Watu wasiopungua 22 wamefariki dunia
na wengine zaidi ya 70 hawajulikani waliko baada ya jahazi waliyopanda
kuzama nchini Guinea Bissau. Taarifa zinasema kuwa, jahazi hilo lilizama
huku ikiwa imebeba zaidi ya abiria 97 ikitoka katika kisiwa cha Boloma
kilichopo katika bahari ya Atlantiki na kuelekea bandari ya Bissau
magharibi mwa Afrika. Duru za hospitali zinasema kuwa, hadi sasa
viwiliwili vya wahanga 22 vimehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi
maiti, huku juhudi zikiendelea za kuwatafuta wahanga wengine 72 ambao
hawajulikani waliko. Chanzo cha ajali hiyo imeelezwa kuwa ni kupakia
abiria kupita kiasi na shehena kubwa ya mizigo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment