Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, November 13, 2012

Msumbiji: Dhlakama hataanzisha tena vita vya ndani



Msumbiji: Dhlakama hataanzisha tena vita vya ndaniPolisi ya Msumbiji imesema kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani na kamanda wa zamani wa waasi wa nchi hiyo Afonso Dhlakama hatatekeleza vitisho vya kuitumbukiza tena nchi hiyo katika vita vya ndani.

Msemaji wa polisi ya Msumbuji Pedro Cossa amesema Dhlakama si mtoto mdogo na kwa msingi huo serikali inaamini kwamba hatatekeleza vitisho vya kuanzisha tena vita vya ndani nchini. Amesisitiza kuwa Afonso Dhlakama ameahidi mara nyingi kwamba hataanzisha tena vita vya ndani na inatarajiwa kwamba hatabadili msimamo wake.
Kiongozi wa waasi wa zamani wa Msumbiji ametishia kuwa ataanzisha tena wimbi la damu nchini humo iwapo serikali haitagawa utajiri unaoongezeka kila kwa watu wote na kufanyia marekebisho mfumo wa uchaguzi.

No comments:

Post a Comment