Viongozi wa kidini nchini Misri
wamefanya maandamano ya kulaani hatua ya wafuasi wa rais wa zamani wa
nchi hiyo, dikteta Hosni Mubarak, ya kufanya mashambulizi dhidi ya
viongozi hao na misikiti nchini humo. Duru za habari zimeunukuu muungano
wa viongozi hao ukisema kwamba, leo wamefanya maandamano hayo mbele ya
msikiti wa "Ibrahim" katika mji wa Alexandria kaskazini mwa Misri.
Wamesema kuwa, wafuasi wa utawala wa kidikteta wa Hosni Mubarak kwa
kushirikiana na makundi yanayochukia dini ya kisekula na kileberali,
wamekuwa wakiwashambulia viongozi wa kidini na kuwazuia kuadhini na
kuqimu sala katika baadhi ya misikiti,
suala ambalo wanasema halijawahi
kushuhudiwa katika historia ya Misri. Ripoti hiyo imeeleza kuwa, lengo
la vitendo hivyo dhidi ya Uislamu vinavyofanywa na wafuasi wa dikteta
Hosni Mubarak na makundi ya kisekula na kileberali, ni kuzusha fitina
kati ya wafuasi wa dini mbalimbali nchini humo, suala ambalo wamesema,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri inatakiwa kukabiliana nalo vilivyo.
Muungano huo umesisitiza kuwa, shambulizi la hivi karibuni dhidi ya
Sheikh Ahmad al-Mahlawi na Waislamu wapatao 150, wa msikiti wa Ibrahim
mjini Alexandria ni ushahidi tosha wa kushadidi vitendo hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment