Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, November 15, 2012

Ugonjwa wa Ebola waripuka tena Uganda



Ugonjwa wa Ebola waripuka tena Uganda
Waziri wa Afya wa Uganda, Christine Ondoa ametangaza kuwa, watu 2 wamefariki dunia baada ya kutokea mripuko mpya wa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Luweero, nje kidogo ya mji mkuu Kampala. Waziri Ondoa amesema kuwa hatua za tahadhari zimechukuliwa ili kukabiliana na hali hiyo. Amewataka wananchi kuepuka mikusanyiko ya watu wengi kutokana na ukweli kwamba ugonjwa huo unaenea kwa kasi hususan katika maeneo yenye watu wengi.
Watu wengine 5 wamelazwa katika wodi maalumu hospitalini Mulago jijini Kampala. Mwezi Julai mwaka huu, zaidi ya watu 15 walifariki dunia huko Magharibi mwa Uganda kutokana na Ebola. Hadi sasa ugonjwa huo hauna tiba na wataalamu wa afya wanasema kuwa, asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa hufariki dunia katika kipindi kifupi. Uganda imekuwa kitovu cha virusi vya ugonjwa huo na tukio baya zaidi lilikuwa la mwaka 2000 ambapo zaidi ya watu 450 waliambukizwa na zaidi ya 200 kati yao walifariki dunia.

No comments:

Post a Comment