Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa
Uingereza, Justine Greening amesema serikali ya London imesitisha
misaada ya takribani dola milioni 18 kwa serikali ya Uganda kutokana na
kuwepo tuhuma za ufisadi katika ofisi ya Waziri Mkuu. Greening amesema
misaada hiyo haitatolewa hadi pale Kampala itakapochunguza tuhuma hizo
na kuchukua hatua zifaazo. Waziri huyo amesema fedha hizo zinatokana na
ushuru wa wananchi wa Uingereza na kwa mantiki hiyo wanataka kuona fedha
zao zikitumika kuwasaidia wale wanaohitaji misaada ya dharura. Katibu
wa kudumu katika ofisi ya Waziri Mkuu nchini Uganda anatuhumiwa kufuja
fedha za umma hususan zinazotokana na misaada ya kigeni lakini kiongozi
huyo amekanusha tuhuma hizo sambamba na kukataa kujiuzulu. Ikulu ya Rais
mjini Kampala pia imeonekana kumkingia kifua katibu huyo kwani imesema
haiwezi kumuachisha kazi iwapo hakuna ushahidi unaoonyesha ameiba mali
ya umma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment