skip to main |
skip to sidebar
Jeshi la Nigeria kutuma wanajeshi Darfur, Sudan
Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa litatuma wanajeshi 800 katika
jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan ili kuisaidia serikali ya Khartoum
na kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa
jimboni humo. Akiwahutubu wanajeshi hao watakaopelekwa huko Darfur,
Ahmad Jibrin kamanda wa kikosi cha pili cha jeshi la Nigeria amevitaka
vikosi hivyo kuheshimu haki za binadamu na utamaduni wa watu wa Sudan
katika muda wote wakataokuweko huko Darfur wakilinda amani. Kamanda huyo
wa jeshi la Nigeria amesema kuwa askari wake yoyote atakayetekeleza
jinai au uhalifu jimboni Darfur atakabiliwa na hatua kali. Hii ni katika
hali ambayo jeshi la Nigeria jana lilitangaza kuwa lina mpango wa
kuondoa baadhi ya wanajeshi wake walioko kaskazini mwa Mali baada ya
kuboreka hali ya mambo katika eneo hilo na baadaye kuwapeleka wengine.
No comments:
Post a Comment