Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 16, 2012

Mkutano wa OIC waanza Djibouti



Mkutano wa OIC waanza DjiboutiMkutano wa 39 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ulianza jana nchini Djibouti kwa kaulimbiu ya "Umoja kwa Ajili ya Ustawi Endelevu katika Ulimwengu wa Kiislamu."
Mkutano huo wa siku tatu unajadili masuala muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu hususan hali ya Syria, Myanmar, Somalia na Sudan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Akbar Salehi ambaye anashiriki katika mkutano huo amekutana na waandishi habari nchini Djibouti akiashiria mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu nchini Myanmar na kusema Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imekuwa mstari wa mbele kueleza hali na masaibu ya Waislamu wa Myanmar na inataka kuzishirikisha jumuiya nyingine za kimataifa katika suala hilo. Salehi pia ameashiria jinai zinazofanywa sasa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema inasikitisha kwamba nchi za Kiislamu hazijachukua hatua ya maana ya kuwalinda raia wanaodhulumiwa wa Palestina na suala hilo limeupa utawala haramu wa Israel fursa zaidi ya kutenda jinai kubwa huko Gaza.
Amesema inatarajiwa kuwa OIC itachukua hatua za dharura katika uwanja huo.

No comments:

Post a Comment