Hapo Jana Netanyahu alimpigia simu Rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas akimtaka kutokwenda Umoja wa Mataifa na badala yake arudi kwenye meza ya mazungumzo na Wazayuni. Netanyahu ametishia kwamba endapo Abbas ataenda Umoja wa Mataifa, mazungumzo eti ya amani yatakosa maana na kwamba Wapalestina watakabiliwa na mashinikizo zaidi.
Palestina ikipata uanachama kamili itakuwa na uwezo wa kuiburuza Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) jambo ambalo Tel Aviv inaliogopa mno.
No comments:
Post a Comment