Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, February 17, 2015

WAUTHMANIYA: MAJEMEDARI WAO WALIOTUKUKA NA TAASISI ZAO ZENYE KUHESHIMIKA



Alhamdulillah, Mwenyezi Mungu Mtukufu ametunyooshea tawfiq Yake kwa kumaliza tarjuma na tafsiri ya kitabu hiki muhimu kuhusu historia ya Dola Kuu ya Wauthmaniya.

Ni hishma na adhama kubwa kwangu kwa mara nyingine kuuletea Ulimwengu wa Kiswahili historia hii iliyotukuka juu ya kuchomoza, kustawi, kudhoofika na kuanguka kwa Dola hii iliyotawala mabara matatu kwa muda wa miaka 623.

Kitabu hiki chenye kurasa 778 ni tafsiri ya kitabu maridhawa cha: Al-Uthmaniyyuun, rijaaluhum al-idhaam wa muassasaatuhum al-Shaamikhah kutoka kwa mwalimu wetu Sheikh Uthman Nuri Topbash kutoka Uskudar, Istanbul.

Wakati wa kutafsiri kitabu hiki cha 35 katika mfululizo wa tarjuma zangu za vitabu na cha 39 katika vitabu vyangu vyote, ilinilazimu kuchukua mtindo maalumu wa maisha, khususan maisha ya kimaanawi ya mhandisi mkuu wa Dola hii, Sinan Pasha au Mimar Sinan aliyeupa ulimwengu tunu za kiuhandisi zisizomithilika ambazo ziliakisi uhandisi maridhawa wa Kiislamu katika majengo na miradi yake. Mfumo wa Mimar Sinan Pasha wakati wa ujenzi wa “Sulaymaniyah Jami”, moja katika uhandisi bora kabisa aliowahi kuufanya, ulitiririsha nguvu na ithibati katika moyo wangu, khususan tukio la kutoweka kwake kwa kipindi cha mwaka mzima na kuzusha wasiwasi juu ya himma na azma yake kuu ya kukamilisha ndoto muhimu sana ya Sultan Sulayman Al-Qaanuuni.

Ujasiri na uthubutu wa Sultani Muhammad Al-Faatih aliyeifungua Konstantinopoli katika umri mdogo kabisa na kuthibtisha Bisharah ya Mtukufu Mtume (s.a.w) juu ya ufunguzi wa mji huo muhimu kwa Wabezanti, ilikuwa kioevu cha hamasa na nguvu wakati wa kufanya tarjuma hii.

Himma ya Sultani Salem I aliyeliongoza jeshi kubwa na kutembea umbali wa kilometa 2500 akivuka milima, mabonde na misitu mpaka alipokutana na Dola ya Safawiya, ambayo ilikuwa miongoni mwa madola makubwa wakati huo, akaishinda; himma yake katika kampeni yake ya kijeshi dhidi ya Misri, ambapo alivuka jangwa lenye kuogofya la Sinai, ambalo wakati huo ilikuwa ikiaminika kuwa hakuna anayeweza kulivuka, na ambapo mpaka leo hakuna aliyeweza kutoa tafsiri ya uvukaji huo ulivyokuwa kwa nyenzo za kimaada, ni miongoni mwa mambo yaliyokuwa nguzo ya ujasiri katika kampeni yangu ya kutafsiri kitabu hiki.

Kupitia kwake, historia iliandika kwenye kurasa zake za dhahabu wasifu wa mtawala adhimu asiye kifani. Katika umri wake wote, hakuwahi kupungukiwa na umahiri au kushindwa. Kwani alikuwa akitaka msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kila jambo na kuamini kuwa kwa kufanya hivyo jambo hilo litapata ufumbuzi.

Jangwa la Sinai wakati wa mchana huwa kama moto wa Jahannam, na wakati wa usiku hugeuka kuwa mithili ya mji wenye baridi kali. Lakini Sultani Salem alilivuka ndani ya siku 13 bila kupoteza askari hata mmoja, huku Napoleon aliyekuja miaka 300 baadaye akishindwa kulivuka jangwa hilo na askari wake kuuana wao kwa wao. Hata katika Vita Kuu ya Dunia, baada ya kuvumbuliwa kwa zana na ufundi wa hali ya juu, askari wa vita hiyo walilivuka jangwa hilo ndani ya siku 11.

Beti za ushairi wa Yunus Emre zilikuwa kama ala tamu katika moyo wangu na kunipa hamasa na saadah kuu. Hakika, kilichomfanya Yunus kuwa Yunus kimekuwa na taathira kwangu.

Ushupavu na ushujaa wa Khayrud-Din Barbarossa Pasha aliyeigeuza Bahari ya Mediterania kuwa mithili ya ‘Ziwa la Wauthmaniya’ na kuwaadabisha wazungu katika vita vya Baharini, ilikuwa kama karamu ya moyo kwangu. Hakika, Khayrud-Din Barbarossa ni tunu ya historia hii iliyotukuka.

Nakumbuka mzee wangu mmoja nilipomsimulia kuhusu khabari ya Barbarossa Pasha jina hili liliendelea kutoa mwangwi katika akili yake.

Miongozo ya kimaanawi ya wahandisi na masultani wa kiroho wa Dola hii kama vile Sheikh Adibali, Aziz Mahmud Hudayi na Mawlana Khalid Al-Baghdadi ilitoa mwanga adhimu kila nilipozifunua kurasa za kitabu hiki na kunifanya niamke mapema nikiwa na himma kubwa ya kuikamilisha kwa wakati. Alhamdulillah, baada ya wiki 4 za juhudi na himma kubwa, kazi hii iliyokuwa na kurasa 656 ilikamilika.

Hakika ni mengi ninayoweza kuyasema kuhusu kitabu hiki, lakini ni imani yangu kuwa wachapishaji wake, Darul-Arqam, watakuwa na hamasa ya kuwapatia wazungumzaji wa Kiswahili duniani chakula hiki maridhawa chenye virutubisho adhimu.

Shukrani zangu za dhati kwa wale wote walionitia moyo wa hamasa, bila  kumsahau mhariri wangu mahiri, Ali Hassan Kingu ambaye aliupitia kwa umakini muswada wa kitabu hiki muhimu.
Panapo majaaliwa, hivi karibuni nitaandika hapa mukhtasari wa anguko la Dola hii adhimu wakati tukisubiri wachapishaji watuletee meza hiyo ya karamu.
Na kwa kuwa “hadhi ya akili ya mtu huonekana katika aathari zake, basi: HIZO NI AATHARI ZETU, BAADA YETU ZITAZAMENI AATHARI HIZO”.

Wabillah tawfiq.

Monday, February 9, 2015

Amkirudi nyuma basi allaha ataleta badala yenu

Binti Mmoja Wakislamu huko France alikua
Supermarket Anafanya Shopping Yake, Alipofika
Kwa Cashier Kulipia Shopping, Yule Cashier
Mwenye Asli Yakiarabu, Akawa anamtizama Yule
Binti Kwa Madharau Huku Akisonya Nakumwambia
"Sisi Wakimbizi Kutoka Nchi Zetu Za Kislamu na
Kiarabu Tunakumbana Na Matatizo Mengi Sana
Hapa France, Namoja ya Hayo Matatizo Ni Hyo
Hijab & Niqab Uliyoivaa Wewe, Kama Kweli
Wapenda Dini & Mila Yako basi Rudi Kwenu, Sisi
Hatukutoroka Kuja Kutangaza Dini Bali Kutafuta
Maisha Mazuri.." Yule Binti Alitoa Niqab Yake na
Kumwambia Yule Cashier "Nitizame Vizuri Na Kwa
Makini.." Yule Cashier Alishtuka Kwani Kweli Yule
Binti Alikua Mzungu Mwenye Macho Ya Blue.. Binti
Akaendelea "Mimi Ni Mfaransa, Hii ni Inchi Yangu &
Islam Ndio Dini Yangu, Nyinyi Mumeitupa na
Kuiuza Dini Yenu, Tukainunua Sisi Kutoka Kwenu."
Katika Quran sura Muhammad 47:38 Allah
Anasema "Wa Intatawallaw Yastabdil Qawman
Ghayrakoum Thumma Laa Yakunuu Amthalakoum"
-Na Kama Mkirudi Nyuma (Mkaupa Mgongo
Uislamu) Allah Ataleta Watu Wengine Badala Yenu,
Nao Hawatakuwa Kama Nyinyi (Watakuwa Bora)".

Sunday, February 8, 2015

Simulizi na Nasaha: NDANI YA KAPU

By: Abuu Luqman

Miaka mingi nyuma nilikuwa nimehajiriwa na tajiri mmoja kuwa mlinzi wa getini katika jumba lake la kifahari.

Maisha kwa upande wangu hayakuwa mazuri hata kidogo, kilichokuwa kikiniweka na kuendelea kufanyakazi nyumbani kwake ni kwa kuwa nilikuwa nikipata baadhi ya vitu ambavyo viliniwezesha kupata mlo wangu wa kila siku.

Kila siku nilitakiwa kufika kazini saa kumi na mbili jioni na kualiza kazi saa mbili asubuhi.

Kazi yangu kubwa ilikuwa ni kumfungulia bosi wangu mlango wa geti kila anapotoka na kurudi kwenye miangaiko yake. Tatizo ambalo lilikuwa likinisumbuwa ni kwamba kila nikimsalimia alikuwa hajibu salamu yangu.

Hali ya nyumbani kwangu kwa kweli haikuwa nzuri hata kidogo. Na haswa kwenye maswala ya chakula, ukizingatia nilikuwa nina mke na watoto.

Hali ilikuwa mbaya nikamua kupekuwa pipa la taka lilokuwepo nje ya geti la nyumba ili kutafuta tafuta mabaki ya chakula kilichobakia kutoka kwa bosi wangu.

Bosi wangu aliniona, lakini hakusema chochote akaendelea na shughuli zake kama siyo yeye. Nami wala sikumjali kwa sababu mtu mwenyewe hata salamu haitikii, vipi anaweza kusikiliza shida ya mtu masikini kama mimi.

Siku ya pili yake nikaona kikapu cha sokoni pembeni ukutani kama hatua tatu toka kwenye lile pipa la takataka.

Nikiwa ni mlinzi wa getini nikaingiwa na udadisi wa kutaka kujuwa kuna nini ndani labda kuna mtu kasahahu kapu lake naweza kumuifadhia.

Kuangalia ndani ya lile kapu nikakuta kuna bidhaa za sokoni, inaonyesha kama vile huyu aliyesahau kapu lake alikuwa ametoka sokoni kununua bidhaa na kwa bahati mbaya kasahau kapu lake.

Muda wa kumaliza  kazi ulipowadia nikaondoka na kapu lile hadi nyumbani kwangu na kwa kuwa tulikuwa na shida ya vyakula tukavipika vilivyoko kwenye lile kapu na kuvistiri matumboni mwetu, tukashukuru MwenyeziMungu na kumuombea dua mwenye lile kapu.

Lakini ajabu ikawa kubwa zaidi, kwa maana siku ya pili yake nikakuta tena kikapu kama kile kimejaa bidhaa za sokoni tele, sehemu ile ile.

Safari hii sikujiuliza mara mbili kama ni mtego na ninase maana shida ya nyumbani kwangu aijuwae ni MwenyeziMungu tu.

Hali hii ikaendelea karibia miezi miwili hivi kiasi mimi na familia yangu tukawa tumeanza kuizoea ile hali ya kapu la chakula kuwepo pale nami kulichukuwa maana siku taka kujua ni mjinga gani ambaye alikuwa akiweka lile kapu pale, maana kila nikifanya uchunguzi sikupata hata kumjuwa aliyeliweka pale.

Nikawa nahisi labda mama mwenye nyumba anamuwekea hawala yake, au baba mwenye nyumba anamuwekea mwanamke wake na mimi nachukuwa na wao bila kujuwa wanaendelea kuweka pale kwa kudhani labda kinachukuliwa na huyo waliyemkusudia.

Mwishoni nikajifariji kama wanamuwekea mtu ambaye wanamtaka basi ndio wamekosa nami najifaidia vya bure.

Siku moja nilipoingia kazini kwangu, nikakuta watu ambao nilikuja kuwajuwa kuwa ni ndugu jamaa na marafiki wa bosi wangu, na nikaambiwa kuwa bosi wangu amefariki ghafla kwa presha.

Nilisikitika japo si sana kwa sababu nilijuwa kuwa labda mama mwenye nyumba au watoto zake wanaweza kuniachisha kazi kwa kuwa baba mwenye nyumba amekwisha fariki.

Nikaenda kuangalia ile sehemu ambayo nakuta lile kapu, siku hiyo sikuliona, nikahisi labda mmoja kati wa wageni walio udhuria mazishi kalibeba au mama mwenye nyumba hakuweza kumuwekea hawara wake kwa sababu ya msiba, basi ilihali fikra zote zilikuwa zikipita mara nikiwaza hili mara lile.

Siku ikapita, siku ya pili hali kadhalika, sikuona kapu, zikapita wiki mbili hali haikuwa kama nilivyoanza kuizoea. Sikuona kapu wala kikapu.

Hali ilipoanza kuwa mbaya, nikaona ni bora nionane na mama mwenye nyumba, ili aniongeze mshahara kwa sababu hali si nzuri tena.

Mama mwenye nyumba akanisikiliza ombi langu na kuniuliza, kama hali ni mbaya siku zote hizo kwanini niongezwe mshahara sasa, kwanini sikuwahi kumuomba Baba mwenye nyumba ambaye ni marehemu sasa aniongeze mshahara wakati alipokuwa hai?

Nikampa sababu hii na ile, lakini yule mama hakuridhika na majibu yangu, mwishowe nikaamua kumwambia ukweli na hali halisi ilivyokuwa.

Nikamwambia kuwa wakati ule nilikuwa nikiokota kapu lilowekwa nje ya nyumba likiwa na bidhaa mbalimbali za sokoni, na likinitosheleza mimi na familia yangu, kwa hiyo sikuona sababu ya kuomba kuongezwa mshahara, lakini sasa sioni tena kapu na hali uko kwangu si nzuri. Na ninaomba msamaha kwa kuchukuwa mali ambayo haikuwa halali yangu, shida ndio zilinipelekea kufanya vile.

Akaniuliza mara ya mwisho ni lini kuto ona kapu lile, nikamfahamisha ni siku ile ya msiba wa bosi.

Kwa mara ya kwanza ndipo nilipo baini kuwa, inawezekana kuwa marehemu ndio alikuwa akiweka kapu lile kwa sababu kama angekuwa ni mkewe au mtoto wake basi kapu lingendelea kuwekwa pale. Lakini hata hivyo nikawa nastaajabu, vipi mtu ambaye hata salamu yangu kuitikia alikuwa haitikii aweze kuwa mwema kiasi kile?

Nikashtushwa na kilio cha mke wa marehemu, nikamuomba msamaha kama nimemkumbusha mumewe mpenzi, akanambia lah hasha, siku zote hizi alikuwa anamtafuta mtu wa saba ambaye alikuwa akipewa bidhaa za sokoni na mumewe, kwa sababu mumewe alikuwa kila siku akilisha watu saba kwa kuwanunulia bidhaa mbali mbali za sokoni.

Watu sita Alisha wapata, ila mtu wa saba, ndio alikuwa akimtafuta na leo ameweza kumgundua, kumbe ni mlinzi wao wa getini. Binafsi machozi yalinitoka na sikuweza kuficha huzuni yangu na machozi yakawa yananitoka kama mtoto mdogo.

Tangia siku hiyo nikaanza kuletewa kikapu cha bidhaa za sokoni kama alivyokuwa akiniwekea bosi wangu marehemu, ila safari hii, si getini tena, bali aliyekuwa akiniletea ni mtoto wa bosi wangu na akiniletea nyumbani kwangu.

Siku ya kwanza nilipoletewa kapu na mtoto wa marehemu nilipomshukuru kwa ukarimu wake, nikastaajabu kwa kuto itikiwa nikawa najiuliza isije kuwa huyu mtoto karithi tabia za marehemu baba yake za kutowajibu watu wanaposalimiwa.

Lakini yule kijana kabla ya kuondoka akanifahamisha kuwa ninapozungumza naye basi nijaribu kuongea nae kwa sauti ya juu kidogo kwa sababu, yeye ana matatizo ya kutosikia vizuri, kama alivyokuwa marehemu baba yake, tena yeye ana afadhali maana baba yake kusikia kwakwe kulikuwa ni kwa shida sana.

Kwa kweli nilijisikia vibaya sana na kujilaumu, ni vipi tunaweza kuwadhania watu vibaya, tena bila ya kuwauliza au kutaka kujuwa sababu yake.

Ama kweli kapu lile lilikuwa si limeweka bidhaa za sokoni tu, bali lilikuwa limeweka ukarimu na upendo ambao sikuweza kuugundua, mpaka aliyeliweka kuaga dunia.