Waziri Mkuu wa serikali halali ya
Palestina huko Ghaza amesema kuwa wakazi wa Ukanda wa Ghaza wako tayari
kukabiliana na mashambulizi ya jeshi la utawala haramu wa Kizayuni.
Ismail Hania amesema kuwa kushadidi mashambulizi ya utawala ghasibu wa
Kizayuni huko Ghaza hakutadhoofisha azma na irada ya wakazi wa eneo
hilo.
Hania ameyasema hayo baada ya kuwatembelea katika hospitali ya al
Shifaa baadhi ya Wapalestina waliojeruhiwa katika mashambulio ya hivi
karibuni ya jeshi la Israel huko Ukanda wa Ghaza. Hania ameongeza kuwa
serikali halali ya Palestina imeanzisha harakati kadhaa katika nyanja
mbalimbali zikiwemo za kidiplomasia kupitia kuwasiliana na viongozi wa
nchi za Kiarabu na pia taasisi za kieneo na kimataifa ili kusaidia
kudhibiti mashambulizi ya utawala ghasibu wa Kizayuni huko Ghaza. Waziri
Mkuu wa serikali halali ya Palestina huko Ghaza amesema wameziomba
pande za Kiarabu na kimataifa kuwashtaki na kuwahukumu viongozi wote wa
utawala ghasibu wa Israel waliohusika na jinai chungu nzima dhidi ya
raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Ghaza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment