Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 30, 2012

KESI YA WAATHIRIKA WA MABOMU MBAGALA YAHAMISHIWA BARAZA LA USULUHISHI



KESI ya madai ya fidia iliyofunguliwa na wakazi wa Mbagala, Wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam walioathirika na mabomu mwaka 2009 imehamishiwa Baraza la Usuluhishi ili kutafuta muafaka  kati yao na serikali.
 
baraza la usululishi ili kufanya mazungumzo baina ya pande hizo mbili yaani serikali na wananchi hao.

Mamia ya Polisi wa Kongo DRC wapelekwa Goma



Mamia ya Polisi wa Kongo DRC wapelekwa  Goma
Karibu askari polisi 300 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo wameingia katika mji wa Goma makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini, baada ya kuondoka wanamgambo wa kundi la waasi wa M23 katika mji huo waliokuwa wakiudhibiti kwa zaidi ya wiki moja. Manodje Mounoubai Msemaji wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo MONUSCO amesema kuwa,

Vikwazo vya Marekani dhidi ya vyombo vya habari Iran



Vikwazo vya Marekani dhidi ya vyombo vya habari IranBaraza la Seneti la Marekani liko katika mikakati ya kuweka vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ikiwemo kuzuia fedha zote zinazofungamana na Taasisi ya Redio na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB. Taarifa zinasema kuwa, vikwazo hivyo vipya vya Marekani dhidi ya IRIB ni mwendelezo wa njama za nchi za Magharibi na hasa Marekani za kuvinyamazisha vyombo vya habari vya hapa nchini. Taarifa hiyo imeeleza kuwa,

Maalim Seif, Pinda waongoza mazishi mke wa Hamad Rashid

Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na serikali wameshiriki katika mazishi ya bibi Kisa Mohd ambaye ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd.
Mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya kisutu, yaliongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Meli ya kivita ya Iran yawasili Sudan



Meli ya kivita ya Iran yawasili Sudan
Meli ya kivita ya Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetia nanga katika bandari ya Sudan katika Bahari Nyekundu.
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran Admeli Habibollah Sayyari amesema manowari hiyo ijulikanayo kama  'Jamaran' na ambayo imetengenezwa kikamilifu nchini Iran imewasili Sudan ikiwa na ujumbe wa amani na kirafiki kwa nchi za eneo na rafiki.

Thursday, November 29, 2012

Mashari Rashid AlAfasy - Mahiye lilbi3a Al Kuwayt

Waasi wa M23 wajitayarisha kuondoka Goma


    Waasi wa M23 wajitayarisha kuondoka Goma
    Waasi wa mashariki mwa Kongo DRC wamesema kuwa wanaanza kuondoka katika mji waliouteka wa Goma, ikiwa ni siku kadhaa baada kufikia makubaliano na serikali kwa upatanishi wa Uganda. Amani Kabashi msemaji wa waasi wa M23 amesema kuwa, wanaanza kundoka katika mji wa Masisi ulioko kilomita 50 kutoka katika jiji la Goma, kisha wataondoka katika

    Zaidi ya watu 30 wauawa kwenye milipuko Syria


      Zaidi ya watu 30 wauawa kwenye milipuko Syria
      Habari kutoka Syria zinasema kuwa milipuko kadhaa imetokea karibu na mji wa Damascus na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa. Habari zaidi zinasema kuwa, milipuko minne ya mabomu imesikika kandokando mwa Damascus ukiwemo mji wa Jaramana yapata kilomita 10 kusini magharibi mwa Damascus.

      Wimbi la mashambulio ya kigaidi nchini Iraq


        Wimbi la mashambulio ya kigaidi nchini IraqJumanne tarehe 27 Novemba ilikuwa siku ya umwagaji damu mkubwa kwa Iraq na Wairaqi. Milipuko minane iliitikisa miji mbalimbali ya ya nchi hiyo na kwa akali watu 29 walipoteza maisha yao na zaidi ya mia moja na ishirini kujeruhiwa. Miji ya Kirkuk, Al Anbar na Baghdad ndiyo iliyolengwa na magaidi hapo jana. Polisi ya Iraq imelinyooshea kidole cha tuhuma kundi la mtandao wa al-Qaeda.

        Mapambano ya polisi na waandamanaji Cairo


          Mapambano ya polisi na waandamanaji CairoMapambano baina ya waandamanaji Misri na polisi yameendelea leo mjini Cairo kwa siku ya sita mfululizo kwa lengo la kupinga hatua ya Rais Mohammad Mursi kujiongozea madaraka.
          Wafanya maandamano wanataka kufutwa amri iliyotangazwa wiki iliyopita na Rais Mursi wa nchi hiyo ambayo inamzidishia uwezo wake wa kimadaraka.

          Wednesday, November 28, 2012

          'Israel inakiuka haki za binaadamu za Wapalestina'


          •  
          'Israel inakiuka haki za binaadamu za Wapalestina'
          Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amelaani hatua ya Israel ya kukiuka haki za binadamu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Nabil al Arabi amesema hayo leo alipokutana na Richard A. Falk Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu katika ardhi

          Tuesday, November 27, 2012

          UNDP: Ukosefu wa amani huenda ukaongezeka Kenya


            UNDP: Ukosefu wa amani huenda ukaongezeka Kenya
            Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) limeeleza wasiwasi wake juu ya uwezekano wa kuzidi hali mbaya ya ukosefu wa amani nchini Kenya kutokana na harakati za makundi ya wanamgambo nchini humo.

            Jenerali Nyakairima: Waasi wa M23 kuondoka Goma


              Jenerali Nyakairima: Waasi wa M23  kuondoka GomaMkuu wa Majeshi ya Uganda Jenerali  Aronda Nyakairima amesema kuwa, Kanali Sultani Makenga msemaji wa kundi la waasi wa M23 amemthibitishia kwamba, wamekubaliana na mpango wa kuondoka kwenye mji wa Goma wanaoudhibiti kwa muda wa wiki moja, ili kuandaa mazingira ya kufanyika mazungumzo na serikali ya Kinshasa.

              Kiongozi Mkuu: Iran imefanikiwa katika malengo yake


              Kiongozi Mkuu: Iran imefanikiwa katika malengo yake Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo amekutana na makamada wa jeshi la majini la Iran na kusisitiza juu ya nafasi muhimu ya jeshi hilo katika kulinda amani na usalama wa Ghuba ya Uajemi.
              Ayatullah Khamenei ambaye amekutana na makamanda hao wa jeshi kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Jeshi la Majini, ameashiria malengo ya muda mrefu ya Jamhuri ya Kiislamu na mafanikio mtawalia ya utawala wa Kiislamu hapa nchini katika kufikia malengo yake na akasema kuwa, hali ya mambo katika eneo la Mashariki ya Kati na katika uga wa kimataifa inaonesha kuwa Jamhuri ya Kiislamu imepata mafanikio makubwa.
              Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa moja ya sababu za makelele ya kipropaganda yanayofanywa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mafanikio hayo na kuongeza kuwa: Tunapofanya ulinganisho kati ya siasa za Mashariki ya Kati za nchi za Magharibi na siasa za Jamhuri ya Kiislamu kuhusu eneo hilo tutaona kuwa siasa za Iran zimekaribia zaidi kwenye malengo yake.
              Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Iran amesema pwani kubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hususan pwani ya Bahari ya Oman ni utajiri mkubwa wa kitaifa. Ameongeza kuwa iwapo viongozi wa serikali na asasi nyingine hapa nchini watayatazama maeneo ya baharini kwa mtazamo wa kistratijia basi maeneo hayo muhimu yanaweza kuwa sababu ya nguvu na uwezo mkubwa wa Jamhuri ya Kiislamu.

              Israel yatuhumiwa kuwa ilifanya jinai za kivita Gaza


                Israel yatuhumiwa kuwa ilifanya jinai za kivita GazaJumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu leo imetoa taarifa mjini Tehran ikitangaza kuwa mashambulizi ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza ni tishio kwa amani na usalama wa Mashariki ya Kati.
                Jumuiya hiyo pia imeitaka jamii ya kimataifa ikiwemo Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu kukomesha jinai za Israel kwa kuchukua hatua za dharura za kuwalinda watu wa Gaza na kuunda muungano wa kimataifa wa kulilinda eneo hilo.

                Monday, November 26, 2012

                MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AFUNGUA MKUTANO WA ARIPO ZANZIBAR BEACH RESORT


                Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akitoa Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Baraza la Utawala la ARIPO linaloratibu na kusimamia haki za Mali za wabunifu Barani Afrika huko katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort ilioko Mazizini Nje ya Mji wa Zanzibar.
                PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
                ………………………………………………………………………………….
                                    NA RAMADHANI ALI/HABARI MAELEZO
                 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema ipo haja kwa  Baraza la Utawala linaloratibu na kusimamia haki za Mali za Ubunifu Afrika (ARIPO) na Jumuiya za kimataifa zinazosimamia sekta hiyo kuandaa  miongozo na kuimarisha  mikakati itakayo wabana  wezi wa haki miliki.

                UN: Unyanyasaji dhidi ya wanawake ukomeshwe



                UN: Unyanyasaji dhidi ya wanawake ukomeshwe
                Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kukomeshwa vitendo vya utumiaji mabavu na kuwanyanyasa wanawake. Ban Ki Moon amesema hayo katika risala yake kwa mnasaba wa Novemba 25, Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Unyanyasaji wa Wanawake. Ban Ki Moon amesema, licha ya kuweko hatua zilizochukuliwa za kupambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake, asilimia 70 ya wanawake hukabiliwa na vitendo vya utumiaji mabavu na unyanyasaji wa kijinsia katika kipindi cha maisha yao na kwamba, robo ya wanawake huwa ni wajawazito. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, utumiaji mabavu dhidi ya wanawake ni misdaqi ya wazi ya ukiukaji wa haki za binadamu na kwamba, nchi zanachama za umoja huo zinapaswa kuandaa mipango na mikakati ya kung'oa mizizi ya vitendo hivyo vibaya.

                Waasi wa Syria wauteketeza Msikiti kwa makombora



                Waasi wa Syria wauteketeza Msikiti kwa makomboraWaasi wa Syria ambao wanaungwa mkono na nchi za Magharibi na hasa Marekani na zile za Kiarabu kama vile Saudi Arabia, Qatar na Uturuki wameendeleza jinai zao kwa kuushambulia kwa makombora msikiti mmoja ulioko katika mji wa Halab nchini humo. Picha ya mkanda wa video iliyotolewa hivi karibuni inawaonyesha wapiganaji hao wa kundi la waasi wakitenda jinai hiyo na baada ya kuuangamiza kikamilifu msikiti huo wakaanza kushangilia na kucheza dansi kwenye mabaki ya msikiti huo. Kundi hilo la waasi limefanya jinai kadhaa nchini humo ikiwa ni pamoja na kuwafyatulia risasi wanajeshi wa serikali baada ya kuwa wameshawakamata na kuwafunga kamba miguuni na mikononi. Waasi walianzisha machafuko nchini humo mwezi Machi 2011, kwa shabaha ya kuiondoa madarakani serikali halali na iliyochaguliwa na wananchi ya Rais Bashar Assad wa Syria.

                Sunday, November 25, 2012

                Madaktari Zanzibar wakutana kuajadili katiba yao


                 
                Dk. Juma Salum Mambi ambae ni Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, akifafanua jambo  kwa wajumbe kuhusu katiba yao
                .………………………………………………………
                Na Fatma Mzee, Maelzeo
                JUMUIYA ya Madaktari Zanzibar, imefanya mkutano wa kujadili katiba yake kwa lengo la kuifanyia marekebisho ili iende na wakati wa sasa.

                Saturday, November 24, 2012

                WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUAWA MKOANI ARUSHA


                 
                Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo zilikutwa  kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali . (Picha na Mahmoud Ahmad Arusha)


                MNAMO TAREHE 22/11/2012 MUDA WA SAA 3:45 ASUBUHI KATIKA ENEO LA OLMATEJOO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA, WATU WATATU (AMBAO MAJINA YAO  BADO HAYAJATAMBULIKA) WANAOSADIKIWA KUWA  NI MAJAMBAZI WALIUAWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKATI WA WAJIBIZANO YA KURUSHIANA RISASI.

                Friday, November 23, 2012

                Tanzania kuanzisha kadi za simu za mkononi zinazoweza kutumika kwa mitandao tofauti


                Serikali ya Tanzania itaanzisha mfumo wa kadi za namba za simu za mkononi zinazoweza kutumika kwa mitandao tofauti mwaka ujao ambao utawawezesha watumiaji kuhifadhi namba zao za simu wakati wanapobadilisha kutoka kwa mtoa huduma mmoja kwenda kwa mwingine, kwa mujibu wa Mamlaka ya Sheria za Mawasilaino Tanzania (TCRA).
                • Mteja akijadilana na muuzaji wa simu za mkononi katika duka la Tecno katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam tarehe 17 mwezi Novemba. [Deodatus Balile/Sabahi] Mteja akijadilana na muuzaji wa simu za mkononi katika duka la Tecno katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam
                "Wateja hawataendelea kushikiliwa kwa mtoa huduma mmoja," Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA John Nkoma aliiambia Sabahi. "Kwa kutumia mfumo huu unaweza kubadilisha watoa huduma wakati unapotaka kutegemeana na ubora na gharama."

                Wanne wauawa kwenye maandamano nchini Nigeria



                Wanne wauawa kwenye maandamano nchini Nigeria
                Watu wasiopungua wanne wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa, baada ya kutokea ghasia kati ya jeshi la polisi na waandamanji huko kaskazini magharibi mwa Nigeria. Taarifa zinasema kuwa, kundi la Waislamu katika mji wa Bichi katika jimbo la Kano kaskazini magharibi mwa Nigeria lilimiminika barabarani

                Wafuasi wa Rais Mursi waandamana hadi ikulu



                Wafuasi wa Rais Mursi waandamana hadi ikulu
                Mamia ya raia wa Misri wanaoumuunga mkono Rais Muhammad Mursi wa nchi hiyo leo wameandamana hadi katika ikulu ya rais wa nchi hiyo na kutangaza kuunga mkono uamuzi wake wa kumfukuza kazi mwendesha mashtaka mkuu na kuzuia  kuvunjwa baraza la kutunga katiba la nchi hiyo. Mamia ya Wamisri wanaomuunga mkono Rais Muhammad Mursi mapema leo wameandamana huku wakipiga nara za kumuunga mkono rais wao katika maamuzi aliyochukua  hapo jana ya kutangaza mabadiliko ya katiba ili kupanua uwezo wake. Rais wa Misri jana alitoa taarifa ya kisheria na kueleza kuwa hakuna chombo chochote cha kisheria kinachoweza kulivunja baraza la kutunga katiba la nchi hiyo. Mabadiliko hayo ya kisheria yanasisitiza kuhukumiwa upya Hosni Mubarak dikteta aliyeng'olewa madarakani huko Misri pamoja na viongozi wa zama za utawala wake wanaotuhumiwa kuwauwa wanamapinduzi na kufanya ufisadi katika uga wa kisiasa nchini humo.

                Mufti Mkuu wa Tanzania alaani jinai za Israel, Gaza



                Mufti Mkuu wa Tanzania alaani jinai za Israel, GazaMufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shaaban Simba amelaaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza Palestina ambapo makumi ya  wanawake, watoto, wazee na vijana wasio na hatia wameuawa hivi karibuni kufuatia hujuma na amshambulio ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza. Mufti Simba amesema, analaani mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya wananchi wa Palestina. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mufti Mkuu wa Tanzania amesema, anatoa wito kwa viongozi wa kitaifa na wale wa kimataifa, likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kutafuta haraka suluhisho la kudumu la kadhia ya Palestina. Amesema, Baraza Kuu la Waislamu nchini Tanzania BAKWATA siku zote limekuwa na itaendelea kuwa mstari wa mbele kuunga mkono harakati za Wapalestina za kupigania haki zao za kimsingi ikiwemo ya kuwa na nchi yao huru ya Palestina.

                Ziara ya Dk Shein Vietnam - siku ya pili




                  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akisalimiana na Makamo wa Rais Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,alipowasili Ikulu nchini Vietnam,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja
                 Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwamamwema Shein, akisalimiana na Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,alipowasili Ikulu nchini Vietnam,alipofuatana na Rais wa Zanzibar katika ziara Rasmi ya Kiserikali Nchini Vietnam ya wiki moja
                 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakipokea mashada ya mauwa kama ni Ishara ya ukaribisho katika Ikulu ya Vietnam,alipofika kwa mazungumzo na Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.[Picha na Ramadhan Othman Vietnam.]
                  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akisalimiana na Mawaziri na Viongozi mbali mbali wa Nchini Vietnam ,alipofika ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo na Makamo wa Rais Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja
                 
                Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akiwatambulisha Viongozi aliofuatana nao kwa Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi,Nguyen Thi Doan,walipowasili Ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo,ya kuimarisha uhusiano na Ushirikiano baina ya pande zote, akiwa katika ziara rasmi ya wiki moja nchini humo.

                Viongozi wa Serikali waliofuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakiwa kwenye mkutano maalum na uongozi wa serikali ya Vietnam.
                Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein,(katikati) akiwa ujumbe aliofuatana nao katika Mkutano maalum na Uongozi wa Serikali ya Vietnam,ukiongozwa na Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Bibi Nguyen Thi Doan,(hawapo pichani) katika ukumbi wa Ikulu ,katika kuimarisha Uhusiano na Ushirikiano baina ya pande mbili hizo,katika ziara rasmi ya Kiserikali.
                [Picha zote na Ramadhan Othman Vietnam.]

                Wanajeshi wa Tanzania kuelekea Kongo DRC



                Wanajeshi wa Tanzania kuelekea Kongo DRCTanzania imetangaza kuwa tayari kupeleka kikosi cha askari wake 800 kwenda kupambana na waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
                Hayo yamedokezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe ambaye amesema askari hao watajiunga na askari wengine wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ili wafikie 3,200 kwa ajili ya jukumu hilo.

                Wednesday, November 21, 2012

                Viongozi wa Uamsho wapunguziwa masharti ya dhamana


                Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la polisi

                ZANZIBAR JUMATANO NOVEMBA 21, 2012. Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar leo imepunguza masharti ya dhamana kwa Viongozi saba wa Jumuiya mbili za Kiislamu Zanzibar, wanaokabiliwa na mashtaka ya kusababisha vurugu na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya barabara mjini Zanzibar, leo tena wameshindwa kupata dhamana.


                Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa uwamuzi huo umetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mh. Ame Pinja, baada ya kukubali maombi ya Mawakili wa Watuhumiwa waliomba kupunguzwa kwa masharti hayo kwa wateja wao.


                Watuhumiwa hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimam ZanzibarSheike Farid Hadi Ahamed na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselemu na wenzao watano.




                Inspekta Mhina amesema kuwa kutokana na uwamuzi huo, kila mshitakiwa sasa atatakiwa kuwa na wadhaminiwa wawili ambao ni watumishi wa Serikali na kwa kila mmoja awe na kiasi cha shilingi 500,000 tofauti na mashrti ya awali ya wadhamini watatu na kwa kila mmoja kwa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila mmoja.


                Hata hivyo pamoja na kupunguzwa kwa masharti hayo, hakuna hata mshitakiwa mmoja aliyedhaminiwa kutokana na kukosekana kwa wadhamini ambao ni watumishi wa serikali.


                Inspekta Mhina amesema kuwa Watuhumiwa hao ambao wanakabiliwa na kesi tatu tofauti za kuzusha ghasia na kupelekea vurugu katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar, wamerudishwa rumande hadi desemba 4, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.


                Amesema wakati wote mahakama hiyo ikiiendelea, hali ya ulinzi nje na ndani ya Mahamakama uliimarishwa vya kutosha ambapo Makachero wa Jeshi la Polisi pamoja na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na wale wa vikosi.vya Ulinzi vya Zanzibar

                Tuesday, November 20, 2012

                Ujumbe wa Arab League wawasili Gaza



                Ujumbe wa Arab League wawasili GazaUjumbe wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) ukiongozwa na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Nabiil al Arabi umewasili leo mjini Gaza kuonesha mshikamano na wananchi wa eneo hilo wanaoendelea kushambuliwa na jeshi la Israel.
                Baada ya kuwasili Gaza al Arabi amesema nchi za Kiarabu zinapaswa kuwasaidia na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina mbele ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesisitiza pia juu ya udharura wa kusitishwa mashambulizi hayo haraka iwezekanavyo.
                Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Muhammad Kamil Amru ambaye pia yuko kwenye ujumbe huo amesema mashambulizi ya Israel yanayowalenga raia wa Gaza yanapaswa kusitishwa mara moja.
                Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan anayeandamana na ujumbe huo wa Arab League Ali Karti amelaani jinai za Israel huko Gaza na kusisitiza kuwa mashambulizi hayo ya kidhalimu yameukasirisha ulimwengu mzima wa Kiarabu na Kiislamu.
                Ujumbe huo wa nchi za Kiarabu unaojumuisha zaidi ya mawaziri kumi wa mambo ya nje umewasili Gaza huku ndege za kivita za Israel zikiendelea kushambulia vikali baadhi ya maeneo ya mji huo. Kanali ya televisheni ya al Manar ya Lebanon imeripoti kuwa Wapalestina 6 wameuawa shahidi leo sambamba na safari ya mawaziri hao katika Ukanda wa Gaza.

                Erdogan: Israel inafanya mauaji ya kimbari Gaza



                Erdogan: Israel inafanya mauaji ya kimbari GazaWaziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa utawa wa Kizayuni wa Israel unafanya mauaji ya kimbari huko katika Ukanda wa Gaza.
                Erdogan amelaani vikali mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa utawala huo ghasibu umekiuka sheria za kimataifa na kufanya mauaji ya kimbari huko Palestina. Amesema utawala huo pia unaendelea kuzikalia kwa mabavu ardhi zaidi za Palestina.
                Ameutaja utawala wa Israel kuwa ni wa kigaidi kutokana na mashambulizi yake dhidi ya watu wa Gaza na kwamba unaendelea kuwaua ovyo Waislamu hususan watoto wadogo wa eneo hilo.
                Takwimu zinaonesha kuwa raia zaidi ya 116 wa Ukanda wa Gaza wameuawa hadi sasa katika mashambulizi makali yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel kwa siku saba sasa katika eneo hilo.

                BARUA YA MSAADA KWA WAISLAMU WOTE.............



                JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
                (JUMIKI)
                للجنة الدعوة الإسلامية
                THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
                P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145-
                FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
                MKUNAZINI ZANZIBAR

                Ref. JMK/VOL/12/2012 05 Novemba, 2012
                Bimillahir Rahmanir Rahiim

                Ndugu Muislam,

                YAH: OMBI LA MCHANGO WA MAAFA

                Tafadhali husika na mada kama inavyosomeka hapo juu.

                Kila sifa njema zinamstahikia Allah (S.W.T), rehma na amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, masahaba zake na waliowema katika Uislamu.

                Kutokana na hali mbali mbali zilizojiri nchini mwetu hususan katika kuitetea Zanzibar huru yenye mamlaka yake kamili imepelekea baadhi ya watu kuathiriwa na hali hiyo ikiwemo kuuwawa kwa watu wasio na hatia, kuingiliwa majumbani mwao na kuibiwa mali zao na vyombo vya dola, pia wengine kuwekwa rumande wakiwemo Sheikh Msellem Ali, Amir Farid Hadi, Sheikh Khamis, Ustadh Hassan Bakar, Ustadh Ghalib na wengineo. Kutokana na hali hiyo jumuiya ya UAMSHO inakuomba uchangie kwa kadir ya ulivyojaaliwa na Allah (S.W.T) ili kuwasaidia waathirika hao, na ujira wako utaukuta siku yenye shida na hakutakua na msaada ila kwa kile ulichokitanguliza.

                Tunamuomba Allah (S.W.T) akulipe badala na kilicho na kheri zaidi kwa unachokitoa.

                Wabillahi Taufiq

                KATIBU MKUU.
                JUMUIYA YA UAMSHO.

                TUHUMA ZA UAMSHO KUNYOLEWA NDEVU WAKIWA GEREZANI, MAHAKAMA KUU YAWASHAURIWA WAFUNGUE KESI MADAI


                Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
                 Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar imetoa ushauri kwa Viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislam Zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa Taifa ya kutotendewa haki wakiwa Gerezani wafungue kesi ya madai.
                Ushauri huo umetolewa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mh. George Kazi mara baada ya kupitia kwa makini maombi ya watuhumiwa hao yaliyofikishwa mbele yake Novemba 8, mwaka huu kupitia kwa mawakili wa watuhumiwa hao.
                Kesi hiyo inawakabili watu wanane akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar
                na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselem.
                Wengine katika kesi hiyo ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na  Ghalib Ahmada Omar.
                Akitoa uwamuzi huo, Mh. Kazi amesema watuhumiwa wana haki ya kufungua kesi mahakama kuu ya kile wanachokilalamikia na kwamba mahakama kuu itakuwa na uwamuzi wa kuyasikiliza madai yao tofauti na kesi ya msingi kwa watuhumiwa.

                Monday, November 19, 2012

                Pinda awataka Watanzania kuishi kwa amani



                Pinda awataka Watanzania kuishi kwa amani
                Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda ametoa wito kwa Watanzania kuishi kwa amani na kuweka kando tofauti zao za kidini ili nchi isonge mbele.
                Akizungumza wakati wa kuzindua Taasisi ya Kiarabu Tanzania jijini Dar es Salaam, Pinda amesema Watanzania wameishi kama ndugu kwa muda mrefu bila ya kujali itikadi zao za kidini na ametaka jambo hilo liendelee kuwepo. Amesema machafuko yaliyoshuhudiwa majuzi Tanzania bara na Visiwani Zanzibar ambapo viongozi wa Kiislamu walikamatwa na vilevile makanisa kuchomwa yanatishia historia ndefu ya umoja na mshikamani miongoni mwa Watanzania wa dini mbalimbali.
                Wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo, Pinda alikutana na baadhi ya Mashekhe wa Dar es Salaam na kuwaahidi kwamba kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda itaendeshwa kwa uadilifu.

                Hali ya Usalama Kenya yazidi kuwa mbaya



                Hali ya Usalama Kenya yazidi kuwa mbaya
                Siku moja baada ya kuuawa raia 10 kwenye shambulio la guruneti mjini Nairobi, Kenya, wanajeshi 3 wameuawa kwa kupigwa risasi leo mjini Garissa na watu wasiojulikana.
                Habari zinasema kuwa wanajeshi hao walikuwa wakibadilisha gurudumu la gari lao lililokuwa limetoboka wakati watu wenye silaha walipowamiminia risasi na kuwaua. Mauaji ya hapo jana mjini Nairobi na ya leo mjini Garissa yametokea wiki moja tangu kuuawa zaidi ya maafisa 40 wa polisi katika eneo la Samburu, kaskazini mwa Kenya.
                Wananchi wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na kuzidi kudorora hali ya usalama na wameitaka serikali kuchukua hatua za dharura kuimarisha usalama haswa katika kipindi hiki ambapo nchi hiyo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu baadaye mwaka ujao.

                OIC yataka Wapalestina wa Gaza wasaidiwe haraka



                OIC yataka Wapalestina wa Gaza wasaidiwe haraka Mashambulizi ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza unaozingirwa yameingia siku ya 6 leo, huku idadi ya wananchi wa Palestina wanaouawa na kujeruhiwa ikizidi kuongozeka.
                Mwakilishi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ametaka kupelekwa haraka misaada ya tiba katika Ukanda wa Gaza. Wakati huo huo Naibu Waziri wa Tiba wa serikali halali ya Palestina ametahadharisha juu ya hatari zinazotokana na ukosefu wa dawa na vifaa vya tiba katika ukanda huo. Hassan Khalaf amesema, hali ya tiba na matibabu huko Gaza ni mbaya na kwamba ongezeko la majeruhi kutokana na mashambulizi ya Israel limesababisha ukosefu wa dawa na vifaa vya tiba. 
                Wapalestina wasiopungua 96 wameuawa shahidi na wengine 900 kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya siku 6 ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Gaza.
                Wakati huo huo msemaji wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amelaani mashambulio ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na kutaka mashambulizi hayo yasitishwe mara moja. Vilevile walimwengu wameendelea kuandamana katika kona mbalimbali duniani kulaani na kupinga mashambulizi hayo ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza.

                Sunday, November 18, 2012

                UN yalaani mashambulizi ya M23 mashariki mwa DRC



                UN yalaani mashambulizi ya M23 mashariki mwa DRC
                Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  limelaani vikali mashambulizi ya waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwenye maeneo ya Kibumba, Mboga na Ruhondo, pamoja na kuendelea kuukaribia mji wa Goma.
                Katika kikao cha Jumamosi mjini New York, Baraza la Usalama pia limewataka waasi hao kuheshimu majukumu ya vikosi vya usalama vya Umoja wa Mataifa, MONUSCO. Baraza la Usalama pia limetoa wito kwa nchi zilizo na ushawishi kwa waasi wa M23 yawashawishi waasi hao wakomeshe mashambulizi. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema Uganda na Rwanda zinaunga mkono waasi hao wa M23. Kikao hicho cha Baraza la Usalama kiliitishwa kufuatia ombi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kutokana na hali ya usalama inayoendelea kuzorota. Baraza la Usalama limesema kamati namba 1533 itaundwa, ambayo itapokea mapendekezo ya mataifa wanachama, na baadaye hatua zitachukuliwa kulingana na mapendekezo hayo.

                Israel yaendeleza ukatili wake Ukanda wa Ghaza



                Israel yaendeleza ukatili wake Ukanda wa GhazaUtawala haramu wa Israel umeendeleza ukatili wake kwa kuwaua shahidi Wapalestina wawili katika hujuma ya hivi karibuni  Ukanda wa Ghaza. Tayari Wapalestina karibu 50 wameuawa shahidi katika mashambulio ya  siku nne ya ndege za kivita za Israel dhidi ya watu wa Ghaza. Wanawake na watoto ndio whanaga wakubwa wa jina zinazoendelea za Israel dhidi ya Wapalestina huko Ghaza. Aidha katika hujuma ya hivi karibuni, ndege za kivita za Israel zimelenga jengo la mashirika ya habari mjini Ghaza ambapo waandishi habari sita wamejeruhiwa.
                Wakati huo huo katika hatua ya kulipiza kisasi jinai za Israel, wanamapambano wa Palestina wamevurumisha makombora zaidi katika mji wa Tel Aviv.
                Wakati huo huo viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu wamekutana mjini Cairo Misri na kusema wanaunga mkono Wapalestina katika kipindi hiki ambacho wanakabiliana na hujuma ya Israel. Hata hivyo viongozi hao wa nchi za Kiarabu wameshindwa kuchukua hatua za kivitendo za kukabiliana na ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina.

                Jalili akutana na mshauri wa Rais wa Ghana

                Jalili akutana na mshauri wa Rais wa Ghana
                Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kustawishwa mahusiano na nchi huru na zile zisizofungamana na siasa za upande wowote, ni miongoni mwa malengo makuu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Akizungumza na Mshauri wa Rais wa Ghana mjini Tehran Saeed Jalili ameitaja nafasi muhimu ya Ghana katika kuundwa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM na kukosoa misimamo ya kindumakuwili ya nchi za Magharibi katika kuamiliana na kadhia kama vile haki za binadamu, ugaidi na kuizuia  Iran isitumie nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani.

                Tanzania na Malawi kutatua mgogoro wa Ziwa Nyasa



                Tanzania na Malawi kutatua mgogoro wa Ziwa Nyasa
                Serikali za Tanzania na Malawi zimefikia makubaliano ya kumtafuta mpatanishi wa kimataifa atakayetatua hitilafu za mpaka wa majini kati ya nchi hizo mbili. Bernard Membe Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania ameyasema hayo mjini Dar es Salaam alipokutana na mwenzake Ephrahim Muganda Chiume wa Malawi na kuongeza kuwa, pande hizo mbili zimechukua uamuzi wa pamoja wa kuupeleka mgogoro huo kwa jopo la maraisi wastaafu wa Afrika linaloongozwa na Joaquim Chissano Rais wa zamani wa Msumbiji ambalo linashughulikia kutatua hitilafu na migogoro mbalimbali barani  Afrika.

