Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, July 12, 2014

PRAY FOR GAZA

I don't have any word to express my feeling when I see a MAN is crying !!
if you see Man is crying, you have to know that there is a PAINFUL thing that breaks his heart. He may lose his friend, or one of his member family, or his home was destroyed.
Anyway, there is always pain in #Gaza

Nothing is new in the sixth day of Israeli aggression on the Gaza Strip; just more destruction in civilians houses 


I know that I DON'T have home now! But at least I have my bicycle to play on the ruin of my home .
We Palestinian teach life to the whole world 




Thursday, March 27, 2014

KESI YA UAMSHO YAHAIRISHWA HADI JULIA 3






na harith subeit

zanzibar.

kesi inayowakabili viongozi wa jumuiya na taasisi zakiislam zanzibar imeakhirishwa hadi julai 3 mwaka huu ambapo imewekewa pingamizi na mkurugenzi wa mashtaka kuhusu dhamana iliyotolewa kwa washtakiwa hao.

mapema muendesha mashitaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka dpp raya mselem aliwasilisha pingamizi ya kupinga uamuzi wa mahkama kuu kusikiliza ombi la dhamana ya watuhumiwa hao.

licha ya mahakama kuu kutoa dhamana kwa watuhumiwa bado upande wa mashtaka unapinga suala hilo na umeamua kukata rufaa ili washtakiwa warejeshwe tena rumande baada yakukaa ndani mwaka mmoja na miezi minne.

hata hivyo wakili wa upande wa utetezi abdalla juma ameiomba mahkama hiyo kuakhirisha shauri hilo hadi mahakama ya rufaa itakapokaa na kusikiliza rufaa hiyo.

hata hivyo jaji isack sepetu hakupingana na hoja hiyo.

watuhumiwa waliofika mahakamani leo ni pamoja na amiri mkuu wa jumuiya ya maimamu zanzibar samahatu sheikh farid hadi ahmed,amiri mkuu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar fadhilatu sheikh mselem bin aly, naibu amiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar zanzibar al-ustadh azan khalid hamdan.

wengine ni katibu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar al-ustadh abdalla saidi, maustadh mussa juma mussa, suleiman juma sleiman, khamis ali sleiman, hassan bakari sleiman, gharibu ahmada juma, na majaliwa fikirini majaliwa.

mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu mali, uchochezi,ushawishi , kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula njama ya kufanya kosa
kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne al-ustadh azan khalid ambae anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi vitendo vinaweza v kusababisha uvunjifu wa amani.

vitendo hivyo vinadaiwa kufanyika kati ya oktoba 17,18 na 19 mwaka ,2012 katika maeneo tofauti katika manispaa yaa mji wa zanziba ambapo washitakiwa hao wote wamekana makosa yote hayo.

viongozi hao walipewa dhamana na mahakama kuu ya zanzibar tarehe 27 mwezi wa pili mwaka huu baada yakutekeleza masharti yaliyowekwa.

Thursday, February 27, 2014

UAMSHO WAACHIWA KWA DHAMANA



MAHKAMA KUU VUGA MJINI ZANZIBAR IMEPUNGUZA MASHARTI MAGUMU YA DHAMANA YALIYOKUWA YAKIWAKABILI VIONGOZI JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU ZANZIBAR YA KULIPA SHILINGI MILIONI 25 NA BADALA YAKE SASA ZIMEKUWA ZA MAANDISHI.

JAJI WA MAHKAMA HIYO FATMA HAMID MAHMOUD AMETOA UAMUZI HUO NA KUSEMA KUWA KUTOKANA NA WATUHUMIWA HAO KUKAA NDANI KWA MUDA MREFU MAHAKAMA IMEONA WANA HAKI YA KUPATIWA DHAMANA.

MASHARTI YENYEWE YALIKUWA NI KUTOA FEDHA TASLIM SHILINGI MILIONI 25, KUWA NA WADHAMINI WATATU WAKIWA NI WATUMISHI WA SERIKALI MMOJA WAO AWASILISHE MALI ISIYOHAMISHIKA PAMOJA NA KUTOSAFIRI NJE YA ZANZIBAR.

HATA HIVYO BAADA YA MAOMBI YA WATUHUMIWA WAKIONGOZWA NA MAWAKILI WAO SALUM TOUFIQ JAJI FATMA ALIKUBALI KILA MSHITAKIWA KUJIDHAMINI KWA SHILINGI MILIONI 25 ZA MAANDISHI PAMOJA NA KUWA NA WADHAMINI WAWILI MOJA AKIWA MFANYIKAZI WA SERIKALI NA WA PILI AWASILISHE MALI ISYOHAMISHIKA BADALA YA WADHAMINI WATATU WAFANYAKAZI WA SERIKALI.

WATUHUMIWA HAO NI AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH FARIDI HADI AHMED,AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR FADHILATU SHEIKH MSELEM ALI MSELEM, USTADH MUSA JUMA MUSSA,NAIBU AMIRI WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR AL-USTADH AZAN KHALID HAMDAN,KATIBU WA JUMUIYA YA UAMSHO USTADH ABDALLA SAIDI NA MAUSTADHI SLEIMAN JUMA SLEIMAN, KHAMIS ALI SLEIMAN, HASAN BAKARI SLEIMAN, GHARIBU AHMADA JUMA, NA FIKIRINI MAJALIWA .

MASHTAKA WALIOSOMEWA WASHITAKIWA HAO NI KUHARIBU MALI, UCHOCHEZI,USHAWISHI NA KUHAMASISHA FUJO NA KOSA LA TATU NI KULA NJAMA YA KUFANYA KOSA

KOSA LA NNE LIKIMKABILI MSHITAKIWA NAMBA NNE AZAN KHALID AMBAE ANADAIWA KUTOA MANENO YA MATUSI KWA KAMISHNA WA POLISI VITENDO VINAVYOWEZA KUSABABISHA UVUNJIFU WA AMANI.

VITENDO HIVYO VINADAIWA KUFANYIKA KATI YA OKTOBA 17,18 NA 19 MWAKA ,2012 KATIKA MAENEO TOFAUTI KATIKA MANISPAA YAA MJI WA ZANZIBA AMBAPO WASHITAKIWA HAO WOTE WALIKANA MAKOSA YOTE HAYO .

KESI HIYO ILIAKHIRISHWA HADI MACH 27 MWAKA HUU KESI HIYO ITAKAPOSIKILIZWA TENA.

Tuesday, February 25, 2014

TIZAMA PICHA:Maelfu ya wananchi wa mkoa wa Hiraan wajitokeza na kupinga Wanajeshi wa Ehiopia.

Maelfu ya wananchi wa Kislaam wa Somalia wamejitokeza barabarani katika maeneo mbalimbali ya Miji ya Hiraan iliyoko katikati mwa Ardhi ya Somalia.
Maandamano hayo yalikuwa ya kupinga uingiliaji kati na uchokozi ulio wa wazi wa Serikali ya Ethiopia dhidi ya Ardhi ya Kislaam ya Somalia.
Kwenye Barabara ya mji wa Buula Barde walionekana mamia ya Wananchi waliokuwa wakipita kweye Barabara hizo huko wakitamka maneno dhidi ya Adui asilia ya Uvamizi wa Ethiopia aliyovishwa vazi la AMISOM.
Wazee wa koo wa Mkoa wa Hiraan,wanataaluma,walizungumza kwenye Maandamano hayo na kusema kuwa watakuwa tayari kuingia vita itakayochukua muda mrefu dhidi ya wanajeshi wa Ethiopia ili kuilinda Dini na Ardhi yao,waandamanaji wote hao waliokuwa wakipinga Wanajeshi wa Ethiopia kwa ujumla wamekubaliana kuwa Uingiliaji wa Ethiopia uliokuja na sura mpya hautoweza kuathiri chochote harakati iliyokuwa ikiendelea dhidi ya Maadui wa Kigeni walioivamia Rdhi ya Kislaam ya Somalia.

Tuesday, February 11, 2014

Morocco inaamiliana vibaya na wahajiri wa Kiafrika


Morocco inaamiliana vibaya na wahajiri wa KiafrikaShirika la Kutetea Haki za Binadmu la Human Rights Watch limeitaka serikali ya Morocco kuamiliana  kiubinadamu na wahajiri wa Kiafrika wanaopita nchini humo. Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imeeleza kuwa, wahajiri wanaopita nchini Morocco wakitokea maeneo ya kusini mwa jangwa la Sahara na kuelekea barani Ulaya, wanakabiliwa na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kupigwa na kuwekwa rumande bila ya kufunguliwa mashtaka. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la HRW limeeleza kuwa, licha ya kufanyiwa marekebisho sheria za wahajiri na wakimbizi nchini humo, lakini bado vinaendelea kushuhudiwa vitendo visivyo vya kibinadamu vinavyofanywa na askari usalama  dhidi ya wahajiri.
Wimbi kubwa la wahajiri kutoka kusini mwa jangwa la Sahara limekuwa likipita nchini Morocco na kuelekea Uhispania, lakini limekuwa likikumbana na mateso wakati wa kuondoka nchini humo. Morocco inahesabiwa kuwa kivuko muhimu cha wafanya magendo ya dawa za kulevya na wahajiri haramu ambao hujaribu kuingia Ulaya kinyume cha sheria.

Jeshi la Syria lasisitiza kupambana na magaidi


Jeshi la Syria lasisitiza kupambana na magaidi
Mkuu wa vikosi vya  ulinzi na usalama nchini Syria amesisitiza juu ya kutiwa mbaroni wale wote waliohusika na mauaji ya halaiki ya wananchi wasiopungua 71 wa Syria hapo jana. Mkuu wa majeshi ya Syria ameongeza kuwa, serikali ya Damascus inafanya juhudi za kutatua mateso yanayowakabili  wananchi zinazosababishwa na  njama za baadhi ya mataifa ya nchi za Magharibi na vibaraka wao walioko katika eneo la Mashariki ya Kati. Mkuu wa Majeshi ya Syria amesisitiza kuwa, jeshi la nchi hiyo litaendelea kupambana kikamilifu na kuhakikisha kwamba watenda jinai wa kundi la al Nusra wanahilikishwa kikamilifu.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, magaidi walioko nchini Syria, baada ya kukiteka kijiji cha Maan kilichoko Hamah magharibi mwa Syria waliwauwa kwa halaiki watu 71 wakiwemo wanajeshi 50 wa serikali ya Syria. Mauaji hayo yanatokea katika hail ambayo, leo hii inaanza duru ya pili ya mazungumzo kati ya ujumbe wa serikali ya Syria na wapinzani huko Uswisi.

Ulaya kutuma wanajeshi 500 Jamhuri ya Afrika ya Kati

    Ulaya kutuma wanajeshi 500 Jamhuri ya Afrika ya Kati
Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje  wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wamepitisha mpango wa kupelekwa wanajeshi 500 wa umoja huo huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa lengo la kusaidiana na vikosi vya nchi za Kiafrika na vile vya Ufaransa katika kuleta amani nchini humo. Catherine Ashton Mkuu wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa, lengo la kutumwa wanajeshi hao ni kutekelekeleza operesheni za kukomesha machafuko na mauaji dhidi ya wananchi wa nchi hiyo na hasa Waislamu ambao wamekuwa wakilengwa na mashambulio ya wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka. Siku ya Jumapili iliyopita, Shirika la
Kutetea Haki za Bindamu la Human Rights Watch HRW lilitahadharisha kuwa, machafuko yanaondelea kushuhudiwa nchini humo yatasababisha Waislamu wote kuwa wakimbizi.  Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, karibu watu milioni mbili wanahitaji misaada ya kibinadamu nchini humo.

Ikhwanul Muslimin ya Misri yakadhibisha kuunda jeshi

Ikhwanul Muslimin ya Misri yakadhibisha kuunda jeshi
Kiongozi mmoja mwandamizi wa harakati ya Ikhwanul Muslimiin ya Misri amesema kuwa, harakati za kundi hilo zitaendelea kuendeshwa kwa njia za amani na kusisitiza kwamba kundi hilo halina mpango kabisa wa kuanzisha tawi la kijeshi.
Muhammad Ali Beshr amekadhibisha vikali taarifa zilizotolewa na serikali ya Misri kwa vyombo vya habari kwamba, harakati ya Ikhwanul Muslimin imeanzisha tawi la kijeshi kwa lengo la kupambana na polisi na jeshi la nchi  hiyo. Kiongozi huyo mwandamizi wa Ikhwanul Muslimiin amesisitiza kuwa, harakati hiyo itaendelea kupigania haki zake zote kwa njia za amani. Inafaa kuashiria hapa kuwa, hivi karibuni kundi la watu waliobeba silaha lilishambulia kituo cha polisi  na kuwauwa  askari watano na wengine wawili kujeruhiwa. Serikali ya Misri ililifungamanisha shambulio hilo na kundi la Ikhwanul Muslimiin. Wakati huohuo, Mahakama moja nchini  Misri imetoa hukumu ya adhabu ya kifo kwa watu 14 na wengine wanne kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma eti walishiriki katika shambulio dhidi ya kituo cha polisi nchini humo.

Friday, January 17, 2014

kesi inayowakabili viongozi wa harakati ya jumuiya na taasisi zakiislam zanzibar .






mahkama kuu vuga mjini zanzibar imeutaka upande wa mashtaka  kuwasilisha vielelezo na maelezo ya ushahidi vitakavyotumika  katika kesi inayowakabili viongozi wa  harakati ya jumuiya na taasisi zakiislam zanzibar .



jaji wa mahkama hiyo fatma hamid mahmoud ametoa ombi hilo alipokuwa akiendesha kesi  inayowakabili viongozi hao katika mahakam kuu vuga mjini zanzibar .



jaji huyo pia ameutaka upande wa mashtaka kuwasilisha kwa maandishi sababu za  kuzuiya dhamana ya  viongozi hao waliokaa rumande  kwa mwaka mmoja sasa.



hatua hiyo imekuja  baada ya mwendesha mashtaka wa serikali rashid abdalla kudai kuwa vielelezo vya ushahidi wa kesi hiyo tayari vimekamilia hivyo  ipangiwe tarehe nyengine ili kuwasilisha vielelezo vya mashahidi.



kwa upande wake wakili anaesimamia watuhumiwa wa kesi hiyo abdalla juma  ameiomba mahkama kupanga tarehe ya kusikilizwa  kwa kesi hiyo na vielelezo viwasilishwe mahkamani hapo kutokana na  ushahidi wa kesi hiyo kukamilika.



hata hivyo upande wa mashitaka haukuwa na pingamizi na na ombi hilo na  umedai kuwa unaiachia mahkama kuamua.



watuhumiwa katika kesi hiyo  ni   amiri mkuu wa jumuiya ya maimamu zanzibar samahatu sheikh farid hadi ahmed  mkaazi wa mbuyuni,amiri mkuu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar fadhilatu sheikh mselem ali mselem  mkaazi wa kwamtipura, ustaddh mussa juma mussa  mkaazi wa makadara 

wengine ni  maustadh suleiman juma suleiman  mkaazi wa makadara, khamis ali suleiman mkaazi wa mwanakwerekwe, hassan bakar suleiman mkaazi wa tomondo, ghalib ahmada juma mkaazi wa mwanakwerekwe ,katibu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar  al-ustadh abdallah said mkaazi wa misufini na fikirini majaliwa fikirini.



mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu mali,  uchochezi,ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula njama ya kufanya kosa.



kosa la nne linamkabili mshitakiwa namba nne al-. naibu amiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar  al-ustadh azan khalid ( mkaazi wa mfenesini.



ustadh azan khalid hamdan anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.



vitendo hivyo vinadaiwa   kufanyika kati ya oktoba 17,18 na 19 mwaka 2013 katika maeneo  mbali mbali katika manispaa ya mji wa zanzibar.



jaji fatma ameikhirisha kesi hiyo na kutaka upande wa mashitaka kuwasilisha vielelezo na maelezo ya kesi hiyo  kabla ya  januar 31 mwaka huu. 

Thursday, January 9, 2014

Abdiweli Mohamed, rais mpya wa Puntland, Somalia


Abdiweli Mohamed, rais mpya wa Puntland, Somalia
Dakta Abdiweli Mohamed Ali, Waziri Mkuu wa zamani wa Somalia leo amechaguliwa kuwa Rais wa eneo lenye mamlaka ya ndani la Puntland, baada ya kumshinda mpinzani wake Abdirahman Mohamed Mohamud kwa zaidi ya kura moja, katika uchaguzi huo uliojaa ushindani mkubwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Puntland, wabunge 66 wa eneo hilo waliochaguliwa na wakuu wa makabila mwezi uliopita, ndio wenye jukumu la kumchagua Rais wa eneo hilo lililoko kaskazini mashariki mwa Somalia.
Tume ya Uchaguzi ya Puntland ilipitisha majina ya wagombea 11 kati ya 15 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo, katika eneo hilo lililojitangazia mamlaka ya ndani tokea 1998.
Dakta Abdiweli Mohamed Ali aliwahi kuhudumu nafasi ya Uwaziri Mkuu wa Somalia tangu mwaka 2009 hadi mwaka 2012. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mapigano yaliyoanza mwaka 1991 nchini Somalia baada ya kuangushwa utawala wa Jenerali Muhammad Siad Barre, yalisababisha baadhi ya maeneo ya Somalia kujitangazia mamlaka ya ndani, kama Somaliland na Puntland. 

WFP yawapatia chakula wakimbizi wa ndani CAR


WFP yawapatia chakula wakimbizi wa ndani CAR
Shirika la Mpango wa ChakulalaUmoja wa Mataifa (WFP) limeanza tena kugawa chakula kwa familia za wakimbizi wa ndani ya nchi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa ya WFP imesema chakula kitatolewa kwa watu wapatao 100,000 ambao wamepata hifadhi katika uwanja wa ndege wa Bangui, mjii mkuu wa nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya ndani. Ugawaji huo umeanza tena baada ya kusitishwa kwa wiki tatu kutokana na hali ya usalama kwenye eneo hilo.  WFP inashirikiana na mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na viongozi wa kijamii ili kuhakikisha mazingira yanaruhusu kusambaza msaada wa chakula na misaada mingine kwa wakimbizi wa ndani. Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaituhumu Ufaransa ambayo ni mkoloni wa zamani wa nchi hiyo kuwa inachochea mapigano hasa uhasama baina ya Waislamu na Wakristo nchini humo. Jamhuri ya Afrika ya Kati ni nchi yenye umuhimu mkubwa kwa madola makubwa ulimwenguni kutokana na kuwa kwake katika kitovu cha bara la Afrika. Nchi hiyo inakodolewa jicho la tamaa na nchi kubwa duniani kutokana na utajiri mkubwa wa maliasili za madini kama almasi, urani na dhahabu.

Mapigano makali yaendelea nchini Sudan Kusini


Mapigano makali yaendelea nchini Sudan KusiniMapigano makali yanaripotiwa kuendelea kati ya wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini na waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa rais Riek Machar.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Philip Aguer amesema siku ya Jumatano walipambana vikali na waasi katika kupigania udhibiti wa Bor, mji mkuu wa Jimbo la Jonglei. Aidha mapigano yanaripotiwa kuendelea katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Nile ya Juu. Msemaji wa waasi Youhani Musa Pauk amesema hakutakuwa na usitishaji mapigano hadi pale serikali ya Juba itakapowaachilia huru wanasiasa wapinzani ambao walitiwa mbaroni punde baada ya machafuko kuibuka wiki tatu zilizopita. Huku hayo yakijiri wapatanishi kutoka jumuiya ya kieneo ya IGAD wanasema mazungumzo baina ya pande hasimu yanaendelea vizuri na kwamba Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesitiza kuwa mgogoro wa sasa ni wa kisiasa na kwamba anaunga mkono suluhisho la kisiasa. Machafuko nchini Sudan Kusini yalianza Disemba 15 katika mji mkuu Juba, pale wanajeshi wanaoaminika kuwa watiifu kwa Riek Machar, walipojaribu kuipindua serikali ya Rais Salva Kiir. Uhasama wa kisiasa nchini humo ulianza mwezi Julai mwaka jana baada ya Kiir kumfuta kazi Machar. Kiir ni kutoka kabila la Dinka ambalo ndilo lenye nguvu zaidi na Machar ni wa kabila la Nuer.