Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 1, 2012

Meli Mpya ya Abiria ya Azam Marine Yawasili Zanzibar Leo.






 Meneja wa Kampuni ya Meli za Azam Marine,m Husssein M Said, akizungumza na Waandishi wa habari katika bandari ya Malindi Zanzibar wakati wa kuwasili meli yao mpya ya Sea Link katika bandari ya Malindileo mchana.

Meli hiyo ikitokea nchi Ugiriki ilikotengenezwa meli hiyo itaanza kazi baada ya kumaliza taratibu zote za Kisheria za Baharini na Taasisi husika kukaguliwa kwa kupata leseni ya kuchukulia abiria na mizigo.

Amesema meli hiyo ina uwezo wa kuchukuwa abiria 1500 na mizigo pamoja ya magari 270 kwa wakati mmoja,na itaanza safari zake baada ya kupata kibali na kufanyiwa ukaguzi.

Amesema itafanya safari zake kati ya Unguja Pemba na Dar-es-Salaam hivi karibuni ili kuondoa tatizo la usafiri wa maji kati ya visiwa vya Pemba na Unguja ambako kuna tatizo la usafiri, tangu kutokea kwa ajili ya meli kuzama na baadhi ya meli kufutiwa leseni zao kuchukuwa abiria kutokana na vyombo hivyo haviko katika hali ya kutowa huduma kwa wananchi.


Wananchi wamefarijika kuona meli hiyo katika bandari ya Zanzibar na kuona tatizo la Usafiri kati ya Unguja na Pemba limepata ufumbuzi baada ya kuwasili meli hiyo na kuwa na imani na huduma yake itakuwa nzuri na ya kuridhisha.

Wananchi pia wamewataka wafanyabiashara kupunguza nauli za vyombo ili kila mwananchi aweze kumudu huduma hiyo na wasiwe katika biashara zaidi kuliko kutowa huduma kwa wananchi wa hali ya chini ambao hutegemea usafiri huo.

Nae Meneja Hussein Said amesema meli yao itakuwa katika kutowa huduma zaidi kuliko biashara ili kuona kila Mwananchi anafaidika na huduma zao na wataweka nauli za bei nafuu kwa wananchi hao ili kuweza kutowa huduma za uhakika na safi wakati wate wa safari zao.

 Na kuwataka Wananchi kuwa na subira kama walivyokuwa kwa muda mrefu kupata ufumbuzi wa tatizo lao la usafiri karti ya pande hizi mbili za Visiwa, na kuwataka kupokea huduma zao kwa furaha wakati wote wa safari zao.  

No comments:

Post a Comment