Rais Mwai Kibaki wa Kenya ametoa wito kwa Wakenya kujisajilisha
kama wapiga kura kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika Machi 2013 nchini humo.
Akizungumza mjini Nairobi katika Siku ya Jamhuri kwa mnasaba wa kusherehekea mwaka wa 49 wa uhuru wa Kenya, Kibaki pia amewataka Wakenya kuhakikisha kuwa wanawachagua viongozi waaminifu, wenye uono wa mbali, wachapa kazi kwa bidii na wanaojali maslahi ya wananachi.
Hata hivyo Rais Kibaki ambaye alikuwa akizungumza mbele ya halaiki kubwa ya wananchi katika Uwanja wa Nyayo, hakuzungumzia suala la ni nani atakayerithi kiti chake. Sherehe hizo zimehudhuriwa na wanasiasa kadhaa vigogo wanaotaka kurithi kiti cha Kibaki kama Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, Waziri Mkuu Raila Odinga na manaibu wake Uhuru Kenyatta na Musalia Mudavadi.
Kibaki amewahakikishia Wakenya kuwa serikali itachukua hatua imara kukabiliana na makundi ya wahalifu na magaidi nchini humo.

No comments:
Post a Comment