Karibu askari polisi 300 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo
wameingia katika mji wa Goma makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini,
baada ya kuondoka wanamgambo wa kundi la waasi wa M23 katika mji huo
waliokuwa wakiudhibiti kwa zaidi ya wiki moja. Manodje Mounoubai Msemaji
wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo MONUSCO
amesema kuwa,
lengo la kutumwa askari polisi hao katika mji wa Goma baada ya kuondoka waasi wa M23, ni kudhamini na kuleta amani na usalama katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini. Manodje Mounoubai ameongeza kuwa, kwa mujibu wa mipango iliyoratibiwa, hadi sasa askari polisi wa Kongo wapatao 270 kati ya 450 wameshajizatiti katika mji wa Goma. Wiki iliyopita, wakuu wa nchi wanachama wa eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika walikutana nchini Uganda na kuchukua uamuzi wa pamoja wa kuwataka waasi hao kuondoka haraka katika mji huo. Hatimaye, waasi wa M23 walikubali kuondoka kwenye mji huo baada ya kusikilizwa takwa lao la kufanya mazungumzo na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

No comments:
Post a Comment