Waziri wa Habari na Utamaduni wa Sudan amesisitiza kwamba,
Khartoum ina haki ya kutoa jibu kwa hujuma na uchokozi wa Israel. Ahmed
Bilal Othman amesema, kwa mtazamo wa Khartoum ni kuwa faili la hujuma,
uchokozi na shambulio la Israel dhidi ya Sudan bado liko wazi na kwamba,
muda ukiwadia nchi hiyo itatoa jibu kwa uchokozi huo. Amesema, nchi
hiyo inaendelea kukusanya nyara na ushahidi kuhusu shambulio la
kichokozi la Israel dhidi ya Sudan ili kuwasilisha ushahidi huo kwa
asasi za kieneo na kimataifa likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa. Itakumbukwa kuwa Oktoba 24 mwaka huu, ndege nne za kivita za
Israel zilishambulia kiwanda cha kutengeneza silaha cha Yarmouk huko
Sudan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment