Kundi la watu wenye silaha waliokuwa
na lengo la kumuua Waziri Mkuu wa Libya Ali Zaidan jana walilishambulia
gari la Waziri Mkuu huyo katika mji wa al Baida umbali wa kilomita 200
kutoka mji wa Benghazi hata hivyo alinusurika kifo. Ali Zaidan alikutwa
na mashambulizi hayo akiwa njiani kuelekea katika mji wa al Baida kwa
ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa mji huo.
Hata hivyo magari
yaliyokuwa yakifuatana na Waziri Mkuu wa Libya yameharibiwa vibaya
katika mashambulizi hayo. Baadhi ya maeneo ya Libya hadi sasa yangali
yanashuhudia mapigano ambapo serikali mpya ya nchi hiyo imeamua kuchukua
hatua kali za kupambana na makundi hayo yenye silaha ambayo yanamiliki
silaha kinyume cha sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment