
Ongeri amesema kuwa, wanadiplomasia wa nchi za Ulaya wanafanya njama za kuathiri matokeo ya uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Kenya amesisitiza kuwa, matamshi ya wanadiplomasia wa nchi hizo kuhusiana na uchaguzi ujao wa rais nchini Kenya yanachochea anga ya kisiasa nchini humo.
Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ambaye anawania nafasi ya urais kwa tiketi ya muungano wa CORD aliwataka wasimamizi wa uchaguzi kutoka Ulaya kufanya tathmini ya kina na uhakika katika hatua za awali za uchaguzi mkuu wa Kenya. Uchaguzi mkuu wa nchi hiyo umepangwa kufanyika tarehe 4 Machi mwaka huu.
No comments:
Post a Comment