Maafisa wa usalama wa Kenya wamesema kuwa, watu wenye silaha bado
wanaendelea kuwashikilia mateka makumi ya watu katika jengo la maduka
la Westgate jijini Nairobi. Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za Majanga
cha Kenya kimesema kuwa askari usalama wanaendelea na operesheni dhidi
ya watu hao wenye silaha tangu tukio hilo lilipoanza hapo jana na kwamba
kila jambo linalowezekana litafanyika ili kuwaokoa raia. Kundi la wanamgambo la al Shabab la Somalia limetangaza kuwa ndilo
lililohusika na shambulizi hilo huko Nairobi katika shopping Mall ya
Westgate. Taarifa zinaeleza kuwa vikosi vya jeshi la Kenya vimeanza
kumiminika katika eneo la tukio huku duru za usalama zikithibitisha
kwamba milio ya kurushiana risasi inasikika kwenye eneo hilo. Hapo jana Rais Uhuru Kenyata alisema kuwa, watu zaidi ya 40 wameuwa
na wengine 150 kujeruhiwa kwenye tukio hilo na kwambaserikali yake
itawasagasaga na kuwamaliza watu hao wenye silaha.
No comments:
Post a Comment