Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, August 26, 2012

HICHI NDICHO NINACHOKIAMINI: WAZANZIBARI KUPINGA SENSA NI KUPANDIA AGENDA SI YAO, HAINA MASLAHI YOYOTE NA ZANZIBAR

Wapingaji wa sensa kwa upande wa Zanzibar ni miongoni mwa vinara waliounga mkono wazo la Maalim Seif na Amani karume kwamba tuwaunganishe watu, tusiwagawe tena watu, tuondoe chuki, visasi na mapambano miongoni mwetu. Mimi mawazo yao nayaheshimu lakini sitowacha kuangalia pande zote mbili za shilingi na kulichambua kwa umakini suala hili na kamwe sitafuata mkumbo.

Tuliwahi kukusanyika siku moja katika viwanja vya Maisara wazanzibari na na viongozi wa serikali yatu kumuomba Mungu atuzidishie nguvu umoja wetu na ailinde serikali yetu ya umoja wa kitaifa. Bila shaka kufanya lolote kwa lengo la kuikwaza serikali hii isifanye shughulki zake, hususan za kuwatumuikia watu ni kupingana na kile kilichofanyika siku hiyo. Na kwa lugha hii mwenye kupingana na anachokiamini kwa nini asiitwe MNAFIQ?

Wazanzibari hawakuwa na agenda ya kususia sensa hapo kabla. Baada ya kupigiwa debe agenda hiyo na waislamu kutoka Tanganyika, na UAMSHO nao wakaibeba agenda hiyo ili angalau kupata agenda mpya kwa kuwa ile ya muungano, wenyewe CUF ndio wanaoonekana kwenda nayo kwa taratibu zinazoeleweka na kwa muelekeo unaotoa matumaini makubwa.


Sababu za kususiwa sensa na waislamu wa Tanganyika ni kupingana na mfumo KRISTO kwa kuwa wanahisi kwa kutowekwa wazi  takwimu halisi za wakristo na waislamu, mfumo kristo utaendelea kuwakandamiza waislamu kwa visingizio wakristo ni wengi nchini kama zilivyowahi kudai baadhi ya  takwimu za kubuni.

Kwanza hatuna budi tufahamu kwamba waislamu wa Tanganyika hawana nia ya kweli ya kuwa na umoja na waislamu wenzao wa Zanzibar. Huko nyuma haikuwa hivyo na hata sasa haiku hivyo. Waislamu wa Tanganyika huonekana kutafuta uungwaji mkono kutoka Zanzibar pale wao tu wanapobanwa na sio pale wazanzibari nao wanapobanwa. Na kama hiyo haitoshi wao pia waislamu wa Tanganyika ndio washiriki wakuu wa maonevu ya wazanzibari.

Ni akina nani waliokuja kuwauwa wazanzibari wasio na hatia mwaka 1964? Si Peter wala Kurwa ni waislamu wenzetu ambao wakiingia misikini na kusali pamoja nasi. Sitaki nizungumze sana kuhusu hili kasome “kwaheri ukoloni, kwaheri uhuru, Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia”.

Wazanzibari walipita katika misukosuko mingi tokea miaka ya 1980, 1990, 2000, hadi mwaka 2009 walipoingia katika maridhiano. Katika kipindi chote hicho wazanzibari ambao ni waislamu  waliteswa, kupigwa, kudhalilishwa, kunajisiwa, kuuliwa, kutiwa ulemavu, kuachwa mayatima na vizuka, je taasisin hizi za waislamu wa Tanganyiak wanaotaka waungwe mkono kugomewa sensa walikuwa wapi? Mbona hawakuwahi kutoa matamko makali wala kususia chochote kuonyesha kuwaunga mkono waislamu wenzao wa Zanzibar wanaodhalilishwa na majeshi ya Mkapa wakati huo?  Jibu ni kwa kuwa hapakuwa na maslahi yao. Lakini kupinga sensa ya mwaka 2012 kuna haja muhimu kutetea maslahi yao.

Serikali haiwezi kufanya shughuli zake bila ya takwimu hizi ambazo zinachukuliwa kila baada ya miaka 10 tu. Pamoja na kwamba suala la takwimu ni la muungano lakini matumizi ya takwimu hizo yanaihusu  serikali yetu ya Zanzibar. Hivyo basi wazanzibari kususia sense si kuikwaza serikali ya Tangantika bali ni kuikwaza serikali yao wenyewe, inayosimamia mahitaji yao kwa gharama zake bila hata ya senti 5 kutoka Tanganyika.

Sensa ndio ilyotumika kupunguza majimbo ya CUF mwaka 2002 na kuongeza majimbo ya CCM. Kwa kuwa kasi ya mabadiliko imekuwa kubwa katika muungano CCM wanayo hamu kubwa watu kususia sensa ili wapate kupunguza nguvu za CUF Zanzibar ili iweze kuunusuru mfumo wa muungano wa serikali 2.  Wako wanaojidanganya kuwa hoja hii ina maslahi kwa CUF. Wakidhani hivyo sawa, ila ambAcho CUF inakifanya ni kwa maslahi ya Zanzibar. Hata kama ni kunusuru majimbo ya CUF yasije yakamegwa kwa kisingizio cha sensa ndio pia kunusuru na bunge la katiba lisije likawa na wingi wa wajumbe wa CCM na kufanikiwa kurejesha mfumo wa serikali 2.

Wanaokebehi CUF kwa kisingizio cha kukebehi siasa na kurukia eti dini ndio njia ya ukombozi katika mifumo hii tulio nayo dunianai ni kujidanganya mchana. Bado utaratibu wa kuweka dola, kushikilia dola na nguvu zake na hata utakaoiweka dola huru ya Zanzibar tunayoitamani hapo baadae  ni mfumo huu huu wa kisiasa. Hakuna utaratibu mwengine wowote. Kwa mwana CUF kuikejeli CUF na kuona NGO ya kidini ndio italeta dola huru ya Zanzibar si sahihi. Mimi sibezi taasisi za dini. Taasisi yeyote iliyo makini inaweza kutusukuma mbele zaidi katika njia yetu lakini pia taasisi yenye kupoteza muelekeo inaweza kuturejesha nyuma zaidi.

Mimi kwa ufahamu wangu agenda za kususia tume ya katiba zilizokuwepo kabla, kususia sensa na nyengine ambazo zitakuja mbeleni zenye lengo la kutukwaza ni mipango na mikakati inayosukwa kiufundi na idara ya usalama wa taifa na kutumbukizwa katika kila sekta ya maisha hapa Zanzibar ambamo CUF wamo  li kupambana na CUF bila ndugu zangu wafuasi wa UAMSHO kufahamu kuwa wanabeba agenda pachikizi. Usalama wa taifa wasiofahamika na raia katika CCM wamo, katika CUF wamejiingiza, katika jumuiya za kidini wamo na kwengineko pia wamo. Hawajulikani, wakifanya hili na lile kwa ufundi mkubwa huku wafuasi wetu wa CUF wakiwaona ni wenzao na hivyo kukaa nao na kupanga nao mambo ya kuwahujumu wenyewe.

Mimi binafsi nawambia watu waliobeba agenda za kisiasa kupita taasisi za dini angalau wangeshauriana na wanasiasa. Siasa wenyewe ni wanasiasa ndio wanaoona mbali katika siasa. Hata Maalim Seif aliziahidi taasisi zote kuwa milango yake yote iko wazi kwa mtu yeyote mwenye agenda yake kufika kwake kwa mashauriano ili kujenga umoja. Lakini bahati mbaya haya yote yanatendwa bila ya angalau kumfika na kumshauri Maalim. Kila mtu anajiona bingwa wa siasa. Siasa za CUF ni kuifikisha Zanzibar kuwa yenye mamlaka kamili, bila shaka ni taasisi hii ndio inayovifahamu mbinu, mikakati, njiavichochoro vya kuopitia kufikia huko. Wanaorukia ngoma si yao na si kwa lengo la kusaidia bali kutafuta njia yao wenyewe inayopingana na ile ya CUF tuanawatanabahisha bado ingali mapema. CCM na idara zake za kiusalama wapo na wanafanya kazi zao, si hasha kuwa wao ndio wanawapeleka watu upande ambao si sawa sawa.

Sisi wengine bado tunawaomba sana wenzetu wafikirie mara nyingi maamuzi yao kabla ya kutangamiza kabisa badala ya kutuokoa. “Wazanzibari kwa kuungana kwetu tutaweza kulifuikia kila jambo ambalo hapo kabla hatukuweza kulifikia kwa kugawika kwetu” Maalim Seif.

Haya ni mawazo yangu binafsi si ya chama changu.

ZECO Pemba yatumia 29m/= kununua transfoma, nguzo




Mafundi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) tawi la Pemba wakiwa katika harakati za kuwafungia transfoma wananchi wa kijiji cha Kichaka Shehia ya Mtangani Jimbo laKiwani Wilaya ya Mkoani Pemba , ambapo transfoma hiyo pamoja na nguzo 25 zimesgharimu zaidi ya shilingi 39 milion ambapo ni mchango wa wananchi zaidi ya shilingi 18 milion (picha na Haji Nassor, Pemba)

Na Haji Nassor, Pemba
ZAIDI ya shilingi 39 milion, zimetumiwa na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Tawi la Pemba, kwa ajili ya ununuzi wa trasfoma na nguzo 25, ambapo tayari jana trasfoma hiyo, imeshafungwa katika kijiji cha Kichaka Jimbo la Kiwani Wilaya ya Mkoani Pemba.
Kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi 18 milion, ni mchango wa wananchi na shilingi 20 milion na laki nane, zimetolewa na ZECO ili kukamilisha upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi zaidi ya 1000 wa eneo hilo.
Akizungumza mara baada ya kazi ya ufungaji wa transfoma hiyo, huko Kichaka Msaidizi Afisa Uhusiano wa ZECO Tawi la Pemba Faki Othuman Sharif, alisema kuwa shirika kwa sasa limekuwa na utamaduni wa kusaidiana gharama na wananchi, iwapo wanahitaji kuwekewa transfoma.

Faki alieleza kuwa, hilo linatokana na shirika kujipanga upya kwa sasa, ili kuwaletea huduma bora wananchi kwenye sekta ya umeme, katika miji na vijiji mbali mbali ili uweze kuwasaidia katika kuinua kipato chao.
Afisa huyo aliwaambia wanavijiji vya Kichaka juu, Kinyasini, Utaani, pamona na Nga’ambu kuhakikisha wanajiungia umeme kwa lengo la kujinasua na umasikini uliokithiri miongoni mwa jamii za kizanzibari.
‘’Leo tumekamilisha ile kiu yenu ya miaka zaidi ya 20 mliokuwa nayo ya kutaka huduma ya umeme, na leo tayari tumeshafunga transfoma mpya kwa kushirikiana na nyinyi, hivyo huduma hii iwe kwa ajili ya maendeleo yenu’’,alifafanua .
Katika hatua nyengine Msaidizi huyo Afisa Uhusiano wa ZECO Tawi la Pemba amewahakikisha wananchi wa vijiji hivyo kuwa, kabla ya wiki tatu shirika la umeme litasambaaza waya mdogo, ili kutoa fursa kwa wananchi kuvuta majumbani mwao.
Mapema wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kazi hiyo wananchi wa kijiji hicho na vyengine, walisema kuwa walisubiri huduma ya umeme tokea mwaka 1993 mara baada ya kuwekewa laini kubwa ya umeme.
Mohamed Omar Hamad (55) alisema kuwa hata hivyo ameliharakisha shirika la Umeme juu ya kuweka waya mdogo kijijini hapo, ili kila mwananchi mwenye uwezo aweze kuvuta badala ya kuwepo kwa transfoma kama pambo.
‘’Mje tena mtufungie waya mdogo, ili wenye uwezo wavute umeme na sisi tunywe juisi baridi kama mnavykunywa nyinyi huko mijini mtokeako’’,alifafanua na kusema kuwa iwapo watafungiwa waya huyo watavuta majumbani mwao.
Nae kijana Chande Khamis Rashid (28) aliwataka vijana wenzake kuanza kujipanga ili huduma hiyo ya umeme iwawezeshe kujiajiri ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo, saluni pamoja na maduka ya vinywaji baridi.
‘’Vijana wenzangu umeme sasa tayari maana tumeshawekewa trasfoma mpya sasa kilichobakia ni sisi tu ndio wakujipanga ili kuona huduma hii inatunufaisha kwa kuweza kujiajiri ‘’,alifafanua kijana huyo.
Kijiji cha Kichaka na vijiji jirani kwenye Jimbo la Kiwani Wilaya ya Mkoani, vilipitiwa na laini kubwa ya umeme tokea mwaka 1994 uliosambaaza na kampuni na NEREMKO bila ya kuwepo kwa transfoma, hadi mwaka huu walipoamua kuchangana fedha na kufungia mashine hiyo.
Shirika la umeme tawi la Pemba katika mwaka huu, tayari limeshafunga transfoma zaidi ya tano kwa vijiji kadhaa ikiwa ni pamoja na Msuka, Wambaa, Kichaka ambapo zoezi hilo hutokana na wananchi wenyewe kulisaidia gharama shirika la umeme

Saturday, August 25, 2012

UN kusaidia kunyanyua Uchumi wa Zanzibar

Balozi mpya wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tavaku Manongi amesema Uongozi wake utajitahidi kuangalia maeneo yanayoigusa Zanzibar moja kwa moja katika jitihada za kunyanyua Uchumi na kustawisha Maendeleo ya Jamii. 

 Balozi Tavaku akiambatana na Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi  alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Nyumbani kwake Mtaa wa Namanga Mjini Dar es salaam. 

 Alisema yapo masuala ambayo Zanzibar ina fursa ya kuyafanya na kuyafuatilia bila ya kuathiri yale maeneo ambayo hushughulikiwa moja kwa moja kwa mujibu wa taratibu za Kimuungano.

 Balozi Tavaku alisisitiza kwamba utendaji wake mara zote utazingatia zaidi Umoja na Ushirikiano kati yake, Watendaji atakaowaoongoza pamoja na Taasisi, Jumuiya na Nchi washirika. “ Nitahakikisha muda wangu pia nautumia katika kuangalia maeneo yanayoigusa Zanzibar kuyafanyia kazi katika muda wangu wote” Alisisitiza Balozi Tavaku. 

 Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza nguvu na msimamo wa Tanzania katika ushiriki wake kwenye Nyanja za Kimataifa. 

 Balozi huyo wa Tanzania Umoja wa Mataifa alimuomba Balozi Seif kuendelea kuwapa msaada watumishi hao wapya kutokana na uzoefu alionao wa muda mrefu kwenye masuala ya Kimataifa. 

 Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimpongeza Balozi Tavaku kwa kuteuiwa kushika wadhifa huo na kumtaka awe makini katika kupambana na changa moto zitakazomkabili katika utumishi wake huo mpya. 

 Balozi Seif alimueleza Balozi Tavaku kwamba miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja mchakato wa Tanzania kuelekea katika katiba mpya ambayo tayari Wananchi wameanza kutoa maoni yao. 

 Alisema yapo matatizo katika katiba ya sasa na kitachozingatiwa zaidi katika fursa ya Wananchi ya utoaji wa maoni ni kuhakikisha kasoro na upungufu uliopo unaondoshwa kwa kujenga katiba madhubuti itakayokidhi mahitaji ya Jamii yote ya Watanzania. “ Naamini Katiba mpya ijayo kwa kuwa itahusisha Wananchi wote itaondowa kero na mapungufu yaliyokuwa yakileta migongano miongoni mwa Wananchi wa pande zote”. Alifafanua Balozi Seif.

Thursday, August 23, 2012

ATAKAE KUBALI KUHESABIWA AMEUSALITI UISLAM NA KAWASALITI WAZANZIBAR

 
Waaislamu nchini Zanzibar wametakiwa wasishiriki sensa kwani ndani ya sensa kuna mtego ambao utasababisha madhara makunwa dhidi ya waislamu.
Hayo yameelezwa na amiri wa jumuiya hiyo Sh Mselem bin Ally katika mkutano ambao uliwashirikisha waandishi wa habar ambao ulifanyika katika viunga vya msikiti wa mbuyun zanzibar kwa lengo la kutoa tamko la waislamu kwa nini  wanakataa  sensa.
Akibainisha miongoni mwa sababu ambazo zinawafanya wasikubali sensa ni pamoja na kuondoshwa kipengele cha dini licha ya kwamba Serikali imejitetea kwa kudai ya kwamba wao hawapangi mambo ya maendeleo kwa kuzingatia dini, jambo ambalo si kweli bali ni kuendeleza ile desturi ya serikali ya muungano katika kutii matakwa ya maelekezo ya ya mfumo Kristo ambao umekua ukiendesha Serikali hiyo kwa maslahi ya makanisa na wakiristo kwa muda mrefu.
akiongezea amesema wazanzibar na waislamu hawashiriki sensa mpaka yafanyike mambo yafuatayo;
1-Wazanzibar wote wenye haki ya kisheria wapatiwe vitambulisho  vya Uzanzibari na wale wote wasiostahiki wakapewa kwa utashi wa kisiasa virejeshwe.
2-Wazanzibar wana vitambulisho vyao kwa hiyo vitambulisho vinavyotoka Tanganyika kwa jina la  Tanzania visitishwe mara moja kuletwa Zanzibar.
3-Ili wazanzibar washiriki sensa kwanza wapatiwe nchi yao ya Zanzibar yenye mamlaka kamili iksha watajihesabu.
4-kipengele cha dini kiingizwe katika dodoso la sensa kwani hili si geni katika sheria za kimataifa za sensa ili kujua nchi inaendeshwa vipi ili kuchunga maslahi ya wenye dini zao.
5-Serikali zote mbili zitoe tamko la kulaani vitendo vya jeshi la polisi vya kinyama vya kunajisi miskiti na kuharibu nyumba za ibada  kama walivyolaani wakati yalipoharibiwa makanisa na hatimae kuzawadiwa nafasi ya uwakilishi katika baraza la uwakilishi.
6-vyombo vya habari (ikiwemo ZBC) vilivoripoti taarifa zisizo sahihi na kuwachafua JUMIKI ndani na nje ya nchi iwaombe radhi waislamu kwa kupotosha habari kitu ambacho kimewasababishia wapate maafa makubwa.
Kutokana na mikakati hiyo  wazanzibar  wametakiwa wasusie zoezi la sensa hadi pale madai yao yatakaposikilizwa na kufanyiwa kazi kwa uakmilifu wake. kwa hiyo kila mwenye uchungu wa Zanzibar na chembe ya imani ya Uislamu haimfalii kushiriki zoezi la sensa kwani kufanya hivo ni kuusaliti Uislamu na kuisaliti Zanzibar.

Tuesday, August 21, 2012

TAMKO RASMI LATOLEWA NA SHEIKH MSELEM


Amir wa Taasisi za kislamu na jumuiya ya uamsho zanzibar ametoa tamko rasmi leo nakuwagiza waislamu wote nchini wasishiriki sensa mpaka serikali itakapo amua kuweka kipengele cha dini.
Vile vile Amir Mselem amepinga vikali matamko ya KATIBU WA MUFTI ust SORAGA kwa kuwapotosha wananchi kwa kudai eti ofisi ya Mufti wamekubaliana na uamsho nakwamba watashiriki sensa.Amesema kweli tulifanya kikao na ofisi ya Mufti lakini hakuna tulichokubaliana hayo maneno wanayosema SORAGA sikweli.

Kwahyo waislamu tamko ndo lishatoka watekelezaji ndo sisi.

Kama muislamu wa iman thabit tunatumai utaungana na sisi katika kuipinga sensa.

WAISLAMU MTASHARIKI SENSA

Sunday, August 19, 2012

Jengo jipya uwanja wa ndege kuhudumia abiria 800

Na Husna Mohammed
JENGO jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, linatarajiwa kuchukua abiria 800 wa kuingia na kutoka mara baada ya kukamilika kwake.
Meneja wa Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar, Mzee Abdalla Mzee, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari vilivyofika katika kiwanja cha kimataifa cha ndege Zanzibar, kwa ajili ya kupata maelezo juu ya ujenzi wa kiwanja hicho.
Hata hivyo, Meneja huyo alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwake wataangalia uwezekano wa kuona kiwanja hicho kutumika kwa wageni pekee au mchanganyiko.
“Tutaangalia uwezekano kama tutumie kwa wageni pekee na wenyeji watumie ule wa awali au la”, alisema.
Aidha alisema kwa mwaka wanakusudia kuchukua abiria milioni 1.1 kwa mwaka kutoka nchi mbalimbali duniani.
Meneja huyo alisema jengo hilo litakuwa la kisasa ambalo litakuwa na ubora kama viwanja vyengine duniani.
Jengo hilo jipya la abiria limeanza ujenzi wake mwaka 2010 na kukamilika mwaka 2013, ambapo litagharimu dola milioni 70.4 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya EXIM.
Ujenzi huo unajengwa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group ya China.

Baraza la Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar











EID MUBARAK

Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLlaah wa Barakaatuh, Ndugu wapenzi,







Kwa Munaasabah huu wa furaha wa siku hii tukufu ya ‘Iyd Al-Fitwr tunapenda kuchukua fursa hii kuwawasilishia salaam zetu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie 'amali zetu na zenu ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNA WA MINKUM’ (Hivi ndivyo Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi wanapokutana katika siku ya 'Iyd).
 
Na tunamuomba Yeye Aliyetukuka na Mweza, Awajaalie furaha, amani, mapenzi, siha na Iymaan pamoja na karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu. Mwisho, bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu leo na kila siku. Ndugu zetu Waislam walio katika dhiki za ukandamizwaji, vita, njaa na machafuko huko Burma, Syria, na palipokuwa Qiblah cha kwanza cha Uislam, na Msikiti wa tatu kwa utukufu na hadhi, Palestina, na pote walipo Waislamu ulimwenguni.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutakabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn 
Tafadhali bonyeza kwenye picha ifuatayo upate Takbiyrah ya 'Iyd

EID MUBARAK








Nachukua nafasi hii kuwatakia eid njema wanamzalendo na wazanzibari walio hapa nyumbani na walio popote duniani,Mola atujaalie maqbul katika saumu zetu ,ibada zetu, zakka na sadaka zetu ,kwa hakika ni Rehma kubwa kwetu na furaha iliyoje kwani kubahatika kupata siku za ramadhani kukukutia ukiwa hai na ukaweza kukamilisha huwa umejiongezea fungu kubwa katika maisha yako ya kesho na hayo ndio tunayoyaombe mbele ya Mola wetu.
Pia kwa siku hizi tukufu namuomba Mola wetu atukubalie dua zetu katika kupata taifa letu la zanzibar na kujiamulia mambo yetu bila ya mkono wa kidudu mtu.
Namalizia nikikutakieni wazanzibari walio hapa na duniani kote eid njema na ya furaha .amin

Friday, August 17, 2012

Breaking News – Saudi Arabia Sikukuu itakuwa Jumapili

Assalam alaykum
Kwa ndugu zetu Waislam wanaofuata Saudi Arabia kuandama kwa mwezi, Sikukuu itakuwa Jumapili, Inshaallah
Makkah, Ramadan 29, 1433, Aug 17, 2012, SPA — The Royal Court issued the following statement:
‘According to the two Royal Orders No. 7311/MB dated 24/9/1429 H. and No. 6605/B dated 15/6/1430 H. and the regulation of sighting the crescent of lunar months issued according to the Cabinet decision No. 143 dated 22/8/1418 H., the Supreme Court held a meeting at its summer headquarters in Taif Province this evening, corresponding to Friday 29th of Ramadan 1433 H. regarding the blessed Eid Al-Fitr.
After having reviewed all reports it received in this concern and studied them and according to the Supreme Court’s decision No. 36/H. dated 29/8/1433 H. stating the start of the current Ramadan on Friday 1/9/1433 H. corresponding to 20/7/2012, the meeting issued the following decision No. 37/H. dated 29-30 Ramadan 1433 H.
Thanks to Allah Almighty and Prayer and Peace be Upon the Prophet who instructed us to fast and breakfast upon sighting the crescent and if it was not visible, you complete your fasting for the 30th day and due to the lack of evidence of sighting the new moon this evening of Friday the 29th of Ramadan of this year 1433 H corresponding to 17/8/2012, the Supreme Court decides that Saturday corresponding to 18/8/2012 is the complementary day of Ramadan 1433 H. and that Sunday corresponding to 1/10/1433 H. according to Ummal Qura calender which falls on the 19th of August 2012 is the first day of Eid Al-Fitr which falls on the first day of Shawal 1433 H.
On this occasion, the Supreme Court, extends congratulations to the Custodian of the Two Holy Mosques, his Crown Prince, the government and people of the Kingdom of Saudi Arabia, the expatriates residing in this country and the entire Islamic Ummah (nation) all over the world on the advent of the blessed Eid Al-Fitr, appealing to Allah Almighty to accept our good deeds and forgive us and ask Allah to bestow the virtue of stability, prosperity and security on all of us, and have Muslims united and reconciled.’
–SPA

Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM yakutana Zanzibar



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa CCM,alipowasilikatika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,kushiriki katika kikao cha siku moja cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar,kilichofanyika leo.
Makamo Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume, akiendesha kikao cha kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar,katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Ali Mohamed Shein

Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,wakiwa katika kikao cha siku moja chini ya Mwenyekiti wake, Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,wakiwa katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,kilipofanyika kikao hicho leo. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

MJI HUU WANAUME MARUFUKU


 

Kwa mara ya kwanza duniani, mji ambao wanaume hawataruhusiwa kuishi unajengwa nchini Saudi Arabia ambapo ni wanawake pekee watakuwa wakiruhusiwa kuishi na kufanya kazi kwenye mji huo mpya utakaojengwa kisasa katika nchi hiyo ya kislam.
Mji mpya kwaajili ya wanawake pekee ukiwa na viwanda mbalimbali unajengwa nchini Saudia Arabia ambapo katika mji mzima wanawake wataishi wenyewe na wakifanya kazi bila ya kuwepo ya hata mwanaume mmoja.
Katika kuwapa nafasi wanawake kufanya kazi kwa uhuru kama wanawake wa sehemu zingine duniani, Saudi Arabia inatarajia kujenga mji wa kisasa kwa ajili ya wanawake pekee.
Mji huo utakaogharimu dola za Marekani milioni 133 utaanza kujengwa mwakani karibu na mji wa mashariki mwa Saudi Arabia wa Hafuf.
Mji huo utakuwa na viwanda vya nguo, madawa na vyakula na inakadiriwa kuwa jumla ya wanawake 5,000 watapata ajira.
Hatua hii ya kuanzishwa kwa mji wa wanawake pekee inakuja ili kuwapa nafasi wanawake kuendana na wakati na kufanya kazi na pia kuwapa mazingira ya kazi yatakayoenda sambamba na sharia za kiislamu.
Mamlaka ya viwanda ya Saudia, Modon imesema kuwa ina mpango wa kuanzisha mji wa pili wa wanawake pekee mbali na mji wa Hafuf.