Rais Omar al Bashir wa Sudan (kushoto) na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Ethiopia imeainisha tarehe 13
Januari kuwa siku ya kufanyika mkutano kati ya Marais wa Sudan na Sudan
Kusini Omar al Bashir na Salva Kiir huko Addis Ababa mji mkuu uwa
Ethiopia. Hailemariam Dessalegn, Waziri Mkuu wa Ethiopia amewataka
marais hao wawili kuhudhuria mkutano huo kama ilivyopangwa. Wiki
iliyopita Waziri Mkuu wa Ethiopia alizitembelea Khartoum na Juba na
kuhakikishiwa kwamba Marais hao wa Sudan mbili watashiriki kwenye
mkutano huo. Mkutano ujao kati ya Rais Omar al Bashir wa Sudan na
mwenzake wa Sudan Kusini,
Salva Kiir utajaribu kutafuta njia za
kufanikisha makubaliano ya pamoja ya ushirikiano yaliyosainiwa na nchi
mbili hizo mwezi Septemba mwaka huu huko Addis Ababa sambamba na kutatua
pia masuala yaliyokwamisha utekelezaji wa makubaliano hayo. Waziri
Mkuu wa Ethiopiai amesema kuwa, ziara yake ya hivi karibuni huko
Khartoum ilikuwa na lengo la kuimarisha uhusiano uliasisiwa na hayati
Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia.
No comments:
Post a Comment