Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 10, 2012

Hamas yataka kutekelezwa mapatano ya kitaifa


Hamas yataka kutekelezwa mapatano ya kitaifa
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesisitiza kutekeleza mapatano ya kitaifa ya Palestina. Yahya Musa mmoja wa viongozi wa harakati ya Hamas ya Palestina amepinga pendekezo la Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuhusu kufanyika uchaguzi wa bunge la Palestina na kutangaza harakati hiyo haitakubali uchaguzi wowote ule huko Palestina bila ya kwanza kutekelezwa mpango wa mapatano ya kitaifa.
Yahya Musa ameongeza kuwa baadhi ya wanachama wa harakati ya Hamas huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wanakabiliwa na hali isiyoridhisha na wala hakuna mazingira yaliyoandaliwa kwa wanachama hao ili kuendesha kampeni na kushiriki kwenye uchaguzi ujao huko Palestina. Viongozi wa Hamas na Fat-h walisaini makubaliano mwezi Februari mwaka huu huko Doha Qatar na mwezi Mei mwaka jana huko Cairo Misri ili kuweka kando hitilafu zao na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kuendesha uchaguzi, hata hivyo makubaliano hayo hayajatekelezwa hadi sasa.

No comments:

Post a Comment