Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 31, 2012

Waasi wa A.ya Kati kufikiria kugawana madaraka



Waasi wa A.ya Kati kufikiria  kugawana madaraka
Waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekutana na Mwenyekitiwa  Umoja wa Afrika na kusema kuwa wako tayari kuchunguza pendekezo lililotolewa na Rais wa nchi hiyo la kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa.
Msemaji wa muungano wa waasi hao wa Seleka amesema kwamba, hata hivyo lengo lao si kuingia serikalini bali ni kuwawezesha wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati  kupata maendeleo na kujitegemea.
Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati jana alisema kuwa yuko tayari kugawana madaraka na viongozi wa muungano huo wa waasi na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Bozize alisema hayo baada ya kukutana na Thomas Yayi Boni, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mjini Bangui.

Migodi 4000 ya dhahabu yagunduliwa Darfur


Migodi 4000 ya dhahabu yagunduliwa Darfur Waziri wa Madini wa Sudan ametangaza habari ya kugunduliwa migodi 4000 ya dhahabu huko Jebel Amir katika jimbo la Darfur ya Kaskazini yenye uwezo wa kuzalisha tani 15 za dhahabu kwa mwaka sawa na kilo 70 kwa siku. Kamal Abdullatif amewaambia waandishi wa habari baada ya mkutano wa baraza la mashauriano la Wizara ya Madini ya Sudan kwamba wizara yake itaendelea kuzalisha madini hayo ili kuboresha uchumi wa taifa.

Serikali ya Syria inaunga mkono mazungumzo


Serikali ya Syria inaunga mkono mazungumzo
Waziri Mkuu wa Syria Wael al Halqi amesema kuwa serikali ya Damascus itakubali mpango wowote utakaobuniwa ili kutatua mgogoro wa nchi hiyo kupitia mazungumzo.
Damascus imesema hayo baada ya Lakhdar Brahimi, mpatanishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syra kutangaza kwamba, ana mpango wa kuhitimisha mapigano nchini humo. Al Halqi amesema, serikali ya Damascus inaunga mkono mpango wa maridhiano ya kitaifa na itakubali suluhisho lolote la kumaliza mgogoro wa nchi hiyo kwa njia za amani,

Waasi wa A.ya Kati kufikiria kugawana madaraka


Waasi wa A.ya Kati kufikiria  kugawana madaraka
Waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekutana na Mwenyekitiwa  Umoja wa Afrika na kusema kuwa wako tayari kuchunguza pendekezo lililotolewa na Rais wa nchi hiyo la kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa.
Msemaji wa muungano wa waasi hao wa Seleka amesema kwamba, hata hivyo lengo lao si kuingia serikalini bali ni kuwawezesha wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati  kupata maendeleo na kujitegemea.
Rais Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya Kati jana alisema kuwa yuko tayari kugawana madaraka na viongozi wa muungano huo wa waasi na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Bozize alisema hayo baada ya kukutana na Thomas Yayi Boni,

Idadi ya Watanzania yaongezeka na kufikia milioni 44.9


Idadi ya Watanzania yaongezeka na kufikia milioni 44.9Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo ametangaza matokeo ya sensa ya makazi nchini humo.
Akihutubia katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Kikwete amesema, kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwezi Agosti mwaka huu wa 2012, Watanzania waongezeka kutoka watu milioni 34.4 hadi kufikia watu milioni 44.9. amesema idadi ya watu Tanzania bara ni 43.6 milioni na Zanzibar watu milioni 1.3.

Sunday, December 30, 2012

Jinai za utawala wa Aal Khalifa hazitaendelea milele

Jinai za utawala wa Aal Khalifa hazitaendelea milele
Mkuu wa Kamati ya Kupambana na Mateso nchini Bahrain ameeeleza kuwa vitendo vya mabavu vya utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa na kuwakandamiza raia wa nchi hiyo vimebadilika na kuwa siasa za kila siku za utawala huo na kwamba bilaya  shaka yoyote siasa  hizo haziwezi kudumu milele.
Rodney Shakespeare, Mkuu wa Kamati ya Kupambana na Mateso nchini Bahrain amemtaja Waziri Mkuu wa Bahrain ambaye kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita anashikilia wadhifa huo kuwa ndiye mhusika mkuu wa kuuliwa watoto, kutiwa mbaroni wanawake na kuteswa wafungwa huko Bahrain.

UN yahuzunishwa na kifo cha aliyebakwa India


UN yahuzunishwa na kifo cha aliyebakwa IndiaKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitishwa na kifo cha mwanachuo wa kike aliyekuwa akisomea taaluma ya udaktari huko India, aliyefariki dunia baada ya kubakwa na wanaume sita ndani ya basi la abiria lililokuwa katika mwendo.  Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Ban Ki Moon amesikitishwa na kifo cha msichana huyo wa Kihindi na kutoa mkono wa pole kwa familia na ndugu wa mhanga wa jinai hiyo. Ban Ki moon pia ameitaka serikali ya India kuchukua hatua kali ili kuzuia kukaririwa tena janga kama hilo huko India. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kupewa adhabu kali waliotenda jinai hiyo na kuwasaidia waathiriwa wengine wa jinai kama hiyo huko India. Msichana huyo wa Kihindi aliyekuwa na umri wa miaka 23 alivamiwa na kubakwa na wanaume sita tarehe 16 mwezi huu na aliaga dunia jana akiwa hospitalini kwa matibabu nchini Singapore.

Mkutano wa al Bashir na Kiir kufanyika Januari 13


Rais Omar al Bashir wa Sudan (kushoto) na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Rais Omar al Bashir wa Sudan (kushoto) na Rais Salva Kiir wa Sudan KusiniEthiopia imeainisha tarehe 13 Januari kuwa siku ya kufanyika mkutano kati ya Marais wa Sudan na Sudan Kusini Omar al Bashir na Salva Kiir huko Addis Ababa mji mkuu uwa Ethiopia. Hailemariam Dessalegn, Waziri Mkuu wa Ethiopia amewataka marais hao wawili kuhudhuria mkutano huo kama ilivyopangwa. Wiki iliyopita Waziri Mkuu wa Ethiopia alizitembelea Khartoum na Juba na kuhakikishiwa kwamba Marais hao wa Sudan mbili watashiriki kwenye mkutano huo. Mkutano ujao kati ya Rais Omar al Bashir wa Sudan na mwenzake wa Sudan Kusini,

Mazoezi ya kijeshi ya "Velayat 91" yaendelea Iran


Mazoezi ya kijeshi ya fukweni angani na baharini ya JKI katika maji ya ghuba ya uajemi ya "Velayat 91" Mazoezi ya kijeshi ya fukweni angani na baharini ya JKI katika maji ya ghuba ya uajemi ya "Velayat 91"
Mazoezi ya kijeshi ya "Velayat 91" yameendelea leo hapa nchini Iran katika siku yake ya tatu.
Maneva hayo ya siku sita yalianza juzi, tarehe 28 Disemba, na yanafanyika katika eneo pana la fukweni, baharini na angani kwenye lango la Hormuz, Bahari ya Oman, kaskazini mwa Bahari ya Hindi, Ghuba ya Aden na lango la Babul Mandab.

Marekani yazidi kujizatiti kijeshi barani Afrika


Wanajeshi wa Chad wakipiga doria katika mji mkuu N'djamena
Wanajeshi wa Chad wakipiga doria katika mji mkuu N'djamena
Marekani imetuma vikosi vyake nchini Chad katika hatua ambayo inaonekana wazi ni kuzidi kujizatiti kijeshi barani Afrika.
Sababu iliyotajwa na Marekani ya kutuma vikosi vyake nchini Chad ni wasiwasi wa Washington kuhusu usalama wa raia wake kutokana na kuzidi kusonga mbele waasi katika nchi jirani na Chad yaani Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Katika barua yake kwa maspika wa mabunge mawili ya Marekani, Rais Barack Obama wa nchi hiyo amesema kuwa, raia kadhaa wa Marekani wameondolewa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui tangu tarehe 27 Disemba na hivi sasa kikosi cha wanajeshi 50 wa Marekani kimetumwa nchini Chad.

Saturday, December 29, 2012

Utawala wa Bahrain wafananishwa na Wanazi


Utawala wa Bahrain wafananishwa na WanaziMkuu wa Kamati ya Kupambana na Vitendo vya Utesaji nchini Bahrain ameufananisha utawala wa Aal Khalifa wa nchi hiyo na utawala wa Wanazi nchini Ujerumani  na kuongeza kuwa, Waziri Mkuu wa Bahrain ni mtuhumiwa nambari moja katika kuwauwa wanawake na kuwatesa wananchi wa nchi hiyo. Amesema kuwa utawala wa Aal Khalifa hauthubutu hata mara moja kuitisha uchaguzi huru nchini Bahrain, kwani unajua wazi kwamba uchaguzi wowote utakaofanyika nchini humo utaung'oa utawala huo wa kifalme. Ameongeza kuwa, Waziri Mkuu wa Bahrain ni mtenda jinai nambari moja katika kuwauwa watoto,

22 wafa katika ajali ya jahazi Guinea Bissau


22 wafa katika ajali ya jahazi Guinea Bissau
Watu wasiopungua 22 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 70 hawajulikani waliko baada ya jahazi waliyopanda kuzama nchini Guinea Bissau. Taarifa zinasema kuwa, jahazi hilo lilizama huku ikiwa imebeba zaidi ya abiria 97 ikitoka katika kisiwa cha Boloma kilichopo katika bahari ya Atlantiki na kuelekea bandari ya Bissau magharibi mwa Afrika. Duru za hospitali zinasema kuwa, hadi sasa viwiliwili vya wahanga 22 vimehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti, huku juhudi zikiendelea za kuwatafuta wahanga wengine 72 ambao hawajulikani waliko. Chanzo cha ajali hiyo imeelezwa kuwa ni kupakia abiria kupita kiasi na shehena kubwa ya mizigo.

Waasi wa J/A/Kati wakubali kuzungumza na serikali



Waasi wa J/A/Kati wakubali kuzungumza na serikali
Wawakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na waasi wa Seleka wameafikiana juu ya kufanya mazungumzo ya amani. Guy - Pierre Garcia Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika ya Kati amesema kuwa, wawakilishi wa  serikali ya Bangui na waasi wa Seleka hapo jana walikubaliana  kuanza  kufanya mazungumzo bila ya masharti. Baadhi ya duru zinasema kuwa, mazungumzo kati ya pande hizo mbili yenye lengo la kuleta amani na uthabiti nchini humo yatafanyika tarehe 10 Januari mwakani huko Libreville, mji mkuu wa Gabon. Waasi wa Seleka walianzisha operesheni kamambe ya kijeshi wiki mbili zilizopita, na sambamba na kuteka miji kadhaa walikuwa wanaukaribia mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

Nigeria kutuma majeshi ya kulinda amani Somalia


Nigeria kutuma majeshi ya kulinda amani SomaliaSerikali ya Nigeria imetangaza kuwa hivi karibuni itatuma wanajeshi 140 nchini  Somalia chini ya mwamvuli wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika AMISOM. Kayode Aderanti Afisa Mwandamizi wa Vikosi vya Kulinda Amani katika jeshi la Nigeria amesema kuwa, wanajeshi hao wa Nigeria wanatumwa nchini Somalia kutokana na makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya serikali ya Abuja na Umoja wa Afrika. Nchi ya Somalia inashuhudia mapigano na machafuko tokea ulipopinduliwa utawala wa Jenerali Muhammad Siad Barre mwaka 1991, kati ya serikali ya mpito na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka likiwemo al Shabab. Umoja wa Afrika tokea mwaka 2007 uliunda kikosi cha kulinda amani AMISOM kwa shabaha ya kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia kukabiliana  na makundi ya waasi nchini humo.

Wednesday, December 26, 2012

Israel iliua watoto 41 katika vita vya Gaza


Israel iliua watoto 41 katika vita vya Gaza Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadmau Amnesty International limethibitisha kwamba watoto 41 wa Kipalestina waliuawa katika mashambulizi ya siku 8 yaliyofanywa na majeshi ya utawala wa Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza. Taarifa iliyotolewa leo na shirika hilo imeeleza kuwa, maafa yaliyosababishwa na majeshi ya Israel katika kipindi cha siku 8 ni makubwa zaidi kuliko mashambulizi yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka 2008 huko Gaza. Amnesty International imeeleza kuwa, mauaji dhidi ya watoto katika vita vya utumiaji silaha, yanahesabiwa kuwa jinai kubwa dhidi ya binadamu. Amnesty International imezitaka kamati maalumu za Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na asasi nyingine za kimataifa kuendeleza uchunguzi wao kuhusiana na mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa Palestina wa eneo la Gaza.

Asilimia 63.8 ya Wamisri waunga mkono katiba mpya


Asilimia 63.8 ya Wamisri waunga mkono katiba mpya
Jumla ya asilimia 63.8 ya Wamisri waliopiga kura katika kura ya maoni ya hivi karibuni nchini humo wameunga mkono kuidhinishwa rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo. Samir Abu al Matti Mkuu wa Kamisheni Kuu ya Uchaguzi ya Misri ametangaza matokeo hayo jana katika mkutano na vyombo vya habari huko Cairo mji mkuu wa nchi hiyo. Wakati huo huo Hisham Qandil Waziri Mkuu wa Misri ametoa taarifa akisema kuwa hakuna aliyeshindwa kwenye kura hiyo ya maoni na kwamba katiba mpya ya Misri itakuwa ya Wamisri wote. Ameyataka pia makundi yote ya kisiasa kushirikiana na serikali ili kuisaidia nchi hiyo kufufua uchumi wake. 

Padri Ambros Mkenda apigwa risasi Zanzibar



Padri Ambros Mkenda apigwa risasi ZanzibarWatu wasiojulikana wamempiga risasi Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar na kumjeruhi. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma Muhammed amethibitisha tukio hilo huku jeshi la polisi likiendelea kuchunguza ili kubaini wahusika wa uhalifu huo.  Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikan la Mkunazini alidai hivi karibuni kumekuwepo vipeperushi vilivyosambazwa vikiwatisha watu wenye imani ya Kikristo na kuiomba serikali iongeze ulinzi na kuimarisha usalama. Aidha ameiomba serikali kuchukua hatua za tahadhari kwani matukio kama hayo yameanza kutokea kwa viongozi wa dini kuanzia kwa Sheikh Soraga aliyemwagiwa tindikali na hivi sasa Padri Ambros.

Marekani katika magendo ya silaha Afrika


Marekani katika magendo ya silaha Afrika
Nchi zilizoko katika eneo la kusini mwa Sahara Kuu huko kaskazini mwa Afrika, zimegeuka kuwa moja kati ya masoko muhimu ya magendo ya silaha ulimwenguni katika kipindi cha miongo ya hivi karibuni. Duru zinasema kuwa, Marekani imekuwa kinara katika kulibadilisha eneo hilo kuwa soko kuu la magendo ya silaha duniani. Duru hizo zimeeleza kuwa, nchi za China na Russia nazo pia zimetumbukia kwenye mkumbo huo kwani zinatoa mikopo kama inavyofanya Marekani kwa minajili ya kuuza silaha zao katika eneo hilo. Silaha zinazouzwa kwa magendo katika eneo hilo la Sahara Kuu zinaangukia mikononi mwa maeneo yanayokumbwa na mapigano ya kikabila, na maeneo ambayo yanadhibitiwa na waasi kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Somalia. Taarifa zinasema kuwa, silaha hizo licha ya kuchangia machafuko, huongeza hatari ya kuibuka mapigano mapya ya ndani na nje ya mipaka ya nchi hizo.

Kiongozi wa upinzani Zambia akamatwa na kuachiliwa


Kiongozi wa upinzani Zambia akamatwa na kuachiliwaKiongozi wa upinzani Zambia Nevers Mumba amekamatwa leo Jumatano na vikosi vya usalama na kuachiliwa baada ya kusailiwa.
Hii ni mara ya pili kwa Mumba kukamatwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita kwa tuhuma ya kuitisha mkutano wa hadhara bila kibali.
Mumba ambaye zamani alikuwa mwanachama wa chama tawala cha MDC sasa yuko katika chama kikuu cha upinzani cha MMD na katika siku za hivi karibuni ameongoza maandamano dhidi ya serikali ya Rais Michael Sata.
Wanasiasa wa upinzani wanamtuhumu Rais Sata kuwa anawakandamiza wapinzani. Serikali ya Zambia imekataa kuwapatia wapinzani vibali vya maandamano katika mji mkuu Lusaka.
Alipochaguliwa mwaka jana, Rais Sata aliahidi kupambana na ubadhirifu wa fedha za uma na kubuni nafasi za ajira. Wapizani wanadai serikali imeshindwa kutekeleza ahadi hizo.

Monday, December 24, 2012

Maharamia wawaachia huru mateka 22 Somalia


Maharamia wawaachia huru mateka 22 SomaliaMateka 22 waliokuwa wametekwa nyara na maharamia kwa kipindi cha miaka miwili na miezi tisa nchini Somali, wameachiwa huru.
Hayo yametangazwa na viongozi wa serikali ya Somalia na kuongeza kuwa, mateka hao wameachiwa huru na maharamia hao katika pwani ya Puntland. Miongoni mwa walioachiwa huru ni pamoja na wafanyakazi wa meli ya Panama ya MV Iceberg 1, ambayo ilitekwa nyara mwishoni mwa mwaka 2010. Wafanyakazi hao ni raia wa Yemen, India, Ghana, Pakistan, Sudan na Uphilipino. Kuachiwa kwa watu hao kumefanyika baada ya wiki kadhaa tu ya kumalizika kwa oparesheni ya kikosi cha Gadi ya Pwani ambacho kiliasisiwa hivi karibuni na kupata mafunzo kutoka kwa shirika moja la usalama katika eneo hilo la Puntland. Juhudi za vikosi vya polisi kwa ajili ya kuwaokoa mateka hao na meli yao zilishindwa hapo tarehe 10 mwezi Septemba mwaka huu. Duru za habari kutika makao makuu ya Puntland, Garowe zimearifu kuwa, mateka hao wamekuwa wakipewa mateso mbalimbali na kwamba, alama za mateso na magonjwa mbalimbali zinaonekana katika miili ya watu hao.

Mpatanishi wa mgogoro wa Syria akutana na Assad


Mpatanishi wa mgogoro wa Syria akutana na  Assad
Lakhdar Brahimi mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syria amekutana na Rais Bashar al Assad mjini Damascus na kujadili mgogoro wa nchi hiyo.
Brahimi amesema pande hizo mbili zimebadilishana mawazo na kuchunguza njia gani zichukuliwe kwa ajili ya mustakbali wa nchi hiyo.
Katika upande mwingine Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amekosoa uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa magaidi wa Syria na kusema kwamba jambo hilo halikubaliki kabisa. Sergei Lavrov amesema, uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa magaidi wa Syria kwa kisingizo kuwa ni magaidi wazuri, ni jambo lisilokubalika. Ameongeza kuwa, iwapo pande za Magharibi zitaanza kuyagawa makundi ya kigaidi kati ya magaidi wabaya na magaidi wanaokubalika, suala hilo litahatarisha usalama wa Mashariki ya Kati na dunia nzima kwa ujumla.

Watoto 11 wafariki dunia katika ajali ya gari huko China


Watoto 11 wafariki dunia katika ajali ya gari huko China
Watoto 11 wa shule wamefariki dunia baada ya basi dogo lililokuwa limebeba abiria wengi kutumbukia kwenye dimbwi huko katika mkoa wa Jiangxi nchini China.
Basi hilo lililokuwa na watu 17 asubuhi ya leo kwa wakati wa China lilitumbukia katika dimbwi lililokuwa kando ya barabara karibu na mji wa Guixi. Maafisa wa eneo hilo wameripoti kuwa watu sita wakiwemo wanafunzi wanne, mwalimu na dereva wameondolewa kutoka sehemu ya ajali hiyo  na kupelekwa hospitalini.
Wahanga wa ajali hiyo walikuwa watoto waliokuwa na umri wa kati ya miaka minne na sita. Polisi ya China imemlaumu dereva kwa ajali hiyo na imefanikiwa kumtia mbaroni masaa machache baada ya ajali hiyo. Itakumbukwa kuwa baadhi ya barabara za China ni miongoni mwa barabara hatari duniani zinazosababisha makumi ya maelfu ya vifo vya watu kila mwaka.

Nigeria yaimarisha usalama kabla ya Krismasi


Nigeria yaimarisha usalama kabla ya Krismasi
Vikosi vya usalama vya jeshi la Nigeria vimeimarisha usalama nchi nzima kwa kuhofia mashambulizi ya wanamgambo wa Boko Haram wakati wa sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Maafisa wa polisi wametakiwa kutokwenda mapumzikoni na kuimarisha usalama wa kiwango cha juu, huku harakati za watu zikipunguzwa na makanisa kulindwa.
Kwa miaka miwili sasa Nigeria imekuwa ikikumbwa na milipuko na mashambulizi yanayolenga makanisa wakati wa sikukuu ya krismasi. Ripoti zinasema kuwa mashambulizi hayo yanafanywa na kundi lenye misimamo mikali la Boko Haram.
Licha ya ulinzi huo kuimarishwa hasa katika miji ya kaskazini mwa Nigeria, Jumapili ya jana kulitokea mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika ofisi za shirika la simu za mkononi katika mji wa Kano ingawa hakuna mtu aliyeuawa au kujeruhiwa.

Wapalestina zaidi ya 700 wameuawa nchini Syria


Wapalestina zaidi ya 700 wameuawa nchini Syria
Harakati ya Ukombozi ya Palestina (PLO) imetangaza kuwa Wapalestina zaidi ya 700 wameuawa huko Syria tangu kuzuka kwa mgogoro nchini humo  zaidi ya miezi 21 iliyopita.
Zacharia al Bahja, afisa wa PLO anayehusika na masuala ya wakimbizi amesema kuwa Wapalestina zaidi ya 700 wameuawa huko Syria tangu kuanza kwa machafuko nchini humo yaliyoyajumuisha pia kambi ya Yarmuk nchini humo. Roketi kadhaa zilivurumishwa jana jioni katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Yarmuk huko kusini mwa Damascus mji mkuu wa Syria, eneo ambalo wiki iliyopita lilishuhudia mapigano makali kati ya vikosi vya jeshi la Syria na wanamgambo wanaofadhiliwa na nchi za kigeni. Syria ilisisitiza jana kuwa wanajeshi wake hawajahusika kwa njia yoyote ile katika machafuko hayo.

Sunday, December 23, 2012

Wazanzibari waijia juu SMZ kuhusu Uamsho


WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU

WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU
KUFUATIKA KUKAMATWA KWA VIONGOZI WA JUMUIA YA KIISLAMU UAMSHO TAKRIBANI MIEZI MIWILI SASA NA MAHAKAMA JUZI KUTUPILIA MBALI OMBI LA DHAMANA LIMEWAPELEKEA WAISLAMU KUJA JUU NAKUTAKA VIONGOZI WAO HAO WAACHIWE HARAKA SANA.
HATUWA HIO IMEKUJA KUFUATIA KUTOLEWA KWA WARAKA ULIOELEZA KILA KITU WANACHOKIDAI WAISLAMU WARAKA AMBAO UMETOLEWA BAADA YA KUMALIZIKA KWA SALA YA IJUMAA NDANI YA MASJID JIBRIL ILIOPO MJI MKONGWE ULIOSEMA KAMA HIVI IFUATAVO.
UJUMBE MUHIMU KWA WAISLAMU WOTE.
WANANCHI NA WAISLAMU WA ZANZIBAR TUMECHOKA KUDHALILISHWA NA KUDHALILISHWA VIONGOZI WETU WA DINI YA KIISLAMU.
KWAMBA KATIKA NCHI HII HATUJAONA TANGU UHURU WA MAPINDUZI KUDHALILISHWA KWA MKIRISTO YOYOTE WALA KIONGOZI YOYOTE WA KANISA.
UDHALILISHAJI HUU UNATOKANA NA VIONGOZI WA SERIKALI DHIDI YA UISLAMU KUTOKANA NA SHINDIKIZO LA MAKANISA
INAONEKANA KUWA VIONGOZI WA SERIKALI WAKO TAYARI KUDHALILISHA HESHMA YAO, DINI YAO, WATU WAO NA NCHI YAO KWA AJILI YA KUTII AMRI ZA MAKANISA
KUTOKANA NA HAYO SISI WAISLAMU WA ZANZIBAR AMBAO TUMECHOSHWA NA VITIMBI UDHALILISHAJI WA DINI YETU,TUNAOMBA SERIKALI IWAACHIE HARAKA VIONGOZI WA KIISLAMU KABLA YA KRISMAS TAREHE 25/12/2012
ENDAPO MAOMBI HAYA YA WAISLAMU NA WANANCHI YATADHARAULIWA NA KUPUUZWA.WAISLAMU WATAAMUA CHA KUFANYA.
TAFADHALI FIKISHA UJUMBE HUU KWA MUISLAMU MWENZAKOAU TOA KOPI UIENEZE.
SORCE MASJID JIBRIL.

Friday, December 21, 2012

Watu wenye silaha wawashambulia askari Kodivaa


Watu wenye silaha wawashambulia askari Kodivaa
Duru za habari kutoka nchini Kodivaa zinaarifu kuwa, watu wasiojulikana wenye silaha wamekishambulia kituo cha upekuzi nchini humo na kuwajeruhi askari wawili. Watu walioshuhudia wamesema kuwa, askari walilazimika kujibu na hivyo kusababisha kuzuka mapigano kati ya vikosi vya usalama na watu hao wenye silaha. Tangu mwezi Agost mwaka huu Ivory Coast imekuwa ikishuhudia silsila ya mauaji ya kuvizia, yanayofanywa na watu wasiojulikana wenye silaha,

Makumi ya waasi wajisalimisha kwa serikali Sudan


Makumi ya waasi wajisalimisha kwa serikali SudanMakumi ya waasi wamejisalimisha kwa jeshi la Sudan. Mtandao wa habari wa Sudan Safari umeeleza kuwa, karibu viongozi 22 wa kundi la waasi la "Mrengo wa Mapinduzi" na makundi mengine ya waasi ambayo yanaendesha shughuli zao katika eneo la Abyei, wameamua kuweka chini silaha zao na kujisalimisha kwa askari wa serikali. Rahmat Abdur-Rahman, mmoja wa viongozi wa eneo la Abyei huko kusini mwa Sudan, amenukuliwa akisema kuwa, viongozi hao wa waasi wamethibitisha kuwa, makundi ya waasi hivi sasa yamedhoofika na yanazidi kupoteza nguvu zao siku hadi siku. Kwa mujibu wa viongozi hao wa waasi,

Viongozi wa kidini nchini Misri waandamana


Viongozi wa kidini nchini Misri waandamana
Viongozi wa kidini nchini Misri wamefanya maandamano ya kulaani hatua ya wafuasi wa rais wa zamani wa nchi hiyo, dikteta Hosni Mubarak, ya kufanya mashambulizi dhidi ya viongozi hao na misikiti nchini humo. Duru za habari zimeunukuu muungano wa viongozi hao ukisema kwamba, leo wamefanya maandamano hayo mbele ya msikiti wa "Ibrahim" katika mji wa Alexandria kaskazini mwa Misri. Wamesema kuwa, wafuasi wa utawala wa kidikteta wa Hosni Mubarak kwa kushirikiana na makundi yanayochukia dini ya kisekula na kileberali, wamekuwa wakiwashambulia viongozi wa kidini na kuwazuia kuadhini na kuqimu sala katika baadhi ya misikiti,

Thursday, December 20, 2012

Athari za uvuvi haramu na ydhubutu wake yafanyika Zanzibar


 Baadhi ya Wajumbe walioshiriki katika Semina ya Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mjiwa Zanzibar.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdillahi Jihad Hassan akifungua Semina kuhusu Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
 Mkurugenzi wa wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Mussa Aboud Jumbe akionyesha Nyavu za kukokota ambazo ni hatari kwa kuuwa matumbawe na mazalio ya Samaki katika Semina kuhusu Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
 Mkurugenzi wa wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Mussa Aboud Jumbe katikati akionyesha Dema lililotengenezwa kwa Waya ambalo ni baya kwa kuharibu Matumbawe na kuvuwa samaki wachanga katika Semina kuhusu Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Mussa Aboud Jumbe akionyesha Kikopo ambacho hutumika kwa Kuvulia Pweza na kinacho kubalika kisheria katika Semina kuhusu Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.20/12/2012

Somalia tayari kuwafungulia mashtaka maharamia


Somalia tayari kuwafungulia mashtaka maharamiaMkuu wa Mahakakama ya Juu ya Somalia Aydiid Abdullahi IIka Hanaf amesema maharamia Wasomali waliokamatwa katika maji ya kimataifa watafunguliwa mashtaka ndani ya Somalia.
Katika mahojiano na tovuti ya Shabelle, IIka Hanaf amesema mfumo wa sheria wa Somalia sasa una uwezo wa kuwafungulia mashtaka maharamia na kwamba hakuna haja ya wahalifu hao kufikishwa katika mahakama za nchi za kigeni.
Katika miaka ya hivi karibuni, maharamia Wasomali wamekuwa wakikamatwa katika eneo la Bahari ya Hindi na kufunguliwa mashtaka katika nchi za Ulaya, Asia, Afrika na hata Marekani. Maharamia wakiwa na silaha nzito nzito huteka nyara meli na kuziachilia baada ya kupokea mamilioni ya dola kama kikomboleo.

Lebanon yakataa ombi la US la kujenga kituo


Lebanon yakataa ombi la US la kujenga kituo
Wizara ya Mawasiliano ya Posta na Simu ya Lebanon imelikataa ombi la Marekani la kutaka kujenga kituo cha mawasiliano ndani ya ardhi ya nchi hiyo. Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo inakinzana na misingi ya kidiplomasia na inakiuka pia mamlaka ya kujitawala ya Lebanon. Wakati huo huo Faisal Daud, kiongozi wa harakati ya mapambano ya Kiarabu ya Lebanon amesema, kutokana na kugunduliwa mitandao kadhaa ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya ardhi ya Lebanon kujengwa kituo cha mawasiliano ya posta na simu cha Marekani ndani ya ardhi ya nchi hiyo ni hatua ya kwanza ya kutumikia na kudhamini maslahi ya utawala wa kizayuni katika eneo.

24 wauawa katika mapigano Sudan Kusini


24 wauawa katika mapigano Sudan Kusini Watu 24 wameuawa katika mapigano kati ya jeshi la Sudan Kusini na wapiganaji wa kundi la wanamgambo linaloongozwa na mtu aliyejitangazia unabii katika jimbo la Jonglei huko mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi la Sudan Kusini limetangaza kuwa liliwashambulia waasi hao wanaoongozwa na Dak Kueth ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuwatomokeza wanamgambo wa makundi ya kikabila katika eneo hilo. Luteni Jenerali Kuol Deim Kuol amesema wanamgambo 19 na askari watano waliuawa katika mapigano hayo.

Ikhwan yapinga kuridhiwa takwa la wapinzani Misri


Ikhwan yapinga kuridhiwa takwa la wapinzani MisriMuhammad Mahdi Aakif, kiongozi wa zamani wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri ameukosoa msimamo wa makundi ya kisiasa ya nchi hiyo wa kuyakataa matokeo ya awamu ya kwanza ya kura ya maoni ya katiba na kusisitiza kwamba takwa la wapinzani hao la kutaka kubatilishwa kura hiyo ya maoni halina msingi. Matokeo ya awamu ya kwanza ya kura ya maoni ya katiba mpya ya Misri yanaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 56 ya wapiga kura wameunga mkono rasimu ya katiba hiyo kulinganisha na asilimia 43 walioipinga. Kiongozi wa zamani wa Ikhwanul Muslimin amesema msimamo wa mirengo ya kisiasa wa kung’ang’ania takwa lao la kubatilishwa kura ya maoni na kuundwa baraza jengine jipya la kutunga katiba mpya ya Misri haukubaliki. Awamu ya pili ya zoezi la kura ya maoni ya katiba mpya ya Misri itafanyika siku ya Jumamosi katika mikoa mingine 17, na matokeo rasmi ya kura hiyo yatatangazwa baada ya awamu hiyo…

Waasi wadhibiti mji wa mpakani Afrika ya Kati


Waasi wadhibiti mji wa mpakani Afrika ya Kati
Waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameudhibiti mji wa kaskazini wa Kabo ulioko karibu na mpaka wa nchi jirani ya Chad. Afisa mmoja wa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema waasi hao wa muungano wa Seleka wamekata mawasiliano yote na mji wa Kabo ambao wanaushikilia hivi sasa. Shambulio hilo la waasi limefanywa siku moja baada ya vikosi vya jeshi la Chad kuingia katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kuitikia ombi la serikali ya Bangui la kuisaidia kuzima uasi nchini humo. Wakati huohuo Umoja wa Afrika umewataka waasi wa Seleka kuondoka katika mji huo wanaoushikilia huku waasi hao wakisisitiza kusonga mbele kuelekea kusini mwa nchi hiyo.

Wednesday, December 19, 2012

KESI YA VIONGOZI WA JUMUIYA YA UAMSHO MAHAKAMANI VUGA

 

KESI YA INAYOWAKABILI VIONGOZI WAKUU WA JUMUIYA YA UAMSHO ILIOENDESHWA LEO KATIKA MAHAKAMA KUU YA VUGA MJINI ZANZIBAR IMEBAINISHA KULIKATAA OMBI LA DHAMANA NA KUPELEKEA VIONGOZI HAO KURUDI TENA RUMANDE.

WASHTAKIWA HAO WALIFIKISHWA MAHAKAMANI HAPO MNAMO MAJIRA SAA MBILI NA NUSU ASUBUHI HUKU WAKIWA CHINI YA ULINZI MKALI ULIOKUA UKIONGOZWA NA GARI TATU ZA FFU PAMOJA NA BAADHI YA ASKARI WA VIKOSI VYA KMKM.

KATIKA KESI HIYO JAJI MKUSA SEPETU AMELAZIMIKA KULIKATAA OMBI LA DHAMANA KWA WASHTAKIWA HAO AMBALO LILIKUA LIKIFUATILIWA KWA MUDA MREFU LAKINI LILIKUA LIKIWEKEWA PINGAMIZI TOFAUTI.
AMEBAINISHA YA KWAMBA OMBI HILO LIMEKATALIWA KWA KUDAIWA YA KWAMBA HALIKUFUATA TARATIBU SAHIHI ZA KISHERIA, HIVYO MAHAKAMA IMEWATAKA WATETEZI WA WATEJA HAO KUFUATA TARATIBU ZILIZO SAHIHI JUU YA OMBI LAO LA KUPATIWA DHAMANA VIONGOZI HAO.

KWA UPANDE WA UTETEZE WAWASHTAKIWA HAO KIMSINGI HAUKUFURAHISHWA NA MAAMUZI YALIOAMULIWA NA MAHAKAMA HIO YAKULITUPILIA MBALI OMBI HILO LA DHAMANA KWANI WAMESEMA HOJA ILIOTOLEWA UAMUZI SI MIONGONI MWA HOJA ILIOWASILISHWA KWA DPP KIMSINGI WAMESEMA NI HOJA ILIOIBULIWA NA MAHAKAMA WENYEWE JAMBO AMBALO LINAWAPA MASHAKA MAWAKILI HAO.

AIDHA WAMESEMA KUWA WALLIPANGA KUWASILISHA OMBI JIPYA LEO HII LA KUDAI DHAMANA KWA WATEJA WAO LAKINI KUTOKANA NA MUDA KUTOKURUHUSU KWA SIKU YA LEO

WAMEAMUWA KUJIPANGA UPYA ZAID NA KUWASILISHA MAOMBI HAYO HAPO KESHO.

KESI HIO ITASIKILIZWA TENA MNAMO TAREHE 3/1/2013

Aal Khalifa watumia hospitali kutesea wapinzani


Aal Khalifa watumia hospitali kutesea wapinzani Utawala wa Aal Khalifa wa Bahrain unatumia hospitali kuwatesa wapinzani. Vijana wanaharakati wa haki za binadamu huko Bahrain wameripoti kuwa utawala wa Aal Khalifa unatumia baadhi ya hospitali kuwatesea wapinzani. Hospitali ya Suleimaniya ni moja kati ya maeneo ambayo wapinzani hupelekwa kama majeruhi hata hivyo wakiwa huko huteswa vibaya na vikosi vya usalama vya Bahrain. Taasisi ya vijana watetezi wa haki za binadamu ya Bahrain imeashiria pia namna wapinzani wanavyowekwa na kuteswa katika hospitali hiyo na kueleza kuwa ghorofa ya kwanza na ya pili  za hospitali hiyo zimetengwa makhususi kwa ajili ya wagonjwa,

Mahakama ya ICC yamtoa hatiani Ngudjolo Chui


Mahakama ya ICC yamtoa hatiani Ngudjolo Chui
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imemuondoa hatiani Methieu Ngudjolo Chui kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo aliyekuwa akituhumiwa kutenda jinai dhidi ya binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mahakama ya ICC yenye makao yake mjini Hague Uholanzi ilitoa uamuzi huo hapo jana na kuamuru kuwa Ngudjolo Chui aachiwe huru mara moja. Kiongozi huyo wa zamani wa wanamgambo huko Kongo DRC alikabiliwa na tuhuma hizo baada ya kuuliwa watu mia mbili katika kijiji cha Bogoro katika mkoa wa Ituri huko mashariki mwa Kongo mwaka 2003.  Ngudjolo alikuwa akikabiliwa na makosa saba ya kutenda jinai za kivita na matatu dhidi ya binadamu.

Marekani yawawekea vikwazo viongozi wa M23


Marekani yawawekea vikwazo viongozi wa M23Wizara ya Fedha ya Marekani imetangaza kuwa inawawekea vikwazo viongozi wawili wa waasi wa harakati ya Machi 23 ambayo imeunda serikali yake huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wizara ya Fedha ya Marekani jana iliwatuhumu Baudoin Ngaruye na Innocent Kaina kwa kuwatumia watoto vitani. Imesema kuwa watu hao wawili wamepewa adhabu hiyo kwa kuhusika katika kuwakusanya watoto na kisha kuwatumia kama askari vitani huko Kongo DRC na kwa kuwa viongozi wa harakati ya waasi ya M23.

Mubarak atakiwa kuhamishiwa jela ya kijeshi Misri


Mubarak atakiwa kuhamishiwa jela ya kijeshi Misri
Idara ya jela za Misri iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo imetaka Hosni Mubarak, dikteta wa zamani wa nchi hiyo ahamishiwe katika jela ya kijeshi ya al Maadi. Idara ya jela za Misri imeiomba Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo kuafiki suala la kumhamishia Hosni Mubarak katika hospitali ya kijeshi iliyo karibu na jela hiyo kwa kuzingatia hali mbaya aliyonayo katika chumba maalumu anakoshikiliwa huko katika hospitali ya  jela ya Tura, kusini mwa Cairo. Muhammad Ibrahim Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri ambaye pia ni mkuu wa idara ya jela za Misri ameeleza kuwa hali ya Hosni Mubaraka ni mbaya na kwamba anapasa kulazwa hospitalini.

Mufti wa Syria asisitiza mazungumzo ya kitaifa


Mufti wa Syria asisitiza mazungumzo ya kitaifaMufti wa Syria amesisitiza juu ya umuhimu wa kufanyika mazungumzo ya kitaifa ili kuhitimisha mgogoro unaoikabili nchi hiyo. Sheikh Ahmad Badruddin Hasun Mufti wa Syria amesema kuwa njama zinazofanywa na baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu dhidi ya Syria zina lengo la kutoa pigo kwa utambulisho wa kiarabu na Kiislamu na kuongeza kuwa njia pekee ya kujiondoa katika mgogoro huo ni  kufanyika mazungumzo ya kitaifa kati ya serikali na wapinzani wa nchi  hiyo. Sheikh Ahmad Badruddin Hasun amewaalika wapinzani wa ndani na nje ya Syria kushiriki vilivyo katika mazungumzo ya kitaifa ya nchi  hiyo na kuwataka kuungana na wananchi na mfumo wa kiraia wa Syria ili kuilinda nchi hiyo na mustakbali wake. 

Monday, December 17, 2012

Makubaliano ya kusitisha vita yakiukwa tena Gaza


Makubaliano ya kusitisha vita yakiukwa tena Gaza Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine tena limekiuka makubaliano ya kusimamisha vita kati yake na Wapalestina baada ya kuifyatulia risasi boti ya uvuvi ya Palestina huko kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza.
Wanajeshi wa Israel lmapema eo wameifyatulia risasi boti ya uvuvi ya Wapalestina na kumjeruhi abiria mmoja aliyekuweko ndani ya boti hiyo. Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel waliifyatulia risasi boti hiyo kwa kisingingizio kwamba ilivuka mipaka iliyoainishwa kwa wavuvi wa Kipalestina.

Watunisia waandamana mwaka wa pili wa mapinduzi


Watunisia waandamana mwaka wa pili wa mapinduzi
Wananchi wa Tunisia wameandama leo katika mji wa Sidi Bouzid kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa pili wa mapinduzi yaliyotokea nchini humo na kuung'oa madarakani utawala wa Rais Zainul Abidin bin Ali.
Waandamanaji hao waliwatupia mawe Rais Munsif al Marzouq wa Tunisia na Spika wa Bunge la nchi hiyo Mustafa bin Jaafar ambaye alikuwa akijiandaa kuhutubia wananchi. Vikosi vya usalama vya Tunisia vilijibu hatua hiyo ya waandamanaji na kuwaondoa haraka viongozi hao katika eneo palipokuwa pakifanyika maandamano hayo.

Polisi yapinga uhusiano kati ya ANC na waliokamatwa


Polisi yapinga uhusiano kati ya ANC na waliokamatwa Polisi ya Afrika Kusini imetangaza leo kuwa imezuia njama ya kutaka kuuvamia mkutano wa chama tawala cha ANC iliyokuwa imepangwa na raia wanne wa nchi hiyo wenye misimamo mikali.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Rais Jacob Zuma na makumi ya maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Afrika Kusini. Wanaume hao wanne wenye umri kati ya miaka 40 hadi 50 walikamatwa jana Jumapili. Msemaji wa polisi ameeleza kuwa kuna ushahidi kwamba watu hao walikuwa wakipanga njama ya kutekeleza vitendo vya ugaidi katika maeneo mbalimbali ya Afrika Kusini na si katika mkutano wa ANC pekee unaoendelea kufanyika katika mji wa Bloemfontein huko katikati ya nchi hiyo.

Sudan yakaribisha AU kutatua mzozo wa Abyei


 Sudan yakaribisha AU  kutatua mzozo wa Abyei
Chama tawala cha Sudan cha Kongresi ya Taifa kimekaribisha uamuzi wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika wa kubuni mpango kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Abyei katika kikao chake kijacho.
Chama hicho kupitia mwenyekiti wake Adam Yusuph ambaye ni Makamu wa Rais wa Sudan sambamba na kusifu nafasi ya AU katika kutatua migogoro ya kieneo, kimesema kuwa kadhia ya Abyei inapaswa kujadiliwa kwenye kikao hicho cha AU kilichopangwa kufanyika mwezi Januari. Chama hicho pia kimesisitiza kwamba, viongozi wa Kiafrika wanapaswa kuutafutia mgogoro wa Abyei suluhisho litakalokubaliwa na pande zote mbili.
Eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei lililoko kusini mwa Sudan lilitakiwa kupigia kura ya maoni Januri mwaka huu ili kuainisha hatima yake lakini hitilafu za Sudan na Sudan Kusini juu ya watu wanaopaswa kushiriki kura hiyo zimesababisha zoezi hilo liakhirishwe.

Chama cha Chavez chashinda uchaguzi wa kieneo


Chama cha Chavez chashinda uchaguzi wa kieneo
Chama cha kisoshalisti cha Rais Hugo Chavez wa Venezuela kimeshinda katika uchaguzi wa kieneo nchini humo.
Matokeo yanaonesha kuwa, wafuasi wa Chavez wameshinda ugavana katika majimbo 20 kati ya 23 kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili.
 Hii ni katika hali ambayo nchi hiyo bado inashughulishwa na hali ya kiafya ya Chavez ambaye amepata nafuu baada ya kufanyiwa operation hivi karibuni huko Cuba. Huo ulikuwa upasuaji wa 4 kufanyiwa kiongozi huyo tangu ilipojulikana kuwa ana ugonjwa wa saratani mwaka 2011.
Chavez anatarajiwa kuanza kipindi chake kipya cha urais Januri 10. Lakini iwapo atashindwa kuongoza nchi kutoakana na hali yake ya kiafya itabidi uchaguzi mpya wa rais ufanyike katika kipindi cha siku 30.

Saturday, December 15, 2012

Wahadhiri wa kiislamu waaswa kufanya tafiti juu ya maisha ya Sheikh Abdullah Saleh Alfarsy

 Kadhi Mstaafu wa Kenya Sheikh,Hamad Kassim akitoa Historia ya Maisha ya Sheikh Abdalla Saleh Farsy katika Tamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh huyo aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960 kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar.
 Mwanafunzi wa Sheikh Abdalla Saleh Farsy Sheikh Machano Hamadi Machano akitoa Historia ya Madarasa aliokuwa akifundisha Sheikh huyo na Masomo yake katika Tamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akitoa hotuba katika Tamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar.
 
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk kulia akibadilishana Mawazo na Kadhi Mstaafu wa Kenya Sheikh,Hamad Kassim katika Tamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar.
Baadhi ya Walimu wa Madrasa na Wanafunzi waliohudhuria katikaTamasha la Kiislamu la kumuenzi na kumkumbuka Sheikh Abdalla Saleh Farsy aliewahi kuwa Kadhi wa Zanzibar Mwaka 1960 kisha akawa Kadhi Mkuu wa Kenya Mwaka 1968.Tamasha lililofanyika People Palace Forodhani Zanzibar.