Tanzania imetangaza kuwa tayari kupeleka kikosi cha askari wake
800 kwenda kupambana na waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Hayo yamedokezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe ambaye amesema askari hao watajiunga na askari wengine wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ili wafikie 3,200 kwa ajili ya jukumu hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, Membe amesema nchi za SADC zimeazimia kupeleka jeshi Kongo kwa kuwa kuwapo kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo hakujasaidia lolote. Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania amesema Umoja wa Mataifa unazizuia nchi za SADC na Maziwa Makuu kupeleka majeshi yake, huku hali nchini DRC ikizidi kuwa mbaya kwa kuwa waasi hao, wanaendelea kuua na kubaka watoto na kinamama jambo ambalo linapaswa kuchukuliwa hatua za haraka. Hivi karibuni waasi wa M23 waliteka mji wa Goma na wametangaza nia yao ya kuelekea hadi Kinshasa kuiondoa madarakani serikali ya Rais Joseph Kabila.

No comments:
Post a Comment