofi?
Lakini pia kuna mambo mengi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye utata, kuna mambo ambayo si ya Muungano,lakini yamejumuishwa katika EAC je uwakilishi wa Zanzíbar utakuwaje?
Mambo ya kilimo,afya, vijana, utamaduni nikiyataja kwa uchache haya kila upande una mamlaka yake ya uendeshaji kwa msingi huo kutakuwa na mgongano wa maslahi maana idadi ya wajumbe inakuwa sawa,Tanzania haiwezi kupeleka kwa mfano Mawaziri wawili wa Kilimo au wa Afya.
Kama kutakuwa na muundo wa Muungano kama ule wa Umoja wa Ulaya ambao unaruhusu kila nchi kuwa na mamlaka yake, Muungano huu utakuwa wenye nguvu katika ukanda wa maziwa makuu.

Wednesday, June 6, 2012

muhadhara wafanyika kwa amani


Wazanzibari wakiwasikiliza viongozi wa uamsho (hawapo pichani) katika mhadhara uliofanyika leo jioni katika msikiti wa Mbuyuni baada ya jeshi la polisi kupiga marufuku kufanyika mhadhara katika viwanja vya Lumumba ambapo ulinzi mkali uliimarishwa katika viwanja hivyo.
Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) jana imefanikiwa kufanya mhadhara wake katika viwanja vya Malindi katika hali ya amani kabisa. Mhadhara huo awali ulipangwa kufanyika katika viwanja vya shule ya Lumumba lakini jeshi la polisi lilipiga marufuku na kutaka wananchi kutoshiriki katika mhadhara huo kutokana na hali ya kiuslama.
Viwanja vyote vya Lumumba jana vilionekana vimezingizwa na ulinzi mkali tokea majira ya saa sita mchana huku magari ya polisi wa kutuliza ghasya FFU wakizunguka zunguka katika maeneo yote ya mji wa Zanzibar.
Mwananchi ilishuhudia vijana mbali mbali wakiwa kando ya uwanja wa Lumumba na wengine kujibanza vipembeni wakisubiri kuingia uwanjani lakini kutokana na hali ya ulinzi kuimarishwa wananchi hao walishindwa kusogea na walikaa umbali mkubwa wa uwanja huo.
“Ulinzi naona sio wa kawaida na inaonesha hawataki watu hata kusogea umbali wa mita mia mbili, si mnaona mabunduki yake yalivyosimamishwa? Kila mmoja amebeba bunduki yake wamefunga kabisa uwanja” alisema kijana mmoja ambaye alikuwa amekaa kusubiri kuingia uwanjani.
Maelefu ya waumini walihudhuria katika viwanja vya Malindi katika manispaa ya mji wa Zanzibar ambapo viongozi wa jumuiya hiyo walikutana na kukaa msikitini na kuanza kwa sala ya alaasiri na baadae kuanza mhadhara ambapo awali baadhi ya watu walikuwa wakiogopa kusogea katika ameneo ya msikiti huo kutokana na ulinzi mkali kuka kando ya barabara zote za darajani, malindi na barabara ya kuendea Bwawani.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamishana wa polisi Mussa Ali Musa alisema mhadhara wa Lumumba haukuweza kufanyika kwa kuwa jeshi la polisi lilitekeleza amri ya serikali ya kutoruhusu mihadhara na mikusanyiko katika kipindi hiki.
Lakini alisema kufanyika kwa mhadhara huo katika viwanja vya Malindi wanahesabu kwamba bado hapo ni maeneo ya msikiti na hivyo hawajakataza watu kuendelea na shughuli zao za kidini iwapo watadumisha amani na usalama wa nchi.
Akizungumza katika mhadhara huo Sheikh Farid Hadi Ahmed amesema jumuiya na taasisi za kidini zitaendelea kufanya mihadhara yake na wataendelea kudumisha amani kwa kuwa lengo lao ni kutoa sauti yao ambao wanadai Zanzibar huru yenye mamlaka kamili.
Sheikh Farid alitoa pongezi wa jeshi la polisi na kamishna Mussa kwa kufahamu lengo la jumuiya hizo na kueleweshana namna ya kudumisha amani na utulivu hasa katika kipindi hiki ambacho wananchi wa Zanzibar wamegawanyika kutokana na misingi yao ya kivyama.
“Sisi bado tunahitaji kupata utulivu, amani na umoja na hivyo tunapaswa kuwa makini na watu ambao wamekusudia kutugawa lakini tuwe macho na watu kama hao” alitahadharisha Sheikh Farid.
Kwa upande wake Kiongozi wa Uamsho Sheikh Mselem Ally alisema wazanzibari wanadai Zanzibar yao na hivyo hakuna kitu ambacho kitawarejesha nyuma katika madai hayo hadi hapo watakapopata haki yao lakini wataendelea kudai mpaka mwisho wa nguvu zao.
“Sisi madai yetu ni kutaka Zanzibar yetu yenye hadhi na mamlaka kamili kwa hivyo haya yanayotokea ni lazima tuwe na busara na tuwe na subira katika kudai haki yetu lakini tutaendelea kudai mpaka mwisho” alisisitiza Sheikh Msellem.
Sheikh Msellem alisema wazanzibari baada ya kutenganishwa kwa miaka kadhaa sasa wanatakiwa kujua wanachodai ndnai ya muungano na wasikubali kabisa kugaiwa kwa misingi ya kivyama kwani kumekuwepo na kitendo cha makusudi cha kuwagawa waumini wa kiislamu.
Azzan Khalid Hamad ambaye alikuwa nje ya nchi kwa matibabu alisema wazanzibari wamegawanywa kiwa muda mrefu na katika hili ilitokea khitilafu na baadhi na watu kuchukua nafasi ya kutaka kuwagawa tena jambo ambalo alisema wameweza kulirekebisha.
“Wakati wenzetu watanganyika wanaendeleza nchi yao sisi tunagombanishwa lakini tunasema kwa sasa hamtugawi tena na tumeshawafahamu “ alisema na kusisitiza suala la umoja na mshikamano kati ya serikali na taasisi hizo za kidini.
Alisema taasisi hizo zina imani kubwa sana na Rais wao Dk Shein na Rais Kikwete lakini wanaamini kwamba kauli walizotoa wamezitoa kutokana na kupotoshwa na watendaji wao lakini wakaahidi kuwa na mashirikiano mema na viongozi wao kwani nia ni kuweka amani na utulivu katika nchi.
Jeshi la polisi lilionekana likiranda randa katika eneo la darajani, michenzani, na barabara za viwanja vya Malindi ili kudhibiti iwapo kutatokea vurugu lolote, lakini hata hivyo mhadhara umemalizika kwa salama bila ya kutokea fujo na wananchi wameondoka katika viwanja hivyo kwa usalama wakati jeshi hilo likiwa kando mno na wananchi waliokusanyika.

Tuesday, June 5, 2012

sheikh saad el ghamidi




Saad El Ghamidi is a Saudian reciter born in 1968 in the Oriental, Saudi Arabia.
Saad El Ghamidi studied in Dammam. As a student, Saad was very active. He often participated in summer journeys, Qur'an Memorization circles, associations. He graduated from the University of Chariîa with a religious studies Degree (Oussoul Din). In 1990, he memorized the whole Qur'an and was distinguished by his soulful voice as a recite.
In 1985, he chose a Monchid (religious singer) career. His first tracks were very successful and earned him a wide recognition such as "Malakna Hadihi Donya Qorounan" and "Gharbane".
Saad El Ghamidi cute his way to recognition as an Imam during Tarawih's prayers in the holy mosque. He later released a first record which met a considerable success. Saad El Ghamidi had a degree in Al Isnad on the recitation of Hafs by Assem.
Saad El Ghamidi has toured many Arab countries such as Koweit and others like Austria, USA and GB.

sheikh ahmed ali al amji

Ahmed Ali Al Ajmi is a Qur'an reciter and a chanter from Khobar, an eastern Province of the Kingdom of Saudi Arabia. He was born February 24, 1968.
After graduating from Mohamed Ben Saud Islamic University, Ahmed Al Ajmi flew to Pakistan where he enrolled in Lahore Public University to prepare a Master and then a Doctorate in Qur’an Interpretation. His thesis was entitled “Minnat Al Aliy Al Kabir Fi Charh Toroq Attafsir” (a study of interpretation means).
Cheikh Ahmed Ajmi is one of the most outstanding reciters in the world. He is currently leading prayers Jeddah’s Holy Mosque.
Other than his recitations’ discography, Ahmed Ali Ajmi has released many religious songs which had some great success. Among his best known nasheeds : “Allaho Akbar”, “Qalo Hazent” and “Ghurabaa”. Ahmed Al Ajmi is married and has six childrens: Abullah, Omar, Fatima, Mariem, Modi and Abdurahmane. Ahmed Ajmi is living with his family in Alorqobia, Khobar (Saudi Arabia).

Sunday, June 3, 2012

uamsho wasisitiza muuhadhara kesho

(b). Kauli iliyotolewa na Mheshimiwa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh Doctor Ali Mohd Sheini kwa waandishi wa habari siku ya tarekhe 31/05/2012 ikulu mjini Zanzibar haikusimama katika kuzuiya Mihadhara, Makongamano wala Mikusanyiko ya aina yoyote bali ilisimama katika kulinda na kudumusha amani, tunampongeza Mh Raisi kwa hilo na hilo kwa kuwa amelitambua wazi ndilo lengo pamoja na dhamira ya Jumuiya yetu.
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR
Afisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mjini/Magharibi,
Sanduku la Posts 237
Zanzibar.
KUH: KUZUILIWA KUFANYA MHADHARA WA AMANI KATIKA VIWANJA VYA LUMUMBA NA JESHI LAKO LA POLISI
Tafadhali rejea barua yako yenye kumb:RPHQ/MJN/58/VOL.V/59 ya tarekh 01, JUNE, 2012 ambayo ina kichwa cha maneno kuhusu Taarifa ya Mhadhara.
Jumuiya yangu imesikitishwa saana na hatua yako pamoja na Jeshi lako la Polisi ya kutuzuilia kufanya mhadhara wa amani ambao kwa mujibu wa Sheria za nchi ni haki yetu na imeonelea ikuandikie barua hii kwa kuwa sababu ulizozitoa za kuzuiya mhadhara huo si za msingi wala si za kisheria.
Baada ya kukaa pamoja na kujadili hoja ulizozitoa na zilizopelekea jeshi lako kutuzuilia kufanya mhadhara huo wa amani tumeonelea kukuomba wewe pamoja na jeshi lako la Polisi kuyazingatia mambo yafuatayo na tunaomba majibu rasmi juu ya hayo-:
(a). Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari pamoja na magazeti ya ndani ya nchi, aliyetoa amri ya kuzuiya kufanyika mihadhara, makongamano, maandamano pamoja na mikusanyiko ya aina yoyote ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi ndugu Mohammed Aboud ambaye kisheria hana nguvu juu ya hilo.
(b). Kauli iliyotolewa na Mheshimiwa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh Doctor Ali Mohd Sheini kwa waandishi wa habari siku ya tarekhe 31/05/2012 ikulu mjini Zanzibar haikusimama katika kuzuiya Mihadhara, Makongamano wala Mikusanyiko ya aina yoyote bali ilisimama katika kulinda na kudumusha amani, tunampongeza Mh Raisi kwa hilo na hilo kwa kuwa amelitambua wazi ndilo lengo pamoja na dhamira ya Jumuiya yetu.
(c). Barua yako uliyoitowa kwa Jumuiya yangu ya tarekh 01/06/2012 haisimami kunizuiliya kufanya na kuendelea na shughuli zangu za Mihadhara, Makongamano bali imesimama zaidi kunipa taaarifa juu ya Kauli ya Serikali ambayo kama nilivyokuelezea hapo juu imetolewa na mtu ambaye Kisheria hana nguvu za kufanya hivyo.
Kwa mantiki ya hoja nilizokuelezea hapo juu inaonekana wazi kuwa Jeshi lako la Polisi limeazimia kufanya uvunjifu wa amani pamoja na kufanya mauwaji kwa raia wasio na hatia, hii inatokana na kauli ya Jeshi lako katika barua uliyoniandikia ya kuwa jeshi lipo tayari kuzuiya kwa nguvu za aina zote mhadhara huo.
Napenda kukufahamisha kuwa kufanya mihadhara, makongamano pamoja na Maandamano ya Amani katika nchi yoyote ile inayofuata Demokrasia ya kweli ni kutii sheria na sio kuvunja sheria kama haya yanathibitishwa katika Katiba zote, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar, tafadhali rejea ibara ya 18 (a,b,c,d) na pia rejea ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia ibara ya 18(1) na 20(1).
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, Jumuiya yangu bado inayofursa ya kufanya Mihadhara pamoja na shughuli zake kwa kufuata Katiba ya nchi na kufuata katiba ya Jumuiya iliyoitunga, hii ni kwa sababu mpaka sasa haina ushahidi wowote wa Kimaandishi juu ya kuzuiliwa kufanya shughuli zake.
Kwa kuwa Jumuiya yangu ni Jumuiya yenye lengo la kulkuza na kudumisha amani katika nchi, viongozi wa Jumuiya wapo tayari kukaa chini pamoja na viongozi wakuu wa Jeshi lako la Polisi kulijadili suala hili na kulipatia ufumbuzi kabla ya madhara makubwa ya umwagaji wa damu ambayo yameazimiwa kufanywa na Jeshi lako la Polisi yasije kutokea.
Kumbuka ni wajibu wa Jeshi la Polisi wanatakiwa wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.
Polisi wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.
Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.
WABILLLAH TAWFIQ
Natanguliza Shukrani
…………………………
ABDALLAH SAID ALI.
KATIBU MKUU.
JUMIKI.
Nakala:
MUFTI MKUU ZANZIBAR
IGP – Tanzania
CP – Zanzibar
RPC – Mjini Magharibi
RCO – Mjini Magharibi
OC FFU Mjini Magharibi
RSO – Mjini Magharibi
DC – Mjini Unguja.
DSO – Mjini Unguja.
Balozi mdogo wa Marekani Nchini Zanzibar
Vyombo vyote vya Habar

25-26 may ,,,,,,, never forget that

Ni siku ambayo zanzibar haitosahaulika kwa yalio tokea,,,, barabara zlifungu kwa mawo na kuchomwa 
mtoto mipira ya gari,,,,,,, ni watu walio sababisha kutoke mambo  yale kwa shindikizo la watu binasfi ila kuipa sifa mbaya  jumuiya ya uamsho kutokana na  kitendo kilicho fanya na serekali kumkamata sheikh Mussa Juma
kuna baadhi ya  vyombo vya habari  vinasema kua uamsho ndio imefanya hivi  bali uamsho imekataa kitu  hicho na iwaseme kua ":hiki kikundi  kimetumwa  kwaajili ya kuichafulia jumuiya ya uamsho"


Saturday, June 2, 2012

soma annur


Sheikh Farid Hadi Ahmed akizungumza na waandishi wa habari leo nje ya msikiti wa Mbuyuni
Kwa taarifa mbali mbali tafadhali bonyeza hapa kusoma Gazeti lako la ANNUUR 115

Friday, June 1, 2012

ISLAM IN EAST AFRICA

Arabs had commercial ties with Africa. Muslims migrated to Habasha (Abyssinia) where An-Najashi (the Negus) was ruling, which formed the first steps of Islam into Africa. By the decline of the Umayyad caliphate some Umayyads fled to Andalusia while others fled to Eritrea where they spread Islam. By the same token, some Arabs belonging to the Qaramitah state migrated to Somalia where they established the city of Mogadishu and the City's ruling council. The city later turned into a sultanate and thus East Africa became a center of Islam and Islamic civilization.
After the decline of Andalusia, the European campaigns to re-discover the continent began to be active. They occupied the island of Zinjibar (Zanzibar) and later on the whole Muslim world came to be occupied by different European countries. Muslims thus started to struggle to gain independence. By then, Muhammad bin Abdullah Hassan, known as Al-Mulla, rose as a Somali figure who could restore independence for twenty years. In Mogadishu, the Youth League Party came into existence. Djibouti was then a part of Somalia which was occupied by France. In Ethiopia (Abyssinia), Islamic rule lasted for 400 years, after which the occupation handed authority to Christians. Later on, successive governments were keen to retain the Christian character of Abyssinia.
As for Eritrea, it was occupied by Abyssinians although it consists of a Muslim majority. Egypt withdrew from Eritrea being under the British occupation. It was later occupied by Italy, which annexed Eritrea to Abyssinia. Muslims then began to be persecuted and Christian missionary work got very active. As for Tanzania, it was ruled by Ottomans before it was occupied by Germany. In this regard, the Ottoman sultan seceded his possessions along the coast to the German Company. Zanzibar later gained independence and was annexed to Tanganyika. The two states united in 1964 to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, which later the same year was renamed the United Republic of Tanzania. Actually, Muslims there suffered severe persecution to the extent that Muslim girls would be forced to marry Christian men.
In fact, such countries consist of a majority of Muslims who face many obstacles. For example, missionary work is active there especially in Eritrea and Ethiopia as well as Mozambique. Another example is the prevalence of poverty and power conflict in such countries as Somalia. This is in addition to economical obstacles and non-exploitation of internal resources in such countries as the Comoros.
Kenya was occupied by Britain, which wished to end the usage of the Arabic language through having it written in Latin letters with the purpose of keeping Kenyans away from the Qur'an. Affected by reform movements that came on the scene in the Muslim world, Sheik Al-Amin Ali Al-Mazrawi issued many Islamic newspapers, schools and projects. As for Uganda, its official religion was Islam and its king would lead people in Salah. Khedive Isma'il of Egypt sent an officer to explore the Nile riverhead, which later resulted in annexing Uganda to Egypt to be known as the Equator governorate. This had a good impact on strengthening the roots of the Islamic creed among Ugandans. However, Britain, after occupying Uganda, banned Muslims from traveling to Uganda unless previously permitted. Uganda later gained independence to dispute with Tanzania.
As for Madagascar, Islam spread therein for a while. However, the French occupation encouraged missionary work and had Muslims to live in isolation and, therefore, many revolutions against the French were staged. Meanwhile, Muslims suffered a problem concerning education in general and religious education in particular.