Idara ya jela za Misri iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya
nchi hiyo imetaka Hosni Mubarak, dikteta wa zamani wa nchi hiyo
ahamishiwe katika jela ya kijeshi ya al Maadi. Idara ya jela za Misri
imeiomba Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo kuafiki suala la kumhamishia
Hosni Mubarak katika hospitali ya kijeshi iliyo karibu na jela hiyo kwa
kuzingatia hali mbaya aliyonayo katika chumba maalumu anakoshikiliwa
huko katika hospitali ya jela ya Tura, kusini mwa Cairo. Muhammad
Ibrahim Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri ambaye pia ni mkuu wa
idara ya jela za Misri ameeleza kuwa hali ya Hosni Mubaraka ni mbaya na
kwamba anapasa kulazwa hospitalini.
Siku tatu zilizopita Hosni Mubarak alianguka chini huko katika hospitali ya Tura na kujeruhiwa sehemu za kichwani.
Siku tatu zilizopita Hosni Mubarak alianguka chini huko katika hospitali ya Tura na kujeruhiwa sehemu za kichwani.
No comments:
Post a Comment