Mamilioni ya raia
nchini Sierra Leone, wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura
Jumamosi hii ili kumchagua rais na wabunge wapya. Hali imekuwa shwari
katika vituo vingi vya upigaji kura hususan mji mkuu, Freetown. Rais wa
sasa, Ernest Bai Koroma anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa
wagombea wengine 8 wa kiti cha rais. Hata hivyo weledi wa mambo
wanaamini kuwa mchuano mkali utakuwa kati ya Rais Bai na mpinzani wake
wa karibu, Julius Maada Bio anayewania wadhifa huo kwa tiketi ya chama
cha Sierra Leone Peoples Party (SLPP). Bai Koroma alichaguliwa kuwa rais
mwaka 2007 na anapania kutetea wadhifa wake kwa kipindi kingine cha
pili. Sierra Leone imekumbwa na vita vya ndani kwa muda mrefu na ni
miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani licha ya kuwa na utajiri mkubwa
wa madini ya almasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment