Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, July 26, 2013

Israel yaruhusu kutumiwa silaha za kemikali


Israel yaruhusu  kutumiwa silaha za kemikali
Waziri wa Afya wa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina inayoongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amelaani vikali hatua ya Mahakama Kuu ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuruhusu utumiwaji gesi ya kemikali yenye mada za fosforasi nyeupe. Mufid al Mukhlalati amesema kuwa, hatua ya mahakama hiyo kuruhusu utumiwaji wa gesi hizo za kemikali zenye mada za fosforasi nyeupe, kunalipa nguvu jeshi la utawala huu kutengeneza silaha hatari za kemikali zitakazotumiwa dhidi ya wananchi wa Palestina. Tarehe 9 Julai mwaka huu, Mahakama Kuu ya Israel ilitangaza kuwa, utumiwaji wa gesi hiyo ya kemikali ni ruhusa kabisa. Waziri wa Afya wa Palestina amesema kuwa, hivi sasa mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yanafanya juhudi za kuzuia jinai zinazofanyika ulimwenguni kote, lakini vyombo vya sheria vya utawala wa Israel vinapuuzia sheria za kimataifa kwa kuruhusu utumiwaji wa gesi za kemikali zenye mada za fosforasi nyeupe

Iran yaomboleza ajali ya treni ya Uhispania


Iran yaomboleza ajali ya treni ya Uhispania
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa mkono wa pole kwa serikali na wananchi wa Uhispania kutokana na ajali ya treni iliyotokea hivi karibuni nchini humo na kupelekea watu wasiopungua 80 kufariki dunia na wengine wasiopungua 140 kujeruhiwa 20, kati ya hali zao mahututi. Sayyid Abbas Araqchi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, ajali hiyo ya treni imeleta majonzi ulimwenguni kote, hivyo serikali pamoja na wananchi wa Iran wanaungana na wenzao wa Uhispania kwenye kipindi hiki kigumu cha huzuni na maombelezo. Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatano, pale treni hiyo kutembea mwendo wa kasi  katika kona na kusababisha mabehewa 13 kuondoka kwenye reli, na manne kupinduka kabisa. Taarifa zinasema kuwa, dereva wa treni hiyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi, ingawa alishatoa tahadhari ya kuanguka kwa treni hiyo, baada ya kushindwa kuidhibiti treni hiyo iliyokuwa kwenye  mwendo wa kasi kubwa. Treni hiyo ilikuwa ikitoka Madrid na kuelekea El Ferrol, na kupata ajali katika mji wa Santiago de Compestela, ulioko katika mkoa wa Galicia. Hii inahesabiwa kuwa ajali mbaya zaidi ya treni kutokea nchini humo tokea mwaka 1972.

M23 waibua wasi wasi mashariki mwa Kongo

M23 waibua wasi wasi mashariki mwa Kongo

Mwanaharakati mmoja wa kutetea haki za binadamu amesema kuwa, waasi wa M23 wanazitishia familia za wahanga ambao walioko kwenye mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda wasitoe taarifa zozote zilizokuwa dhidi yao kwa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch. Mwanaharakati huyo ambayo hakuwa tayari kujitambulisha wasifa wake amesema kuwa, waasi wa M23 wamekuwa wakizituhumu familia za wahanga kwa kutoa taarifa zao kwa shirika hilo la kutetea haki za binadamu. Shirika la Human Rights Watch hivi karibuni lilitoa taarifa na kueleza kuwa, waasi wa M23 walioko mashariki mwa Kongo waliwahukumu adhabu ya kifo watu 44 bila ya kuwafungulia mashtaka katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Kongo, kwa makosa ya kuwabaka wanawake na wasichana 61 na kuwafanyisha kazi kwa nguvu watoto wadogo. Wakati huohuo, waasi wa M23 wanawashikilia vijana wasiopungua 50 kwa tuhuma za kushiriki kwenye maandamano yaliyopelekea kuchomwa moto maduka ya watu wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda huko mashariki mwa Kongo. Hayo yameelezwa na Luteni Kanali Vianney Kazarama Msemaji wa kundi la waasi wa M23.

Wednesday, July 24, 2013

Mufti wa Syria asisitiza kudumishwa amani na udugu


Mufti wa Syria asisitiza kudumishwa amani na udugu
Mufti wa Syria ametaka kudumishwa amani, mapenzi, udugu na utulivu nchini humo na kote ulimwenguni. Sheikh Ahmad Badruddin Hassun  ameashiria jinsi dini tukufu ya Kiislamu inavyosisitizia sana umuhimu wa kudumishwa amani na mapenzi baina ya watu na jinsi Mtume wa Uislamu (SAW) alivyolitia mkazo sana jambo hilo na amelaani vikali jinai zinazofanywa na makundi ya kigaidi huko Syria ikiwemo kuwaua ovyo raia kuharibu miji ya nchi hiyo.
Sheikh Ahmad Badruddin Hasun aidha amesema, magaidi wameshindwa huko Syria na kwamba mafanikio ya jeshi la nchi hiyo katika kuyaangamiza makundi ya kigaidi kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ni dhihirisho tosha kuwa siku za mwisho za magaidi hao zimekaribia. Sheikh Hasun amesema, njama za miaka miwili iliyopita za nchi za Magharibi na vibaraka wao wa Kiarabu katika eneo la Mashariki ya Kati za kutaka kuilazimisha serikali ya Damascus isalimu amri mbele ya matakwa yao  zimegonga ukuta na kwamba nchi hizo sasa zinajaribu kila ziwezalo ili kujipapatua kutoka kwenye kinamasi zilichokwamba ndani yake huko Syria.

US yaitaka Rwanda isiwasaidie waasi wa M23


US yaitaka Rwanda isiwasaidie waasi wa M23
Marekani imeitaka Rwanda kuacha kuwaunga mkono waasi wa Machi 23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Washington imesema, kuna ushahidi kwamba maafisa wa jeshi la Rwanda wanawasaidia waasi wa M23. Hii ni radiamali ya kwanza kutolewa na Washington kufuatia mapigano yaliyojiri hivi karibuni kati ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali ya Kinshasa karibu na mji wa Goma, ambao ndio mji mkubwa zaidi huko mashariki mwa Kongo na ni eneo tajiri kwa madini. Jen Psaki, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani amesema, Washington inaitaka Rwanda iache mara moja kuwaunga mkono waasi wa Machi 23 na kuondoa vikosi vyake huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wito huo umetolewa ikiwa zimesalia siku tatu kabla ya John Kerry, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kuwa mwenyekiti wa kikao maalumu cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kitakachojadili eneo la maziwa makuu ya Afrika.  

11 wauawa katika siku mbili za machafuko Misri


11 wauawa katika siku mbili za machafuko Misri
Watu wasiopungua 11 wameuawa katika siku mbili za machafuko kati ya wafuasi na wapinzani wa Muhammad Morsi, rais aliyepinduliwa na jeshi nchini humo. Watu waliokuwa na silaha waliwavamia wafuasi wa Morsi waliokuwa wameketi chini karibu na Chuo Kikuu cha Cairo hapo jana na kuwauwa wawili kwa riasi.
Kuuliwa wafuasi hao wawili wa Morsi hapo jana kumeifanya idadi ya watu waliouawa huko Misri katika siku za Jumatatu na Jumanne kufikia 11.
Wakati huo huo watu wa familia ya Morsi wamesema watamchukulia hatua za kisheria Abdul Fatah as Sisi na jeshi lake kwa hatua yao ya kumuweka korokoroni Muhammad Morsi.
Itakumbukwa pia kuwa, juzi Jumatatu Rais Adly Mansour wa serikali ya mpito ya Misri alitoa wito wa kufikiwa mapatano ya kitaifa akisema kuwa ni muhimu kwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika na kuna udharura wa kuupa umuhimu mustakbali wa wananchi.  

Saturday, July 20, 2013

Jeshi la Nigeria kutuma wanajeshi Darfur, Sudan


Jeshi la Nigeria kutuma wanajeshi Darfur, Sudan
Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa litatuma wanajeshi 800 katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan ili kuisaidia serikali ya Khartoum na kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa jimboni humo. Akiwahutubu wanajeshi hao watakaopelekwa huko Darfur, Ahmad Jibrin kamanda wa kikosi cha pili cha jeshi la Nigeria amevitaka vikosi hivyo kuheshimu haki za binadamu na utamaduni wa watu wa Sudan katika muda wote wakataokuweko huko Darfur wakilinda amani. Kamanda huyo wa jeshi la Nigeria amesema kuwa askari wake yoyote atakayetekeleza jinai au uhalifu jimboni Darfur atakabiliwa na hatua kali. Hii ni katika hali ambayo jeshi la Nigeria jana lilitangaza kuwa lina mpango wa kuondoa baadhi ya wanajeshi wake walioko kaskazini mwa Mali baada ya kuboreka hali ya mambo katika eneo hilo na baadaye kuwapeleka wengine.

Wahamiaji wanaoelekea Kusini mwa Afrika hatarini


Wahamiaji wanaoelekea Kusini mwa Afrika hatariniIdadi kubwa ya wahamiaji wanaoelekea kusini mwa Afrika wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kiafya.
Hayo yamebainika katika utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM kwa ushirikiano na taasisi ya masuala ya afya kusini na mashariki mwa Afrika, PHAMESA. Utafiti huo unaonyesha hatari za kiafya zinazowakabili raia wanaohama makwao kutoka nchi za Maziwa makuu, Afrika Mashariki na hata pembe ya Afrika kuelekea Kusini mwa Afrika.
Matokeo ya awali ya utafiti huo yamewasilishwa kwenye mkutano wa pili wa mawaziri wa nchi za kusini mwa Afrika kuhusu mashauriano juu ya uhamiaji huko Maputo, Msumbiji.
Utafiti huo unaonyesha wahamiaji hao hukabiliwa na hatari kubwa za kiafya kutokana na mbinu za usafiri wanazotumia na wanapokamatwa hufungwa katika vizuizi vyenye suhula duni ambao wengi huambukizwa magonjwa hatari. Idadi kubwa ya wakimbizi hao hupoteza maisha njiani kutokana na kusafirishwa ndani ya kontena za mizigo zisizo na madirisha. Aidha wengi hukosa maji na chakula huku wanawake wakinajisiwa. Wakimbizi kutoka nchi kama Ethiopia na Somalia hulipa hadi dola elfu tano kwa safari iliyojaa hatari ya kufika Afrika Kusini nchi ambayo wanaoiona yenye fursa nzuri za kimaisha.
 

PICHA ZA MAPOKEZI YA WANAJESHI WA TANZANIA WALIOUWAWA MJINI DARFUR WALIVYOPOKELEWA


  
MAJENEZA YALIYOBEBA MIILI YA WAPIGANAJI HAO IKITOLEWA KUTOKA KWENYE NDEGE 
 
WANAJESHI MAALUMU WAKIWA WAMEBEBA MAJENEZA YALIYOBEBA MIILI YA WANAJESHI SABA WA JWTZ WALIOUWAWA DAFUR NCHINI SUDAN.

Friday, July 19, 2013

Uvamizi wa Wazayuni al-Aqswa walaaniwa


Uvamizi wa Wazayuni al-Aqswa walaaniwaSerikali halali iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina imelaani uvamizi wa mara kwa mara wa Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa. Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Masuala ya Quds katika Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa wa Serikali ya Palestina inayoongozwa na Waziri Mkuu Ismail Hania imebainisha kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kufanya uvamizi wa mara kwa mara katika mji wa Quds na dhidi ya msikiti mtakatifu wa al-Aqswa. Taarifa hiyo imebainisha kwamba, mipango na njama zote za adui Mzayuni zitashindwa kwani eneo hilo takatifu ni mali ya Waislamu wote ulimwengu. Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, Waislamu kote ulimwenguni wanapaswa kuuhami msikiti wa al-Aqswa na kutouruhusu utawala  wa Kizayunio wa Israel kufikia malengo yake haramu.

OIC: Wakazi wa Gaza, Palestina wasaidiwe


Nitajiandaa vipi kwa ajili ya mitihani bila umeme?Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imetoa wito wa kuungwa mkono wakazi wa Ukanda wa Gaza huko Palestina ambao wanakabiliwa na mzingiro. Taarifa ya OIC imewataka walimwengu kuwaunga mkono kwa kuwapatia misaada wananchi wa Gaza ambao kwa sasa wako katika hali mbaya ya kibinadamu. Wito huo wa OIC ambao umekuja baada ya ripoti yake kuhusiana na hali ya kibinadamu huko Gaza katika mwezi uliopita wa Juni, imesisitiza juu ya udharura wa kusaidiwa wananchi hao ili waweze kujidhaminia mahitaji muhimu kama ya chakula, maji, umeme na madawa. Ripoti ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imebainisha kwamba, hali ya kibinadamu huko Gaza inazidi kuwa mbaya na kwamba, kama hali itaendelea hivyo, basi hadi kufikia mwaka 2020, eneo la Ukanda wa Gaza litakumbwa na maafa ya kibinadamu na wakazi wa eneo hilo hawataweza kupata maji ya kunywa hata tone moja kutokana na kuendelea kuharibika vibaya miundo mbinu ya maji na umeme.  Eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina lina takribani wakazi milioni mbili na linakabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta, kukatikatika umeme na uhaba wa maji katika kipindi hiki cha msimu wa joto kali. Utawala wa Kizayuni usio na huruma, ulianza kutekeleza mzingiro dhidi ya Gaza tangu mwaka 2007 na hali ya kibinadamu katika eneo hilo imezidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

UN yataka utulivu urejeshwe Guinea Conakry

UN yataka utulivu urejeshwe Guinea ConakryKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kurejeshwa amani na utulivu huko Guinea Conakry baada ya makumi ya watu kuuawa kufuatia mapigano ya kikabila yaliyotokea katika mji mmoja nchini humo. Ban ki-Moon kupitia msemaji wake ameeleza wasi wasi mkubwa ulionao Umoja wa Mataifa kuhusiana na mapigano ya kikabila yaliyozuka katika mji wa N'Zerekore ambao ni wa pili kwa idadi kubwa ya watu nchini humo baada ya mji mkuu Conakry. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka wananchi wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika kudumisha utulivu na amani na kujiepusha na hatua yoyote ile yenye kupelekea amani na usalama kuwa hatarini. Aidha Ban ki-Moon amewataka viongozi wa kitaifa na kikabila kulinda kudhamini usalama wa roho na mali za watu na kuheshimu sheria. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito pia wa kuandaliwa mazingira mazuri kwa ajili ya uchaguzi wa Bunge uliopangwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu. Zaidi ya watu  54 wameuawa hadi sasa  katika mapigano makali ya kikabila yaliyotokea katika mji wa N'Zerekore nchini Guinea Conakry. Inaelezwa, mapigano hayo yalianza baada ya watu wa kabila la Guerze kumpiga na kumuua kijana mmoja wa ukoo wa Konianke kwa tuhuma za wizi.

Ramadhani yapandisha bei za vyakula Tanzania


Ramadhani yapandisha bei za vyakula Tanzania
Bei za vyakula katika mwezi huu wa Ramadhani zinaripotiwa kupanda nchini Tanzania hususan katika jiji la Dar es Salaam. Baadhi ya vyakula ambavyo hutumiwa na Waislamu kama futari zinaonekana kupanda mno katika masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi zinasema, maeneo ya Dar es Salaam kama Tabata Kimanga, Bima na hata Segerea yanashuhudia bidhaa za vyakula zikiwa juu ukilinganisha na maeneo ya Kariakoo, Vingunguti na hata Magomeni. Bidhaa kama magimbi, viazi zinadaiwa kupanda kutokana na ugumu wa upatikanaji wake katika masoko. Baadhi ya wafanyabiashara wanasema, kwa kipindi hiki mahitaji ni makubwa kuliko upatikanaji wa bidhaa, na kwamba, hali hii imesababishwa na mvua kutokunyesha kwa wakati na kusababisha uhaba wa mavuno. Aidha katika mikoa mingine ya Tanzania pia kumeripotiwa kupanda bei za vyakula vya mwezi wa Ramadhani kama mihogo, magimbi, viazi na maboga. Baadhi ya wafanyabiashara pia wamekuwa wakilangua kwa makusudi vyakula wakifahamu kwamba, katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani bidhaa hizo zinahitajika sana.

