Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, December 24, 2012

Maharamia wawaachia huru mateka 22 Somalia


Maharamia wawaachia huru mateka 22 SomaliaMateka 22 waliokuwa wametekwa nyara na maharamia kwa kipindi cha miaka miwili na miezi tisa nchini Somali, wameachiwa huru.
Hayo yametangazwa na viongozi wa serikali ya Somalia na kuongeza kuwa, mateka hao wameachiwa huru na maharamia hao katika pwani ya Puntland. Miongoni mwa walioachiwa huru ni pamoja na wafanyakazi wa meli ya Panama ya MV Iceberg 1, ambayo ilitekwa nyara mwishoni mwa mwaka 2010. Wafanyakazi hao ni raia wa Yemen, India, Ghana, Pakistan, Sudan na Uphilipino. Kuachiwa kwa watu hao kumefanyika baada ya wiki kadhaa tu ya kumalizika kwa oparesheni ya kikosi cha Gadi ya Pwani ambacho kiliasisiwa hivi karibuni na kupata mafunzo kutoka kwa shirika moja la usalama katika eneo hilo la Puntland. Juhudi za vikosi vya polisi kwa ajili ya kuwaokoa mateka hao na meli yao zilishindwa hapo tarehe 10 mwezi Septemba mwaka huu. Duru za habari kutika makao makuu ya Puntland, Garowe zimearifu kuwa, mateka hao wamekuwa wakipewa mateso mbalimbali na kwamba, alama za mateso na magonjwa mbalimbali zinaonekana katika miili ya watu hao.

No comments:

Post a Comment