Msemaji wa jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia Jenerali Ali Hamiid amesema kuwa milipuko hiyo miwili ilitokea jana mbele ya Hoteli ya Mogadishu, alikokuwa Rais mpya wa Somalia. Watu alioshuhudia wamesema maiti mbili zilionekana mbele ya hoteli hiyo, moja ikidhaniwa kuwa ni ya mtu aliyejitoa mhanga.
Kundi la al Shabaab limetangaza kuwa ndilo lililopanga shambulizi hilo. Hata hivyo Rais mpya wa Somalia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya hawakupatwa na madhara yoyote katika shambulizi hilo.
Kundi la Shabaab limemtuhumu Rais mpya wa Somalia kuwa ni msaliti na kusisitiza kuwa litaendeleza mapambano yake dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
Rais Hassan Sheikh Mahmoud alichaguliwa Jumatatu iliyopita na Bunge la Somalia katika uchaguzi uliotajwa kuwa ni wa kihistoria.
No comments:
Post a Comment