Wednesday, July 17, 2013

HUYU NDIYO IMAMU ALIYEMALIZA QUR-AN YOTE RAMADHANI YA PILI KATIKA SWALA YA TARAWEHE.


Imamu wa Msikiti Mkubwa uliyopo kusini nchini Saudi arabia, Sheikh Ahmad Hawashi, alifanikiwa kuhitimisha Qur-an yote juzu 30 ramadhani ya pili kwa tarawehe Tatu, kawaida swala ya tarawehe huanza usiku unaonekana mwezi.
Kwa mujibu wa Gazeti la Ambaa la nchini Kuwait, Sheikh Hawashi ni maarufu kwa kurefusha swala ya tarewehe, na kawaida uhitimisha Qur-an mara 10 kila Ramadhan.
Imamu huyo alirefusha swala hiyo ya tarawehe mpaka karibu na swala ya alfajiri.
Sheikh Hawashi kitaluma alihitimu masomo ya sayansi katika shule ya sekondari na aliwai kuajiliwa na Taasisi ya kuamrisha mema na kukataza maovu, kutoka na utenaji wake mzuri wa kazi, Sheikh Hawashi aliteuliwa kuwa Msaidizi wa rais wa taasisi hiyo.

SHEIKH WA WILAYA YA ARUMERU AMWAGIWA TINDIKALI

  
 
Sheikh Said Juma Makamba akiwa hospitali
Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha.

Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.

Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei.

Shekhe Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya swala hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao walikuwa wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala.

Alisema hata hivyo, kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu akiwa amesimama jirani na mlango.

Alieleza kuwa wakati akitaka kumwangalia zaidi alishtukia mtu

 huyo akiinua mkono na kumwagia maji yaliyompatia maumivu makali usoni na kifuani.

‘’Wakati natoka msalani nikipitia uwani kwangu niliona kama mtu ameinama pembeni yangu wakati najaribu kumsogelea ili nijue ni nani nilihamaki mtu huyo akinimwagia maji yaliyonisababisha maumivu makali sana yenye asili ya moto na ngozi kuanza kubabuka,’’ alisema shekhe huyo.

Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo alianza kupiga kelele kuomba msaada ambapo majirani walijitokeza na kumpa msaada wa kumpeleka hospitali, kwa vile wakati huo macho yake yalikuwa hayaoni na wakati wote alikuwa  akilia.

Pamoja na kujeruhiwa vibaya sehemu za usoni, kifuani na  mgongoni, pia ana majeraha  kwenye mikono na machoni na hali yake bado ni mbaya japo madaktari wanaendelea kumpatia matibabu.

Kaimu Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud akizungumzia tukio hilo alieleza kushitushwa nalo akisema limefanana na lile la Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdulaziz Jonjo ambaye mwaka jana alilipuliwa kwa bomu nyumbani kwake akiwa amelala.

Alisema kuwa matukio hayo yamekuwa yakijirudia huku wahusika wakishindwa kutiwa mbaroni na kudai kuwa matukio hayo yanahusiana na masuala ya kigaidi. Aliongeza kuwa pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, lakini wamekuwa hawapati matunda ya kukamatwa kwa watuhumiwa ingawa alisema wanajulikana.

Kwa upande wake,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba taarifa zitatolewa pindi washukiwa watakapotiwa mbaroni kwani uchunguzi bado unaendelea na kwamba hakuna  mtu anayeshikiliwa hadi sasa.

Tuesday, July 16, 2013

MTOTO AZALIWA NA TASBIHI SHINGIONI MWAKE


clip_image001Maelfu ya watu walifika hospitali binafsi ya uzazi kwenye jiji la Kotaworo eneo la Bida, iliyopo jimbo la Niger juzi Jumapili, kwa lengo la kwenda kumshuhudia mtoto wa kike aliyezaliwa akiwa amevaa rozari ya Kiislamu (Tasbihi) shingoni mwake.
Inaelezwa kwamba mama wa mtoto huyo ambaye ana miaka ya kati, Adijat, alikimbizwa hospitali karibu na nyumbani kwa Pa Mohammed Bello Masaba, mda wa saa 8 mchana na baada ya pilika za uzazi alifanikiwa kujifungua mtoto huyo.
Kwa mujibu wa mmiliki wa hospitali hiyo ya uzazi, Alhaji Abubakar Baiwa Shasha ambaye ndiye aliyesimamia zoezi hilo la kujifungua alisema, “Nilishtuka nilipoona mtoto anatoka akiwa na Tasbihi shingoni mwake, na wakati wa uzazi mtoto alizaliwa akiwa na Rozari nyeusi.” Alisema Shasha.
“Ila nilishangaa baada ya muda rozari hiyo ilibadilika na kuwa nyeupe huku kukiwa na watu wengine wamezunguka.”
Mara baada ya habari hiyo kusambaa mjini, maelfu ya watu walifika kwenye hospitali hiyo ya uzazi huku wakisema “Allahu Akibar; Allahu Akibar (Mungu ni Mkubwa) huku wakifika na kumgusa mtoto huyo.”
Juhudi za kumpata Baba wa mtoto huyo aitwaye Isah, ambaye anatokea eneo la Loma ndani ya Jimbo la Kwara State zilishindikana baada ya kukataa kuongea na mtoa habari.
Mwanachuo mmoja wa Kiislamu, Malam Idiris Ndajiwo alisema, kuzaliwa kwa mtoto huyo akiwa na rozari
 “inaonyesha ukuu wa Allah. Kuzaliwa kwa mtoto huyu leo, kwenye mji huu na eneo hili (Kutaworo) ni kitu kikubwa kwa Waislamu. Hii hakika inakuja kuonyesha kwamba Allah ndiye mwenye kupanga kwa lolote kutokea kwa yeyote kwenye ulimwengu huu.

RAIS MUGABE AWATAKA MSHOGA NA WASAGAJI NCHINI MWAKE WAZALIANE LASIVYO ATAWAFUNGA JELA


RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametoa kali ya mwaka kwa kuwachimba mkwara Mashoga na Wasagaji kwamba wasipotiana mimba ni lazima atawafunga jela.
Mugabe ametoa kali hiyo Ijumaa  wakati akizindua kampeni za chama chake cha kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika mwezi huu.
 
Isome taarifa nzima ya rais huyo mwenye umri mkubwa aliye madarakani duniani na ambaye wazungu wanamgwaya kwa misimamo yake isiyoyumba.
President Robert Mugabe on Friday threatened to jail gay and lesbian couples who fail to conceive any offspring as he launched his party’s campaign for this month’s general election.
 
The Zanu PF leader also attacked bitter rival and coalition partner Morgan Tsvangirai for his bed-hopping habits saying it was inconceivable that such a character could want to lead the country.Mugabe, a rabid critic of homosexuality returned to the theme as he addressed thousands of supporters in Harare’s Highfield township.He said he was shocked to learn that US President Barack Obama had called on African countries to embrace the practice.

Friday, July 5, 2013

Israel yatishia kujenga hekalu ndani ya al Aqswa


Israel yatishia kujenga hekalu ndani ya al AqswaWaziri wa Nyumba wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa, watajenga hekalu kwa ajili ya Mayahudi ndani ya ua wa msikiti Mtukufu wa al Aqswa. Uri Ariel ambaye ni mwanachama wa chama chenye misimamo mikali cha 'Jewish Home' amesema kwamba, Baraza la Mawaziri la Israel limesimamisha ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan lakini kwamba atahakikisha kuwa hekalu la Mayahudi linajengwa ndani ya Masjidul Aqswa.
Huku akitoa matamshi ya kufurutu ada na ya kibaguzi waziri huyo wa Israel sambamba na kubainisha kuwa, kuna matakwa ya kuundwa serikali mbili za Palestina na Israel amesema kwamba, njia pekee na ya uhakika eti ni kuwepo serikali moja tu ya Israel katika eneo hilo.
Inafaa kukumbusha hapa kuwa, viongozi wa utawala ghasibu wa Israel wanafanya kila njama ili waweze kuharibu athari na utambulisho wa Kiislamu na Kiarabu katika mji wa Quds kwa lengo la kuuyahudisha mji huo

Wafuasi wa Mursi kuandamana leo Misri


Wafuasi wa Mursi kuandamana leo Misri
Maandamano ya mirengo ya Kiislamu yaliyoitishwa na harakati ya Ikhawanul Muslimin ya Misri yanatarajiwa kufanyika leo nchini humo baada ya mshuko wa swala ya Ijumaa, ili kupinga hatua ya jeshi ya kumuuzulu rais Muhammad Mursi.  Ikhawanul Muslimin ya Misri jana iliwataka wananchi wa nchi hiyo kuandamana kwa amani baada ya swala ya Ijumaa katika maandamano yaliyopewa jina la 'Ijumaa ya Kukataa'. Maandamano hayo yataonesha ni kwa kiwango gani rais huyo aliyeuzuliwa bado anaungwa mkono na wananchi, na pia hatua zitakazochukuliwa na jeshi kukabiliana nayo.
Muhammad Musri kiongozi aliyeondolewa madarakani wa Misri anatoka katika harakati ya Ikhwanul Muslimin na alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokraia  na Wamisri baada ya mapinduzi ya wananchi yaliyomng'oa madarakani dikteta Hosni Mubarak.

Serikali ya Kongo DRC yaazimia kukabiliana na M23


Serikali ya Kongo DRC yaazimia kukabiliana na M23
Serikali ya Jamhuri ya Kidomekrasia ya Kongo imetangaza kuwa itakabiliana vilivyo na vitisho vya waasi wa M23 nchini humo. Lambart Mende msemaji wa serikali ya Kongo DRC jana alitangaza kuwa, serikali ya Kinshasa inavizingatia vitsho vya waasi wa M 23 hasa baada ya waasi hao kuuteka tena mji wa Goma, ambao ni makao makuu ya mkoa wa Kivu Kaskazini.
Msemaji huyo wa serikali ya Kongo ameongeza kwamba, suluhisho pekee kwa waasi hao ni kuendelea na mazungumzo ya kusaka amani huko Kampala Uganda na kuwatahadharisha kuwa, vikosi vya Umoja wa Mataifa viko katika eneo la Mashariki ya Kongo ambako vinashirikiana na wanajeshi wa Kongo, hivyo ni bora M23 waache machafuko.

Assad: Wapinzani wangu wameshindwa kunipindua


Assad: Wapinzani wangu wameshindwa kunipindua
Rais Bashar la Assad wa Syria amesema kuwa, wapinzani wake wameshindwa kumpindua ijapokuwa wametumia zana zote walizonazo. Assad amekataa kuitwa matukio yanayojiri nchini Syria kwa zaidi ya miaka miwili kuwa harakati za mapinduzi na badala yake amesisitiza kuwa, ni njama za Wamagharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu za kuidhoofisha nchi yake. Aidha Rais wa Syria amepongeza maandamano makubwa ya Wamisri yaliyopelekea kungushwa serikali ya rais Muhammad Musri na kusema kwamba hatua hiyo ni mafanikio makubwa.
 Hayo yamejiri huku muungano wa wapinzani wa Syria (SNC) unaoungwa mkono na nchi za Magharibi kwa mara nyingine ukifanya jitihada za kuungana na kumchagua kiongozi mpya katika mkutano unaofanyika mjini Istanbul.