Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, Khalid Mash'al ametangaza kuwa
atautembelea Ukanda wa Gaza kwa mara ya kwanza tangu alipobaidishwa
mwaka 1967.
Masha'al amekuwa akiishi uhamishoni nchini Syria hadi nchi hiyo ilipotumbukia kwenye machafuko mwaka jana ambapo kiongozi huyo wa Hamas alilazimika kuhamia Qatar. Utawala ghasibu wa Israel umewahi kujaribu kumuua mara kadhaa bila mafanikio. Mwanamapambano huyo alichaguliwa kuongoza ofisi ya kisiasa ya HAMAS mwaka 1996 na chini ya uongozi wake, harakati hiyo imepata umashuhuri na kuwa na ushawishi zaidi siku baada ya siku.
Dikteta wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak alikataa kumruhusu Khalid Masha'al kwenda Gaza kupitia Misri katika kipindi chote cha zaidi ya miaka 30 ya utawala wake.

No comments:
Post a Comment