Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC
imemuondoa hatiani Methieu Ngudjolo Chui kiongozi wa zamani wa kundi la
wanamgambo aliyekuwa akituhumiwa kutenda jinai dhidi ya binadamu huko
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mahakama ya ICC yenye makao yake mjini
Hague Uholanzi ilitoa uamuzi huo hapo jana na kuamuru kuwa Ngudjolo
Chui aachiwe huru mara moja. Kiongozi huyo wa zamani wa wanamgambo huko
Kongo DRC alikabiliwa na tuhuma hizo baada ya kuuliwa watu mia mbili
katika kijiji cha Bogoro katika mkoa wa Ituri huko mashariki mwa Kongo
mwaka 2003. Ngudjolo alikuwa akikabiliwa na makosa saba ya kutenda
jinai za kivita na matatu dhidi ya binadamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment