Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, October 4, 2012

Askari 18 wa gadi ya rais wauawa nchini Syria

 

Askari 18 wa gadi ya rais wauawa nchini SyriaWanaharakati wa haki za binadamu nchini Syria wametangaza habari ya kuuawa askari 18 wa gadi ya rais nchini humo. Mauaji hayo yametokea katika shambulio lililofanywa katika eneo la Qudsiya magharibi mwa Damascus karibu na kambi ya vikosi vya gadi ya rais wa Syria na kupelekea askari hao 18 kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Hapo jana pia watu wapatao 40 waliuawa na wengine 90 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea mjini Aleppo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo jeshi la Syria bado linaendelea na juhudi zake za kurejesha amani na uthabiti katika maeneo tofauti nchini humo. Kwa upande mwingine hapo jana kombora kutokea Syria liliangukia katika ardhi za Uturuki na kuua watu watano. Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki amedai kuwa Syria imekiri kuhusika na shambulio hilo na kwamba imeomba radhi kwa serikali ya Ankara. Hata hivyo serikali ya Damascus ilikuwa imetangaza kuwa ingeanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo. Waziri wa Habari wa Syria amesema, baada ya magaidi kushindwa na vikosi vya nchi hiyo, wameanzisha awamu nyingine ya kurusha makombora nchini Uturuki ili kwa njia hiyo iwezekane kufungua mlango wa uingiliaji kijeshi dhidi ya taifa la Syria.

No comments:

Post a Comment