Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR
limetahadharisha juu ya hali mbaya inayowakabili Waislamu wa Myanmar.
Taarifa ya UNHCR imeeleza kuwa, karibu Waislamu elfu sabini na tano
wanaishi katika mazingira hatarishi kwenye kambi za muda nchini humo.
Waislamu hao wameamua kuhama makaazi yao na kukimbilia kwenye maeneo ya
amani, baada ya Mabuda wenye misimamo ya kufurutu mipaka wakiungwa mkono
na vikosi vya serikali ya nchi hiyo kuwasaka na kuwaua kwa halaiki.
Taarifa zinaeleza kuwa, Waislamu hao wanakabiliwa na hali mbaya sana ya
kiafya na lishe duni kwenye kambi zao za muda zilizoko umbali wa
kilomita 500 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo. Hata hivyo vitisho vingali
bado vinaendelea vya watu wanaobeba silaha dhidi ya Waislamu laki nane
walioko katika eneo la kaskazini mwa Myanmar. Watu hao wanaobeba silaha
waliwaua kwa halaiki Waislamu wapatao 90 kutoka katika vijiji mbalimbali
yapata miezi minne iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment