Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, November 20, 2012

Erdogan: Israel inafanya mauaji ya kimbari Gaza



Erdogan: Israel inafanya mauaji ya kimbari GazaWaziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa utawa wa Kizayuni wa Israel unafanya mauaji ya kimbari huko katika Ukanda wa Gaza.
Erdogan amelaani vikali mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa utawala huo ghasibu umekiuka sheria za kimataifa na kufanya mauaji ya kimbari huko Palestina. Amesema utawala huo pia unaendelea kuzikalia kwa mabavu ardhi zaidi za Palestina.
Ameutaja utawala wa Israel kuwa ni wa kigaidi kutokana na mashambulizi yake dhidi ya watu wa Gaza na kwamba unaendelea kuwaua ovyo Waislamu hususan watoto wadogo wa eneo hilo.
Takwimu zinaonesha kuwa raia zaidi ya 116 wa Ukanda wa Gaza wameuawa hadi sasa katika mashambulizi makali yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel kwa siku saba sasa katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment