Alkhamisi, 11 Oktoba, 2012
Leo ni Alhamisi tarehe 24 Mfunguo Pili Dhilqaada mwaka 1433 Hijria sawa na tarehe 11 Oktoba 2012 Miladia
Siku kama ya leo miaka 1233 Imam Ridha (a.s) alianza safari yake kutoka Madina kuelekea Marv huko kaskazini mashariki mwa Iran ya zamani. Imam Ridha (a.s) alifanya safari hiyo kwa kulazimishwa na kushinikizwa na Maamun, khalifa na mtawala wa saba wa Bani Abbasi. Lengo la safari hiyo lilikuwa ni kumuweka Imam Ridha chini ya uangalizi. Maamun alitoa pendekezo kwa Imam huko Marv kwamba akubali kuwaa mrithi wake. Maamun alifanya hivyo ili kujionyesha kuwa ni mtu mwenye mapenzi na Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad(s.a.w). Hata hivyo katika fursa mbalimbali Imam Ridha si tu kwamba alionyesha kuwa hakubali kushirikiana na utawala wa Bani Abbasi bali aliutambua utawala huo kuwa ni wa kupenda makuu na wa kidhalimu.
Miaka 113 iliyopita sawa na tarehe 11 Oktoba 1899 vilianza vita vya umwagaji damu kati ya wazungu wa Uholanzi huko Afrika Kusini waliokuwa wakijulikana kama maboa (Boers) na Waingereza. Vikosi vya Uingereza viliwasili Afrika Kusini mwaka 1841 kwa lengo la kuikoloni Afrika. Wahajiri wengine wa Ulaya hususan Waingereza, waliongezeka huko Afrika Kusini baada ya kugunduliwa madini ya dhahabu na almasi nchini humo. Maboa
waliwasili Afrika Kusini katika karne ya 17 na walikuwa wakipinga wahajiri wapya kuhamia nchini humo. Suala hilo ndilo lililowapeleka kupigana vita na wahajiri wa Kiingereza.
Na siku kama hii ya leo miaka 21 iliyopita shughuli za Shirika la Ujasusi la Urusi ya zamani (KGB) zilifikia kikomo muda mfupi kabla ya kusambaratika muungano wa Sovieti. KGB iliundwa mwaka 1954 ili kukabiliana na harakati za kutaka kuupindua mfumo wa Kikomonisti wa Urusi ya zamani. Majukumu ya Shirika la Ujasusi la Urusi ya zamani (KGB) yalikuwa kuwakandamiza wapinzani wa chama cha Kimomonisti na kuendesha oparesheni za kijasusi dhidi ya ujasusi ndani na nje ya nchi hiyo.

Ijumaa, Septemba 21, 2012
Leo ni Ijumaa tarehe 4 Mfunguo Pili Dhil-Qaada mwaka 1433 Hijria sawa na tarehe 21 Septemba 2012 Miladia
Siku kama ya leo miaka 33 iliyopita vikosi vya jeshi la utawala wa zamani wa Iraq vilianzisha mashambulizi makubwa ya anga na nchi kavu dhidi ya Iran. Jeshi la Iraq lilikuwa limefanya uvamizi katika maeneo ya mpakani ya Iran kuanzia miezi kadhaa nyuma. Hata hivyo katika siku hiyo kikosi cha nchi kavu cha jeshi la Iraq kilivamia na kushambulia eneo lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita elfu moja la ardhi ya kusini magharibi ya Iran.
Katika siku za awali za mashambulizi hayo makubwa ya jeshi la Saddam Hussein, jeshi la nchi hiyo liliikalia kwa mabavu miji kadhaa na makumi ya vijiji vya Iran vilivyoko katika maeneo ya mpakani na kuuwa mamia ya wanawake na watoto wadogo wasio na ulinzi wa Iran.
Miaka 48 iliyopita katika siku kama ya leo Malta iliyoko kusini mwa bara Ulaya ilipata uhuru. Nchi hiyo ilivamiwa na kukaliwa na wakoloni wa Kifaransa mwaka 1798 na miaka kadhaa baadaye kisiwa hicho kiliwekwa chini ya himaya ya Uingereza. Malta inaundwa na visiwa kadhaa vilivyoko katika bahari ya Mediterania huku ikipatikana kusini mwa bara Ulaya.
Siku kama ya leo miaka 103 iliyopita Dakta Kwame Nkrumah, mwanasiasa na mpigania uhuru wa Ghana alizaliwa. Nkrumah alishiriki pakubwa katika mapambano ya kupigania uhuru ya wananchi wa Ghana dhidi ya Uingereza. Kwame Nkrumah ambaye alikuwa mkuu wa Chama cha Taifa cha Wananchi alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Ghana baada ya kufanyika uchaguzi wa kwanza kote nchini humo mwaka 1951. Hatimaye mwaka 1957 Ghana ilipata uhuru kutokana na mapambano ya wananchi chini ya uongozi wa Dakta Kwame Nkrumah.
Na miaka 220 iliyopita katika siku kama ya leo miaka mitatu baada ya ushindi wa mapinduzi ya Ufaransa, utawala wa kisultani ulifutwa nchini humo na mfumo wa jamhuri ukachukua nafasi yake. Bunge la Ufaransa la wakati huo ndilo lililochukua mamlaka ya kusimamia masuala ya uongozi wa nchi hiyo baada ya matukio hayo.
jumamosi, Septemba 22, 2012
Leo ni Jumamosi tarehe 5 Dhilqaadah mwaka 1433 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 22 Septemba mwaka 2012 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 152 iliyopita, yaani tarehe 22 Septemba 1860 Miladia, vilianza vita vya Beijing kati ya vikosi vya Uingereza na Ufaransa dhidi ya China. Katika vita hivyo vikosi vya jeshi la China vilishindwa kutokana na kutokuwa na zana na silaha za kutosha. Kushindwa kwa China katika vita hivyo kuliwafanya wakoloni wa Uingereza na Ufaransa kuikalia na kupora mali za Beijing na kuilazimisha China kutia saini mkataba wa kikoloni. Kwa mujibu wa mkataba huo, fursa nyingi zilipewa Uingereza na Ufaransa sambamba na wakoloni hao kukabidhiwa bandari ya China.
Siku kama ya leo miaka 52 iliyopita, nchi ya Mali iliyo kaskazini magharibi mwa Afrika ilijipatia uhuru. Karibu miaka elfu mbili iliyopita nchi ya Mali ilikuwa na tamaduni mkubwa. Hata hivyo nchi hiyo tangu karne ya 18 hadi ya 19 Miladia ilikuwa ni moja ya tawala za ufalme wa Sudan. Baada ya Morocco kutwaa baadhi ya maeneo yaliyokuwa chini ya tawala za ufalme wa Sudan ikiwemo Mali, tawala mbalimbali za kikabila nchini Mali zilifanikiwa kuingia madarakani. Satwa ya Wafaransa nchini Mali ilianza mnamo karne ya 19 na hadi kufikia mwaka 1898 nchi hiyo ilikuwa chini ya usimamizi wa Ufaransa. Hata hivyo Mali ambayo ilikuwa ikiitwa Sudan ya Ufaransa, mwaka 1958 ilianza kujitawala na mwaka 1960 ikajipatia uhuru wake kamili.
Na miaka 769 iliyopita mwafaka na siku hii ya leo alifariki dunia mtaalamu wa fiqhi, hadithi, historia na mwanafasihi wa Kiislamu Radhiyyud-Din Ali bin Musa, maarufu kwa jina la Sayyid Ibn Tawus. Ibn Tawus alipitia kipindi cha utoto na ujana wake mjini Hillah, Iraq sambamba na kusoma elimu tofauti za dini. Aidha Sayyid Ibn Tawus alifahamika kwa zuhudi na uchaji Mungu na kwa sababu hiyo alikataa vyeo vyote alivyopewa na watawala wa wakati huo.

Jumapili, 6 Dhilqaadah 1433
Leo ni Jumapili tarehe 6 Dhilqaadah mwaka 1433 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 23 Septemba mwaka 2012 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 34 iliyopita, vikosi vya usalama vya utawala wa Baath nchini Iraq na katika fremu ya ushirikiano na utawala wa Shah, viliivamia nyumba ya Imam Khomein MA, mjini Najaf. Kutokana na uhusiano mwema uliokuwepo kati ya utawala wa zamani wa Iraq na utawala wa Shah, serikali ya Iraq ilimtaka Imam Khomein ajiepushe kufanya mahojiano na waandishi wa habari, kutoa tangazo lolote na kuhutubu masuala ya kisiasa dhidi ya utawala wa kiimla wa Shah. Hata hivyo Imam Khomein alikataa amri hiyo na kusema kuwa atatekeleza wajibu wake wa Kiislamu popote pale atakapokuwa. Baada ya hapo utawala wa Iraq ulimtaka Imam Khomein aondoke nchini humo. Imam Ruhullah Khomein alielekea Paris, Ufaransa na kutayarisha uwanja wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Siku kama ya leo miaka 700 iliyopita alifariki dunia Ibn Hani, malenga, mwandishi na mtaalamu maarufu wa lugha wa Kiislamu. Alizaliwa kusini mwa Andalusia, Uhispania ya leo na baada ya kumaliza masomo yake ya awali katika kipindi ujana Ibn Hani alipata elimu kutoka kwa wasomi mashuhuri wa fasihi wa zama hizo na kwa kipindi kifupi alipata kuwa mahiri katika elimu tofauti za fasihi. Ibn Hani pia alikuwa akitunga mashairi. Miongoni mwa athari za Ibn Hani ni pamoja na kitabu kiitwacho "Sharhut-Tas'hiil."
Siku kama ya leo miaka 73 iliyopita, aliaga dunia Sigmund Freud, daktari wa magonjwa ya akili na raia wa Austria. Sigmund alizaliwa mwaka 1856. Alifanya utafiti na kutwalii matatizo mbalimbali ya kiakili yanayomkumba binadamu na kutoa maoni na nadharia mpya kuhusu chanzo cha magonjwa ya akili.
Na siku kama yaleo miaka 80 iliyopita nchi ya Saudi Arabia iliasisiwa na Abdul-Aziz bin Saud akawa mfalme wa nchi hiyo. Katika mji wa Makka huko Saudi Arabia ndipo alipodhihiri mtukufu Mtume wa Uislamu Muhammad (saw). Tangu mwanzoni mwa karne ya tatu Hijiria sawa na karne ya tisa Miladia Saudia ilitoka chini ya watawala wa Bani Abbasi na kupitia kipindi cha ukosefu wa amani na machafuko yaliyodumu kwa karne kadhaa.

No comments:
Post a Comment