CHAMA
cha Wafanyakazi wa Reli nchini (TRAWU), kimetishia kugoma iwapo
Serikali haitatekeleza madai yao ya kuligawa Shirika la Reli la Tanzani
na Zambia (TAZARA), ili kila nchi ijiendeshe yenyewe.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Erasto Kihwele, alisema
uwamuzi huo umefikiwa hivi karibuni kwenye mkutano wa kujadili kwa
kina hali ya uendeshaji wa shughuli za Reli nchini, uliyofanyika mjini
Morogoro.
Alisema wamefikia hatua hiyo
kutokana uendeshaji shirika hilo kuwa mgumu sana kutokana na maamuzi
mengi kuingiliana katika utekelezaji wake.
“Tunataka tugawane reli
kiuendeshaji, Tanzania kivyake na Zambia kivyake vinginevyo uendeshaji
utasimama toka Dar es Salaam hadi Tunduma”alisema Kihwele.
Aidha, wafanyakazi wote
wanaanza vikao kuanzia kesho, katika kanda za Dar es Salaam, Mlimba na
Mbeya kwa ajili ya kujadili hoja nzito kama vile kukosekana mafuta tangu
Oktoba 21 mwaka huu ya magari moshi ya mizigo ambapo iiliwafaya
wafanyakazi kurudishwa nyumbani.
Hoja nyingine ni kurudishwa kwa
mameneja saba waliokuwa wamesimamishwa kazi, muundo wa mshahara, posho
za kazi katika mazingira magumu, ucheleweshwaji wa mishahara.
Vilevile malimbikizo ya makato
ya wafanyakazi ya mifuko ya Hifadhi ya jamii, ilipwe kuanzia mwezi
Septemba mwaka huu ya jumla ya milioni 258 ili waanze kupata mafao
wanayostahili kuanzia mwezi huo.
Akizungumzia kuhusu Shirika la
Reli Tanzania (TRL), Kihwele alisema wanamtaka Waziri Mkuu awapatie
fursa ya kzungumza naye kuhusu utata wa serikali kumiliki shirika hilo
kwa asilimia 100.
Ili kumaliza utata kuhusu
nyaraka na zinazoonyesha kuwa kweli serikali imevunja mkataba
uliyokuwepo hapo awali na wawekezaji kutoka nchini India.
Alisema maombi yao kwa
serikali, itoe tamko kwa maandishi kuhusu kumiliki Reli hiyo kwa
asilimia 100 kutokana na kuwa hilo ndio hitaji kubwa kwa taasisi za
fedha (NBC).
No comments:
Post a Comment