Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji amepongeza ripoti ya
Umoja wa Mataifa inayoonesha kuwa kiwango cha maambukizo ya virusi vya
Ukimwi kimepungua kwa asilimia kubwa katika nchi zilizoko chini ya
Jangwa la Sahara na ametaka juhudi zaidi zifanywe ili kiwango hicho cha
maambukizi kiende chini zaidi. Akihutubia wananchi katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani hapo
jana, Waziri Duni Haji alisema unyanyapaa bado unaendelea kukita mizizi
miongoni mwa jamii ya Waswahili na ametoa wito kwa Wazanzibari kubadili
mwenendo huo. Ripoti ya UN inaonyesha kuwa kiwango cha maambukizo ya VVU kimepungua
katika nchi masikini na kupanda katika nchi zilizoendelea hususan
Marekani na nchi kadhaa za Ulaya.
No comments:
Post a Comment