                Mkutano wa Ziwa Nyasa waendelea nchini Tanzania



                Mkutano wa Ziwa Nyasa waendelea nchini TanzaniaMkutano kati ya Tanzania na Malawi wa kujadili suluhu ya mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa umeingia siku yake ya pili jijini Dar es Saalam huku washiriki wakitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu jinsi ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo. Mkutano huo unaowahusisha wataalamu kutoka Wizara na Idara mbalimbali za Serikali za Tanzania na Malawi, unatarajia kuandaa mazingira ya kufanyika mkutano wa ngazi ya mawaziri baadaye hapo kesho. Akifungua Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bw. John Haule alisisitizia umuhimu wa wajumbe kutoka nchi zote mbili kujadili na kupendekeza njia zitakazosaidia kupata suluhisho la kudumu la mgogoro huo. Aidha, Bw. Haule aliweka bayana kuwa serikali ya Tanzania ina dhamira ya dhati kufanya kazi pamoja na serikali ya Malawi kutafuta suluhu ya mgogoro huo jambo ambalo pia lilisisitizwa na Bw. Julius Chisi, Kiongozi wa Ujumbe wa Malawi. Mazungumzo kati ya nchi mbili hizo yalivunjika mwezi Septemba baada ya Tanzania kutangaza ramani mpya ya nchi hiyo. Malawi ilijiondoa kwenye mazungumzo hayo kwa madai kwamba ramani hiyo mpya ya Tanzania inajumuisha eneo la Ziwa Nyasa linaloendelea kuzozaniwa na pande mbili hizo.

                OIC: Mauaji ya Waislamu wa Myanmar ni ya Kimbari


                OIC: Mauaji ya Waislamu wa Myanmar ni ya Kimbari
                Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC wamemaliza mkutano wao wa siku tatu nchini Djibouti leo Jumamosi ambapo wito umetolewa wa kuchukuliwa hatua za dharura kukomesha mauaji ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar. Mkutano huo ulioanza siku ya Alhamisi umejadili kwa kina mashambulizi ya jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Taarifa ya mwisho ya mkutano huo sambamba na kulaani jinai za Wazayuni huko Gaza, imezitaka nchi wanachama kuchukua hatua za kivitendo kukomesha jinai hizo. Pia wajumbe wamekubaliana kwamba OIC ipewe nafasi zaidi ya kushughulikia kadhia ya Syria. Jumuiya hiyo imepinga uingiliaji wowote wa kigeni katika mgogoro wa Syria na kusisitiza kwamba Wasyria wenyewe ndio watakaoweza kutatua mgogoro wao bila kushinikizwa na madola ya kigeni.

                Mapigano makali yaendelea mashariki mwa Kongo



                Mapigano makali yaendelea mashariki mwa KongoMapigano makali yanaendelea kuripotiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baina ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali. Mashuhuda wanasema, mapigano baina ya pande mbili yanaendelea kushuhudiwa katika eneo la Kibumba lililoko jirani na mpaka wa nchi hiyo na Rwanda. Taarifa zaidi zinasema kuwa, milio ya risasi imeendelea kusikika na kuzusha wasi wasi mkubwa huku baadhi ya raia wakilazimika kuyakimbia makazi yao. Tayari Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Augustin Matata Ponyo ameutaka Umoja wa Mataifa uwawekee vikwazo viongozi wa serikali ya Rwanda kutokana na kuchochea machafuko mashariki mwa Kongo.

                UK yaikatia Uganda misaada kwa tuhuma za rushwa


                UK yaikatia Uganda misaada kwa tuhuma za rushwa
                Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Justine Greening amesema serikali ya London imesitisha misaada ya takribani dola milioni 18 kwa serikali ya Uganda kutokana na kuwepo tuhuma za ufisadi katika ofisi ya Waziri Mkuu. Greening amesema misaada hiyo haitatolewa hadi pale Kampala itakapochunguza tuhuma hizo na kuchukua hatua zifaazo. Waziri huyo amesema fedha hizo zinatokana na ushuru wa wananchi wa Uingereza na kwa mantiki hiyo wanataka kuona fedha zao zikitumika kuwasaidia wale wanaohitaji misaada ya dharura. Katibu wa kudumu katika ofisi ya Waziri Mkuu nchini Uganda anatuhumiwa kufuja fedha za umma hususan zinazotokana na misaada ya kigeni lakini kiongozi huyo amekanusha tuhuma hizo sambamba na kukataa kujiuzulu. Ikulu ya Rais mjini Kampala pia imeonekana kumkingia kifua katibu huyo kwani imesema haiwezi kumuachisha kazi iwapo hakuna ushahidi unaoonyesha ameiba mali ya umma.

                Wananchi wa Sierra Leone washiriki uchaguzi mkuu



                Wananchi wa Sierra Leone washiriki uchaguzi mkuu
                Mamilioni ya raia nchini Sierra Leone, wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura Jumamosi hii ili kumchagua rais na wabunge wapya. Hali imekuwa shwari katika vituo vingi vya upigaji kura hususan mji mkuu, Freetown. Rais wa sasa, Ernest Bai Koroma anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wengine 8 wa kiti cha rais. Hata hivyo weledi wa mambo wanaamini kuwa mchuano mkali utakuwa kati ya Rais Bai na mpinzani wake wa karibu, Julius Maada Bio anayewania wadhifa huo kwa tiketi ya chama cha Sierra Leone Peoples Party (SLPP). Bai Koroma alichaguliwa kuwa rais mwaka 2007 na anapania kutetea wadhifa wake kwa kipindi kingine cha pili. Sierra Leone imekumbwa na vita vya ndani kwa muda mrefu na ni miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya almasi.

                Friday, November 16, 2012

                MILIONI SITA ZINAHITAJIKA KWA AJILI YA MATIBABU YA MTOTO SELEMANI SAID



                MILIONI sita zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Selemani Said (1), ambaye anajisaidia haja kubwa kupitia utumbo mkubwa huku ukiwa nje ya tumbo lake imeleezwa.
                Akizungumza na wandishi wa habari Katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),jijini Dar es Salaam leo, mama wa mtoto huyo, Veronika Laurent ambaye ni Mkazi wa Bunju, alisema mtoto huyo alizaliwa huku akiwa na sehemu ya kutolea haja kubwa lakini cha kushangaza, haja kubwa ilikuwa ikitokea mdomoni.
                Alisema msaada wa fedha hizo utasaidia katika kumfanyia operesheni mtoto huyo ambaye kwa sasa anaishi akiwa katika mateso makubwa.
                Veronika alisema hivi sasa yeye pamoja na mwanaye huyo wanaishi maisha ya kubahatisha baada ya baba wa mtotohuyo kuitelekeza familia hiyo kutokana na hali ya ugonjwa wa mtoto huyo.

                AU: Serikali ya Mali ifanye mazungumzo na waasi



                AU: Serikali ya Mali ifanye mazungumzo na waasiUmoja wa Afrika umeitaka serikali ya Mali kufanya mazungumzo na makundi ya waasi nchini humo.
                Mwakili wa ngazi za juu wa Umoja wa Afrika katika mauala ya Mali Pierre Buyoya ameitaka serikali ya Mali kufanya juhudi kubwa zaidi za kufanya mazungumzo na makundi ya waasi wanaobeba silaha huko kaskazini mwa nchi hiyo.
                Buyoya amesema iwapo serikali ya Bamako itaanza mazungumzo na makundi yenye silaha waasi wa makundi mengine watapoteza uwezo wa kukabiliana na jeshi la serikali.
                Wito huo wa Pierre Buyoya umetolewa baada ya mazungumzo ya Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore ambaye ni mpatanishi katika mgogoro wa kaskazini mwa Mali na mwakilishi wa kundi la Ansaruddin ambaye ameyataka makundi mengine ya waasi kufanya mazungumzo na serikali ya Bamako.
                Mwakilishi wa kundi la waasi la Ansaruddin amesema makundi yote ya Mali yanaweza kujadili njia za kukomesha hitilafu zilizopo kupitia mazungumzo ya kisiasa baada ya kukomeshwa machafuko ya sasa.
                Makundi ya waasi ya Mali yalilidhibiti eneo la kaskazini mwa nchi hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo tarehe 22 Machi mwaka huu.

                Mkutano wa OIC waanza Djibouti



                Mkutano wa OIC waanza DjiboutiMkutano wa 39 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ulianza jana nchini Djibouti kwa kaulimbiu ya "Umoja kwa Ajili ya Ustawi Endelevu katika Ulimwengu wa Kiislamu."
                Mkutano huo wa siku tatu unajadili masuala muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu hususan hali ya Syria, Myanmar, Somalia na Sudan.
                Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Akbar Salehi ambaye anashiriki katika mkutano huo amekutana na waandishi habari nchini Djibouti akiashiria mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu nchini Myanmar na kusema Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imekuwa mstari wa mbele kueleza hali na masaibu ya Waislamu wa Myanmar na inataka kuzishirikisha jumuiya nyingine za kimataifa katika suala hilo. Salehi pia ameashiria jinai zinazofanywa sasa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema inasikitisha kwamba nchi za Kiislamu hazijachukua hatua ya maana ya kuwalinda raia wanaodhulumiwa wa Palestina na suala hilo limeupa utawala haramu wa Israel fursa zaidi ya kutenda jinai kubwa huko Gaza.
                Amesema inatarajiwa kuwa OIC itachukua hatua za dharura katika uwanja huo.

                Nasrullah awataka watu huru kuwasaidia raia wa Gaza



                Nasrullah awataka watu huru kuwasaidia raia wa GazaKatibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amewataka Waislamu, Waarabu na watu huru kote duniani kupigana bega kwa bega na watu wa Ukanda wa Gaza dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
                Sayyid Nasrullah ambaye alikuwa akizungumzia mashambulizi ya sasa ya Israel dhidi ya watu wa Gaza amesema yanayotokea sasa katika eneo hilo ni mpambano baina ya utawala unaopenda kumwaga damu za watu wa Israel na mataifa ya Mashariki ya Kati hususan Wapalestina. Amesema watawala katili wa Tel Aviv hawahitaji sababu yoyote kwa ajili ya kutekeleza ukatili na kusisitiza kuwa viongozi hao wameshtushwa na uwezo wa kujihami wa makundi ya wapigania uhuru wa Palestina. Amesema majibu ya makombora ya makundi ya jihadi ya Palestina dhidi ya mji wa Tel Aviv yamewaacha bumbuazi Wazayuni na kudhihirisha uwezo wa wanamapambano wa Kipalestina.
                Katibu Mkuu wa Hizbullah amewataka viongozi wa kisiasa wa Mashariki ya Kati kutupilia mbali hitilafu zao na kuungana kwa ajili ya kujibu uchokozi wa adui Mzayuni huko katika Ukanda wa Gaza.
                Wapalestina wasiopungua 19 wameuawa shahidi katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel dhidi ya raia wa Gaza.