Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imetoa wito wa kuungwa
mkono wakazi wa Ukanda wa Gaza huko Palestina ambao wanakabiliwa na
mzingiro. Taarifa ya OIC imewataka walimwengu kuwaunga mkono kwa
kuwapatia misaada wananchi wa Gaza ambao kwa sasa wako katika hali mbaya
ya kibinadamu. Wito huo wa OIC ambao umekuja baada ya ripoti yake
kuhusiana na hali ya kibinadamu huko Gaza katika mwezi uliopita wa Juni,
imesisitiza juu ya udharura wa kusaidiwa wananchi hao ili waweze
kujidhaminia mahitaji muhimu kama ya chakula, maji, umeme na madawa.
Ripoti ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imebainisha kwamba,
hali ya kibinadamu huko Gaza inazidi kuwa mbaya na kwamba, kama hali
itaendelea hivyo, basi hadi kufikia mwaka 2020, eneo la Ukanda wa Gaza
litakumbwa na maafa ya kibinadamu na wakazi wa eneo hilo hawataweza
kupata maji ya kunywa hata tone moja kutokana na kuendelea kuharibika
vibaya miundo mbinu ya maji na umeme. Eneo la Ukanda wa Gaza huko
Palestina lina takribani wakazi milioni mbili na linakabiliwa na uhaba
mkubwa wa mafuta, kukatikatika umeme na uhaba wa maji katika kipindi
hiki cha msimu wa joto kali. Utawala wa Kizayuni usio na huruma, ulianza
kutekeleza mzingiro dhidi ya Gaza tangu mwaka 2007 na hali ya
kibinadamu katika eneo hilo imezidi kuwa mbaya siku baada ya siku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment