Wizara ya Fedha ya Marekani jana iliwatuhumu Baudoin Ngaruye na Innocent Kaina kwa kuwatumia watoto vitani. Imesema kuwa watu hao wawili wamepewa adhabu hiyo kwa kuhusika katika kuwakusanya watoto na kisha kuwatumia kama askari vitani huko Kongo DRC na kwa kuwa viongozi wa harakati ya waasi ya M23.
Waasi wa M23 walijitenga na jeshi la Kongo mwezi Aprili mwaka huu wakilalamikia miamala mibovu waliyokuwa wakitendewa katika jeshi la nchi hiyo. Waasi hao awali waliingizwa jeshini chini ya mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment