Bei za vyakula katika mwezi huu wa Ramadhani zinaripotiwa kupanda
nchini Tanzania hususan katika jiji la Dar es Salaam. Baadhi ya vyakula
ambavyo hutumiwa na Waislamu kama futari zinaonekana kupanda mno katika
masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi zinasema, maeneo
ya Dar es Salaam kama Tabata Kimanga, Bima na hata Segerea yanashuhudia
bidhaa za vyakula zikiwa juu ukilinganisha na maeneo ya Kariakoo,
Vingunguti na hata Magomeni. Bidhaa kama magimbi, viazi zinadaiwa
kupanda kutokana na ugumu wa upatikanaji wake katika masoko. Baadhi ya
wafanyabiashara wanasema, kwa kipindi hiki mahitaji ni makubwa kuliko
upatikanaji wa bidhaa, na kwamba, hali hii imesababishwa na mvua
kutokunyesha kwa wakati na kusababisha uhaba wa mavuno. Aidha katika
mikoa mingine ya Tanzania pia kumeripotiwa kupanda bei za vyakula vya
mwezi wa Ramadhani kama mihogo, magimbi, viazi na maboga. Baadhi ya
wafanyabiashara pia wamekuwa wakilangua kwa makusudi vyakula wakifahamu
kwamba, katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani bidhaa hizo
zinahitajika sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment